KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, January 30, 2012

DIWANI ALIYE FUNGWA MIAKA 60 AACHIWA HURU

Wilaya ya Tunduru ambayo ilimtuhumu Atingala Mohamed kuhusika na Rushwa na kufungwa miaka 60
Diwani wa viti malumu kupitia tiketi ya CCM Atingala Mohamed katika wilaya ya Tunduru akiwa inje ya Gereza baada ya Rufaa yake kushinda,

Saturday, January 28, 2012

mwandishi wa gazeti la majira ajifungua

Mwandishi wa Habari wa Gazeti la majira akifurahia uja uzitoalio nao, Napenda kuwa fahamisha kupitia blog hii kuwa mwandishi huyu kajifungua mtoto na jina lake anaitwa Fadhila tumupe hongera.
WAKATI MWINGINE UNA WAJIBIKA KUKUBALIANA NA HALI HEBU ONA MWANDISHI WA HABARI MACHACHARI CERENSECIA KAPINGA AKIWA KATIKA PIKIPIKI YA WAGONJWA NI KWELI HIZO PIKIPIPI ZINAWEZA KUMUDU MILIMA YA MBINGA AMBAKO NI NYUMBANI KWA MWANDISHI HUYU

Monday, January 23, 2012

JESHI LA KUJENGA TAIFA WATAKIWA KUJIAJIRI BAADA YA KUHITIMU BADALA YA KUNGOJA AJIRA KUTOKA SERIKALINI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu akiwaasa wahitimu 822 wa Mafunzo ya awali ya Operation Maalum ya Miaka 50 ya Uhuru wa Kikosi cha 842 KJ Mlale kutobweteka kwa kutarajia kupata ajira baada ya kupata Mafunzo ya JKT badala yake wayatumie Mafunzo hayo katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kazi za kujiajiri.

Mkuu wa Kikosi cha 842 KJ Mlale Meja Thomas Mpuku akitoa taarifa ya Jinsi Kikosi cha JKT kinavyojimudu na Mambo ya Uchumi hasa katika Sekta ya Kilimo. Msimu wa 2011/2012 JKT imeweza kulima Ekari 300 za Shamba la Kuzalisha Mbegu za Mahindi.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akikagua Gwaride Maalumu la Vijana wahitimu 822 wa Mafunzo ya awali ya Operation Maalum ya Miaka 50 ya Uhuru.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu katikati akiingia katika Kambi ya Kikosi cha 842 KJ Mlale, Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Meja Thomas Mpuku, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Sabaya.

Bwana Shamba wa Kikosi cha Mlale Luteni Jackson Otaite akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu Mipaka ya shamba la uzalishaji wa Mbegu za Mahindi lenye Ukubwa wa Ekari 300 lijulikanalo jwa jina la Embakasi.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akipokea Maelekezo kutoka kwa Bwana Shamba wa Kikosi cha JKT Mlale jinsi wanavyoweza kuzalisha Mbegu za Mahindi. Bwana Shamba huyo akionyesha tofauti kati ya Mahindi dume na jike.

MAAFALI BEROYA SEKONDARI

Meneja wa shule ya Secondari ya Beroya Sebasitian Waryuba akiwaasa walio hitimu wa kidato cha sita kuwa mara wamalizapo masomo waachane na mambo ya anasa wa mkumbuke mungu mara zote

Afisa Elimu secondari Manspaa ya Songea amewataka wahitimu wa kidato cha sita kuzingatia Masomo baadala ya kujiingiza katika anasa pia kuepuka na mambo ya kisiasa mda huo bado Mwalimu Mkuu wa Secondari ya Beroya Matiko amewapongeza wazazi kwa juhudi wanazo zionyesha katika ushirikiano na Uongozi wa Beroya Secondari


Mwenyekiti wa Bodi Michael Mahecha amesema juhudi katika masomo ndiyo mshahara wa mwanafunzi siku za baadaye, kudharau masomo ni moja ya kuyaweka maisha yako hapo badaye katika matatizo

wahitimu wa kidato cha sita katika sekondari ya Beroya wakisikiliza nasaha mbalimbali za uongozi

wahitimu wakitafakali maisha baada ya kumaliza masomo ya kidato cha sita

Monday, January 16, 2012

MWANA HARAKATI WA MAMBO YA UCHUMI BARANABASI MPOMBO ATUTOKA MKOANI RUVUMA

Mdogo wa Marehemu Baranabasi Mpombo akiongoza uwekaji wa Taji la Maua katika kaburi la Marehemu Baranabasi Mpombo aliye zaliwa Mwaka 1950, na kupata elimu ya msingi wilaya yambinga liuli,hatimaye kuhitimu secondary hatimaye kupata majunzo ya kijeshi,na kuajiriwa na jeshi,amepata mafunzo ya kuandika miradi nchini India, amefariki akiwa katika shirika la SONNGO ,Amefariki kwa ugonjwa wa kisukari

