KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, October 23, 2010

uchaguzi nchini tanzania

Ndugu zangu popote pale mlipo Tanzania inaingia katika uchaguzi mkuu hapo tarehe 31/10/2010 nijambo la kujivunia kuona utawala bora una tekelezwa.

kwa mda wa miaka 49 toka tupate uhuru tume kuwa na amani na utulivu, hakuna anajua kabla la mwenzake au mtu kumtenga mtu kwa ajili ya dini huo ni ushi mkubwa kwa nchi yetu.

S.asa tunaingia katika kutayarisha maisha ya amani na utulivu jambo tunalo lifanya tarehe 31/10/2010 nijambo ambalo tuna weza kununua kifo au kuongeza amani. Ninge omba ndugu zangu kwa kuwa kuchagua mtu mwenye busara kuna tegemea akili zako ziko namuna gani ni mtu wa kufuata mkumbno au ni mtu ambaye una tegemea akili zako?

kama huna jibu ingia ndani ya chumba chako uombe Mungu ili akusaidie, kura yako ni risasi ya mwisho ya kulinda uhai wako kwa miaka mitano inayo kuja.

kura hihiyo ni sumu ya chokochoko ya kupoteza amani na utulivu tulio nao nimategemeo yangu kuwa kila mtu atazingati busara zake kutoa uamuzi Tumwombe Mungu atuongeze busara na utashi ili uchaguzi tutakao uamua uwe wa heri na amani.tuchague Diwani mwadilifu,Mbunge mwadilifu,na Rais mwadilifu vile vile

wenu Adamu Mzuza Nindi SongeaRuvuma Tanzania

Friday, October 15, 2010

Ndugu zangu Wakristo na wale ambao hawana Dini.


Mimi kwa jina naitwa Adamu Mzuza Nindi napenda sana kusoma na kuheshimu mawazo ya kila mtu, jambo la kushangaza ni moja ya machapisho yaliyo tolewa huko Marekani kwa kudai kuwa ifikapo tarehe 11Sepember kanisa lijulikanalo kwa jina la wainjilis wa kikristo kanisa la USA [THE DOVE QUTREACH CENTER] lina jianda kuchoma moto Kurani Tukufu ikitaja kuwa islaam ni dini ya kishetani.

Kwanza hiyo Dini ijue kuwa mtu anapo tumia jina la Kiislam siyo maana kuwa Dini ndiyo iliyo mtuma mtu fanye maovu la ,kila mtu ana wajibika na lile analo tenda. kumbuka Yesu Kristo akiwa msalabani mmoja wawana funzi wake alimkata sikio Myahudi mmoja lakini YesuKristo alisema rudisha hilo sikio ulilo likata Yesu alijua kuwa yule mtu ametenda kwa kushurutishwa na shetani jee hawa wakikristo wange fanyeje .

wailio fanya maangamizi 11september kwa kushambulia balozi za marekaniwalikuwa hawana utu wa kibinadamu.

Wako waungwana katika Uislam na wako waungwana katika ukristo.
Mungu alipo kuwa akiumba ulimwengu alisema na tumfanye mtu kwa mfano wetu [bibilia] kurani inasema wanakuuliza kuhusu roho sema hatukupewa elimu isipo kuwa kidogo , hiyo inaonyesha kuwa mtu huwezi kujua kiundani tabia ya mtu isitumike Dini kwa kufanya maangamizi, jamani kwanza tuna takiwa kulaani kitendo cha kutaka kuchoma moto KURANI kina takiwa kilaaniwe na watu wanao penda amani.

Ni juu ya kila mmoja kulinda heshima za Dini iwe Ukrito au Uislamu. watu walio wengi hupenda kuzima Moto kuliko kutafuta chanzo cha Moto.

ukiangalia idadi ya wakristo ina kadiliwa kuwa bilioni 2 Duniani kote pia nao waislamu wapo idadi ya bilioni bili na kitu. sasa ikifikia hatua ya kuchoma Moto Kurani ni sawa na kutangaza vita kati ya waislamu na wakristo.

Dini ya wakristo iliyoko Marekani ni mmoja ya nchi inayo tawaliwa na kiongozi shupavu Mh.Obama sasa kuendeleza kusikiliza swala la kuchoma vitabu vya mwenyezi Mungu ni kutangaza hali ya hatari miongoni mwa Dini hizi mbili.

nimategemeo yangu kuwa mtu anapo ingia Dini yoyote ile shabaha ya kwanza ni kuleta amani. Naomba wana ulimwengu huu wa Sayansi na Ttecolonojia kuliangalia kiundani jambo hili.

kumwingilia Mwenyezi Mungu nikutaka laana, Adhabu ya ukimwi hatuja maliza, vita kati ya nchi na nchi nayo ina tukabili.
naomba jambo hili tuli angalie na kuchangia mawazo yetu kwa kina wenu mpenda amani Adam Mzuza Nindi kutoka Songea Ruvuma Tanzania

Sunday, October 3, 2010

Walimu wajikomboa mkoani Ruvuma

Jengo la walimu ambalo lilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Mungano Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete na kuwa himiza wafanyakazi webgine wafuate mtindo huo wa kujikomboa kiuchumi.

