KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, December 30, 2013

UCHAGUZI WA WAKILISHI KUTOKA MITANDAO YA KIRAIA TANZANIA KWENDA KATIKA BUNGE LA KATIBA

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Deuki kibanda akifungua mkutano wa uchaguzi wa wajumbe wa bunge la katiba jijini Dodoma
 Mwandishi wa Habari kituo cha Dodoma kutoka Star Tv Ndugu Twaha akichukua tarifa za Ufunguzi wa Wajumbe wa baraza la Katiba kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserekari yatayo shiriki katika bunge la katiba
 Wajumbe kutoka mikoa ya Ruvuma Lindi na Mtwara wakichagua wajumbe wawili watakao wakilisha katika bunge la katiba
 Wajumbe kutoka Mashirika Mbalimbali yasiyo ya Kiserekali wakiwa jijini Dodoma kuchagua wa jumbe wakuwakilisha katika bunge la Katiba
 Mjumbe kutoka Mkoa wa Ruvuma Adamu Nindi akisikiliza kwa Makini hoja mbalimbali zilizo kuwa zikitolewa na wajumbe walio kuwa wakiomba kura
 Wajumbe wa Asasi mbambali kutoka Tanzania Bara na Tanzania Kisiwani
Wajumbe kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakiwa Jijinni Dodoma kuchagua majina ya watu  201 yatakayo pelekwa mbele ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi

Wednesday, December 25, 2013

JUMULA YA WATU 111 WAMEPOTEZA MAISHA MKOANI RUVUMA KWA AJALI ZA BARABARANI

Adam Nindi, Songea.
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limewataka Madereva wote wanaoendesha Mabasi ya Abiria kuwa na Tahadhari wakati huu wa Sikukuu za Krismas na Mwaka mpya ili kuepusha ajali ambazo zinaweza kuepukika.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki akieleza hali halisi ya ajali katika mkoa wa Ruvuma kwa mwakla 2012 na 2013 ameanisha kama ifuatavyo

Kwa kipindi cha Mwaka 2013 hadi mwezi November jumla ya Ajali zilizotokea ni  454   zilizosababisha vifo 111 
.  Ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo jumula ya ajali zilikuwa 537 zilizo sababisha vifo vya watu 93
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki amesema Ajali nyingi hutokea kutokana na Abiria kushabikia Mwendo mkali kwa Madereva pia Madereva kutokuwa waangalifu katika sehemu tete zinazosababisha ajali mara kwa mara.

Sunday, December 22, 2013

MABADILIKO YA UONGOZI HULETA HAUENI AU HUENDELEZA KUMGANDAMIZA MWANANCHI ?

 Ngao hii ni moja ya alama kuwa maamuzi yoye yanayo tolewa na serekari ni faida kwa wananchi wa Tanzania bara pia ni moja ya kielelezo cha utawala  bora wenye sheria zinazo lenga haki za Binadamu juu ya jambo linalo linalo amuriwa na serekali , jee ngao hii ina eleweka na Wananchi au dhumuni la Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa na Ngao lina fahamika kinaganaga
 Viongozi wakisiasa huwa kama Mshumaa unapo waka huangaza watu na kutoa Nuru lakini ukizima ndivyo unavyo kuwa kwenye mioyo ya watu hebu tutathinini ni mema mangapi ameya fanya Emanuel John Nchimbi  na Mabaya mangapi kayafanya, Kumbikumbi akiona Taa hukimbilia kumbe ni mtege wa Binadamu jee kwa hili la Kiongozi Emanuel John Nchimbi Tuna semaje ?
 HATIMA YA KIONGOZI SAWA NA MSHUMAA AU NGOMA ISIYO WAMBWA ONA WASIFU     WA MH, EMANUEL JOHN NCHIMBI
Honourable
Emmanuel Nchimbi
MP
In office
7 May 2012 – 20 December 2013
President
In office
28 November 2010 – 7 May 2012
President
In office
13 February 2008 – 28 November 2010
Minister
In office
17 October 2006 – 13 February 2008
In office
6 January 2006 – 16 October 2006
Assumed office
December 2005
Preceded by
Majority
27,582 (59.09%)
Personal details
Born
24 December 1971 (age 41)
Nationality
Political party

