KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, July 28, 2013

WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANZA PINDA AWATAKA MAFISA UHAMIAJI KUWA MACHO NA WAHAMIAJI HARAMU WANAO SAFIRISHWA KWENYE MABOKISI


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda ameitaka Idara ya Uhamiaji kuwa macho na wahamiaji haramu wanao  ingia nchini kwa njia ya kusafirishwa kwenye mabokis.
 Mheshimiwa kayanza panda ameya sema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya Uhamiaji Mkoani Ruvuma jengo linalo kadiriwa mpaka kumalizika kugharimu shilingi  milioni 712,111,068/=


Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akikagua jengo la Uhamiaji lilioko katika kata ya Mahenge Manspaa ya Songea

 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akipokea Tarifa kutoka kwa kamishimishana wa Uhamiaji wa Utawala na fedha Taifa Piniel  Mgonja


Kamishana wa Uhamiaji wa Utawala na fedha Taifa Piniel  Mgonja amesema mafanikio ya ujenzi kwa ofisi za uhamiaji umetokana na gawio linalo tolewa na serekari hivyo kutokana  na punguzo kutoka asilimia 61% hadi asilimia41 % lita asili kasi ya miradi ya ujenzi ameiomba serekari kuendelea kutoa gawio kwa asilimia hiyo ya zamani ya asilimia 61% au zaidi ili kila mpaka wa nchi yetu uwe na ofisi bora

WAZIRI MKUU AWATAKA WAZAZI KUWA PELEKA WATOTO WAO VETA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda amesema Serikali kwa sasa imejitahidi kupunguza ongezeko la Ajira kwa Vijana kutoka asilimia 16% hadi kufikia asilimia 11.5%.

Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameyasema hayo alipotembelea Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Songea na kuweza kuweka la Msingi Ujenzi ambao mpaka sasa umegharimu kiasi cha fedha ya Tanzania  1,568,019,848.[Bilioni moja milioni mitano sitini na nane na kuminatisa elfu mianane arobaini na nane
 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akikagua Mashine zinazo tumika kuwa fundishia wanafunzi wanao chukua Mafunzo ufundi stadi
 Waziri Mkuu Mizengo Kanza Pinda akionyeshwa gari lililo tengenezwa na Chuo cha VETA Songea
 Moja ya Mazao ya Chakula yanayo Patikana Mkoani  Ruvuma [Mihogo]
 Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda alielewzwa faida ya Mihogo kuwa pia una weza kutengeza Biscuti,Keki ,pamoja na kutengeneza vitafuno mbalimbali
 Chuo cha VETA Pia kina jihusisha na ufundi wa Kushona kama vinavyo onekana vitambaa mbalimbali
 Katika ufundi Veta  ina weza hata kuandaa nguo za Maarusi kama wanavyo onekana kwenye picha
 Waziri Mkuu akionyeshwa Jiko la Kisasa ambalohutumia kuni lenye thamani ya shilingi laki sita [600,000/=]
Waziri Mkuu akikabidhiwa jiko la Kuni kama zawadi kutoka chuo cha VETA  Lilwe kielelezo cha kutunza Mazingira miba kutumia Miti mingi

WAZIRI MKUU AZUNGUMUZA NA WAANDISHI WA HABARI RUVUMA




Waandishi wahabari wakiwa ikulu ndogo Songea wakisikiliza Rasilimali tulizo nazo Nchini Tanzania ikiwemo Pamoja na Madini,Nafaka malimbali jambo lililo pelekea mkoa wa Ruvuma kuwa ya moja ya Mag’hala ya mahindi kitaifa

 Mwandishi wa Habari Mkongwe wa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisikiliza kwa makini maelezo ya maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma
 Mwandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Crencesia Kapinga wa Gazeti la Majira akimwomba Waziri Mkuu kuwa shirikisha wandoshi wa Mikoani ili waweze kujifunza anapo kwenda safari za Nje ya Nchi
 Katibu Msaidizi wa Ruvuma Press Club akimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda alipo kuwa akielezea Michango inayo Tolewa na Wandishi wa Habari katika Kuleta Maendeleo
 Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma kutoka Wilaya zote wakiwa Katika Majumuisho ya Ziara ya Waziri Mkuu katika Mkoa wa Ruvuma


Waziri mkuu wa  Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Pinda akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu kukua kwa uchumi wa Mkoa wa Ruvuma n KUWA WA Nne kitaifa.

Wakuu wa wilaya za Tunduru,Nyasa,Mbinga,Namtumbo wakiwa kattika Majumuisho ya Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda katika ikiulu ndugo Songea

WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANZA PINDA AWATAKA WANANCHI WANAO ISHI MPANI MWA MALAWI KUWA WATULIVU


Waziri mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzani Mizengo Kayanza  Pinda amewataka Watanzania wanao ishi Mpakani na Malawi kuwa watulivu ,Kwani wao ni ndugu siasa haziwezi kutenganisha undugu ,Mvumilivu hula mbivu. Picha ya hapo juu ni Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzani Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Malawi Joece Banda wakiwa katika tabasamu la nguvu kunyesha upendo uliopo kati ya Tanzania na Malawi

JEE UMEWAHI KUONA MWANA MKE MNNE ?