Watoto wa Marehemu Baranabasi Mpombo wakiweka Taji la Mauwa katika kaburi la Baba yao


Umati wawatu walio furika katika katika mazishi ya mwanaharakati Baranabasi Mpombo

JESHI LA POLICE MKOA WA RUVUMA LA PATA TUNZO KWA UTOAJI WA HUDUMA KATIKA ZAHANATI

Kamanda wa POLICE Mkoa waRuvuma Maiko Kamhanda akitoa tarifa kwa wandishi wa Habari kuhusu ushindi ulio pata Jeshi la POLICE Katika utoaji huduma kwa mama na mtoto kuhusu kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.


Hati iliyo tolewa na USAID Shirika la kimarekani ambalo limetoa tunzo kwa jeshi la POLICE Mkoa wa ruvuma baada ya kutoa huduma bora kwa wananchi kuhusu swala la UKIMWI,Baki ya tunzo hiyo USAID Ita jenga Zahanati FFU Kikosi cha kuzuia Ghasia Mkoa wa Ruvuma ambvacho kita kuwa cha kisasa

BIMA WA PATA GARI JIPYA KUBORESHA HUDUMA VIJIJINI

Moses Senje Meneja wa Bima Mkoa wa Ruvuma akichambua Bima zilizo iva kwa wateja wa wilaya 5 za mkoa wa Ruvuma ,Bima Mkoa wa Ruvuma Umesha Toa zaidi ya shilingi milioni 600 kwa wateja wake

Meja wa Bima Mkoa wa Ruvuma akiwa amekaa karibu na Gari ambalo yeye ameliita kuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi wa Vijijini katika kuhakiki bima zilizo iva

Meja Moses Senje akiwa amekaa kwa masikitiko kutokana na wateja ambao huhama bila tarifa , wafanyakazi wa Bima wanapo enda Sehemu hizo hukuta wamesha hama na hiyo huwa hasara kwa shirika

Wateja ambao bima zao zime iva wakipokea hundi zao, Huku mfanyakazi wa Bima akipata mawasiliano juu ya ulipaji wa hundi kwa wateja wake


Mteja baada ya kupokea hundi yake anaihifadhi kwenye begi lake tayari kwa matumizi, kupeleka watoto shule,kununua pembejeo

WANDISHI WA HABARI WAPATA MAFUNZO YA JINSI YA KUANDIKA HABARI ZA MAHAKAMANI

Mwezeshaji wa Kimataifa Juma Tomas anaye tarajia kutoa mafunzo ya jinsi ya kuandika habari za kimahakama kwa waandishi 18 wa mkoa wa Ruvuma

Mwandishi wa Chaneli 10 akiwa katika kuratibu habari kuhusu Wandishi wa Habari kuandika habari za Mahakama ,Aliye simama ni Amoni Mtega akishangaa mada za kuandika habari mahakamani na mnukuru [ kumbe ni Hatari ] Mwisho wa Kunukuru

Mzee wa Zengwe Gidioni Mwakanosya akifikiri Zengwe la Mahakama linavyo weza kumweka Mahali pabaya Mwandishi wa Habari


Katibu wa Waandishi wa Habari Andrew Chatwanga akieleza kuhusu Mshiko ulivyo kuwa Mdogo lakini cha kuzingatia ni Mafunzo ingawa fedha ni ndogo, Pia pamoja na Hilo PRESS Haita sita kutunisha mfuko wake kila mwandishi atakatwa shilingi 12,000/= kwa ajili ya ada PRESS bila Ada haiwezi kwenda alisisitiza Katibu

Sunday, January 15, 2012

NINDAI POVERTY ALLEVIATION ASSOCIATION NA KUZUIA RUSHWA MKOA WA RUVUMA

Naibu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Mussa Msalaba akitoa Mada jinsi Rushwa inavyo weza kuongeza umasikini katika jamii kamaJamii haitakuwa Macho, Mwananchi anaweza kutoa tarifa za rushwa na hataweza kwenda Mahakamani kutoa ushahidi bora tarifa yake iwe ya ukweli.