UKOMBOZI WAMWALIMU UTATOKANA NA MWALIMU MWENYEWE.WALIMU NCHINI TANZANIA WAMEAMUA KUJIKOMBOA KWA KUJENGA MAJENGO YA KITEGA UCHUMI MAJENGO YAPATAYO 21 YAKIWA NA GHARAMA YA SHILINGI 7,350,000,000/= [Picha na Adam Nindi -Songea]

Huyu ndiye bwana Adam Nindi

Ndugu Msomaji wa Mtandao huu YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA kwa Jina na itwa Adamu Mzuza Nindi , kazi yangu ni Mwandishi wa Habari napenda sana Kusoma vitabu mbalimbali kama vya dini,siasa, mambo ya Uchumi pamoja na kuelimisha wanchi kwa njia ya TV, RADIO na Magazeti ukitaka kuwasiliana nami unaweza kutumia E-mail adam_nindi@yahoo.com au tumia simu nomba 0755 731 234, 0658 731 231

MAISHA YA ADAMU MZUZA NINDI

Ndugu zangu ni vizuri kwanza kujua nani una zungumza naye pili ana pendelea nini.
Kwa jina naitwa Adamu Mzuza Nindi, nilizaliwa 7/7/1954 katika kijiji cha Chiulu wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Elimu ya shule ya msingi nilianza nikiwa na miaka 7 katika shule ya msingi Gatoma nchini Zimbabwe ambako wazazi wangu waliamu kwenda kufanya kazi katika machimbo ya Gatoma Mine zimbwabwe,

Nikiwa Zimbwabwe nilisoma hadi darasa la nne wazazi walipo amua kurudi Tanzania ,baada ya kusitahafu .baada ya kufika Tanganyika 1960 kutokana na kuto jua kiswahili nili rudia darasa la kwanza katika shule ya msingi chiulu liyoko Tarafa ya Mbambababay Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma, Nilianza maisha mapya katika kijiji cha Zoole kata ya Chiulu Tarafa mbambabay wilaya ya mbinga mkoa wa Ruvuma.

Nilisoma katika shule ya msingi chiulu baadaye nilihamia shule ya msingi Nyoni Mbinga baada ya kufaulu darasa la nne na kuchukuliwa na dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo alikuwa mwalimu wa shule ya msingi nyoni mbinga kilometa 40 kutoka kijiji cha chiulu .

Nikiwa darasa la tano nilihama tena kwenda kusoma wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa na kujiunga na shule ya msingi Mdete nikiwa dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo aliolewa na na Oddo Matembo ambaye alikuwa ana fanyia idara ya kazi Wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa.

Nikiwa darsa la sita nilihama tena na kwenda kusoma shule ya msingi Wangingombe katika wilaya iringa nilisoma kwa mdu wa miezi sita hatimaye kurudi tena shule ya msingi mdete hadi nilipo maliza shule ya msingi mwaka 1967.

Wakati nikingoja majibu ya mtihani wamatokeo ya darasa la nane dada yangu Alice Nindi aliamua kunipeleka shule ya kulipia mkoani Dodoma ijulikanayo kwa jina la Y.P.Insitute Ovada ambayo ili kuwa iki milikiwa na Father super .

Nilijiunga na Secondary ya Ovada 1968 na kumaliza masomo yangu mwaka 1972 nilijihusisha na maswala ya biasha kwa kufanya biashara kati ya Tanzania ,Malawi.Zambia,Zimbabwe, Msumbiji, Mpaka Africa kusini. Katika biashara zangu kwa asilimia kubwa likuwa na Tembea kwa mguu pale ilipo bidi biashara za Mkononi hatimaye nafaka mbalimbali.

Mwaka 1974 ili jiunga kuandikia gazeti la Watu ambalo lilikuwa likichapishwa Dar –es –Salaam nilifanya kwa mwka mmoja na kujiunga na Gazeti la Sani nako sikudumu nikajiunga na Gazeti la Mwenge la dini linalo chapishwa Peramiho Songea kipindi chote hicho lilikuwa nikijiendeleza na masomo ya uandishi wa habari,

Mwaka 1980 nilichukua masomo ya dini ya kiislamu na kuweza kufaulu vizuri nilianza kufanya mahubiri katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia, na kuweza kufungua misikiti zaidi ya 5

Mwaka 1985 nililijiunga na Televisheni CNN ambayo makao yake yalikuwa Dar –es – Salaam nime fanyia Tv hiyo kwa muda wa miaka 4 na mwaka 1989 lianza kutuma habari Radio Free Africa na badaye kuanzishwa tv ambako niko mpaka sasa. napenda kuwa fahamisha elimu niliyo pitia na vyeti nilivyo pata na ambatisha hapa chini.

Friday, October 1, 2010

Ona Mambo

Ndugu Mtanzania kuna usafiri mwingi kutoka bara hadi Dar - es - salaam ,utokapo Songea ni bora kutumia usafiri Rahisi ambao ni wa Super Fello , Nembo yao ni hiyo kulia kwako


MAKAA YA MAWE RWANDA MBINGA YA UNGUA KWA MOTO

Adam Nindi – Radio Free Afika – Moto Mbinga – 6/05/2006

Wananchi wanaoishi Kijiji cha Mdunduwalo Kata ta Rwanda Tarafa ya Naswea Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wapo hatarini kuteketea kwa Mto kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuuzima Moto huo.

