KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, February 27, 2013

MKOA WA RUVUMA WAWAKUMBUKA MASHUJAA WALIO KUFA KWA KUNYONGWA WAKATI WA VITA VYA MAJIMAJI MWAKA 1906

Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Tanzania Balozi Hamis Kagasheki ameweza kuongoza Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji walionyonga tar 27/02/1906 na Wajerumani ambapo Mashujaa 61 walizikwa katika Kaburi moja.
  1. Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hukumbuka Mateso waliyoyapata Babu zao, Hapo wapo katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea kushuhudia Maombolezo yaliyoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki. 
Uwanja wa Mashujaa Mahenge umezungukwa na picha za Mashujaa wa Vita vya Majimaji hiyo ni picha ya shujaa Chifu Songea Mbano
Hapo Mh. Balozi Hamis Kagasheki akiongoza Maandamano yaliyoanzia Sehemu waliyonyongwa hadi katika Uwanja wa Mashujaa

  1. Katika Maombolezo yaliyofanywa Viwanja vya Mashujaa Mahenge Mgeni Rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki aliweza kuweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa Mashujaa wa Vita vya Majimaji, hapo anaonekana akiweka Ngao.
  1. Waziri wa Maliasili Balozi Hamis Kagasheki akienda kuweka Ngao na Mkuki katika Mnara wa Mahujaa Mahenge.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu akiweka kinjenje
 Mkuu wa mkoa akirudi jukwaani baada ya kuweka silaha ya jadi aina ya kinjenje
 Bregedia akiwa katika mnara wa Mashujaa Mahenge akiweka Upinde na Mshale
  1.  Chifu wa Wangoni Mbano akiwakilisha Wangoni kwa kuweka Kinjenje na Rungu (Kibonga)  katika Mnara wa Mashujaa
  1. Katika kuwakumbuka Mashujaa waliotangulia mbele za Haki Jeshi la Wananchi limeweka Utaratibu Maalumu ikiwa ni pamoja na kulipua mizinga na Fataki katika kuwakenzi Mashujaa.
 Hapo wanajeshi wakiendelea kutoasalamuza maombelezikwa njia ya kijeshi
 Hiyo yote ninjia ya kuwakumbuka Mashujaa walio  Tangulia
 Ukiwa umepitia mafunzo ya kijeshi  utajua uchungu wanao upata waombolezaji hawa
 Nimoja ya kuomboleza kuinamisha kichwa chini ni dalili ya kumwomba mwenyezi Mungu awaweke Mahali pema Mashujaa  walioo tangulia Mbele zahaki


 Jeshi  unatakiwa kungangamala ,hebu ona jinsi mashujaa wanavyo omboleza katika kuwa kumbuka Mashujaa waliotangulia
 Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wakiwa katika viwanja vya mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea
Jeshi la Wananchi wa Tanzania likitoka nje ya Uwanja wa Mashujaa baada ya
             kumaliza taratibu zote za Maombolezo kwa kuwakumbuka Mashujaa 61
             walionyongwa na kuzikwa katika kaburi moja

 Mwalimu Kaisi Ally kutoka dhehebu la Ahamadiya Mkoa wa Ruvuma akiwaombea mashujaa walio Tangulia wakati wa maombolezo  katika uwanja wa mashujaa manispaa ya songea
Mkuu wa Wilaya ya Rudewa Juma Madaha akiwa mmoja wa waombolezaji wa
           Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji.
Wanajeshi wakilipua Mizinga kuashiria kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji.

Friday, February 22, 2013

KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU CHA KAMATWA LIZABONI SONGEA

KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU CHA KAMATWA LIZABONI

Katika Tanzania tuna kabiliwa na Vita vya aina mbalimbali kiuchumi, kiafya, pamoja na vita ya kulinda utulivu na amani tuliyo nayo.

Wapo wanao tegemea kufanikiwa katika biashara kwa kutumia viungo vya Watu wengine, kutaka viungo vya Albino na Kadhalika

Kwa mujibu wa Tarifa zilizo tolewa na RPC Mkoa wa Ruvuma  Desdedit Nsimike zina sema ,juu ya kukamatwa kijana Denes Fransis Kafinje  akiwa na kiganja cha Mkono wa Mtu nini maana ya Vitendo hivyo

Kwa hapa Ruvuma ni tofauti Kijana unayemwona hapo chini Denes  Francis Kafinje Mkazi wa Lizaboni anatuhumiwa kwa kupatikana na Kiganja cha Binadamu, akiwa ameweka ndani ya Box kwa umahiri mkubwa

