KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, October 30, 2012

jJENGO LA WANDSH WA HABAR LA BOMOLEWA

Na Adam Nindi -Jengo la waandsh wa Habari Mkoa wa Ruvuma Lina tegemewa kuvunjwa fikapo mwezi wa 12 mwaka huu. Meya wa Manspaa ya Songea Chares Mhagama ameya sema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilcho keti tarehe 30/10/2012.

Baada ya kauli hyo ambayo meendeshwa kisiasa Mwenyekiti wawaandshi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Andrew Kuchonjoma amesema utaratibu wa kumwona mkuu wa mkoa wa Ruvuma Sad Thabti Mwambungu unafanyanyika

Monday, October 29, 2012

APIGWA MSHALE NA KUFA PAPO HAPO -SERENGETI

MWANAFUNZI WA SEKONDARI ATUHUMIWA KUUA KWA MSHARE,


Na Anthony Mayunga-Serengeti.

Oktoba 27,2012.

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika sekondari ya Busawe kata ya
Majimoto wilayani Serengeti mkoani Mara Peter Lucas
Wambura(17)anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mshare kifuani
Chacha Damiani Mangali(18) na kufa papo hapo.

Tukio hilo linalodaiwa kutokea oktoba 26,majira ya saa 2 mwaka huu
usiku nyumbani kwa marehemu Mangali limethibitishwa na uongozi wa
kitongoji na polisi linahusishwa na wivu wa kimapenzi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Daud Mgendi aliliambia Mwananchi
Jumapili kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni jilani yake na marehemu
alimpiga mshare kifuani na kufa papo hapo wakati anafungua mlango
atoke nje ya nyumba yake.

“Sababu hazijajulikana kuwa ni vijana waliokuwa wanalingana huenda
wamegongana kwa wanawake ,maana inaonekana marehemu alifungua mlango
akidhani ni mambo ya kawaida ndipo akapigwa mshare kifuani na kupiga
kelele kisha akakata roho”alisema Mwenyekiti.

Alisema mara baada ya kutenda unyama huo mtuhumiwa aligeuka kama
kichaa na kitishia usalama wa wananchi kwa kuwa alikuwa na upinde na
mishare mingi ,na kutokana na giza walishindwa kumdhibiti na kutokomea
kusiko julikana.

“Kumdhibiti ilikuwa vigumu kwa kuwa alionekana kuwa kama kichaa na
kutishia watu kwa kurusha mishare ovyo na kutokana na giza kila mtu
aliamua kuchukua tahadhari kwa kuwa hakuwa katika hali ya
kawaida”alisema.

Baba mzazi wa marehemu Damiani Mangali akiongea na gazeti hili kwa
njia ya simu alisema kuwa kijana wake alikuwa hajaoa na wanahisi
huenda wamegongana kwa wanawake kwa kuwa hakuna madai mengine ambayo
ameyasikia.

“Kama ingekuwa deni tungesikia lakini kwa matatizo ya wanawake mara
nyingi huwa siri zao maana wote walikuwa vijana na majilani,nilipigiwa
simu na kaka yake na marehemu kuhusiana na tukio hilo,tunaendelea
kufuatilia chanzo lakini inauma kifo cha ghafla namna hii bila hata
kuwaeleza sababu”alisema.

Polisi wilayani hapa waanaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na
kumsaka mtuhumiwa ,ambapo wameomba wananchi watoe ushirikiano wa
chanzo na alikojificha kwa kuwa anaweza kusababisha madhara makubwa
zaidi.

Hivi karibuni mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili Mugumu sekondari
wilayani wilayani hapa Mwang’omba Kegocha(16)amefikishwa katika
mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kumchoma kisu Chacha Pasta(29)

Tukio ambalo linadaiwa lilitokea wakati wanacheza kamali ambapo
mtuhumiwa inadaiwa alikuwa ana mdai marehemu ths 5,000 na katikakudaiana wakakorishana ndipo akamchoma kisu ubavuni na kufa papo hapo.

Mwisho.

