KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, May 25, 2015

KIJANA ANA MTAFUTA BABA YAKE AMBAYE INA SEMEKANA YUKO ARUSHA Nikolaus Mramba



ATT RABEKA MLESI RFA

KIPINDI CHA KUTAFUTA NDUGU:

Raimond Nikolaus Mramba ni kiojana mwenye umri wa miaka 23 Anamtafuta Baba yake Mzazi Nikolaus Mramba. Alipotezana naye miaka ya 1992/1993 akiwa mdogo wakati wakiishi Dar-es-Salaam na Mama yake Edeleana Kalenga wao wakiwa wawili na Mdogo wake Ombeni Mramba.

Amesema Miaka ya 1993 Inadaiwa baba yao huyo Nikolaus Mramba ni mwenyeji wa Moshi Mkoani Arusha aliondoka Dar es – Salaam na kuhitaji kuondoka na wanae ambapo Mama yao hakupenda watoto wachukuliwe na Baba yao , aliamua kuwatorosha Kijijini kwa Mama yao Usokami wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa ambako aliwaacha kwa Bibi yao na kurudi tena Dar-es Salaam ambako alikuwa akiishi hadi kifo kilipomkuta mwaka 2011.

Katika kipindi chote wamekuwa wakiishi kwa kuhangaika na Mdogo wake hawana Mtu maalumu wa kuwatunza hawakuweza kuzuru kaburi la mama yao na hawajui Baba yao yuko wapi.

Raimond Nikolaus amejaribu kuhangaika ili aweze kumsaidia mdogo wake asome ameshindwa kufanikiwa kwani alijitahidi kumsomesha hadi kidato cha nne mwaka jana akakwama kumlipia ada ndoto yake ikaishia hapo kwa sasa Yeye mwenyewe Raimond Nikolaus Mramba kwa sasa anaishi Makambi Mjini Songea ambako alikwenda kwa Rafiki yake kwa lengo la kutafuta maisha akijishughulisha na Biashara ndogondogo 

Popote alipo Nikolaus Mramba anatafutwa na wanae Raimond nikolaus Mramba na Omben Nikolaus Mramba awatafute kupitia Redio Free  Afrika Songea Simu namba: 0755 731234/0784731238.  0658 731234