Cha kujiuliza Kiganja hicho alimkata nani hakuna mtu aliyeripotiwa kukatwa Kiganja Mkoani hapa

Ndugu zangu mambo haya ni ya kutisha lakini tutafanikiwa ikiwa tutatoa taarifa kwa kuyaripoti matukio kama haya.
 Ona jinsi watu walivyo wakatili huo ni mkono wa Mtu ulio katwa angalia jinsi ulivyo katwa kwa makini tuta fikakweli
 Mtuhumiwa aliye kamatwa na kiganja  cha Binadamu Denes Fransis Kafinje akihojiwa na Jeshila Police Mkoani Ruvuma
Kiganja cha mkono  wa binadamu  hakijulikani nani alikatwa ni juu ya Watanzania kuwa fichua hawa wahalifu

Wednesday, February 20, 2013

BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJIWANANCHI KIUCHUMI LA DHAMINI VYAMA VYA USHIRIKA NA KUWEZA KUKOPESHWA SHILINGI BILIONI 8 .5

Washiriki wa Semina ya Ujasiliamali katika Kijiji cha Mapipili Kata ya Kitumbalomo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wakisikiliza mada za ujasilia mali zilizo tolewa na Baraza laTaifa la uwezeshajiWananchikiuchumi

Afisa Mwandamizi wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Raymond Justine Ritte akiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbinga . Wa kwanza kulia ni Oswald Yohana Karadisi Afisa Mwandamizi Ujengaji uwezo na uendelezaji Biashara kwa wajasiliamali na aliye katikati ni Dada Sarah Lupembe

Afisa Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Raymond Justine  Ritte akiwa katika Ofisi ya Ushirika Wilaya ya Mbinga
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga akiwa na Afisa Ushirika Wilaya ya Mbinga akitambulisha ugeni kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi
 Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh Kahindi akiwa na Afisa Mwandamizi wa ujengaji uwezona uendelezaji wa biashara kwa wajasilia mali Oswald Yohana Karadisi akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Nyasa

Washiriki wa Semina ya Ujasiliamali wapatao 100 kutoka kijiji cha mapipili wakisikiliza Mada ya Jinsi ya kufanya Biashara na Kanuni zake

Washiriki wa Semina ya Ujasiliamali katika Ukumbi wa Mapipili kata ya Kitumbalomo wilayani mbinga wakisikiliza kwa Makini Mada ya Ujasiliamali

Washiriki wa Semina ya Ujasiliamali katika Kijiji cha Mapipili Kata ya Kitumbalomo Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Washiriki wa Semina ya Ujasiliamali wapatao 100 wakisikiliza Mada ya Jinsi ya kufanya Biashara na Kanuni zake
Kijiji cha Mpipili Kata ya Kitumbalomo Wilaya ya Mbinga kilometa 25 kutoka Mbinga Mjini kinavyoonekana kikiwa kimezungukwa na Milima mikali

Kijiji cha Mpipili Kata ya Kitumbalomo Wilaya ya Mbinga kilometa 25 kutoka Mbinga Mjini kinavyoonekana kikiwa kimezungukwa na Milima mikali.

 Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpipili Esau Esau akiwa nje ya Ukumbi wa Semina.

Friday, February 8, 2013

MILA NA DESTURI ZA MWAFRIKA KWA NINI HAZI FUATWI VILIVYO


 GOGO LA MAAJABU AMBALO VIONGOZI MBALIMBALI WALIKAA JUUYA GOGO HILO WALIFANIKIWA    KATIKA MAPAMBANO YA VITA VYA UKOMBOZI

Ndugu Msomaji wa Blog ya Songea Habari.blogspot.com. Napenda kukukaribisha ili uweze kuona Kitu kinachoitwa Imani kina maana gani.

Jambo la Msingi napenda kukurudisha katika Mila na Desturi ambazo zilikuwa zikiwafaa Wabantu. Ukumbuke kuwa Mila na Desturi za wenzetu hawa watu weupe au Wazungu ndio waliotuteka katika mila zao, huyu tunayemwita Mungu ambaye yupo katika Biblia na katika Kurani Tukufu .

Lakini hiyo haifanyi kuwa sisi Wabantu tulikuwa hatuna Mungu wetu. Hebu rudisha Mawazo yako nyuma, Jee hawa watu weupe tunaowaita Wazungu walikuwa wakijua lugha zetu la, 

Sasa hebu uone mimi Mungu wangu kwa Lugha yangu Mungu nilikuwa namwita Chapanga, wengine Nguluwi, Mulungu, Mnungu, Mluku .  hayo yote ni majina ya kibantu  yaliyo kuwa ya kitumika kumwita Mungu  hii ni kuthibitisha kuwa Waafrika walikuwa na Dini zao za Asili.