Tuesday, October 9, 2012

MKURUGENZI WA HOSPITALI YA PERAMIHO DR ANSIGAL STUFE OSB AMETOA MCHANGO WA SHILINGI MILIONI 5 KWA AJILI YA KUANZISHA RADIO YA WAANDISHI WA HABARI WA SONGEA

Mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho  Dr Ansigal Stuffe ameweza kuchangia uanzishaji wa Radio kwa kutoa shilingi milioni tano
 Mratibu wa Afya ya Msingi Tarafa ya Maposeni Abeli Mapunda akitoa Shilingi Milioni 5 alizo pewa na Dr Ansigal Stufee azikabidhi kwa Ruvuma Press Club
 Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrew Kuchonjoma akimpa maelezo Abeli Mpunda jinsi Radio itakavyo toa Huduma kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma
 Abeli Mapunda akiwa Tayari kukabidhi cheki ya shilingi milioni 5 hiyo aliyo ishika mkononi
Picha yas pamoja na Wandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakwanza kulia Mwenyekiti Andrew Kuchonjoma ,ayefuatia Abeli Mapunda Mratibu wa Afya Hosipitali ya Peramiho Mama aliye kaa katikati makamu mwenyekiti wa Ruvuma press Club Letesia Nyoni ,Wamwisho kushoto Katibu wa RPC Andrew Chatwanga walio simama kulia ni Catherini Nyoni,Mosses Konara,Adamu Nindi, na wa mwisho kushoto Joseph Mwambije

WAANDISHI WA HABARI WAPIGA HATUA KIMAENDELEO MKOANI RUVUMA

 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mkoani Ruvuma  Cencesia Kapinga amepiga hatua kwa kuweza kujenga nyumba ya kisasa ilyo katika Manspaa ya Songea . Cha mhimu ni kumunga mkono kumchangia  aweze kumaliza nyumba yake
Hii ni nyumba ambayo Mwandishi wa Habari  Cerencesia Kpinga ameijenga ina hitaji kumalizia ni vizuri mtu anapo piga hatua ni wajibu wawatu wenye mapenzi mema kumchangia

Sunday, October 7, 2012

Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima: MJANE WA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI AKANUSHA KUHUSU H...

MJANE WA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI AKANUSHA KUHUSU HABARI ILIYOANDIKWA KATIKA GAZETI LA HABARI LEO


Mjane wa marehemu mwangosi, Aneth ajibu shutuma za kile yaliyoandikwa Katika gazeti la Habari Leo toleo la Tarehe 05/10/2012 kuna habari inayomnukuu mjane wa Marehemu Mwangosi akimlaumu Dkt. Slaa na CDM kuwa ameshindwa kutimiza ahadi yake ya rambirambi na hata msaada wake wa kusomesha mmoja wa mtoto wa Marehemu Mwangosi.
Akizungumza hayo wakati akihojiwa na chombo kimoja mjini hapa nyumbani kwake asubuhi hii kwa masikitiko makubwa ameshangazwa kuona kile kilichoandikwa katika gazeti la Habari leo na kusema si kweli kwani yale aliyojibu si hayo yaliyoandikwa.
Mjane anaeleza kuwa Dr Slaa hakuahidi rambirambi bali aliahidi kumsomesha mtooto wake wa pili ambaye amemaliza darasa la saba. Ambaye kwa sasa ameanza kupata masomo ya Tuition ambapo msaada huo umetolewa na mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa ambaye ni jirani yake.Mjane wa marehemu ameeleza kuwa kutokana na habari hiyo amekuwa akipata shida sana kwani ndugu zake wamekuwa wakimpigia simu na kumlaumu kutokana na upotoshwaji katika habari hiyo.
Pia amewashukuru wote walioshikiana nae katika msimba wa marehemu mumewe Dadudi Mwangosi na kueleza kuwa ushirikiano ulioneshwa mwanzo wazidi kuonesha.
Mbunge Msigwa akihojiwa ameeeza "kuwa njaa ya siku moja isimfanye mwanahabari yeyote kuvunja maadili na kuandika habari zinazopotosha na kuleta madhara kwa jamii" na kuwataka wanahabari wote kuzingatia maadili yao ya kazi ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii.

