KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, May 31, 2012

KIKWETE ANA KOSA GANI JAMANI ?













MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE ANA SITAHILI SIFA ZA KUMWAGA -

Adamu Nindi -Songea "

Has Good Sense of Humour"

Watanzania wenzangu, Mara nyingi na msikiliza mheshimiwa, Rais Jakaya Kikwete akiwa hewani!Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!
Hebu tuone alivyo kuwa akitoa Elimu ya kilimo kijijini kwake
Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!Angalizo:Watanzania Wenzangu , tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kuponda tuu, mara moja moja tupongeze yale mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

Sasa ndugu zangu napenda kuwa fahamisha kuwa mwenye macho haambiwi ona mambo alliyo yafanya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni ya kuigwa na ya kujivunia hakuna Rais ambaye mwenye uwezo wakufanya hayo zaidi ya Rais Gadafi ambaye wananchi wake walimsaliti.

Hebu sasa niainishe yale ambayo hata wewe una weza kuya ona na kuweza kuniunga mkono1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha. 2. Dar –es – salaam tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu. 3.Vyombo vya Usafiri kama Magari yameaanza kutumia Gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55% 4. Kujenga Kivuko na daraja kigamboni. 5.

Ujenzi wa Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma 6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5. 7Ujenzi wa Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

8. Ujenzi wa Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza9. Ujenzi wa Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

10.Ujenzi wa Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.eg Mkoa wa Mbeya

11.Kuweza furusa kwa wawekezaji kusambaza gesi kutoka Songas.pamoja na Kurekebisha mkataba wa Songas, uliokuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini. 12.Kuongeza huduma zaq nishati kwa kutoa Mkataba kwa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

13.Ujenzi wa Barabara Dodoma, Manyara lami. 14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

17.Kuongeza Mradi wa kilimo kwa kutumia njia ya Umwagiliaji maji karibu hekari 20,000 zimejengwa na lengo la Serekari ni kufikia Ekari milioni moja.18. Kilimo kwanza mashamba darasa ya meongezeka na mavuno kuwa makubwa mfano mzuri ni kutoka Mkoa wa Ruvuma lengo lili kuwa kuzalisha kilo milioni 300,000 lakini lengo lilivuka hadi kufikia kilo milioni 400 ,000 mavuno kwa ekari.

19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma ,Lwanda Mkoani Ruvuma makaa ambayo yana uwezo wa kutoa MG 400 za Umeme na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400 na Kuweza kuajiri watu 400 na kupunguza tatizo la Ajira.

23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

26. Ujenzi wa barabara za kisasa nane Dar hadi chalin27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

28. Uboreshaji maabara shule za kata ($ 90Milion

29. Idadi ya walimu kwa ajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom Dodoma uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco Iringa elf 2.5, MkwawaIringa elfu 2.5 Tumaini Iringa elfu 2, Open University elfu 20 nk.

32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele Term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.
36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%. Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000. Jee mpaka hapo huoni hakuna lawama kwa Rais wa Jamhuhuri ya Mungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete

KAMANDA MPYA MKOANI RUVUMA AONGEA NA WANDISHI WA HABARI

Kamanda Mpya Mkoa wa Ruvuma awasili na kukaribishwa na Kamanda Michaeli Kamhanda kamama unavyo ona katika picha kulia ni kamanda Deusdedit Kaizilege Nsimeki na aliye kulia ni kamanda Michael Kamhanda wakiwa makao makuu ya Police Songea

Mwandishi wa Star Tv Adamu Mzuza Nindi akiwa amepiga picha ya Pamoja na Kamanda anaye Hamia Iringa Kamanda Maiko Kamhanda

Kamanda Mpya kushoto Deusdedit Kaizelege Nsimeki akiwa na aliye kuwa kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma kulia Maiko Kamhanda walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari kuhusu swala la kuzua uhalifu na kuweka mahusiano mema na Wandishi wahabari

wandishi wa habari wakipiga picha ya pamoja na makamanda wa mkoa wa Iringa na Ruvuma katika makao makuu ya Police Mkoa wa Ruvuma.Picha hii ni kuonyesha mahusiano mema yaliyo kuwepo kati ya waandishi wahabari na Jeshi la police Jee kwa Kamanda huyu Mpya Mahusiano yata kuwaje aliko toka alikuwa RCO Jee baada ya kuingia nafasi hii mpya hali itakuwaje mkoani hapa ,Jee juhudi zake zitaweza kumpita mwalimu wake Kamhanda au atakuwa chini ya yeye majibu tuta yaona katika utendaji wa kazi za kila siku,Waandishi tumpe moyo, tumpe nguvu,tushirikiane ,Mungu wabaliki waandishi Mungu libariki Jeshi la Police