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Mh. Gaudens Kayombo amedai kuwa mlipuko na Moto katika eneo la Mto NYAKAGUNDA umetokana na Makaa ya Mawe ambayo huenda Mlipuko huo umetokana na Gesi au wawindaji haramu ambao huchoma Moto ovyo kwa ajili ya kuwinda wanyama na Mto huo hatimaye Moto kudaka katika makaa ya mawe.

Mh. Gaudens Kayombo amedai kuwa eneo hilo liliwahi kuchimbwa Makaa ya Mawe na Wajerumani Mwaka 1945 na Uchimbaji huo ulikoma Mwaka 1953 Tabaka la Makaa ya Mawe yaliyopo katika eneo hilo, katika vijiji vya Mkapa, Ngaka, Liyombo, Mkulu na Mbuyula inakadiriwa kuwa ni Tani 99.25 Milioni. Tani zinazokisiwa kuungua mpaka sasa ni Tani Milioni 6. Moto huo umeanza kuwaka toka Mwaka 2003 Septemba.

Mh. Gaudens Kayombo amedai Moto huo usipozimwa mapema utaweza kuvuka wilaya jirani ya Makete Iringa na kuunguza Madini ya Mchuchuma ni Kilomita 32 kutoka Mto unapowaka. Pia Vijiji vilivyotajwa hapo juu vinaweza kuteketea. Radio Free Africa na Star Tv imeshuhida kuteketea kwa Makaa

UZIMWAJI WA MOTO ULO KUWA UKITEKETEZA MAKAA YA MAWE RWANDA MBINGA

Serekari ya Jamuhuri ya Mungano baada ya kusikia kilio cha wana mbinga hatari ya kuteketea kwa Moto ili tuma watalamu wake ili waweze kuuzibiti Moto huowatalamu baada ya kufanya utafiti ili baini kuwepo kwa madini ya makaa yamawe zaidi tani 400

Watalamu hao ambao waliongozwa na katibu mkuu wa widhara ya Madini kutoka Taifa alikuja na mwana Jiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Geologia Dr Pascal Semkiwa kwa ajili aya kuangalia jinsi ya kuweza kuuzima moto huo

Watalamu walipanga mbinu ya kuchimba urefu wa mita 10 kwenda chini kuzunguka eneo lote linalo unguza madini ya makaa yam awe
Serekari ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania ilitumia kiasi cha shilingi milioni 59 kuuzima moto huo.

Nini faida ya kuuzima Moto huo jambo lakwanza wananchi wataweza kufaidi Madini yao kwa kufaidika katika nyanda zifuatazo, Elimu,Afya,Michezo, Pamoja na kupata mawazo tofauti na waliyo ya zoea kutoka kwa Wawekezaji wa kutoka nje.

Mwaka ulio fuata mbunge wa jimbo la mbinga mashariki Gaudensia Kayombo alitafuta wawekezaji ambao walitoka .

Mkurugenzi Campuni ya TANCOAL ENERGY Emmanuel Constantinides amesema uchunguzi uliofanywa mwaka 1952 ulibaini kuwepo kwa Madini ya Makaa ya Mawe Tani Milioni 79 Lakini utafiti uliofanywa Mwaka 2001 umebaini kuwepo kwa Madini ya Makaa ya Mawe Tani Milioni 200 – 4000
Campuni ya TANCOAL ENERGY kutoka Dar –es- salaam ikifadhiliwa na campuni ya Atomic Resources ya Asutaria imesema Inaanza malinganisho ya uchimbaji wa mkaa ya Mawe kazi itayo chukua mwaka mmoja

Nao Mtambo wa kufua Umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe ambao uta kuwa na uwezo wa kufua Megawat 400 uta kamilika baada ya miaka 3 kuanzia 2010 – 2013
Mtambo huo wa Umeme utaweza kutoa ajira kwa Watu 400, na uchimbaji wa Mgodi wenye urefu wa mita 300 kwenda chini wa makaa ya mawe utaweza kuajiri watu 400.

Naye mfadhili kutoka Kampuni ya Atomic Resources Limited iliyopo Australia, bwana Cilinton Cain amesema mradi mzima wa kujenga Mtambo wa Umeme wa Makaa ya Mawe utagharimu US Dolla za Kimarekani Bilioni 1.2

Mtaalam wa Geologia Dr Pascal Semkiwa amsema Tanzania itapata faida kubwa kwa kuweza kupata Salpha kwa ajili uengenezaji wa Simenti na Mbolea.Salpha itakayo patikana hapo itakuwa chini ya asilimia 1.

Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki amesema juhudi zilizo fanywa na Serekari kuzima Moto uli kuwa ukiangamiza rasilimali za watanzania kwa kutumia shilingi milini 59 sasa uta kuwa ukombozi kwa taifa kuongeza kipato na uchumi wa Watanzania.