KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, May 31, 2013

NIVIZURI KUCHUKUA SHERIA MKONONI PALE MTU ANAPO KOSEA ?

 Katika kuadhimisha siku ya unywaji wa maziwa dosari lazima itokee jee hii ni halali kuchukua sheria mkononi wakati tukijua hawa ni wasomi waelimishaji. kosa la kijana nikuchukua maziwa bila idhini lakini alicho ambua ni kipigo hebu ona.
 Bado kijana akiendelea kupata kipigo mpaka anasema heli nisinge shiriki  wiki hii ya unywaji maziwa Mkoani Ruvuma.kipindi chote akipata kipigo hakuna Mgambo wala Asikarini juu ya kamati za ulinzi kulinda hali kama hizo ili sherehe isipate dosari
 Masikini kijana pamoja na kutoka nje ya banda mafisa wa banda hilo linalo onekana waliamua kuchukua mazoezi ya masumbwi sijui wana jitayarisha na pambano gani
 Pole kijana hata ladha ya maziwa kwako imekuwa chungu lakini nilazimavijana wajifunze rahisi ni gh;ali Vya bure mara zote huwavina adhabu yake,huwezi kujua aliye pewa kusimamia banda hilo kwao ana malezi gani
Banda limependeza lakiniusijaribu kugusa kitu utakiona chamoto ,
 Angalia aliye shika bomba anavyo jitayarisha kuweza kuongeza kipigo kwa kijana kweli hawa ni mabondia, lakini turudi nyuma kwa maafisa kama hawa kuchukua sheria mkononi kwao ni halali au vyeo vina wafanya wawe juu ya sheria ?
KIJANA POLE HAYO NDIYO MALEZI YA BAADHI YA VIONGOZI WASIO FUATA UTAWALA WA SHERIA

TGNP NINI KIFANYWE NA MABLOGER WA RUVUMA ILI WA SHIRIKI WASHA ZENU ?

 Mkongwe wa Habari Mkoa wa Ruvuma  Adamu Mzuza Nindi  adammzuza@yahoo.com, mzuzanindi@gmail.com  akipandisha picha mbalimbali zenye kuleta mwamko wa kuweza kuondoa mfumo dume pamoja na kuleta maendeleo kwa mama na mtoto. Jee TNGP Tufanye nini ili mjue Songea kuna Bloger
 Afisa Uhusiano kutoka TGNP Liliani Liundi akiwa katika kazi malumu ya kuweza kuinua vipaji vya Mwanamke katika Tamasha Malimbali, Jee Tufanyeje ili TGNP ijue kuwa Ruvuma kuna Bloger
 Mtoto Selina Fussi aliye weza kusaidiwa na Mh.Steven Wasira ambaye Moyo ume Toboka na kupata Ufadhili wa Kwenda kutibiwa India, Jee kazi hiyo haitambuliki na TGNP
Afisa Uhusiano wa TGNP  Liliani Liundi akiwa na Naibu waziriri wa widhara ya Maendeleo ya Jamii jinsia na wato Ummy Mwalimu katika sherehe fupi ya kutambua vipaji vya waandishi wa habari.jee hiyo siyo kazi ya Bloger Adamu Mzuza Nindiwa Ruvuma, Tafadhali kwa kuwasiliana nasi tumia adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZIWA 2013 KITAIFA KUFANYIKA MKOANI RUVUMA