KIJANA HUYU ANA HAMU YA KUENDELEA NA MASOMO YEYOTE AMBAYE ANA WEZA KUMSAIDI MUNGU ATAKUWA NAYE

Monday, May 18, 2015

SIKU YA MKULIMA MADABA SONGEA VIJIJINI

Kilimo kina manufaa endapo mkulima atazingatia kanuni bora za kilimo, Shirika la ACTN kwa kushirikiana na Mashirika mengine yanayojihusisha na masuala ya Kilimo ili kumletea tija mkulima kwa ufadhili wa Shirika la AGRA wanaendesha mradi wa miaka mitatu kupitia  Mtandao wa Kilimo Hifadhi unaolenga kutoa Elimu ya ugan kwa wakulima kupitia Mashamba Darasa na majaribio ya urutubishaji wa Udongo. Katikati ni Mtaalamu wa Kilimo hifadhi kutoka ACTN  Abiud Gamba akitoa Elimu ya Urutubishaji kwa wakulima wa Madaba katika moja ya Mashamba Darasa.
Wakulima wakiwezeshwa Elimu sahihi ya Kilimo wanazingatia kinachowashinda ni namna ya kuifikia Elimu hiyo hapo mkulima wa Madaba akifurahia kupata Elimu ya Kilimo kwa kuzingatia kanuni na taratibu za Kilimo, anaona Elimu ilichelewa kumfikia kwa kuwa ana matumaini ya kupata mazao mengi tofauti na kilimo alichokuwa anakitumia awali ambacho kilikuwa hakimpi tija.
Mtaalamu wa Kilimo kutoka Shirika la ACTN Bw Abiud Gamba akifurahi kuona mabadiliko yaliyojitokeza katika majaribio ya Mashamba darasa waliyoyafundisha kwa wakulima wa Madaba huku wakulima wakiwa na imani ya mafanikio kupitia elimu waliyoipata kutoka kwa Mashirika yanayounda Mtandao wa kilimo Hofadhi.
Wananchi kutoka Vijiji vya Songea Vijijini, Namtumbo,na Rudewa wakifuatilia Elimu ya Kilimo Hifadhi kutoka kwa Wataalamu mbalimbali wa Kilimo katika Maadhimisho ya Siku ya Mkulima Shambani yaliyofanyika Madaba Wilayani Songea Vijijini mkoani Ruvuma.
Baadhi ya Wakulima wakisikiliza kwa Makili Elimu ya Uhifadhi wa Mazao.
Wananchi waliohudhuria katika Elimu ya Mkulima kupitia Mashamba Darasa wamefurahi kufikiwa na Elimu hiyo wameomba Maafisa Kilimo kuwapitia wakulima mara kwa mara na kutoa Elimu ya Kilimo bora na kuyashuru Mashirika yaliyoamua kuwabeba wakulima ili nao waweze kunufaika na kilimo kama ambavyo wafanya kazi wananufaika na kazi wanazozifanya. Wameiomba Serikali kuwatafutia Masoko ya Uhakika ya kuweza kuuzia Mazao yao.
Baadhi ya Mbegu Bora zinazouzwa na Mawakala wa pembejeo walioko Manispaa ya Songea zenye Ubora wa hali ya juu.
Wataalamu wa Vifungashio aina ya vifukofuko wakitoa Elimu ya uhifadhi wa kisasa unaompunguzia gharama mkulima na kuepukana na wadudu waaaribifu wanaoshambulia mazao ambavyo haviitaji mazao yapulizwe dawa ambazo kwa kiasi kikubwa zina uwezekano wa kumuathiri binadamu. Vifukofuko ni hifadhi nzuri ya mazao isiyo na madhara yoyote na inadumu kwa muda wa miaka mitatu.
wataalamu wa vifukofuko wakionyesha kwa vitendo matumizi ya vifungashio aina ya vifuko fuko kwa wakulima katika maadhimisho ya siku ya mkulima kwa wakulima waliohudhuria.
Mtaalamu wa Mbegu kutoka Kampuni ya SEEDCO Michael Rikanga akielekeza aina ya mbegu inayofaa kwa udongo wa wakulima wa Songea Vijijini.
Wataalamu wa Vifungashio wakionyesha aina ya vifungashio ambayo kwa sasa inapatikana Manispaa ya Songea na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Weniselia Swai akiwaasa wananchi wa Wilaya ya Songea vijijini kuchangamkia fursa na kuitumia ipasavyo ili kuendana na kilimo chenye tija.
Viongozi wa Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo Hifadhi wakiwa na Mawakala wa Pembejeo na Viongozi wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mashamba darasa na kujionea hali halisi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea akisalimiana na Viongozi wa Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo wa Hifadhi.
Baadhi ya Wananchi wakiwa Madaba kufuatilia mafunzo ya Kilimo hifadhi wakati wa Maazimisho ya Siku ya mkuma Shambani Madaba.
Wananchi wakitafakari jinsi ya kuboresha Kilimo.
Hiki ni Kielelezo tosha kinachoonyesha jinsi gani Viongozi wanavyothamini kilimo, kielelezo hicho kinaonyesha mashirika yanayounda mtandao wa kilimo hifadhi yakilenga kumkomboa mkulima na umaskini.
Afisa  na Mtalamu katika Shirika la ACTN Abiud Gamba akiwa katika moja ya Mashamba Darasa yaliyoko Madaba Songea Vijijini kujionea hali halisi ya Majaribio ya Mashamba Darasa.
Bw Shamba Mr Waziri kutoka Halmashauri ya wilaya ya Songea akiratibu mambo ambayo yataweza kumsaidia mkulima kuweza kupata kipato zaidi kutokana na kazi yake ya Kilimo, kulia ni Diwani wa Viti Maalum wa Madaba.
 Mgeni Rasmik katika Maadhimisho ya Siku ya Mkulima Shambani Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Weniselia Swai akiwa na viongozi mbalimba
 Wakala wa Pembejeo za Kilimo Mkoani Ruvuma Bi Rose Haule akielekeza Pembejeo zinazopatikana katika kwake Mtaa wa Serengeti Manispaa ya Songea.
 Mtafiti wa Mazao kutoka kutoka Nyanda za Juu Kusini UYOLE Mkoani Mbeya Bw. Remi Mwakimbwala akitoa maelezokwa wakulima juu ya Matumizi sahihi ya Mbolea na aina ya udongo unaotumika katika Viwanja vya soko la Madaba Songea vijijini.
 Wataalamu wa Mfumo mzuri wa uhifadhi wa Mazao kupitia vifuko fuko wakitoa elimu ya uhifadhi wa mazao na matumizi ya vifukofuko kwa wakulima wanaofanya majaribio ya Mashamba Darasa kutoka wilaya za Rudewa na Songea Vijijini .
Meneja wa Mradi kutoka Shirika la RUDi na mwakilishi wa AGRA Mr Frenk Mhando mwenye miwani akiwa kijiji cha Madaba yalikofanyika Maadhimisho ya Siku ya Mkulima Shambani ambako majaribio ya Kilimo Hifadhi kupitia Mashamba darasa ya wakulima yanafanyika ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Mraji wa Miaka mitatu.