 

Mwanamke huyu ajulikanaye kwa jina la Mikell Rrufinel ana umri wa miaka 39 kiuno chake kina ukubwa wa
inchi40 upana wa makalio ni inchi 94 ameolewa na watoto wa nne mme wake anajulikana kwa jina la Ruggie Brooks naye ana umuri wa miaka 40 wote wawili wanaishi Los Angels

Wednesday, July 24, 2013

MAZISHI YA SHUJAA RODNEY NDUNGURU ALIYEFARIKI NCHINI SUDANI AKILINDA AMANI


Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majenshi Nchini Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Familia ya Marehehu Rodney Ndunguru na Watanzania wote kuwa na Moyo wa Subira kwa kifo cha Praiveti Rodney Ndunguru kilicho mpata huko Durfer Sudani  13/7/2013 baada ya kuvamiwa na waasi

Mheshimiwa Amiri Jeshi mkuu Jakayaya Mrisho Kikwete ameya sema hayo wakati akitoa salamu za Rambirambi kwa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru salalamu zilizo somwa na mwakilishi wa  Briged ya 401  Tembo  brged  kanaliGeorge Tomasi Msongole

 Jeneza la Rodney Ndunguru muda mfupi kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mjimwema Songea.
 Afisa Tawala Wilaya ya Songea Joseph John Kapinga katikati akiwa na Maafisa wa Jeshi katika Maombolezo ya Msiba wa Rodney Ndunguru Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma.
 Jeshila la Wananchi (JWTZ) lina taratibu zake katika kutoa heshima za mwisho kwa mwenzao anapofariki, hapo ni wanajeshi wakitimiza taratibu za heshima za mwisho katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema Songea ikiwa ni ishara ya kumuenzi Shujaa Rodney Ndunguru aliyefariki tar 13/07/2013 huko Darful Sudani akitekeleza Jukumu la Kimataifa la kulinda Amani.
 Jeneza lililohifadhi Mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likiwa limetolewa Bendera ya Taifa na Mavazi aliyokuwa akiyatumia tayari kwa kuingizwa kwenye Makao ya milele.
 Wanajeshi wakiwa katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Rodney Ndunguru kadiri ya taratibu za ki Jeshi.
Katika mazishi hayo yaliyo fanyika katika makabuli ya Mjimwema manspaa ya Songea ya liweza kuhudhuliwa na viongozi wa serekari wa kiwakilishwa na katibu tawala Joseph John Kapinga ,jeshi la wananchi wa Tnzania ambapo heshima zote za kijeshi zilitolewa
 Wanajeshi walioshiriki msiba wa Mwenzao Rodney Ndunguru wakitafakari changamoto zinazowakabili katika kulinda amani.
 Mamia ya waombolezaji Wanajeshi wakiwa na huzuni katika kumsikitikia mwenzao aliyekufa kishujaa katika kutekeleza Majukumu ya Kitaifa wakiwa nyumbani kwa Marehemu Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma kabla ya Mazishi.


Padre Noi Duwe akiendesha misa amesema swala la uvunjifu wa amani una tokana na kuto tii sheria zinazo tolewa serekari badala yake kuendeleza migomo na maandamano amewataka waumini waache kukashifu serekari

Msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amewaomba wa Tanzania kudumisha amani katika nchi yao bila ya amani ya kudumisha amani yata tupata yanayo tokea Sudani hivi sasa hatunge weza kumpoteza ndugu yetu Rodney Ndunguru lakini ni kutokana na kukosekana kwa Amani

Maafisa wa Jeshi wakitoa vifaa vya kazi (kofia, Sare, Mkanda na viatu) alivyokuwa akivitumia Marehemu Rodney Ndunguru wakati wa uhai wake tayari kwa Mazishi

 Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wakitoa heshima zao za mwisho kwa Shujaa Rodney Ndunguru kwa kupiga Risasi  hewani mara baada ya mazishi yake katika Makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea

Captaini Patrick Kitosi kutoka kikosi cha 92 akisoma wasifu wa marehemu Rodney Ndunguru amesema Rodney Ndunguru alizaliwa 9/7/1985 Mjimwema mkoani Ruvuma alikuwa kijana shupavu, aliweza kufuzu mafunzo ya ukomandoo dalaja la pili na dalaja la tatu. Alisha wahi kwenda Dur fur mara mbili katika jitihada za kulinda amani Umoja wa Mataifa wa Nchi za Afirika alipata nishani akiwa Durfur Sudani


Mheshimiwa Rais  Jakaya Kikwete amesema Marehemu Rodney Ndunguru alipwatwa na mauti hayo wakati akitekeleza jukumu la umoja wa mataifa wa Africa la ulinziwa amanikatika eneowalilo shambuliwa ghafula ambapo yeye na wenzake 6 waliweza kupoteza maisha.