Uchunguzi wa Habari za kuwa wafaa wananchi ni mhimu sana ,Hebu Tuone sasa tuna Maliza Mwaka yepi mazuri yaliyo fanywa na Wandishi wa Habari na Yepi mabovu yaliyo fanywa na Waandishi wa Habari. Tujitathini wenyewe tusipige katumba kuonyesha vidole kwa wenzetu Pale tulipo kosea tuji sahihishe na Pale tulipo fanya vizuri tuboreshe zaidi Bado siku chache za kumaliza Mwaka lakini lazima Waandishi Tujipange Hapo ni Mwandishi Mwandamizi Juma Nyumayo akiwa na Mkongwe wa Habari Adam Mzuza Nindi wakitathiminji mwaka 2013

Monday, December 16, 2013

HEBU TUONE MAZISHI YA NELSON MANDELA KIJIJINI KWAO AFRICA KUSINI

 Eneo lililo cha guliwa Rasimi na Rais wa kwanza wa Africa Kusini Hayati Nelison Mandela kwa ajili kuzikwa hilo linalo onekana ni Sanduku la Hayati Nelison Mandela
 Sehemu aliyo zikwa Rais wa kwanza wa Africa Kusini Nelisoni Mandela linavyo onekana kwa Mbali
 Wanajeshi wenye vyeo vya juu wakiwa wamebeba Mwili wa Rais wa kwanza wa Africa Kusini Hayati Nelison Mandela wakiwa katika Mwendo wa Heshima zote za Kijeshi
 Mila na Desturi ni Ngao ya Mwafrica hapo watu walio tayarishwa kwa ajili ajili ya mazishi kimila wakiwa wamevalia Rasimi tayari kwa Mazishi ya Kimila
 Kifaa malumu kilicho tayarishwa kwa ajili ya kuburuza Geneza la Rais wa kwanza wa Africa Kusini Hayati Nelison Mandela kikiburuzwa na Wanajeshi wenye vyeo vya juu
 Ndege za Kivita zikitoa Heshima ya Mwisho kwa Mwili wa Rais wa kwanza wa Africa Kusini Hayati Nelisoni Mandela huku zikiwa na Bendela ya Taifa ya Africa Kusini
 Heshima za kijeshi ziliendelea kutolewa wakati mwili wa Rais wa kwanza wa Africa Kusini Marehemu Nelson Mandela ukizikwa huku minga 21 iki pigwa
 Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamuhuri ya Mungano akitoa salamu Rasimi kwa niaba ya watanzania baada ya kupewa nafasi katika Mazishi ya Hayati Rais wa Kwanza wa Afrca Kusini Hayati Nelsoni Mandel
 Nyumba za jadi eneo alilo zaliwa  Raisi wa kwanza wa Africa Kusini Hayati Nelison Mandela
 Nelison Mandela katika uhai wakeakiwa na familiayake  nyumbani kwake Africa Kusini
 Kama unavyo ona utamaduni wa Mwafrica uhuwa una bezwa mara nyingi lakini Hayati Rais wa Africa Kusini Nelison Mandela ameweza kuonyesha kuwa mtu haachi alisi amekubali kuzikwa kimila na heshima za kimila zilitumika, Unaona kitu kama shuka nyeupe hiyo siyo shuka bali ningozi ya Ngombe aliye pea.Kwa desturi ya Machifu wa Africa walikuwa wakivishwa Sanda ya Ngozi
 Mtoto wa Hayati Nelson Mandela akiwa ame Vaa Ngozi ya Chui tayari kwa kuongoza Mazishi ya Hayati Nelson Mandel
 Moja ya Tabia ya Chifu ni kuvaa shanga kichani hii ni alama inayo onyesha cheo cha kimila kwa mtu marufu huyo hapo juu ni Hayati Rais wa Jamuhuri ya Africa kusini Nelson Mandela katika Uhai wake