NINI UFUMBUZI WA KIFO CHA MAREHEMU DAUDI MWANGOSO

Kuhusu swala la Marehemu Daudi Mwangosi lisilete mtafaruku kwa jamii. Ahadi zilizo tolewa wakati wa Msiba wa Marehemu Mwangosi ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu kama mtu alidanganya hiyo ni nafisi yake nasiyo Matakwa ya wafiwa ni Vizuri kuendesha maombi ya kuitaka Roho ya Marehemu Mwangosi istarehe kwa amani mbinguni.
Kingine ni kuhakikisha UTPC na MCT Waandae mpango wakuweza kuihudumia familiya ya Marehehu mwangosi kielimu na kimaisha, Ikiwa utaandikwa Mradi wenye kuonyesha kusaidia Familia ya Marehemu Daudi Mwangosi hakuna Mfadhili atakaye Kataa, Ifike wakati vyama vya waandishi wa habari vichukue majukumu badala ya kuwa tegemea wana siasa.
Tukikubali misaada ya wanasiasa kila wakati hukoni kununuliwa

By Mkongwe wa Habari Kutoka Songea Mkoani Ruvuma

ALEX NCHIMBI ACHAGULIWA KUONGOZA VIJANA MKOANI RUVUMA

Katika uchaguzi ulio fanyika wa kumchagua mwenyekiti wa vijana Mkoa wa Ruvuma Alex Nchimbi aliibuka kuwa mshindi kwa kupata  kura 392  dhidi ya kura 460 zilizo pigwa ,mjumbe wa mkutano mkuu Taifa alichaguliwa Ziada Ntani  kutoka wilaya ya Namtumbo mkoani ruvuma .
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka vijana kuwa Dira ya watanzani katika kulinda amani na utulivu tulio nao. Amesema chanzo cha machafuko Duniani kote kuna tokana na msingi mzima katika malezi ya vijana ka.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa Vijana ambao uliambatana na uchaguzi mkuu wa kuchagua Mwenyekiti na mwakilishi wa mkutano mku Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma  Said Thabiti Mwambungu amesema msingi mzima wa utulivu na amani umetokana na viongozi walio pita kwa kuwajenga vijana katika maadili mema ya uendeleza utulivu na amani  tulio nao ,Hivyo ametaka vijana kufuata msingi ulio achwa na wasisi wa chama  Tawala CCM ,Nakatika kuchagua viongozi msingi mzima achaguliwe kiongozi aliye bora ambaye ana uchungu na nchi yake  na siyo kuwa na  uchu wa madaraka
 Viongozi wa dini walio hudhuria uchaguzi huo Abudul Omary na Mchungaji Benedict Kazimoto  walimwomba mwenyezi Mungu kuwaondolea chuki kwa wale watakao shindwa na pia kuongeza mapenzi mema kwa viongozi watakao shinda.kwani uongozi hutoka kwa  Mungu
 Nikawaida kwa washiri wa uchaguzi kutafakari kila wakati hapo ndugu huyo akipiga usingizi wakati uchaguzi unaendelea

Katibu wa Vijana Mkoa wa Ruvuma Mwajuma Mohamedi amesma shaba kubwa ya vijana katika kipindi hiki nikuongeza wigo wa kiuchumi na kuibua miradi mbali mbali ili kuwainua vijana kibiaqshara .
Mvatano inje ya ukumbi wa open univerity songea wajumbe wakidai uchaguzi umeambatana na mizengo ,Hao ni baadhi ya wagombea wa kiti cha Uwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Ruvuma

Saturday, October 6, 2012

WALEMAVU WANA HITAJI UPENDO NA USHIRIKISHWAJI WA HALI YA JUU


 Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Songea akitoa mada kuhusu haki za Ndoa huku Rehema Nyagawa kushoto akitafisili kwa alama za Vidole
 Katibu wawa lemavu mkoa wa Ruvuma Asha Abdala akisoma Risala kwa Alama ya Vidole
 washiriki walemavu wakifuatilia kwa makini mada zilizo kuwa zikitolewa na wadau mbalimbali huku mkalimani Rehema Nyagawa akitafisiri kwa alama za vidole
 Washiriki ambao ni walemavu wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasimi Joseph Joseph Mkirikiti aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu
 Picha ya Pamoja na walemavu mkoa wa Ruvuma walio hudhuria semina ya uwajibikaji wa viongozi  katika kutokomeza unyanyasaji kijinsia
Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akiwahiimiza watu mbalimbali kujifunza alama za vidole ili waweze kuwasiliana vizuri na walemavu wasio weza kusikia

: HALI YA UCHOMAJI MOTO MKOA WA RUVUMA INAVYO WAASIL...

