KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA MatangazoKILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA

Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, May 23, 2017

WANANCHI WA WILAYA YA NYASA WANUFAIKA NA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA KISASA CHINI YA USIMAMIZI NA UFUATILIAJI WA MBUNGE WA JIMBO LA NYASA NAIBU WAZIRI WA ELIMU MHANDISI STELLA MANNYANYA

 Mhandisi Stella Manyanya akielekea akishuka katika Ndege ya ATCL kwenye uwanja wa Ndege wa Songea tayari kuelekea wilayani Nyasa kwa ajili ya kukabidhi vifaa tiba.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi akikabidhi Vifaa tiba vikiwemoVitanda vya kujifungulia akina Mama, Xray Mashine, Utra Sound, Will chair, Magodoro, Vitanda vya Wodi ya wazazi na vingine  katika Kituo cha Afya cha Mbamba Bay wilayani Nyasa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji amesema ameshirikiana na viongozi wa Halmashauri ya wilaya kupigania kupatikana kwa vifaa hivyo ili kukabiliana na vifo vya Mama na Mtoto wakati wa Uzazi.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi amesema kupatikana kwa Vifaa vilivyokabidhiwa kumetokana na ushirikiano uliopo kati ya Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakiwemo Mkuu wa wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Dr Osca Albano Mbyuzi,  jambo ambalo linasaidia katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya yaNyasa ambao walikuwa wakiifuata huduma hiyo umbali mrefu kwa kutumia usafiri usio salama kama wa Pikipiki na kuhatarisha maisha ya mzazi.
 Wananchi waliohudhuria katika kukabidhi vifaa hivyo wameishukuru Serikali na mbunge wa Jimbo la Nyasa kwa kuwapunguzia adha waliyokuwa wakiipata kwa kufuata huduma za upasuaji na uzazi salama, wamesema awali walikuwa wakitumia kiasi kikubwa cha nauli kuvifikia vituo vyenye huduma bora za Afya ya uzazi jambo ambalo lilikuwa likihatarisha maisha ya wazazi.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi vifaa hivyo ameomba wataalamu kuvigawa kadiri ya mahitaji kwa kuvisambaza katika vituo mbalimbali ili kuwapunguzia umbali wa kutembea kufuata huduma za dharula hasa kwa wazazi.
 Aidha Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya tunduru Juma Homera akipokea Vifaa hivyo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Nyasa na kuwaomba wananchi na wataalamu wa afya kuvitunza vifaa hivyo kadiri ya uthamani wake, amesema si rahisi Kituo cha Afya kikawa na Vifaa vyenye tija kwa wingi huo hivyo wana wajibu wa kuthamini mchango wa wadau waliwezesha kupatikana vifaa hivyo kwa kuvilinda visiharibike au kupotea.
 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa amesema jambo lililofanywa na Naibu Waziri wa Elimu linastahili kuigwa kwa kuwa wapo wabunge ambao wamekuwa wakitelekeza Majimbo yao wapo wananchi wanatamani kupata Vifaa kama hivi kwa ustawi wa wananchi kwa kuwa Afya ndio msingi wa kila jambo.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbamba Bay Dr Aaron Hyera ameshukuru kwa kupata Vifaa tiba ambazo vitasaidia kusovu baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zikiikabili Halmashauri ya wilaya ya Nyasa.
 Akizitaja baadhi ya Changamoto wanazokabiliana nazo katika utoaji wa Huduma za Afya ni pamoja na uhaba maghari kutokana na uchakavu wa baadhi ya Magari ya wagonjwa (Ambulece), upatikanaji mdogo wa fedha za ruzuku za kuwezesha kununua vifaa tiba kadiri ya Bajeti wanazozipitisha, uhaba wa watumishi hususani waganga na wauguzi ambapo kwa sasa kuna upungufu wa watumishi 180 waliopo ni 228 katika vituo vya kutolea huduma za afya, wana Medical Officer mmoja tu na mwingine wanatarajia kumpokea hivi karibuni.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbamba Bay amesema changamoto nyingine ni upungufu wa Dawa kutoka MSd ambapo kati ya Bajeti wanayoomba ya madawa upatikanaji wa dawa zinazokuja ni 50% tu au chini ya hapo jambo ambalo linawawia vigumu namna ya kuzigawa katika vituo kadiri ya Mahitaji.
 Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Mbamba Bay Dr. Aaron hyera amesema upatikanaji wa Vifaa hivi vitasaidia sana kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ambapo amesema kwa sasa takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutokana na elimu ya kuwataka wazazi kuhudhuria kliniki ambapo mwaka 2014 kati ya wanawake laki moja wanaojifungua kulikuwa na vifo 78 vitokanavyo na uzazi ambavyo vimepungua hadi kufikia vifo 23 katika wazazi laki moja kwa mwaka 2016.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mbamba Bay Dr Paulo Matinde na wauguzi wa Kituo cha Mbamba Bay wamepongeza jitihada zilizofanyika na kufanikisha kukamilika kwa ujenzi wa Jengo la Upasuaji na Wodi ya wazazi pamoja na upatikanaji wa Vifaa tiba utaongeza hari ya ufanyaji kazi kwa kuwa vitendea kazi vimeongezeka ambapo kituo kilikuwa hakina mashine ya utrasound na xray na vitanda vya kujifungulia lakini sasa vyote vimepatikana wanachoomba wazazi kuja kujifungulia katika vituo vya Afya.
 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Nyasa anasema kufanikisha kwa upatikanaji na utoaji wa huduma za Afya kunadhihirisha kauli ya Uchungu wa Mwana aujua Mzazi kwa kugusa maendeleo ya wazazi katika kuboresha afya ya mama na mtoto kwa wananchi wa wilaya ya Nyasa.
Wilaya ya Nyasa ina Vituo vya kutolea Huduma za Afya 35 ambapo kati ya hivyo vituo vya Afya  vinne vinamilikiwa na serikali pamoja na Zahanati 21 za Serikali, vingine ni vya Mashirika ya Dini na Binafsi. Kwa sasa haina Hospitali ya wilaya jitihada zinafanyika za kupata eneo la kutosha kuwezesha Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.