UTAFITI WA SHIRIKA LA PADI NA USHAHIDI WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA kwa INSITUTE OF LONDON

Wandishi wakitoa ushahidi jinsi PAD  [Tanzania Mission to the poor and Disabled] inavyo weza kuwa saidia wazee mkoani Ruvuma Kutoka kulia ni Catherine Nyoni wa TBC na anaye fuatia ni Judith Lugoye wa Mwisho kushoto ni Mtafiti kutoka Insitute of London Juliut Tobiasi
Mtafiti kutoka UK Juliute Tobiasi  akihojiana na wandishi wa Habari kuhusu huduma inayo tolewa na PAD kwa Wazee mkoani Ruvuma,Aliye kaa Dirishani ni Mkurugenzi wa PAD Issaca Msigwa
Wageni kutoka UK wakiwa katika mapumuziko baada ya kupokea maelezo ya jinsi vyombo vya Habari Mkoa wa Ruvuma vinavyo shirikiana na PAD kuhamasisha juu ya wazee kupata haki zao za msingi
Mtalamu mtafiti kutoka UK Julute Tobiusi akiwa Manspaa ya Songea kupata maelezo ya kina juu ya shirika lisilo la kiserekari linavyo wajibika kwa kutoa huduma mhimu za wazee

Wednesday, December 11, 2013

MTOTO AOKOTWA JALALANI SONGEA AKIWA MZIMA.MTOTO MMOJA ALIWA NA MBWA

MTOTO HUYU YUKO CHINI YA UNGALIZI WA HOSPITALI ANAHITAJI KULA NA KUVAA KAMA UNA NGUO AU CHOCHOTE KILE WASILIANA NA NDUGU JUDITH LUGOYE AKUPE HABARI KAMILI SIMU YAKE NI 0755 061 588
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Benedict Ngaiza amewataka wanawake kujiepusha na vitendo vya ukatili hasa kwa watoto kwa kujiunga na uzazi wa Mpango.
Akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa Dr Peter Kiula ameya sema hayo baada ya motto mwenye umuri wa siku 7 kuokotwa katika Maeneo ya Mateka akiwa ame tupwa Jalalani
Dakitari  Peter Kiula amesema vitendo vya ukatili vina zidi kukithiri kutokana na wanawake kubeba Mimba bila Maandalizi,Amewaomba wanawake ili kuepukana na utupaji wa watoto wana paswa kujiunga na Uzazi wa Mpango 


Muguzi  Anna Chaula katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma amewaomba wana wake kushirikiana na Vyombo vya Dola kumubaini mama aliye Tupa Mtoto kwa kuwa wanao fanya vitendo hivyo ni wale tunao ishi nao,Makamu mwenyekiti wa Mtandao wa Police wana wake Fadhila Chacha amesema Mtandao wa Police wanawake una endelea kupambana na vitendo vya ukatili,Ndiyo Maana kila wakati huokoa uhai wawatoto.


Wananchi walio enda Hospitalini kushuhudia swala la mtoto aliye tupwa walibaki wa kibubujika na machozi huku wakilaani kitendo hicho na kuitaka dola kuchukua hatua kali dhidi ya Mama aliye tupa Mtoto

 Hebu angalia mtoto alivyo hana kilema kama unavyo mwona tujiulize kwa nini mama wa mtoto huyu amtupe mtoto wake akiwa kama alivyo, Jee tuseme huyu mama hana dini,au malezi ya familia yalikuwa hafifu,au kipato alicho nacho ni kidogo,au mambo ya ujana ya memtinga tujalibu kutafuta jibu pengine tuta weza kuwa okoa hawa watoto


Mkoa wa Ruvuma wakati ukiwa katika kilele cha siku 16 za kulaani vitendo vya ukatili dhidi ya mama na Mtoto tayari watoto watatu wameokotwa jalalani na mmoja kuliwa na mbwa eneo la mfaranyaki baada ya kutupwa na kuliwa nusu kiwiliwili na kubakizwa sehemu za kichwa natumbo