 Ukiangalia kwa juu utaona msitu mkubwa ukiwa umeteketea kwa moto SOWASA kila mwaka ina jitahidi kupanda miti ili kulinda vyo vya maji.Hivi sasa kutokana na ukosefu wamaji uchunguzi ulio fanywa na mtandao huu asilimia 25% ya wakaazi wa Manspaa ya songea ndio wanao oga maja moja kwa siku wengine walio baki  75% huji futa maji mwilini na wengine kunawa uso
 Kutona na wananchi kuto Linda vyanzo vya maji pamoja na uchomaji wa moto ovyo wasababisha wananchi wa Manspaa ya Songea kulazimika kupata mgao wa maji,
Katika kikao cha kutathimini majanga ya Moto katika mkoa wa Ruvuma imeonyesha watu walio wengi hawana elimu ya kutunza mazingira na kujua kuwa kazi ya utunzaji mazingira niya serekari

 Pamoja na kibao hiki kueleza kuwa eneo hili halitakiwi kulima wala kuchoma moto lakini watu bado wana haribu mazingira
Mkurugenzi wa Mamulaka ya Maji safi na Maji taka  SOWASA  Francis Kabongo amesema uchoji wa moto katika vynzo vya maji umeweza kuleta  hasara kubwa kwa kuunguza miti ambayo ni rafiki wa maji  ,miti hiyo imepandwa mfululizo miaka mitano ili kuimarisha vyanzo vya maji .swala  hilo limepelekea kushuka uzalishaji wa maji kwa asilimia 50%

Wednesday, October 3, 2012

AIRTEL YA JIKOMBOA KWA KUTUMIA SOLA IRINGA VIJIJINI

 Wananchi wa kata ya Itundu wakiongea kwa nyakati tofauti wameishukuru serekari kwa kuruhusu mitandao mbalimbali kutoa huduma kwa njia ya simu wamesema wao wamefikiwa na  Mtandao wa airtel ambao umerahisisha huduma za kibenk na biashara za mazao mbalimbli
 Mtalamu wa Blog Michuzi akiwa safarini kujionea Airtel inavyo Toa Huduma Kwa wananchi wa Iringa Vijijini.
 Mtandao wa Airtel unapendwa na watu wengi hebu ona Mtoto anavyo Furahia Mtandao
 Mtalamu wa Blog Ndugu Michuzi akiwa juu ya Mnara Itundu kuangalia jinsi ya Sola inavyo fanya kazi kwenye Mtandao wa Airtel Huko Itundu Iringa Vijijini
Mkongwe wa Habari Adamu Nindi akiwa katika kijiji cha Itundu Iringa Vijijini akiwa juu ya Mnara wa Airtel kuangalia matumizi halisi ya Sola katika kijiji hicho
 Mwenyekiti wa kijiji cha kimande kata ya Itunundu Andasoni Mpululu amesma kata ya Itundu ina shugulika zaidi na kilimo cha umwagiliaji wa zao la Mpunga,Hapo awali kupata soko ilikuwa ni ngumu lakini hivi sasa biashara hiyo huenda kwa njia ya mtandao na mnunuzi hulipa kupitia Airtel Money.

SHULE YA SEKONDARI YA BEROYA ILIYOKO SONGEA IMEKAMILIKA KWA KILA KITU,INA SACCOS,MAABARA,PAMOJA NA ZAHANATI

 Mgeni Rasimi Chares Mhagama Meya wa Manspaa ya Songea katika Maafali ya Beroya kwa wahitimu wa kidato cha nne wa nne kutoka kushoto ni meneja wa Sekondari ya Beroya iliyoko manspaa ya songea
 Kikundi cha SACOS ya Beroya Secondary kikiongozwa na Critina Mahenge
 Meya wa Manspaa ya Songea Chares Mhagama akitoa Nasaha katika maafali hayo
 wanafunzi wa kidato cha nne secondary ya Beroya katika manspaa ya songea wakipokea nasaha kutoka kwa wageni waalikwa
 Shule ya Sekondari ya Beroya imekamilika kima abara huyo unaye mwona ni chatu wa mafunzo katika maabara hiyo
 Mgeni Rasimi Meya wa Manspaa ya Songea Chares Mhagama akiangalia Chatu alioko mabara ya Beroya Sekondary. picha ya chini ni ya wahitimu wa kidato cha nne Beroya Sekondary

TTCL KUNA NINI HADI TUNA KOSA HUDUMA SISI WANYONGE ?


BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MAWASILIANO NA UCHUKUZI KUHUSU KUDORORA KWA TTCL .

Kwa mara nyingine tena najitokeza kuweza kutoa kero ambazo zina tupata Sisi Wananchi tunao tumia huduma za TTCL

Katika Mabadiliko ambayo Serikali ina himiza Wananchi katika kuingia katika Soko la Afrika Mashariki na ya Kati ni kujiendeleza kielimu lakini kuhizwa huko hakuko kwa TTCL wao bado na mfumo wa kizamani, Kwenye Umeme angalao serekari ime gundua kitu fulani kwa nini shirika hili naslo lisi chunguzwe kujua kama kuna masilahi ya watu au kukwama kwao kuna tokana na Elimu au ni watu wana kwamisha :?.

Watanzania tulio kuwepo katika Utawala wa Mwalimu Nyerere tuna usemi wa kusema usiache Mbachao kwa Msala upitao.

Methali hii inatubana kuitelekeza TTCL. katika Mitandao ambayo inaweza kumsaidia Mwananchi asiye na kipato ni TTCL lakini Shirika limekuwa na kiburi hata kama wateja wakilalamika Shirika la TTCL halisikii malalamiko ya wananchi .

Katika kutumia huduma za Internet .wateja wanalazimika kulipa kwenye mtandao wa TTCL Shilingi 30,000 kwa Mwezi au 7000 kwa Bando na hata Shilingi 500 ili waweze kupata huduma.

Cha kushangaza baada ya kulipa kwenye mtandao wa TTCL ili upate huduma unakuwa kama vile umepoteza fedha zako unaweza kuwa na kazi yhati inawezekana ika shindika kutuma yenye MB25 ukianza asubuhi ukiwa na bahati ita enda saa kumi jioni kama huna bahati ndiyo basi

Kama Una Attach file MB 25 unaweza kujanza Attachment Saa 2 Asubuhi ukafanikisha saa 9:00 Alasiri au ikakata.
Ukiingia kwen ye Mtandao mwingine Attachment hiyohiyo unachukua dakika 2 – mpaka dakika 5
Jee TTCL ina Wataalamu waliobobea ni vipi ishindwe kuweka Mazingira mazuri kwa wateja wao.

Wafanya kazi wa TTCL ambao hawakutaka Majina yao yatajwe wamedai wameweza kutoa Taarifa ya Malalamiko ya Wananchi hakuna kiongozi wa juu anaye tilia maanani malalamiko hayo.
Chamsingi kinachoonekana kwa TTCL badala ya kuboresha huduma wao wanawaza kuuza mali za TTCL kama walivyo fanya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ,

Mimi ni Mteja wa TTCL toka ilipo anza Namba yangu ya Simu 0252602425, Naishi Songea.
Ningeomba wa Tanzania kwa Wananchi wanategemea sana Mtandao wa TTCL, endapo hali ikiendelea namna hii basi Wale wote wanao ihujumu TTCL Serekari inge weza kuwa ajibisha. Haiwezekani Mitandao mingine ifanye kazi lakini mtandao wa Serekari Ushindwe kufanya kazi
By Adam Mzuza Nindi.-Songea