Thursday, May 18, 2017

NYUMBA BORA YA WAGENI MKOANI RUVUMA PAPOK HOTEL

 Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amekuwa akisistiza mara kwa mara wananchi kuwekeza katika Utalii kama alivyofanya Mwekezaji wa Nyumba ya Wageni ya PAPOK kwa kujenga nyumba safi ya kulala wageni ambayo inavutia wageni kuja kulala pasipo na shaka ikiwa ni kuitikia wito wa Serikali wa kukuza uwekezaji kuendana na uchumi wa Viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dr. Osca Albano Mbyuzi amewataka wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na wazawa wa Wilaya ya Nyasa kuwekeza kwa kasi Nyumba za kulala wageni katika Mwambao wa Ziwa Nyasa kama ilivyo Nyumba ya Wageni ya PAPOK ukizingatia wilaya ya Nyasa ina fursa nyingi za utalii ambazo sizku zijazo zitaingiza pato kubwa kupitia wageni mblimbali wa Nje na ndani ya Nchi.  
 Ukiangalia kwa mbali utaona Magari aliyo egeshwa ya kionyesha kuwa pambo la la nyumba hiyo ya kulala wageni ina uhakika wa ulinzi, ili kufika hapo wasiliana kwa namba ya Simu 0753 495 161 utafika katika nyumba hiyo ya PAPOK HOTEL
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr Binilith Satano Mahenge akiwahimiza watanzania kuja Ruvuma kuangalia vivutio vilivyoko Mwambao wa Ziwa Nyasa, Milima ya Mbuji, Fukwe za ziwa Nyasa, Pamoja na visiwa vya Pomonda,Lundo na visiwa vya Mbambabay bila kusahau ukiwa Songea utakutana na Nyumba za wageni ikiwa ni pamoja na GEST HOUSE YA PAPOK iliyoko Mtaa wa CCM
 Meya wa Manispaa ya Songea Alhaji Abdull Shaweji akielezea vivutio vya Manspaa ya Songea ikiwemo na  PAPOK
 Mkoa wa Ruvuma kwa sasa hakuna shida ya usafiri wa Anga umeshaanza hivyo kuwepo kwa  PAPOK GEST HOUSE Kumeongeza kutokuwa na ufinyu wa nyumba za wageni
  PAPOK GEST HOUSE ni moja ya kivutio cha Mkoa wa Ruvuma usisikie kwa kuambiwa, wale ambao hawajatumia lifuti basi wanaweza kutembelea kuangalia jinsi unavyoweza kupandishwa juu na Mashine za kisasa ukiwakatika Gest ya PAPOK
 Afisa kilimo wa Halmashauri ya Songea Vijijini Nyakunga akielezea fursa za uchumi kupitia Mazao yanayo patikana mkoani Ruvuma, zaidi ya Tani milioni moja za nafaka ya Mahindi hupatikana kila Mwaka baada ya  mavuno amesema nivizuri ukafanya utalii wa Ndani kwa kulala  PAPOK HOTEL
Moja ya vivutio ni mapambo ya mawe meupe ambayo ufikapo Songea uta kutana nayo bila kusahau kufikia nyumba ya wageni ya  PAPOK
Nyumba ya wageni ambayo imeongeza umaarufu wa Mkoa wa Ruvuma iitwayo PAPOK ni pambo zuri pia ni nyumba yenye vigezo vyote kwa ajili ya kulala wageni Maarufu na watalii wale wenye uwezo wakufanya utalii ndani ya nchi wanapaswa kujenga utamaduni wa kutumia fursa hii badala ya kutegemea watalii kutoka nje ya mkoa pekee ni vizuri kukithamini cha kwako kwa kuwaunga mkono wawekezaji wa aina hii.
Meneja wa wakala wa Huduma za Mazao ya Misitu wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa akiwa katika maswala ya utalii na wageni aliokuwa nao wakisifu nyumba ya wageni iliyoko mtaa wa CCM Manispaa ya Songea iitwayo PAPOK

