KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, June 22, 2014

KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA CHIPOLE SONGEA VJIJINI KINA CHANGAMOTO YA KULEA WATOTO 60 WAHITAJI MSAADA WAKO

  LUKONDONYIKA NAVACHE wawanawake walio olewa na wapare wanao ishi mkoa wa Ruvuma wameguswa na watoto yatima ambao wanaishi kituo cha chipole kinacho milikiwa na watawa wa kikatoriki songea vijijini waliweza kupeleka misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kama wanavyo onekana hapo juu
 sisita Akwinata akiwa Chipole akipokea msaada wa zawadi mbambali kutoka kwa Chama cha wanawake wakipare walio olewa Mkoa wa Ruvuma
 Mama wa Kipare akiwa amempakata mtoto mdogo aliye telekezwa na mama yake na kupelekwa kituo cha kulelea watoto wadogo kilichopo Chipole Songea vijijini
 Mama wa Kipare ambaye pia ni mfanyakazi wa Jeshi la Police Mkoa wa Ruvuma akiwa ameguswa na watoto Yatima walioko Chipole Songea Vijijin alikuwa mmoja wawanawake wakipare walio kwenda kutoa zawadi kwa watoto yatima Mungu awaongezee pale walipo chukua
 Ukiwa mama ,Sifa ya kwanza ya Mama ni kuwa na Huruma wanawake wakipare wanao ishi mkoani Ruvuma w Chipoleameonyesha Huruma hiyo kwa kwenda kutoa zawadi na kuwa fariji watoto wanao ishi katika mazingira magumu kwa kutegemea nguvu za masister wa
 Hata ukiwa umetingwa kiasi gani lakini unapo kutana na mtoto  mdogo moyo wako huwa na furaha kupita kiasi kama unavyo mwona mama huyu hapo juu akiwa amemshika mtotot yatima,jee wewe unaye soma habari hii umewahi kutoa msaada kwa watoto yatima ,unangoja kulizwa na malaika au Mungu ?
 Hawo wote unao waona hapo ni watoto ambao hawana baba wala mama wana hitaji msaada wako ni kweli una lala usingizi mzuri huku watoto kama hao wakiwa katika huzuni ya kukosa wazazi na vyakula ,mavazi,pamoja na kutaka kufarijiwa
 Hebu angalia watoto wanavyo furahia zawadi hata ikiwa nikidogo wanacho furahia watoto hawa ni upendo wako wewe na mimi
 Hebu angalia Mtoto huyu ana hitaji upendo lakini ni Yatima ana taka kuwa karibu na jamii jee wewe hili halikugusi mpaka waje wanawake wakipare na hapa Ruvuma kuna watu,ni vizuri fedha yako kuitumia kwenye pombe,anasa zisizo na faida ?
 watoto hawa walipo tembelewa na Wanawake wa Kipare walifarijika sana hapo wanawake hao wakitoa mipira kwa ajili ya kuchezea hao watoto
 Mtoto amepakwatwa huku akiwa ameshika maziwa ya maji ,huo ni upendo wa akina mama wa kipare wanao ishi Mkoani Ruvuma
 Watoto wakinywa maziwa na wakionyesha furaha kwa wageni wao ndugu yangu na kukumbusha kazi hiui na wewe tafadhali ifanye Mungu ata kuongezea
 Watawa wa kike wa Kanisa katolick Chipole wakionyesha jinsi wanavyo wajali watoto wana tupwa na akina mama wasio na huruma
 Watoto hawa yatima wakisha kua hufanya kazi ambazo zina weza kuwaletea chakula hapo wapo katika busitani wakilima
 Moyo wakufariji Yatima una tegemea na wewe ulivyo lelewa ukiwa Binadamu utafanya anayo fanya mama huyo pichani lakini kuwa hujalelewa uta baki kwenye anasa tu
 Watoto hao hapo juu ni baadhi ya Mayatima kwa ujumula wao wapo mayatima 60 ambao wana hitaji msaada jipime wewe kwanza una mtoto mmoja nyumbani kwako jee hali inakuwaje kibajeti ukipata jibu basi toa msaada kwa watoto hawa
 Akina Mama hawa Wakipare wanahitaji Pongezi kwa kazi kubwa waliyo ifanya watoto hawa Yatima wapatao 60 kwa zawadi hizi zizapunguza maumivu ingawa siyo sana, uliye baki kutoa msaada ni wewe na mimi ingawa mimi nime fikisha ujumbe hiyo haitoshi
Mwenye Macho haambiwi ona bali hutumia Macho yake unaona umati wa watoto ulivyouna ngoja Huruma ya Jamii jisifu umetoa sadaka kwa watoto kama hawa, Nasiyo kusema na tika kula sadaka ya Marehemu fulani iko siku sadaka hiyo itakutokea puani