MWENGE WA UHURU MPAKANI MWA MKOA WA MTWARA NA RUVUMA

Kamanda wa police Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela akiwa na Mkuu wa Wilaya ya wilaya ya Nyasa wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara
Watalamu kutoka Mkoani Ruvuma waki ngoja kukabidhi Mwenge Mpakani mwa Mtwara na Ruvuma
                       Chipukizi kutoka Mtwara wakiwa tayari Kuupokea Mwenge kutoka Ruvuma
       Kijana Chipukizi kutoka Mtwara akitoa Heshima kwa kwa mkimbiza Mwenge Mkoani Mtwara
Viongozi kutoka Mkoani Ruvuma wakiwa nanyumbu wakingoja Mwenge wa Uhuru ukitokea Wilaya ya Tunduru
Viongozi wa Chama na Serekari kutoka Mkoani Ruvuma wakiwa Tayari kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Viongozi wa Mkoa wa Mtwara
Kiongozi wa Ngazi za Juu Mkoani Ruvuma akiratibu mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Mtwara
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bakari Naricho  akikabidhi Mwenge Kwa kiongozi wa Mbio Za Mwenge
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bakari Naricho  akikabidhi Mwenge Kwa kiongozi wa Mbio Za Mwengewa Uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa Noman  Adamson Sigalla


Kaimu mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pro .Noman Sigalla King amsema miradi hiyo iliyo zinduliwa imeshirikisha nguvu za Serekari kuu ,Serekari za Mitaa, Wananchi na Wafadhili


Mwenge wa Uhuru umehitimishwa kukimbizwa katika Mkoa wa Ruvuma kwa kuweza kuzindua Miradi 41 ikiwa na Thamani ya Shilingi Bilioni 10.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Prof Norman =Sigalla Kinga amesema katika Mirai hiyo  itaweza kuwa inua wananchi kimaendeleo katika Nyanja za  elimu, afya,miundo mbinu ya mawasiliano.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chumu akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Norman Sigalla king' mara baada ya kumaliza mbio zake katika Mkoa wa Ruvuma.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Norman Sigalla king akitoa maelezo ya Miradi iliyofunguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Omary Dendego wakisubiri kupokea mwenge kutoka Mkoani Ruvuma.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  Juma Khatibu Chumu amewaomba Wananchi kuendelea kushirikiana katika kazi za maendeleo pia   kuwaombea wakimbiza Mwenge  kitaifa ili  waweze kukamilisha mbio za Mwenge Tanzania nzima.



Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh Halima Omary  Dendego amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Mkoa wa Mtwara na kuzindua Miraidi 47 yenye thamani ya Shilingi Bilioni  96.

viongozi na wananchi mbalimbali wakiwa Wilayani Nanyumbu Mkoa wa Mtwara kushuhudia makabidhiano ya Mwenge kutoka Mkoa wa Ruvuma.
Viongozi mbali mbali wakisubiri kutoka Mkoa wa Mtwara wakisubiri kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru.
Chipkizi wa Halaiki ya Mwenge wa Uhuru wa Mkoa wa Mtwara wakiwa tayari kwa kumpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge wilayani Namnyumbu Mkoa wa Mtwara.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Norman Sigalla king' akiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela na Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma wakisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Mtwara mara baada ya kuwasili wilayani Nanyumbu kwa lengo la kukabidhi mwenge mkoani Mtwara baada ya kumaliza mbio zake katika Mkoa wa Ruvuma.
Kamanda wa Police Mkoa wa Mtwara Yahaya Ramadhani akiwa na RPC Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela wa kiwa Mpakani Mtwara Kukabidhiwa Mwenge
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma wakiwa Wilayani Nanyumbu Mkoani Mtwara.
                                            RPC Mtwara na RPO Ruvuma
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara wakiwa wanasubiri kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoani Ruvuma ili kuanza Mbio zake katika Mkoa wa Mtwara
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara akiwa na Mbunge wa Tunduru wakiwa mpakani Nanyumbu mkoani Mtwara


Mwenge wa Uhuru ambao uliwashwa 29/04/2015  na Rais wa Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein katika Uwanja wa Majimaji wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma utakimbizwa kwa siku 161 na kuhitimishwa mbio zake mwezi wa kumi mwaka huu.Nikiripoti kutoka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara ni Adamu Nindi wa Star tv