JESHI LA POLISI MKOA WA RUVUMA KWA KUSHIRIKIANA NA AFISA TARAFA WA TARAFA YA MUHUKURU SALMA MAPUNDA WAENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA KWA KUTEKETEZA MASHAMBA YA BANGI


Afisa tarafa wa Tarafa ya Muhukuru Salma Mapunda akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Songea katika zoezi la kuteketeza bangi iliyooteshwa shambani amesema shamba lenye ukubwa wa ekari 2 linaloteketezwa lilibainika baada ya wananchi wenye kuchukia biashara ya Madawa ya kulevya kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji kutoa taarifa za uwepo wa shamba hilo.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limefanikiwa kuteketeza Shamba hilo la Bangi lenye ukubwa wa ekari 2 katika Kijiji cha Manyamba Kata ya Muhukulu barabarani Songea Vijijini.

 Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa imara katika mapambano dhidi ya Vita hii ya Madawa ya Kulevya ambayo ni tishio kwa Vijana.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Manyamba akishiriki katika zoezi la kuteketeza Bangi amesema yeye kama kiongozi wa Serikali ataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na Viongozi wengine katika Mapambano dhidi ya Zao la Bangi amesema tatizo lililopo wakulima wa bangi wanahamia kinyemela katika vijiji kwa kutafuta maeneo mazuri ya kulima wanapopata wanaamua kulima Bangi badala ya kulima mazao ya chakula
 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Manyamba anasema, inakuwa vigumu kuyabaini mashamba hayo wanapoanza kilimo kwa kuwa hawaripoti katika Uongozi wa Vijiji husika wao huchukua maeneo kupitia kufuata wenzao na baadaye inabainika bangi ikiwa imeoteshwa na pengine imeshakuwa kupitia doria za msako wa mashamba yanayolimwa bangi hizo.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Manyamba anasema vijana watambue kuendelea kulima Bangi hawatakuwa salama kwa kuwa Serikali ina mkono mrefu badala yake wanaweza kulima Maharege, Ufuta na mahindi mazao ambayo wakilima hawana shida ya kukimbizana na Serikali.
 Mwanasheria wa Serikali akiwa katika Oparesheni hiyo ya Kuteketeza Bangi katika shamba lililopo Msitu wa Kijiji cha Manyamba Muhukuru Songea Vijijini amesema sheria ya sasa hivi iko wazi na endapo mtuhumiwa anabainika na vielelezo vikitimia adhabu yake haina mbadala hivyo ni vyema wananchi wakaacha kabisa kujishughulisha na kilimo cha bangi badala yake watafute kazi zingine.
 Mwanasheria wa Serikali akishiriki zoezi la kufyeka Bangi iliyokuwa imeoteshwa katika Shamba hilo Kijiji cha Manyamba Tarafa ya Muhukuru.

Afisa tarafa wa Tarafa ya Muhukuru amesema wananchi kutokana na kuzungukwa na Hifadhi za Misitu minene za wanyama na milima mikali ndiyo sababu hutumia kulima bangi wakijua hakuna mtu anayeweza kutambua uwepo wa mashamba hayo.

 Kazi ya uteketezaji wa zao la Bangi ikiendelea ikiongozwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Muhukuru Salma Mapunda akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema kwa kushirikiana na Vijana wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Songea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi Mwombeji amesema kampeni ya kuteketeza madawa ya kulevya inaendelea Mwananchi yeyote mwenye Taarifa za kuwepo kwa mashamba ya Bangi au taarifa za uwepo wa Biashara ya Madawa ya Kulevya atoe taarifa Jeshi la Polisi.


Mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limeshafanikiwa kuteketeza  Mashamba ya Bangi Ekari 34

Namna Kilimo cha bangi kinavyohudumiwa kwa umakini hapo shamba lenye ukubwa wa Ekari mbili likiwa limeoteswa bangi pekee pasipo kuchanganya zao lolote. Wakulima wa kilimo hiki sasa wamebuni mbinu ya kulima maeneo ya mbali yenye milima na misitu mizito wakiamini si rahisi vyombo vya dola kuyafikia maeneo hayo.