Saturday, June 21, 2014

KWA NINI WATU HAWAACHI VITENDO VYA USHIRIKINA ,WAONE WACHAWI WA SONGEA MKOANI RUVUMA


Ukishangaa ya Mussa uta Shangaa na ya Filauni ndivyo wasemavyo wa  Swahili . Ndugu yangu mara nyingine na panda kuongelea swala la ushirikina, kama hayajakukuta huwezi kuamini maswala ya Ushirikina.

Mimi mwandishi wa Habari hizi niko mkoani Ruvuma eneo ambalo una ambiwa kulifanyika vita vya majimaji, vita hivi vilikuwa na maana kwa kuwa risasi za mjerumani zili geuka kuwa maji na kushindwa kuwa zuru wangoni,Hata songea alipo taka kunyongwa kamba ili katika mara kadha kama si wasaliti Songea asinge kufa.

Hebu ni achane na hilo wazee wawili kutoka Parango ,mtaa wa Nandutu amekamatwa uchawi baada ya kubainika kuua wajukuu wake wane akidai ili kuwa ni mchezo wa kichawi. Mwingine ni MzeeAlex Haule ambaye naye ameua watoto wa Nne mwenyeji wa Kijiji cha Mshindo Luhila kati Mkoani Ruvuma,

Mzee Alex Haule yeye kasema alikuwa akiua watoto wake kila sikukuu akiona huruma kwa Mtoto wake alikuwa akialikia Mtu mwingine atekeleze tendo la kuua.Ndugu zangu hii siyo hadithi bali ni ukweli ulio wazi ukifika Eneo la Luhila katika Manispaa ya Songea ni kilometa tano kutoka Mjini nji iendayo Tunduru

Ukifika luhila Sheli chepuka mkono wa kulia ni mwendo wa nusu saa kutoka barabara ya Lami uta kuta kambi hapo,Sasa hebu nikuonyeshe picha za Washirikina walio kiri mbele ya Mganga Bint Ndembo kiboko cha Wachawi Ruvuma
Umati wawatu ukielekea Uwanja wa Zambi kuona Washirikina wanavyo umbuka ni kilometa tano tu kutoka Songea Mjini ,Bendera hiyo nyekundu ni kuonyesha eneo unalo ingia ukiwa mchawi ujue ni hatari,
Umewahi kuona kibuyu kikizunguza basi ukipata nafasi ukikutana na Mzee Alex Haule atakueleza kwa kirefu, unakiona kibuyu hicho alicho kamata hapo hana ujanja wa kishirikina kila kitu ana sema mwenyewe
Mzee Alex Haule akiwa amekaa Uwanja wa Zambi na Mganga wa Jadi Binti ndembo akieleza jinsi alivyo ua Watoto wake wa NNE kwa njia ya Ushirikina aliye kulia ni Mzee mshirikina Beda Nchimbi liye vaa shati jeupe ,Hivyo vipara vina maana yake fika uwanja wa zambi uta jua maana ya upara
Mzee Beda Nchimbi kutoka Parango Peramiho Songea Vijijini aliye vaa Shati Jeupe amambaye ameua wajukuu wanne akiwa uwanja wa Zambi akitubu Matendo maovu aliyo yafanya kwa Jamii
Bint Ndembo akiwa na kioo cha ajabu ambacho huangalia matendo mabovu yanayo tendwa na washirikina
Washirikina wakivua viatu mara wanapo ingia uwanja wa Zambi tayari kwa kuumbuliwa Maovu yao
Ukiangalia kwa Makini hapo wanapo kaa hao watu kuna duara la rangi nyeupa kwa hapo chini ukikalia duara hilo basi wewe kama Mshirikina utaeleza kila kitu ulicho kuwa nacho hata dawa unazo tumia uta eleza :Unachezea Bint Ndembo wewe:
Kutoka kulia ni Mzee Alex Haule ambaye ameua watoto wake wa Nne kwa ajili ya Sikukuu mbalimbali. wa kwanza kushoto ni mzee Beda Nchimbi ambaye naye ameua wajukuu wake Nne kwa ajili ya Kitoweo kama alivyo dai mwenyewe,