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akizindua wiki ya Unywaji wa Maziwa kwa kuonyesha Mfano wa kunywa Maziwa ikiwa ni njia moja wapo ya kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujenga Mazoea ya kutumia kinywaji cha Maziwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akikagua Mabanda ya Maonyesho ya Bidhaa mbalimbali za Maziwa katika sherehe za Uzinduzi wa Wiki ya Maziwa ambazo Kitaifa zimefanyika Mkoani Ruvuma. Kulia ni Dr Ruth Rioba Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Taifa.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu akipokea Maelekezo ya Matumizi ya Bidhaa zinazotengenezwa kwa Maziwa alipokuwa akikagua Bidhaa zilizoletwa na wazalishaji na wasindikaji wa Maziwa
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu (aliyeshika maiki) akitoa nasaha kuhamasisha Unywaji wa Maziwa wa mazoea kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma badala ya kusubiri mpaka kuugua ili kuboresha Afya zao. Hayo ameyasema katika Viwanja vya Manispaa ya Songea wakati wa Maadhimisha ya Uzinduzi wa Wiki ya Maziwa  Kitaifa Mkoani Ruvuma, amesema Mkoa wa Ruvuma una Ng`ombe 371,000 kati yao wa Maziwa ni 12,032 tu ambao huzalisha lita 96,256 kwa mwaka.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu kushoto akisisitiza utumiaji wa Bidhaa zinazotokana na Maziwa. Amesema wastani wa unywaji wa Maziwa Kitaifa kwa mtu kwa mwaka ni lita 45 wakati viwango vilivyopendekezwa kimataifa (WHO) na (FAO) ni angalau lita 200 kwa mtu kwa mwaka, wastani wa unywaji wa maziwa katika Mkoa wa Ruvuma ni lita 11.6 tu kwa mtu kwa mwaka.
 Dr Ruth Rioba Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa Taifa akifafanua lengo la kuyaleta Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Mkoa wa Ruvuma katika Uzinduzi wa Wiki ya Maziwa uliofanyika Viwanja vya Manispaa ya Songea.
 Viongozi mbalimbali wa Serikali, Asasi, Taasisi na Mashirika waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya Maziwa Mkoa wa Ruvuma wakitathmini kwa makini kiwango cha chini cha unywaji wa Maziwa katika Mkoa wa Ruvuma.
Ng`ombe wa Maziwa akiwa katika Banda Maalumu katika viwanja vya Manispaa ya Songea yanapoadhimishwa Maadhimisho ya wiki ya Maziwa ambayo kilele chake kitakuwa 1/06/2013

Tuesday, May 28, 2013

WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WATAPATA LINI UKOMBOZI KUHUSU KILIMO CHA TUMBAKU

 Kilimo cha Tumbaku kime kuwa ni ukombozi kwa wakulima wa wa Mkoa wa Ruvuma,Lakini changamoto zinazo wapata zina rudisha mori wa kuendeleza zao hilo.1.wakulima wa Mkoa wa Ruvuma walikuwa na kiwanda cha kusindika Tumbaku ambacho kilikuwa na uwezo wa kuajiri wafanyakazi 2000lakinihivi sasa kiwanda hichohakifanyi kazi kwa muda wa zaidi ya miaka 10
 Katibu wa Kampuni ya LIFADA ya Wilaya ya Namtumbo Mohamed Kakwila akiwa Shambani huku akiwa na masononeko ya kuuza Tumbaku kwa bei ya Chini ambayo ime pangwa na Makampuni, Jambo lingine linalo msonenesha ni liba kubwa inayo tozwa na benk wakati wa kuomba kupata mkopo wa kununua pembejeo,Hapo awali walikuwa wakipewa Pembejeo na ATTT na wakati mwingine umoja huo wa ununuzi wa Tumbaku Mkoa wa Ruvuma walikuwa wakilipa Fidia endapo mkulima ana pata hasara hivi sasa Jambo hilo ni la Mkulima
 Mama akiwa shambani akiwa na Furaha jinsi tumbaku yake ilivyo kubali na akiwa na Tegemeo la Kupata Mahitaji Mhimu kama Matibabu,Kusomesha,na kuwa na Fedha za dharura lakini ndoto hizo hutoweka baada ya kukutana na bei isiyo ridhisha,Wafanye nini wana Ruvuma ili wainue uchumi wao
Juhudi za kuongeza Zao la Biashara lime pata Mwitikio katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma hilo ni shamba lilioko Lionde Namtumbo Vijijini hapo mama anaonekana akivuna Tumbaku yake anacho sikitika ni wakati wa kupanga madaraja ndipo wanapo angushwa wa kulima wameomba serekari kuwa jicho la wakulima pale wanapopangiwa madaraja

Sunday, May 26, 2013

KISAMVU NI MBOGA INAYO WAKILISHA UTAMADUNI WA MTANZANIA

Kisamvu ni mwakilishi wa Mwafirika ,Hakuna Mtu utakaye mwuliza asijue mboga ya kisamvu katika hilo wewe una semaje ?. Waafrica sasa hivi tumeingiwa na Utamaduni wa kisasa ambao lengo lake ni kupotosha maadili ya Mwafrika, Jee wew kama una kumbukumbu una jua Maharage ya Kasuka Nywele sasa hivi yako wapi ?. Lamsingi ninalo taka kuku uliza tanzania Tuna Makabila 120 jee wewe Mtoto wako anaweza kuzungumuza Lugha ya asili yako kama hawezi kosa la nani .