Kamanda wa Police Mpya wa Mkoa wa Ruvuma Desidedit Kaizilege Nsimeki akiwa amepiga picha ya pamoja na Mwandishi wa Star Tv Adamu Mzuza Nindi

Tuesday, May 29, 2012

AMINI USIAMINI MAMA HUYU ANA MIAKA 18 KATIKA KAZI MSHAHARA SHILINGI 30,000/=


Mama huyo hapo juu Eliza Mgohamwende ni mfanyakazi wa Halimashauri ya Mbinga kwa mda wa miaka 19 mpaka sasa. Lakini cha ajabu mama huyu ana fanya kazi kuanzia saa 1.30 asubuhi mpaka saa 12.00 jioni hana Jumamosi wala Jumapili au siku za sikuku lakini mshahara ni shilingi 30,000/= jee huo ni uajibikaji kwa wananchi .Viongozi wa Mbinga Mna semaje kuhusu hilo ?

SHETANI GANI AMEINGIA KATIKA KARINE HII ?

Dakitari wa hospilata ya Mkoa Ruvuma akikagua Maiti ya Mtoto mdogo ambaye mama yake mzazi anatuhumiwa kumnyonga kwa kumvunja shingo

Mama mzazi wa Mtoto aliye nyongwa Mtotot wake kwa kumuvunjwa shingo akiwa chumba cha kuhifadhia maiti wakati mtoto akifanyiwa uchunguzi

Dakitari Mchirika akitoa maelezo kwa insipekita Anna Tembo jinsi mtoto huyo alivyo uwawa


Masikini mtoto mdogo mwenye umuri wa miaka mitatu akiwa amelala chumba cha kuhifadhia maiti baada ya mama yake mzazi akishirikiana na hawara yake ambao wana tuhumiwa kumua mtoto huyo ili asiwabuguzi wawapo kitandani. na baada ya mauaji hayo waliahidi kuoana.Ndugu msomaji wa Blog hii hebu angalia watu walivyo hawana huruma akina mama,akina baba, wazee wetu utamaduni wa Mwafirika Mmeuweka wapi ?

Monday, May 28, 2012

MIDAHALO YA WAFUMBUA MACHO WANANCHI DODOMA

Omana Gouth na Noel Stephen Mpwapwa

Imeelezwa kuwa katika utendaji wa kazi wa Mahakama za Jamahuri waMuungano wa Tanzania haziko huru kama inavyo ainishwa katika Katiba yaJamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa na wajumbe wa mdahalo wa katiba uliofanyikakatika Ukumbi wa ccm Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma ulioendeshwa naMtandao wa Asasi za Kiraia NGOMNET Mpwapwa.Akichanngia mada katika mdahalo huo mmoja wa washiriki Bwana JEMSIKAREIMAHA hakimu mfawidhi wa mahakama wa wilaya ya Mpwapwa alisemakatika utendaji wa kazi katika mihimili mitatu ya dola ambayo ni Serikali,Bunge na Mahakama kunaonekana kuwa serikali inakuwa namadaraka makubwa kuzidi mihimili mingine katika utendaji kazi wake kutokana na muhimili mmoja kuutegemea muhimili wa mahakama kwakuwezeshwa kifedha na vitendea kazi.

Aidha Bwana Kareimaha alidai kuwa katika utendaji wa kazi wa kutoamaamuzi ya kimahakama Rais anaweza kutengua hukumu iliyo iliyotolewana hakimu au jaji kwa madaraka aliyokuwa nayo kikatiba kitu alichosema kinaleta utata wa kiutendaji.

Pia akiongezea mchangiaji mwingine bwana Kandido Mnemele mwakilishiwa kundi la walemavu wilayani mpwapwa (shivyawapwa) alisema kuwa katiba hiyo bado haifahamiki kwa wananchi wa vijijini na wala hawaijuyi rangi yake, na imeandikwa bila kuzingatia uhitaji wa makundi maluumkama walemavu wa macho,

kwa kuandika katiba ya maandishi ya nukta nundu.Bi ELLY MAKALA afisa wa Tasisi wa kuzuia na kupamabana na rushwanchini PCCB alisema kuwa watanzania bila kubadilisha mtazamo wa kuwana maadili na kufuata kanuni na sheria za kazi katiba mpya haiwezi kuwa jawabu la matatizo ya watanzania bila ya viongozi kuwawaadilifu.“Hata tusemeje na tutunge sheria nyingi kiasi gani hatuwezi kutatauamatatizo ya watanzania bila kubadilisha mtazamo wa viongozi kuwawaadilifu,

jawabu la matatizo ya watanzani yamo mikononi mwao wenyewe kwa kujenga moyo wa kushiriki,kupanga na kufuatilia mipango ya kimaendeleo na kuwawajibisha viongozi wabadhilifu’’ Alisema bimakala.Akitoa mada katika mdahalo huo mmoja wa wawezeshaji Daktari Sinda HUSSEN SINDA kutoka chuo kikuu cha Dodoma alisema kuwa TANZANIAhaina Dira na dhima juu ya mstakabali wa Taifa juu ya siasa ujamaa nakujitegemea kuwa wanachi hawajui wanafuata siasa ya mlengo wa namnagani,kibepari,kibwenyenye,ua siasa ya ujamaa na kujitegemea.