Tuesday, October 2, 2012

KUKAA KIMYA KWA WANDISHI WA HABARI KWA SABABISHA ONGEZEKO LA UHALIFU

 Hii ni ajali iliyotokea kilometa 30 kutoka Iringa Mjini wakati Magari matatu yalipogongana na kusababisha Gari la Supper Feo linalotoka Iringa kwenda Songea kubonyea kwa nyuma, ndani ya Basi hilo kulikuwepo na Mkongwe wa habari Adam Nindi ambaye alikuwa Iringa kikazi.
 Moja ya maboresho ni Serikali pale inapotoa elimu kwa waendesha pikipiki na Magari ili kupunguza Ajali za Barabarani, katika picha hii Mkuu wa Mkoa wa ruvuma Mh Said Thabit Mwambungu aliweza kutoa vyeti kwa waendesha pikipiki wapatao 240 katika uwanja wa Majimaji baada ya kuhitimu Mafunzo ya kuendesha pikipiki kwa usalama kupitia Chuo chs mafunzo ya Ufundi VETA Mkoa wa Ruvuma
 Ili kupunguza ajali pikipiki zote zinazoingia barabarani zinatakiwa kukaguliwa kuhakikisha ziko salama na haziwezi kusababisha ajali zikiwa barabarani
 Madereva wanatakiwa kuwa waangalifu na kuweza kuzifahamu alama za usalama Barabarani, Dereva asipofuata kanuni za Usalama Barabarani matokeo yake ni kusababisha ajali. Hebu angalia Barabara ilivyo alama zote zinaonekana ili kumsaidia dereva apite vizuri.
 Ufikapo katika Mji wa Iringa ili uwe na Uhakika wa usalama wako kwa kuepuka kuibiwa au kuuweka mwili wako katika afya nzuri ni bora kufikia NICK MOTEL ambapo pana ulinzi wa uhakika na chakula kizuri. Picha ya hapo juu ni Mkongwe wa habari Adam Nindi akipata kifungua kinywa kulia kwake ni Mkurugenzi wa Hoteli ya NICK MOTEL.
 Mtandao ambao unawasaidia Watanzania kwa kupunguza maumivu ya gharama za mawasiliano ni Air tel hapo watu mbalimbali wakichukua fedha zao kupitia Air tel Money
Kwa kipindi kifupi kilichopita Waandishi wa Habari walisusia kuandika habari za kipolisi, utafiti uliofanywa na Blog hii umebaini kuwa kwa asilimia kubwa wahalifu wamefurahi kuona makosa wanayoyafanya hayaripotiwi pamoja na hayo hata ajali za barabarani zimekuwa zikiongezeka na wananchi kukosa huduma muhimu ya kujua kinachoendelea na kusababisha watu ambao wanapenda uvunjifu wa amani kujiweka katika kivuli cha kuunga mkono Mgomo wa Waandishi wa Habari huku wakijua ni moja ya kumkosesha mwananchi haki ya msingi ya kikatiba ya kupata habari.

Pamoja na hayo Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma walipata joto la jiwe baada ya wao kuibiwa Vifaa vyao na vibaka na hatimaye Jeshi la polisi kuwasaidia kuwapata wahalifu ambao wamefikishwa kwenye chombo cha Dola ambachi ni mahakama lakini kwa aibu habari hiyo haijaandikwa popote pale, Je hii imekula kwa wanahabari au kwa Polisi? ni vizuri vyombo vinavyohusika kuangalia kwa makini suala lililosababisha mgomo wa Waandishi wa Habari. Pichani juu Jeshi la Polisi linaonyesha likiendelea kutoa huduma kwa wananchi.

WAANDISHI WA HABARI WAMETAKIWA KUJIEPUSHA NA HABARI ZENYE KULETA UCHOCHEZI

 WAaandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma walioshiriki Semina ya Maadili iliyofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Songea. Anayesoma gazeti ni Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Bw Andrew Chatwanga.
 Waandishi wa Rvuma Press Club wakifuatilia kwa Makini mafunzo ya Maasemina ya Maadili iliyofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Songea Manispaa.
 Mwezeshaji wa Mafunzo Maadili Rose Ngunangwa Mwalongo akiwa na Mwenyekiti wa Semina ya Maadili Thoma Lipukaliyofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Songea.
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja baada kushiriki semina ya maadili, mwenye suti nyeusi na blauzi ya pundamilia kulia ni Wambura Wasira mwezeshaji kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT)
Wandishi wa Habari wametakiwa kuandika habari kwa kuzingatia kanuni sheria na kufuata maadili bila kuandika habari ambayo ina weza kusababisha uvunjifu wa Amani.
Hayo yamebainika katika semina iliyo andaliwa na MCT Baraza la Habari Tanzania kuhusu kujenga uwezo wa Waandishi wahabari katika kuandika habari bila kuleta uchochezi kwa wananchi