Washiriki wa semina ya NIPAA kutoka wilaya 5 za Mkoa wa Ruvuma wakiwa wamepiga picha ya pamoja na Mgeni Rasimi Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Mussa Msalaba ikiwa ni moja ya ahadi ya kutokomeza Rushwa Mkoa wa Ruvuma


Mkurugenzi wa NIPAA akimkaribisha Mgeni rasimi kufungua Washa kujadili jinsi ya kupambana na RUSHWA Mkoa wa Ruvuma

Saturday, January 7, 2012

MDAHALO WA MCHAKATO WA KATIBA WILAYA YA MBINGA

Mkuu wa wilaya ya Mbinga Col Mstahafu Edimundi Mjengwa akifungua Mdahalo wa mchakato wa katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania


washiriki wa mdahalo kutoka wilaya mbinga wakijadili kuhusu mchakato wa katiba


Mwanasheria wa Mbinga akitoa mada kuhusu mchakato wa katiba na kuwataka wananchi wa some katiba ili ikifika tume ya kuratibu katiba wawe na chakusema

Friday, January 6, 2012

JUHUDI ZA AKINA MAMA NA MWAKA 2012

Mama huyu kazi yake kubwa ni kuuza Matunda alipo ulizwa kwa nini anapendelea biashara hiyo amesema bei ya Ndizi na Mapapai ina tegemea kupanda kwa Dola na kushuka kwa Dola hivyo biashara ya Ndizi na Papai inalipa. ukiniuliza kuhusu Mahindi nitakuambia kupanda kwa bei ya Mahindi mpaka Mkulima afe toka tume anza kulima hatuja sikia Mahindi ya kipanda, lakini Mafuta kilasiku hupanda na Nishati hiyo Mkulima anategemea

Thursday, January 5, 2012

MWAKA MPY NA JWTZ SONGEA

Mkuu wa Wilaya ya Songea Tomasi Sabaya katika siku ya kukaribisha mwaka mpya amelitaka jeshi la wananchi kuwekeza katika ujenzi ili iwe ni Pesheni ya kudumu katika maisha sitarehe ni gharama pia starehe zina leta umasikini katika kaya

Mkuu wa wilaya Tomasi Sabaya na Meja Passian Chausi wakitoa ishara ya kuukaribisha mwaka Mpya wa 2012 katika viwanja vya luhuwiko songea

Mwandishi wa Habari Adamu Nindi Katika kuukaribisha Mwaka Mpya akisherekea kwa kubanika nyama ya mbuzi

katika kusherekea Mwaka Mpya akina mama wakisakata Pembe la Ngombe katika bwalo la Jeshi la wanchi Luhuwiko


Ishara ya kuukaribisha mwaka mpya ni kufyatua fataki ili kuukaribisha mwaka mpya hapo mkuu wa wilaya akiangalia jinsi mwaka unavyo ingia

Wednesday, January 4, 2012

MAFANIKIO YA WAANDISHI WA HABARI KWA MWAKA 2012


Mafanikio ya binadamu ni kuwa na mahali pakuishi hii iliyopo mbele yako ni Nyumba ya JUMA NYUMAYO hiyo ni changamoto kwa waandishi wote mwaka wa 2012 uwe mwaka wa kila mwandishi kuwa na nyumba au kiwanja

Sunday, January 1, 2012

MWAKA MPYA UMEINGIA JEE SEREKALI MBALIMBALI ZINA ZINGATIA HAKI ZA BINADAMU ?


Jee msomaji wa Blog hii una hisi nini katika picha hii ,wewe jionje ni mmoja katika hao hali utakayo kuwa nayo itakuwaje,huu niulimwengu wa dunia ya tatu au ni jehanamu, picha hii ina tupeleka mbali kama wewe ni mmoja wapo naomba tubadilike na kama wewe siyo mmojawapo tufanye nini ?

WATOTO MKOA WA RUVUMA WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WANAVYO FANYIWA JEE MWAKA 2012 ITAKUWAJE ?


Watoto hawa wanapaza kilio chao kulaani vivetendo wanavyo fanyiwa vya kikali dhidi yao, Jee wazazi walio wazaa watoto hawa watafanyaje ili watoto waelewe kuwa kilio chao kina sikika, Nao wazazi ambao hufanya vitendo vya kikatili kwa kuwabaka watoto kuwa lawiti, kuwa choma moto kwa sababu ya kupoteza shilingi, kuwa uwa watoto kwa sabababu ya mapenzi kati ya wazazi wawili.Mwaka 2012 utakuwajee kwa kizazi hiki ? Ndugu yangu wewe ni mmoja ambaye una weza kuondoa tatizo hili kwa kutoa tarifa kwenye vyombo vya dola unapo ona vitendo vya unyanyasaji vina tendeka hapo uta kuwa ume ingia mwakwa 2012 kwa amani.Mungu wajalie wazazi na watoto wapate amani mwaka 2012