KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, May 31, 2009

ELIMU YA WATU WAZIMA

ADAM MZUZA NINDI SONGEA ELIMU YA WATU WAZIMA

Tanzania ilsha piga hatua katika kupambana na adui ujinga, mwaka 1980 enzi ya utawala wa awamu ya kwanza ya hayati mwalimu julius kambarage Nyerere hatua ya kufuta ujinga ilifikia asilimia 10% tu ya watu wasio jua kusoma na kuandika.

hatua hiyo ilifikia hapo baada ya mwalimu Julius kambarage Nyerere kuomba msaada kwa wafidhi ili kufuta ujinga, mabango mbalimbali ya lieleza swala la kufuta ujinga kwa njia ya kujisomea, madarasa yalifunguliwa saa kumi kamili jioni kwe nye miembe na miti mikubwa ndipo lilipo wekwa darasa..

hali hiyo iliwafanya wale wasio jua kusoma na kuandika kusoma kwa bidii kwa kuwa serekari ili kaza uzi kuhusu swala hilo, katika awamu ya pili ya mzee Rukusa Ally Hasani Mwinyi hali ili anza kulegea na watu kuzama zaidi katika biashara. fasheni ya wakati huo ilikuwa ni watu kubeba begi za fedha swala la kusoma lili pungua,

awamu ya utawala wa tatu wakati wa rais Benjamini Mkapa lili anza swala la MEM na kupewa kipao mbele kuliko swala lolote lile, pia kulikuwa na swala la kuinua uchimi , katika swala la kuinua uchumi pia rais Mkapa aliweza kuomba kufutiwa madeni ya nje na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa,

awamu ya nne ya mh. Jakaya Mrisho kikwete Alikuja na mambo mengi ambayo yalibeba nembo ya maisha bora kwa kila mtanzania shabaha ya nembo hiyo ni kumfanya kila mtanzania awe na elimu ya kutosha. mkulima ajue kimomo ni uti wa mgongo, pia kufanya kazi ni njia peke ya kutokana na umasikini.

katika kupambana na ujinga nchi yetu imerudi sana nyuma kwa upande wa elimu ya watu wazima kati yawatu milioni 6 wanao jua kusoma na kuandi asilimia 31% kwa sasa hawajui kusoma wala kuandika.
swala hilo lilijulikana baada ya kufuka mkurugenzi wa elimu ya watu wazima Salum Ramadhan Majagila kufika katika mkoa wa Ruvuma na kuongea na wandishi wa habari katika eneo la msamala saide vila manispaa ya Songea

mkurugenzi Sulum Ramadhani Majagila amesema serekari itaamua kutumia fedha za ndani ili kuendeleza swala kufuta ujinga, mkurugenzi akiwa songea aliweza kutembelea wilaya ya songea vijijini, na manspaa ya Songea

mkurugenzi majagila amesema juhudi kubwa ina takiwa ifanyike ili kuondokana na wsala zima la kuto kujua kisoma na kuandika.

MWISHO BY mzuzanindi@gmail.com

wenu adamu mzuza nindi

Sunday, May 24, 2009

YALIYO JIRI MKOA WA RUVUMA LEO

NDUGU WA PENZI POPOTE PALE MLIPO,

KWA JINA NAITWA ADAM MZUZA NINDI NINA UMURI WA MIAKA 50 NAISHI WILAYA YA SONGEA INAYO SONGA MBELE AMBAYO IPO KATIKA MKOA WA RUVUMA ,RUVUMA INAYO VUMA

MKOA WA RUVUMA UPO KUSINI MWA TANZANIA , UNA PAKANA NA NCHI ZA MSUMBIJI NA MALAWI. KWA UJUMULA MKOA WA RUVUMA UNA WILAYA NNE,
SONGEA, MBINGA,NAMTUMBO,NA TUNDURU.

WILAYA YA SONGEA INA VIVUTIO VINGI KWANZA KABISA MLIMA MATOGORO NI MLIMA AMBAO VIONGOZI HUTUMIKA KWA KU SIMIKWA WANAPO CHAGULIWA KUWA MACHIFU.

WILAYA YA SONGEA PIA INA HISTORIA KUBWA ,KWA NZA KUHUSIANA NA VITA VYA MAJIMAJI . KATIKA VITA HIVYO WAZEE WALIO UWAWA KATIKA VITA HIVYO WALIZIKWA KATIKA KABURI MMOJA WAZEE WAPATAO 57, INGAWA WAZEE 7 HAWAJULIKANI WALIZIKWA WAPI.

PIA KUNA KABURI LA CHIFU SONGEA AMBAYE ALINYONGWA NA KUZIKWA KIWILIWILI TU NA KICHWA CHAKE KUPELEKWA UJERUMANI.

KATIKA MAMBO YA UTALII WILA YA SONGEA INA MBUGA YA SERUU AMBAYO IKO KILOMETA SABA KUTOKA SONGEA MJINI.

KATIKA MBUGA HIYO KUNA WANYAMA WA MAJINI KAMA VIBOKO MAMBA KATIKA MITO ,NA KATIKA MSITU MIKALI KUNA NYOKA WA AINA MBALIMBALI, SONGEA NI MAKAO MAKUU YA MKOA WA RUVUMA

UKIJA WILAYA YA MBINGA NAYO INA VIVUTIO VINGI ,IKIWEMO ZIWA NYASA AMBALO LINA KINA KIREFU IKIWA NA MAJI NYE RANGI YA SAMAWATI, KATIKA ZIWA HILO AMBALO LINA CHANGIWA NA NCHI MBILI MALAWI NA MSUMBIJI KUNA SAMAKI WA MAPAMBO WAAINA MBALIMBALI,

KANDO KANDO MWA ZIWA NYASA KUME ZUNGUKWA NA MILIMA YA LIVNGSTONE , UKIJA KILOMETA 40 KUTOKA ZIWA NYASA ANA KUTANA NA MLIMA WA MBUJI MLIMA HUU UNA SIFA YA PEKEE KWA WAKAAZI BONDE LA AGATA

MLIMA WA MBUJI UNA MAWE MAWILI AMBAYO YAMEPEWA MAJINA MAWILI, DUMENA JIKE MAWE HAYA YALIKUWA KIELELEZO CHA MAOMBI WAKATI MVUA INAPO KOSEKANA AU MARADHI YA MLIPUKO WAZEE MALUMU WALIKUWA WAKIOMBEA KWA DUA ZA KIMILA,

WAZEE WA JADI WALIKUWA WAKIOMBA KWA KUTUMIA KAFARA YA KONDOO MWEUPE AU MBUZI MWEUPE WA TUMIE TOGWA NI KINYWAJI BAIDI KINACHO TENGENEZWA KWA KUTUMIA ULEZI .

TUENDELEA NA WILAYA MBILI ZA NAMTUMBO NA TUNDURU KATIKA MAKALA YAJAYO.