Pia walisema kuwa katika katiba itakayo andikwa iweze kumuangali na kumjali mkulima ya hali ya chini juu umilikaji wa ardhi na sera yauwekezaji ijieleze wazi kwa wakulima wa chini ili kupunguza migogoroya wakulima wawekezaji, na wafugaji.

Mratibu wa mtandao wa mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali wa wilaya ya mpwapwa bwana Noel Stephen alisema kuwa mdahalo huo una lengo lakuongeza uelewa kwa wananchi juu ya katiba kabla ya mchakato wautoaji wa maoni kwenye tume utakapo karibia.

Na alisema kuwa mradi huu umetekelezwa kutokana na ufadhili kutoka The Foundation for civil society juu kuongeza mahusiano wa wananchi na Wabunge wao majimboni.

Sunday, May 27, 2012

SAKATA LA UMEME LIKOJE JEE UNASOMA MITANDAO MBALIMBALI

Rais Jakaya Mrisho KikweteHebel Chidawali, Dodoma na Fidelis ButaheRAIS Jakaya Kikwete jana alitumia maadhimisho ya miaka 34 ya CCM kuvunja ukimya na kuzungumzia sakata la malipo kwa Kampuni ya kufua umeme ya Dowans kiasi cha Sh94 bilioni akisema amaunga mkoTanesco isilipe deni la Dowans."..Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka Tanesco ilipe..," alisema Rais Kikwete akizungumzia sakata hilo.Kauli hiyo ya Rais Kikwete kuhusu Dowans ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitoa maoni mbalimbali,huku baadhi yao wakienda mahakamani kupinga kampuni hiyo isilipwe.Akihutubia wananchi katika kilele cha Sikukuu ya kuzaliwa kwa CCM, ambazo kitaifa zilifanyika mkoani Dodoma jana Kikwete alisema ameamua kusema wazi baada ya kupata shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali waliosema kuwa amekuwa kimya juu ya Dowans.“Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika. Nawalinda. Kwa sababu hiyo, nikaona nami nisema angalau watu wanisikie, lakini sina la ziada ni yale yale yaliyokwishasemwa. “Msemo wa wahenga wa akutukanae hakuchagulii tusi hapa umetimia. Napenda kuwahakikishia wana-CCM na wananchi wenzangu kuwa, sina uhusiano wowote wa kimaslahi, kwa namna yoyote ile na kampuni ya Dowans,” alisema Kikwete.Rais Kikwete alisema hakutaka kuzungumza kuhusu Dowans kwa kuwa tayari lilikuwa limeshatolewa ufafanuzi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati .“Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha Wabunge wa CCM,” alisema Rais Kikwete. Alisema kuwa taarifa ya kutaka Tanesco iilipe Dowans Sh94 bilioni imeshtua wengi na kwamba yeye baada ya kupata taarifa hiyo aliuliza na kupewa ushauri mbalimbali.“ Wapo waliosema lazima tulipe, wapo waliosema tusilipe, wapo waliosema tusiharakishe kulipa kwani kuna uwezekano wa kutokulipa kwa kutumia sheria,” alisema na kuongeza“ Uamuzi wangu ukawa tusiharakishe kulipa, tutafute njia za kuepuka katika kulipa. Ndiyo maana ya taarifa ya Chiligati na ile ya Waziri Mkuu,” alisema Kikwete.Alisema kuwa ni mzigo mkubwa kwa Tanesco kuilipa Dowans, hivyo ifanyike kila njia ili kuepuka kulipa deni hilo.“ Tumewataka wanasheria wetu wasaidiane na wale wa Tanesco kuhakikisha hilo halitokei. Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka Tanesco ilipe," alisema na kusisitiza:"Kauli za mimi kuhusika na Dowans inanishangaza, maana nisingeamua hivyo katika Kamati Kuu(CC) na Kamati ya Wabunge wa CCM. Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi”alisema Kikwete."Alisema kutokana na ukimya wake maneno mengi yalisemwa ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na kampuni hiyo Dowans na kufafanua kwamba jambo jingine lililomfanya kuzungumza kuhusu Dowans ni kauli kwamba hawezi kuzungumza kwa kuwa kampuni hiyo inahusishwa na marafiki zake.“ Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale, Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika. Maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu na Kamati ya Chama ya Wabunge wa CCM yalifanywa chini ya uogozi wangu,”alisema Kikwete.Kuhusu suala la Katiba, Rais Kikwete alisema siyo sera ya wapinzani bali ni mali ya CCM ambayo tangu mtangulizi wake Benjamini Mkapa alishaianzisha, hivyo akasema na yeye ni muumini mzuri wa kutaka mabadiliko.Alisema kuwa atawaambia wasaidizi wake waharakishe kupeleka muswada bungeni ili uweze kujadiliwa na wabunge ambao wataona ni namna gani mchakato huo utakavyotekelezwa ili kupata katiba mpya.Kuhusu matatizo ndani ya CCM, alisema bila ya chama hicho kufanya mageuzi makubwa katika kubadili muundo na uongozi, kitakufa kifo cha mende.Kikwete pia aliwaeleza mamia ya watu waliohudhuria kilele cha sherehe hizo za miaka 34 ya CCM, kuwa chama hicho kimeishiwa fedha na kwamba yako maeneo yanayosababishwa na viongozi wasiokuwa wabunifu. Mwoshoni mwa mwaka jana gazeti hili liliwahi kuchapisha kichwa cha habari kuwa CCM hoi kifedha baada ya kupata habari kutoka ndani yua chama hicho.Alisema katika mabadiliko makubwa yanayotarajia kuja ndani ya chama hicho kikongwe nchini, yataanza mara moja mwishoni mwa mwezi ujao wakati Kamati Kuu itakapokutana kupokea tathmini ya uchaguzi.Akitumia maneno ya ukali Kikwete alisema: “Mabadiliko hayo yanatakiwa kuanza mara moja bila kuchelewa kwani ukongwe wa chama chetu pamoja na baadhi ya viongozi wanaweza kuwa ni mzigo unaokisumbua chama”.Mwenyekiti huyo alisema mabadiliko hayo yanatakiwa kuendana sambambana matakwa ya watu wakiwemo kundi kubwa la vijana, ili wasije kiona chama hicho kuwa ni mzigo usiobebeka.“Lazima chama kianze mchakato wa mageuzi kwani kuwepo kwa muda mrefu ndio hatari ya chama chetu, lakini pia tabia za baadhi ya viongozi zinaweza kuwa ni sehemu nyingine ya hatari hiyo hivyo. Nasema lazima chama kiwe kama nyoka anayeweza kujivua magamba yake na kuwa mpya wakati wote hilo litajadiliwa katika vikao vya kamati na utekelezaji wake utaanza mara moja ili kuongeza mvuto ndani ya chama chetu”.Alisema chama kinatakiwa kukimbia kutokana na hali halisi ya namna walivyoiona katika mchakato wa uchaguzi ulipita hivyo wale ambao wanakwenda mwendo wa kinyonga lazima watabwagwa kuanzia Machi mwaka, huku akisisitiza kuwa mvuto huo uwapendezeshe vijana.Kuhusu suala la mapato, alisema kwa sehemu kubwa CCM imeacha kusimamia vyanzo vyake na badala yake imekuwa ikitegemea zaidi fedha za ruzuku ambazo mara baada ya kupungua kwa viti bungeni, sasa ruzuku hiyo inaishia kulipa mishahara ya wafanya kazi tu.Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alisema hata kwa miujiza hawezi kutimiza matakwa ya Watanzania wote katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 10.Alitolea mfano kuwa hata hayati Mwalimu julius Nyerere alishindwa kumaliza mambo yote ingawa alikaa kwa muda mrefu Ikulu kuliko marais wengine, hali kadharika pamoja na watangulizi wake akiwemo Benjamini Mkapa pamoja na Ali Hassan Mwinyi.“Watanzania wasitegemee kuwa nitafanya mageuzi makubwa hata Mungu mwenyewe hakumaliza kuiumba dunia kwa siku moja, lakini pia hata Mwalimu aliyekaa muda mrefu hakumaliza matatizo ya Watanzania kwa kipindi chake”.Kwa upande wa wananchi wa Dodoma ambao walimpa Kikwete zaidi ya asilimia 81 ya kura za urais , alisema mji huo utaboreshwa pamoja na kufikiria kuipanua Ikulu ya Chamwino iliyo nje kidogo ya mji, ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba ya rais.

JEE KUJIHUDHURU KWA JOHN MAGUFULI NI KWELI ?