Saturday, May 25, 2013

MWALIMU SOFIA MGAYA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA NA WOTE WAFARIKI BAADA YA SIKU MBILI -SONGEA = SONGEA


SISI NI WAMWENYEZI MUNGU NA KWAKWE TUTA REJEA.BWANA ALITOA NA BWANA AMECHUKUA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE, MWENYEZIMUNGU AMEWAPENDA ZAIDI WATOTO HAWA WATOTO WOTE WAMEFARIKI. NDUGU WATANZANIA TUMUSAIDIE MAMA HUYU SOFIA MGAYA MUNGU AMPE AFYA NJEMA

Wednesday, May 22, 2013

MAAJABU YA MUNGU YA TOKEA MKOANI RUVUMA MTOTO MCHANGA WA SIKU 4 AKAA SIKU SITA NDANI YA SHIMO AKIWA HAI

 Ndugu yangu ukishangaa ya Mussa basi shangaa na ya Filauni, Methali hiii methibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe alipo wekwa na mama yake kwenye mfuko wa mbolea na kutumbukizwa kwenye shimo, Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipo okotwa na wasamalia wema, Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa Salama  Salimini Yeyote Mwenyenafasi ya kusaidia mtoto huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba zifuatayo mchango  utafwatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia usalama wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili anaye fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima

Tuesday, May 21, 2013

HIVI UTESAJI WA WATOTO UNA TOKANA NA NINI ?

Mkono wa Fikiri Haus 13 uliounguzwa unavyo onekana kwa karibu huo ni ukatiri ulio kithiri
 Mtoto Fikili Hausi Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Shule ya Msingi ya Majengo Mansipaa ya Songea akiwa amelazwa Hospitali ya Mkoa baada ya Kunguzwa Moto na Mama yake .Jeshi la Police lina endelea kumtafuta mama yake Fikili Hausi 
Msomaji hebu angakila Jamii ya watanzania kila siku ina fanya kongamano ya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na mama jee kitendo hiki sisi watanzania tunaenda wapi ?Masikini mtoto anaonekana kama amelala lakini hayo ni maumivu kiasi hataki hata kuongea na mtu.Kila mmoja pale alipo ajalibu kuzuia vitendo hivi.

Sunday, May 19, 2013

WADAU WA SONGEA HABARI, MABADILIKO YA EMAIL YA YAHOO.COM

NAPENDA KUWA OMBA RADHI KWA USUMBUFU MTAKAO UPATA BAADA YA EMAIL YA adam_nindi@yahoo.com kuto tumika tena naomba wadau wangu kwa hivi sasa mtumie EMAIM ifuatayo adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com

Thursday, May 16, 2013

WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA WANA KOSA GANI KWA SEREKARI YA JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA

 Hii ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambayo ina simamia haki zote za wana Ruvuma wapatao 1,400,000 wakiwemo Waandishi wa Habari wapatao 39 walioko Mkoa wa Ruvuma.
Jambo la kushangaza watu mbalimbali wamekuwa wakilaani wakiona Mwandishi ameuwawa, Laana huwa kubwa kupita kiasi. Sasa Waandishi wa Mkoa wa Ruvuma wanakabiliwa na Changamoto ya kuvunjiwa Ofisi yao ambao ni Tegemeo lao. Jee hii Ofisi ya Serikali Mkoa wa Ruvuma itasaidia vipi Jengo hilo lisivunjwe?
 Ofisi hii ni ya Mkuu wa Wilaya ya Songea ambapo ni Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma kwa ukaribu huo ni juu ya Ofisi hii pia kuangalia Haki za Watu mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari ambao wana Changamoto ya kuvunjiwa Ofisi yao. Jee nayo Ofisi ya Wilaya inachukua Hatua gani kuwasaidia Waandishi? au inangoja kulaani?
 Hizi ni Barabara ambazo zinatakiwa ziweze kufuata Taratibu, Kanuni na Sheria lakini kuna Majengo ambayo yamezuia kuzifanya Barabara hizo zichanue kwa kuwa zinawasaidia Wananchi katika kupata huduma mbalimbali katika Majengo yaliyoziba kupita kwa barabara hizo Serikali haina kelele na wala Wananchi hawasemi chochote.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu ndiye mhimili mkuu wa kuwalinda watu mbalimbali, Jee katika Changamoto hiyo inayowakabili Waandishi wa Habari unawasaidia vipi badala ya kungoja mpasuko kati ya Waandishi na Watendaji.
 Jengo linaloonekana mbele yako ndiyo Ofisi ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma ambalo linategemewa kuvunjwa hivi karibuni na Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Jee ni uhasama gani uliopo kati ya Waandishi wa Habari na Halmashauri ya Manispaa ya Songea? Majengo yaliyopo ambayo yamejengwa kinyume cha taratibu mbona hayaguswi?
 Hili ni Tangazo linalowataka Waandishi wa Habari wahamishe vitu vitu vyao ndani ya siku 14 vinginevyo mali zitaharibiwa pamoja na Jengo kuvunjwa. Jee hii ni halali? kuwanyanyasa waandishi wa Habari wakati Wananchi walioko pembezoni mwa Tanzania wanategemea kupata habari kutoka kwa Waandishi.
 ?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
?????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