Kitu ambacho nataka kukuambia. katika kudai Uhuru Nchi mbalimbali za Africa zilikuwa na mila ya kutambika ili kupata Mafanikio, katika kuomba Mvua , kushinda Vita au Jambo lolote ambaloni Gumu.

Sasa hebu tuone Mfano mdogo katika Nchiya Msumbiji wakati wa Vita vya Frelimo na Wareno, Mkutano wa pili wa Vita hivyo ulifanyika Macheja mpakani na Tarafa ya Mhukuru Nchini Tanzania ,kitu cha ajabu wa kuu wote waliokuwa wakipigania Uhuru walikuwa hawa kai kwenye viti bali wali Tumia Gogo kubwa kukalia wakiwa na imani na gogo hilo kwa kupata ushindi .

Sasa tuingie Nchini Msumbiji tuone wenzetu walivyokuwa na Imani na gogo kubwa ambalo linasadikiwa Viongozi wote wa Afrika wameweza kukaa juu ya gogo hilo na kila aliyekaa hapo alifanikiwa kupata Ushindi.

Ziangalie kwa makini hizo picha hizo uone viongozi walivyokuwa wazalendo kwa kuipenda Nchi yao na mila zao.
 Mke wa Marehemu Moses Machel wakati wa mapambano wa vita vya msumbiji picha hiyo ili pigwa macheje Nchini Mozambiki
 Marehemu Samora Machel akipanga mashambulizi dhidi ya Wreno Nchini Mozambiq wakati ule
 Marehemu Candido Mondlane akiwa uwanja wa mipango ya vita Macheje Nchini Mozambiq
 Njia ya mapambano dhidi ya warenoili tegemea zaidi mto Ruvuma kwa uvushaji wa Silaha
 viongozi wandamizi wa Mozambiq aliye vaa kofia Samora Machel na wa mwisho ni Rais wa sasa wa msumbiji Armando Emillo Guebuza wakiwa wamekaka katitka Gogo la ukombozi
 Marehemu Samora Machel akitoa maagizo kwa ArmandoEmillo Geubuza wakiwa wamekalia gogo la ukombozi

Wednesday, February 6, 2013

MAFANIKIO YA IDARA YA UHAMIAJI MKOANIRUVUMA

Add caption

Afisa UhamiajiMkoa wa Ruvuma Koku Lwebandiza  akielezajinsi Idara ya Uhamiaji ilivyo fanikiwakatikanyanda mbalimbaliikiwemo mawasilianoya uhakika,Gari,Compyuta,Nyumba za wafanyakaziofisi za kisasa.ushirikianokati ya idara ya uhamiajina wananchi.
Add caption

Jengo la utawala laUhamiaji ambalo lime jengwa eneola Mahehenge manspaa ya Songea ilikiwa lina kadidiwa kugharimu zaidiya shilingimilioni700
Add caption

Ofisi ya uhamiajililioko mpakani mwa Msumbijina Tanzania eneola Mkenda tarafa ya Mhukuru wilaya ya Songea Vijijini.
Add caption
Jopo la Maafisa Uhamiaji wakiwa katika kikaocha kuboresha utendaji wa kazi mpani mwa Msumbiji na Tanzania
Jopo la Maafisa Uhamiaji wakiwa katika kikao cha kuboresha utendaji wa kazi mpanimwa Msumbiji na Tanzania

Nyumba za watumishiwa idara ya Uhamiaji zilizo jengwa mpani mwa Msumbijina Tanzania Eneola Mkenda.

Nyumba za watumishiwa idara ya Uhamiaji zilizo jengwa mpani mwa Msumbijina Tanzania Eneola Mkenda.

 Afisa uhamiaji Mkoa wa Ruvuma akiwa na Jopo la wafanyakazi  Wenzie wakitokea nchini Msumbiji katikauimarisha ujirani mwema kati ya Msumbijina Tanzania.
Add caption

 Afisa uhamiaji  Mkoa wa Ruvuma akiwa na Jopo la wafanyakazi wenzie wakitokea nchini Msumbiji katikauimarisha ujirani mwema kati ya msumbijina Tanzania.

Gari lililotelekezwa na wahamiajiharamu na kushikiliwa na uhamiajiMkoa wa Ruvuma.

Kudhibiti uhamiaji haramu kunatakiwa ushirikiano na wananchi hebu ona msitu huu ulivyo kuwa mkubwa ni rahisi wahamiajiharamu kuvuka kama hakuna ushirikiano.