Magufuli ana siri nzito:WIZARA YATOA TAMKO LA KUKANA KUJIUZULU KWAKE
SASA ni dhahiri kuwa Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, ana siri nzito kuhusiana na madai kwamba ameandika barua kwa Rais Jakaya Kikwete, akikusudia kujiuzulu.Katika hali iliyotafsiriwa kuwa waziri huyo anaepuka kutoa mwenyewe msimamo wa kujifunga moja kwa moja kuhusu kuwa na nia ya kujiuzulu au kutojiuzulu, jana Katibu wa Wizara yake, Herbert Mrango, ndiye aliyejitokeza kukanusha taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti zilizohusu kujiuzulu kwake.Mrango akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, alisema habari zilizoandikwa na baadhi ya magazeti: “Magufuli Ajiuzulu” au “Magufuli Azushiwa Kujiuzulu” si za kweli, huku akikataa katakata kuulizwa swali lolote kuhusu undani wa taarifa hizo zinazomhusu mkuu wake.“Mheshimiwa waziri anaendelea na kazi zake vizuri, alikuwepo ofisini jana na leo yupo; na anaendelea na programu zake za kazi kama kawaida.“Tunawaomba muwahakikishie wananchi kwamba Waziri Magufuli hajajiuzulu, hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu ya kujiuzulu,” alisema Mrango.Hata waandishi walipong’ang’ania kumuuliza maswali, Mrango aliwataka wamtafute siku nyingine za kukutana kwa ajili ya maswali bali siku hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kutoa taarifa fupi.“Hiyo ndiyo taarifa fupi nimemaliza sihitaji maswali kwa kuwa sina majibu na kama mnataka kuuliza maswali naomba mnitafute siku nyingine tukutane kwa ajili ya hiyo, asanteni,” alisema Mrango na kunyanyuka huku akitoka nje ya ukumbi huo.Taarifa zinadai kuwa katika majumuisho ya ziara ya Waziri Mkuu Pinda baada ya kauli hiyo mkoani Kagera , Magufuli alilazimika kueleza kuwa amefikia hatua ya kuamua kuchukua maamuzi magumu baada ya kubaini kuwa hataweza kutekeleza vema utawala wa sheria ambao umeonekana kupindishwa.Chanzo kimoja kilicho karibu na waziri huyo kililidokeza gazeti hili kuwa alifikia uamuzi wa kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kusikitishwa na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ya kusitisha zoezi la bomoa bomoa lililokwishaanza katika baadhi ya maeneo nchini.“Ni kweli baada ya kutolewa kauli ile kule mkoani Kagera katika kikao chetu cha majumuisho ya ziara hiyo Magufuli alisikitishwa na kauli ile ambapo aliweka bayana kuchukua maamuzi magumu hatua ambayo haikukubaliwa na viongozi waliokuwa katika ziara hiyo,” kilisema chanzo hicho.Taarifa za kujiuzulu kwa Waziri Magufuli zimeonekana kuwashtua baadhi ya viongozi kutokana na baadhi ya watendaji kujaribu kupeleleza wananchi wamepokeaje juu ya kuzagaa kwa taarifa hizo.Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa ni kweli Magufuli alifikia uamuzi huo hata baada ya kushauriwa na viongozi mkoani humo na kuamua kuandika notisi ikiwa ni njia ya kutaka kumtikisa Waziri Pinda ambayo hajaikabidhi kwa wahusika.Chanzo Tanzania Daima

BINTI NDEMBO NA WACHAWI KATIKA HIMAYA YAKE

Mganga mashuhuri Flola Ndimbo watiba za kienyeji ambaye ana weza kutibu homa kwa njia ya kisayansi pia anaweza kutibu kwa njia za kijadi makao yake makuu yapo Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kambi ya Tiba yake kwa Uchache ina watu sichini ya mia nne [400]


Mganga wa Jadi Flola Ndembo akiwa na Katibu wa wachawi katika eneo la matimila Songea Vijijini kulia kwake akiwa amekuja kujisalimisha baada ya ya kuwa mchawi kwa muda wa miaka 30 na kukabidhi vifaa vyake vilivyo kuwa vikitumika kwa ajili ya kuwangia

Saturday, May 26, 2012

MDAHALO KATIKA WILAYA YA MBINGI KUHUSU UAJIBIKAJI WA VIONGOZI KWA WANANCHI

Mwalishi wawalemavu akitoa hoja juu ya viongozi wasivyo fanya uadilifu kwa walemavu 1,Hakuna vielelezo vinavyo wafanya wao watumie barabara bila kuhatarisha maisha yao kwa kuwa uono wao ni hafifu, 2, walemavu wamiguu wana kosa viatu kutokana na bei ya viatu kuwa juu .Jee serekari haiwezi kutoa Ruzuku kwa viatu vya walemavu.