Monday, June 16, 2014

WATOTO WA MANSPAA YA SONGEA WAOMBA ULINZI KWA VITENDO VYA UBAKAJI



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama amewataka Wazazi kutoa Malezi mema kwa Watoto, kuanzia Malazi, Mavazi, Chakula na Elimu ili Watoto wakue katika Afya nzuri.Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea amesema kuharibika kwa tabia za Watoto kunatokana na Watoto kukosa Malezi mema kutoka kwa Wazazi.
Wazazi waliohudhuria Sherehe hizo wakiwakilishwa na Judith Lugoye wameiomba Serikali kuwa na Silabasi zisizobadilika mara kwa mara katika masomo ili kuweza kumpa ufahamu Mtoto wa kuelewa Masomo anayofundishwa. Pia wameomba adhabu za viboko zitolewe kulingana na umri Fimbo anayopigwa mtoto wa darasa la kwanza itofautiane na anayopigwa wa darasa la saba

 Wafanyakakazi waCRDB wakiwa katika siku ya Mtotot wa Afirica huku wakifanya kazi
kuweka akiba kwa watoto ni mhimu fungua akaunt ya Junior Jumbo imusaidie mtoto wako badaye

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea ameyasema hayo wakati wa Maazimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Majengo Manispaa ya Songea Mstaiki meya amekea adhabu ngumu wanazo pewa watoto kuwa choma moto,kuwafanyisha kazi ngumu pamoja na matendo mabaya ya kuwa baka watoto wakike.
watoto wanahitaji ulinzi wanapo kuwa wana rudi shuleni wewe na mimi ni walinzi wawatoto

Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Songea Enock Lugenge amewataka Wazazi kufungua Akaunzi ya Junior Jumbo ili kuweza kumwekea Mtoto Akiba kwa ajili ya Masomo, Afya na Akiba ya baadaye, Benki ya CRDB Tawila la Songea katika Kuazimisha Siku ya Mtoto wa Afrika wametoa zawadi za Daftari, peni na sare za Mtoto wa Afrika kwa Watoto zaidi ya 100 waliohudhuria Sherehe za Mtoto wa Afrika.