Kanali Goerge Thomas Msongole akisoma salamu hizo kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema msiba huu ni wa wa Tanzania wote na Taifa lote hivyo ni wajibu wetu watanzania wote kushiriki katika maombolezo na maombi ya kumwombea ndugu yetu Rodney Ndunguru

 Jeneza lililohifadhi mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likitolewa ndani nyumbani kwake Mjimwema Songea tayari kwa kuelekea Makaburini kwenye Makao ya Milele.

Wednesday, July 17, 2013

KUFUFUA ZAO LA KOROSHO NCHINI TANZANIA





Dr louis Kasuga Mtaalamu wa Utafiti wa Magonjwa ya korosho alisema baada ya juhudi za serikali kufanya utafiti na kubaini chanzo  cha matatizo na sababu zilizopelekeakuzotota kwa zao la Korosho iliweza kuongeza uzalishaji wake kutoka tani 16,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 158,000 kwa mwaka, kwa kutambua umuhimu wa zao hili la biashara ambalo ni la  pili Tanzania kwa kuingiza pesa za kigeni kutoka Nje.


Miongoni mwa kazi zinazofanywa na Kituo cha Utafiti wa Zao la Korosho Naliendele kilichopo Mkoani Mtwara ni kufundisha wakulima wa zao hilo mbinu bora za upandaji wa zao la korosho kwa njia ya ubebeshaji wa miche ya mikorosho. Picha unayoiona hapo juu ni Miche ya Mikorosho inaweza kupandwa kwa kubebeshwa kitaalamu

Wakulima wa Zao la korosho kutoka mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma wamesema chanzo cha kuzorota kwa zaola korosho ni kuchelewa kwa pembejeo, bei ndogo ya kuuzia na ukosefu wa masoko
 Wahiriki 125 wa Mafunzo ya uendelezaji na ufufuaji wa Zao la Korosho yaliofanyika Manispaa ya Songea ukumbi wa Chuo Kikuu Huria yaliyojumuisha wakulima, Maafisa Ugani, Wapuliziaji na  Maafisa Ushirika wa vyama vya Msingi kutoka wilaya za Songea Vijijini,Namtumbo, Mbinga, Rudewa na Kyela.
 Washirikiwa Mafunzo ya ufufuaji na Uendelezaji wa zao la Korosho wakiwa ndani ya ukumbi wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika Mafunzo hayo yaliyoendesha na wawezeshaji kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Korosho Naliendele chini ya Dr. Louis Kasuga na kugharamiwa na CIDTF (Cashew Industry Development Trust Fund).
 Washiriki wa Semina juu ya ufufuajina uendelezaji wa zao la korosho wakifuatilia elimu Bora ya Kilimo cha zao la Korosho ili kuinua viwango vya ubora na uzalishaji bora wa zao hilo, namna ya kuanzisha zao la korosho, kulihudumia, kulifufua na kuboresha Shamba la zamani.
 Washiriki wa Mafunzo ya uendelezaji wa zao la Korosho kutoka wilaya za mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Njombe wakisikiliza mada kwa makini katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Songea Manispaa.
 Wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa Zao la Korosho Naliendele wakiseti mitambo tayari kwa kuendesha mafunzo juu ya uanzishaji, ufufuaji na uendelezaji wa Kilimo cha zao la korosho.
 Wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Korosho cha Naliendele wakiwa Mkoani Ruvuma katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kuwezesha mafunzo juu ya ufufuaji na uanzishaji wa zai la korosho. mwenye kofia kushoto ni Mtaalamu wa Magonjwa na wadudu wanaoshambulia zao la korosho Mr. Barnaba Maarufu kama BB, na wa pili mwenye laptop mbele ni Bw. Maiko Nkondora mwasibu wa Kituo cha Utafiti cha Naliendele.
Dr. Louis Kasuga aliyeshika Projekta kwenye meza akiendelea kuonyesha changamoto zinazozorotesha zao korosho kwa washiriki wa Mafunzo ya ufufuaji na ufuaji na uanzishaji wa zao la korosho yaliyofanyika manispaa ya songea na kujumuisha washiriki kutoka wilaya 5 za mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya. Mwenye Jaketi ya Bluu katikati ni Mwanahabari Mkongwe wa Kituo cha Utafiti wa zao la korosho Naliendele Bw. Fakii Mussa. na kulia kwake ni Mtaalamu wa uanzishaji wa shamba jipya na upandaji wa zao la korosho Bw. Swrtbert Magani.