Mbunge Gaudence Kayombo akijibu hoja kuhusu matumizi ya mfuko wa jimbo ,amesema mfuko huo una wajumbe 7 hiyo uko kisheria hakuna fedha ambayo ina weza kutumika bila wajumbe kufahamu.Ameahidi kuitisha mkutano ambao uta husisha viongozi wa serekari pamoja na wananchi ili kujibu hoja zilizo tolewa kwenye Mdahalo


Mwakilishi kutoka The Foundation Ciliv Societry akitoa maelekezo kuhusiana na kujaza dodoso



Mwana sheria Komba akiwakilisha mada kuhusu mindo mbinu ya Barabara ,kuwa barabara zetu hazikamiliki kila mwaka zina kuwa mbaya kwa nini tusifuate mfano wa Mwanza wa kujenga barabara kutumia mawe, mawe tunayo kipi kinacho zuia alihoji ?


Mbunge wa Jimbo la Mashariki Mh. Gaudence Kayombo aliye Kulia akisikiliza kwa makini uwakilisho wawananchi kuhusu kero zao kwa Serekari


Mwakilishi wa Radio Maria Jofrey Nilahi akito Live Mdahalo wa Uajibikaji wa Viongozi kwa wananchi na jinsi wananchi wanavyo takiwa kuajibika kwa viongozi wao, watu wasio pungua 3,000,000 waliweza kupata ujumbe kupitia Radio Maria


Washiriki wa Mdahalo wa Uajibikaji viongozi kwa wananchi waliendelea kushangaa pale walipo ambiwa kuwa Tenda za wilaya hiyo hutolewa bila kushirikisha mawazo ya wananchi, wamedai utendaji watenda zinazo tolewa wilayani hapo hazi zingatii utalamu bali zina zingatia zaidi kujuana.


Wananchi walio hudhulia katika mdahalo wa uajibikaji walishangaa kusikia mfanyakazi wa Halimashauri ya Mbinga kusikia katika miaka 19 aliyo fanyia halimashauri hiyo bado ana pata mshahara wa shilingi 30,000/= huku wilaya ya mbinga ikidai kuongoza katika mapato.


washiki katika mdahalo wa uajibikaji wa viongozi wa katika wilaya ya mbinga walihoji vipi katika mdahalo kama huo ulio kusanya watu zaidi ya 250 ukose wawakilishi kutoka serekarini jee huo ndio mshikamano wa viongozi wa serekari na Wananchi ?


Mwanasheria Komba akieleza wajubu wa wabunge na madiwani na pia kuwa fahamisha kuhusu mfuko wa bunge unavyo fanya kazi kila mhula mfuko wa mbunge hutengewa shilingi milini 43 lakini kazi ya mfuko huo haufamiki fedha hizo zina tumika namna gani


Wananchi wanavyo sikiliza hoja juu ya uajibikaji wa viongozi wao viongozi kuanzia watendaji hadi mkurugenzi wapo njia moja katika kuwa puuza hawashirikishwi katika maswala ya maendeleo



Mdahalo ulio fanyika katika wilaya ya Mbinga kuhusu Uajibikaji wa Viongozi kwa wananchi na wananchi wanavyo weza kuajibika kwa viongozi wao ,lakini hilo limeonyesha utengano ulivyo kati ya viongozi na wananchi Viongozi katika kuamua maamuzi ya utekelezaji wa mambo ya maendeleo hawawashirikishi wananchi

Wednesday, May 23, 2012

JEE AGIZO LA MLALE LILIKUWA NA MAANA AU LILIWASAIDIA WANANCHI MKOA WA RUVUMA

Hiyo ni ngao iliyo mkomboa Mwananchi wa Mkoa wa Ruvuma kitabu Hicho kiliitwa Agizo la Mlale ndicho kilicho kuwa mwongozo wa kumpeleka mwananchi wa Mkoa wa Ruvuma Apate Maendeleo .Jee Mwenzangu umewahi Kuona kitabu cha Agizo la Mlale /

Katika kumkomba mwananchi wa Mkoa wa Ruvuma kulikuwa na Ratiba ya Agizo la Mlale kukiwa na Ratiba ya kazi kama ilivyo hapo juu jee vitabu vilivyo Mkomboa mkulima wa Ruvuma mbona havipatikani kwenye Makitaba

FOUNDATION YA TEMBELEA MASHIRIKA

Viongozi wa RUNECISO Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Ujumbe kutoka Foundation kutathimini miradi mbalimbali iliyo tekelezwa

Mwendesha Baiskeli Mashuhuri kutoka Lindi ameingia Mkoani Ruvuma Kwa kuandaa michezo ya mbio za Baikeli katika serehe za kuzindua kituo cha Good hope

Saidi Kengele kutoka Lindi akiwa na Baisikeli aliyo itumia kwa safari hadi kufika mkoani Ruvuma