MHASHAMU ASKOFU MKUU WA JIMBO LA SONGEA


Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Kustahafu kwake kuwa Askofu kutokana na Maradhi yanayo mkabili.

Mhashamu Askofu Mkuu Norbet Mtega amesema ameamua kuweka hadharani Maradhi yanayomsumbua ili waumini wakae wakijua nini kimemfanya Astahafu.

Askofu Mtega amesema anasumbuliwa na Presha ya kupanda pamoja na kuumwa kwa miguu, akiongeza amesema hata kama akihitaji kupumzika hukosa usingizi kwa muda mrefu .

Askofu Mtega amesema anasumbuliwa na Presha ya kupanda pamoja na kuumwa kwa miguu, akiongeza amesema hata kama akihitaji kupumzika hukosa usingizi kwa muda mrefu .

Mhashamu Askofu Mkuu Norbet Mtega amesema pamoja na kustahafu yeye atabaki hapa hapa Songea Mkoani Ruvuma.

Mhashamu Askofu Norbet Mtega ameweza kutumikia Waumini katika uaskofu kwa kipindi cha Miaka 28 .

Hata hivyo alibainisha wazi kwa mujibu wa taratibu za kikatoliki alitakiwa kustaafu akiwa na umri wa miaka 75 lakini kutokana na Maradhi amemuomba Papa Francis wa kwanza  kuomba kustahafu kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria zinazopaswa kuzifuata naye Papa ameridhia.
Kitendawili cha Mshamu Askofu Mkuu kitaweza kuteguliwa na waumini wenyewe kujua kama Mhashamu  kajiudhuru nini kime fanya afikie hatua hiyo.

MHASHAMU ASKOFU MKUU WA JIMBO LA SONGEA

 Kiongozi wa wa waumini wa Dhehebu la Katoliki wana taka kujua Mhashamu Norbet Mtega ni kweli umejiudhuru kuwa ongoza wa umini wa Jimbo la Songea ?
 Waumini wa kiwa njia panda wakingoja kauli ya Uhakika kuhusu Mhashamu Norbet Mtega ni kweli Amestahafu ?
Kitendawili cha Mshamu Askofu Mkuu kitaweza kuteguliwa na waumini wenyewe kujua kama Mhashamu  kajiudhuru nini kime fanya afikie hatua hiyo.

Monday, May 13, 2013

JESHI LA POLICE MKOANI RUVUMA YA KAMATA MENO YA TEMBO KILO 18

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akiwa ameshika pembe ya Ndovu aliyo kamatwa nayo Dereva wa Halimashauri ya Wilaya ya Namtumbo Buhuhani Mntini akisafirisha katika stand ya NamtumboMkoani Ruvuma
 Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma mwenye Begi akiwa amekamata pembe za Ndovu kwa Buruhani Mtini (48) ambaye alikuwa anasafirisha pembe hizo kutoka Wilayani Namtumbo kupeleka Songea
Meno ya Tembo ambayo yalikuwa kwenye Begi vipande 16 vyenye uzito wa kilo 18 vyenye thamani ya Fedha za Kimarekani US Dola 30,000