Saturday, June 14, 2014

WAZEE WAOMBA KUPATA MBUNGE MWAKILISHI WA KUWAKILISHA WAZEE

Wazee zaidi ya 1500 wa mkoa wa Ruvuma  wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza huru la wazee Abdala Mwamba wameshiriki  kutia saini zao kuiomba serikali ya Tanzania kumtuma mwakilishi kwenye mkutano wa Umoja wa mataifa  mwaka huu na kuridhia utungaji wa Sheria ya kimataifa ya” kulinda haki za wazee duniani”. Wazee hao waliendelea kusema wazee kama kundi maalum wanahitaji kuwa na sheria hiyo kama ilivyo kwa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Wazee wa Manspaa ya Songea wakiingia katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Matogoro kuishindikiza Serekari ilki waweze kuwa na Mwakilishi katika Bunge la Tanzania
Mtendaji wa Kata ya Matogoro akitoa neno la utangulizi kuwa karibisha wazee katika ofisi yake Matogoro Manispaa ya Songea
Mkusanyiko wa wazee wapatao 500 waliokuja kuishindikiza Serekari kuwapa mwakilishi Bungeni
Wazee wa Mnspaa ya Songea Wapatao 500 wakiwa viwanja vya Matogoro wakitoa sababu za kutaka kuwa na mwakilishi Bungeni wamedai ni kutokana na kuto sikilizwa kero zao
Afisa Maendeleo Manspaa ya Songea Adam Ngelangela akijibu baadhi ya kero zilizo telewa na wazee na kusema ziko kero nyingi zilizo tatuliwa ikiwa na pomoja na wazee kutibiwa bure
Wazee wakitia sahihi karatasi linalo onyesha wao wanataka kuwa na mwakilishi Bungeni
Mwenyekiti wawazee Manspaa ya SongeaAhamad Mwamba  akiwahutubia wazee wenzake jinsi wanavyo kosa haki za msingi wanapo kosa kuwa na mwakilishi Bungeni ambaye atachaguliuwa kutokana na Wazee
Wazee wanawake wakiwa uwanja wa Matogoro walipo kusanyika kutaka kushindikiza Serekari kutoa na fasi kwa wazee kuingia bungeni ili kuwatetea haki za wazee ambazo zime kuwa nyimbo baadala ya kutekelezwa
Nembo la Shirika linalo shugulikia Wazee wa Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumula

MWENYEKITI WA WAZAZZI TAIFA A WATUHUMIWA WAZAZI WA KIKE KUWAPOTOSHA MAADILI YA WATOTO WA KIKE


Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Bulembo amesema kuharibika kwa Tabia za Watoto kwa Kiasi Kikubwa kunasababishwa na  Wazazi wa Kike, Mtoto anapokuwa anabadilika kitabia na kumiliki Vitu vya Anasa na vyenye thamani ya juu kuliko uwezo wa wazazi  ni juu yao kuhoji ili kujua Mtoto wao amevipata wapi.

Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo akiwa Mkoani Ruvuma amezitaka Halmashauri  za wilaya na manspaa ya mji kutoa Asilimia 10%  zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya kuwasaidia Vijana na Wanawake  kuwainua kiuchumi.


Wazazi waliohudhuria katika Mkutano Kijijini Matetereka wametoa kero zinazowakabili ikiwemo, Watendaji wa Serikali kuwa Miungu watu, Walemavu kukosa Msaada kutoka kwa Viongozi wao, na kwa upande wa Wazazi wa Kike wakijitetetea  wamesema  Utandawazi ndiyo sababu kubwa inayowafanya watoto wao kuharibika.
Mheshimiwa Diwani Teofilo Mlelwa akimkaribisha mwenyekiti wa Taifa wawazazi Alhaji Abdallah Majura Bulembo katika kata ya Mkongotema
Wanafunzi wa Shule ya Wilima wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa  Alhaji Abdallah Majura Bulembo
Viongozi wa CCM Songea vijijini walio shiriki ziara ya Mwenyekiti wa Wazazi taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo
Wazee wakiwa katika mkutano wawazazi katika kijiji Mkongotema songea vijijini
Wazee wa Wilima wakisikiliza hotuba ya Alhaji Abdallah Majura Bulembo

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi CCM Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo amewaasa Wazazi kuacha Tabia ya kusababisha Watoto wa kike  kuharibika kitabia hatimaye kupata uja uzito  .
Mwenyekiti wa Jumuya ya Wazazi Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo ameyasema hayo akiwa katika Kijiji cha Matetereka Kata ya Gumbiro Songea Vijijini Wakati wa Ziara yake Mkoani Ruvuma.
katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma akimpokea Mwenyekiti taifa Alhaji Abdallah Majura Bulembo
Diwani TT wapili akiwa na furaha baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wawazazi TaifaAlhaji Abdallah Majura Bulembo
Mlemavu wa viungo akiwa katika mkutano wa mwenyekiti wa wazazi Taifa Alhaji Abdallah Majura Bulemboakiomba msaada wa Baiskeli