Mgeni kutoka The Foundation Emanuel Kazungu akiwa Ofisi za Star TV akibadilishana mawazo na mwandishi wa Star Tv kushoto ni Katibu Mhutasi wa SONNGO Sofia Ngalimanayo

Uongozi wa RUNECISO ukiwa na Mgeni kutoka The Foundation Emanuel Kazungu wakiwa mtaa wa Zanzibaa



kutoka kulia ni Fransis Mlimilaanaye fuatia Adamu Nindi aliye vaa blauzi nyeupe ni Judith Lugoye anaye fuata Asha Abdala anefuata ni Mwenyekiti wa RUNECISO Michael Mahecha,aliye vaa suti nyeupe ni Insipekita Anna Tembo walipili kutoka kushoto ni Mgeni kutoka The Foundation Emanuel Mzungu mwisho Mwenyekiti wawalemavu mkoa wa Ruvuma

Tuesday, May 22, 2012

SIKU YA VIPIMO DUNIANI



Adam Nindi Songea

Mawakala wa Vipimo Mkoani Ruvuma kwa Mwaka 2011 – 2012 wameweza kukagua Mizani 9473 na kubaini Mizani 162 zikiwa na ubora na kuzitoza faini ya Shilingi 33 . 603 ,00/=

Hayo yamebainika katika kuadhimisha siku ya Vipimo duniani Sherehe ambayo huadhimishwa kila Mwezi mei kila Mwaka mkoani Ruvuma iliambatana na utengenezaji wa mizani katika hosipitari bure.

Meneja wa wawakala wa Vipimo Mkoni Ruvuma Herold Mneney ameyasema hayo wakati alipokuwa katika Ukaguzi wa Mizani Mbovu katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambapo Mizani 5 zilibainika kuwa mbovu na kuweza kutengenezwa.

Meneja wa vipimo amesema wafanya biashara wana njia mbali mbali ya kuwaiba wateja wao kwenye mizani kwa ndani hasa wauzaji wa nyama huweka mfupa ambao umewekwa kwa gundi ili kuongeza uzito, wakati mwingine huweka sumaku ili iende haraka yote ikiwa ni lengo la kumwiba mteja wananchi wawe macho na wizi unao tumiwa na wafanya biashara wakiona hilo watoe tarifa kwa wakala wavipimo songea,

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Philis Nyimbi amesema pamoja na kuadhimisha Siku ya Vipimo duniani kuna umuhimu kila Mwananchi kujua uzito wake ili anapopewa dawa ilingane na uzito wake dawa ikiwa pungufu ni madhara na ikiwa nyingi huweza kuleta madhara mwilini.

Nao Wananchi wakiongozwa na Daria Kapinga wamesema wanapata faida kubwa pale wanapojua uzito wao pia inasaidia kujua Maendeleo ya Mtoto anapokuwa Tumboni.

Mkoa wa Ruvuma unapokuwa na upungufu wa Wafanyakazi Mkoa mzima una Wafanya kazi 6 tu. Pia changamoto inayowakabili watu wa Vipimo ni Ukosefu wa Vifaa vya Vipimo vya kisasa upimaji wa Mionzi pia hata vipimo vya kupimia ongezeko la makelele havipo.

Monday, May 21, 2012

SIKU YA VIPIMO DUNIANI YA FANYIKA KWA KUTENGENEZA MIZANI HOSPITALI YA MKOA RUVUMA

Watalamu wakala wa vipimo mkoa wa Ruvuma wakiwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakifanya kazi ya kutengeneza mizani katika kuadhimisha siku ya Vipimo Duniani
Mganga msaidizi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dr Philips Moris Nyimbi akito changamoto zinazo weza kuwa kabili watu wasio fuata kanuni za kupima uzito hasara ni kupata dawa ambayo haiwezi kuponya
Meneja wakala wa vipimo Mkoa wa Ruvuma Harold Mneney akitoa Maelekezo ya jinsi ya kuzitumia mizani zilizopo Hospitali ya Mkoa amesema nilazima kila mara kuzifanyia usafi kuzik ili zisiweze kuharibika haraka aliye simama ni Dr Philips Moris Nyimbi
Ujumbe wa watalamu mawakala wa Vipimo wakiwa katika ofisi ya Mganga Mfawidhi Hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakiwa katika siku ya Vipimo Duniani ambayo Huadhimishwa kila siku ya tarehe 20/05/kila mwaka
Watalamu ambao ni mawakala wa vipimo mkoani Ruvuma wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wa Kitengeneza mizani zilizo haribika .MizaniTano zilibainika kuwa na ubovu mawakala wa vipimo mkoa wa Ruvuma waliweza kuzitengeneza na sasa zina fanya kazi vizuri .
Katika wodi ya Wajawazito imebainika mizani zao zikiwa na kasoro kwa bahati mzuri mizani hizo ziliweza kutengenezwa
Meneja wakala wa Vipimo Mizani Mkoa wa Ruvuma akibainisha kazi zilizo fanywa na watalamu wake Zaidi ya mizani 9473 zilikaguliwa watu 162 walibainika na makosa na kutozwa faini ya shilingi 33,603,000/= meja wakala wa vipimo ameagiza wananchi kutoa tarifa wanapo ona mizani mbovu au kuzitilia wasiwasi watoe tarifa mara moja .

Sunday, May 20, 2012

MDAHALO KATIKA ZIWA NYASA WA FANA

Ndugu msomaji wa mtandao huu umesikia kuwa hivi sasa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kaanzisha wilaya mpya ya Nyasa sasa ufikapo wilaya hiyo chakula kikuu ni ugali wa Mhogo na Samaki kama unavyo ona hapo juu samaki alioko juu ya ugali anaitwa Mbufu
Nijambo la kihisitoria kuanzishwa kwa ziwa nyasa shirika lisilo kuwa la kiserekari la RUNECISO limekuwa la kwanza kuendesha mdahalo wa uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi pamoja na wananchi ushiriki wao katika kazi za maendeo
Nakukumbusha tu huo niugali wa Mhogo hebu angalia jinsi ulivyo songwa kiufundi ukiwa kwenye sahani niyo njia moja wapo ya kufanya safari na kuja kuona ugali wa mhogo unavyo songwa
Mwandishi Mwandamizi wa Habari Juma Nyumayo akiwa tayari kuonja ugali wa Mhogo akiwa Mbambabay mwambao wa ziwa nyasa
Makamu Mwenyekiti wa wilaya ya Mbinga Prisca Haule akitoa mada kuhusu kuinua uchumi wa wilaya mpya ya nyasa kwani wilaya hiyo katika mapato ya Halimashauri huchangia asilimia 10%
Afisa Mtendaji wa kata ya Matalawe wilayani mbinga akiwa safarini kuhimiza wananchi wa kata hiyo katika kuzingatia kanuni za afya baada ya ugawaji mablanketi yaliyo tolewa na Idarara ya maji katika kuwa kumbuka watu walio asilika na UKIMWI
washiri 250 walio shiriki mdahalo wawazi kuhusu uajibikaji wa viongozi wa Serekari kwa wananchi ulio fanyika katika wilaya mpya ya nyasa
Afisa kutoka Maendeleo ya Jamii wilaya mpya ya Nyasa Ndugu Njau akitoa mada kuhusu maendeleo yanavyo takiwa kuletwa katika wilaya mpya ya Nyasa na kuwa taka wananchi wawilaya hiyo kuachana na uvivu
Washiki waliohudhulia katika mdahalo wawazi katika wilaya mpya ya Nyasa wapatao 250 wakisikiliza kwa makini mada zilizo kuwa zikitolewa
Picha ya pamoja iliyo pigwa kandokando mwa ziwa nyasa kwa washiriki wa mdaho wawazi wa uajibikaji ulio fanya wilaya mpya ya nyasa ulio shilikisha vikundi vyote walemavu,masirika ya dini, na asasi zilizopo wilaya ya Nyasa
Washiriki wa Mdahalo walio hudhuria wilayani Nyasa ulio fadhiliwa na The Foundation Civil Socity
Moja ya washiriki wakiwa wamepiga picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mdahalo wilayani nyasa
moja ya washiriki katika mdahalo ulio endeshwa na RUNECISO Wilaya Nyasa wakiwa wana punga upepo mororo wa ziwa nyasa
mwandishi mwandamizi Juma Nyumayo akiwa katika ziwa nyasa akiroposha samaki tayari kwa kitoweo
Mwandishi mkongwe Adamu Nindi akiwa katika kutafuta kitoweo cha samaki katika ziwa nyasa hiyo ikiwa moja ya utalii katika ziwa nyasa
Mratibu wa SONNGO Mathew Ngalimanayo akiwa katika bandari ya mbambabay ikiwa ni moja ya njia ya kutalii katika bandari ya mbambabay
Juma Nyumayo na mbembe za kutalii katika Ziwa Nyasa hapo yupo Bandarini Mbambabay
Katibu hutasi wa Ruvuma Press Club Judith Lugoye akiwa katika utalii katika bandari ya mbambabay
Kikao cha maandalizi cha kuanda mdahalo wawazi katika wilaya mpya ya Nyasa hao mbele yako niviongozi wa RUNECISO Wakwanza ni Makamu Mwenyekiti Adam Nindi wapili ni Mwenyekiti Michael Mahecha