KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, August 25, 2015

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKOANI RUVUMA


Mgombea Udiwani Kata ya Msamala wilayani Songea Isaack Lutengano akiwa kwenye Kampeni kwa kutumia Mabango ya Vivesheo vya Tayari.

Wagombea  kupitia Chama cha Mapinduzi  Mkoani  Ruvuma wametakiwa kuchagua Viongozi ambao wataleta Maendeleo na siyo kuchagua Kiongozi kwa sababu ya  Umarufu wa Jina.

Mgombea Udiwani Kata ya Msamala kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Isaack  Lutengano amesema vijana walio wengi wapo katika mpango wa kutaka Mabadiliko lakini lazima wawe makini katika Mabadiliko hayo, wasichague Viongozi ambao hapo baadaye watajijutia. La msingi ni wao Vijana kuangalia Viongozi watakao ondoa Kero zao.

Mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya ya Songea OSAMU ULAYA akiwa na Bango la Mgombea Udiwani Kwa tiketi ya CCM wa Kata ya Msamala.

Wanachama wa CCM wakiunganisha nguvu kwa ajili ya Ushindi hapo Oktoba 25.

Mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya ya Songea OSAMU ULAYA akiwa na Bango la Mgombea Udiwani Kwa tiketi ya CCM wa Kata ya Msamala.

Mke wa Mgombea Udiwani Shada Haule akiomba kura kwa wajumbe kwa ajili ya Mumewe.

  Mgombea udiwani Kata ya msamala Isaack Lutengano akipata usingizi baada ya kukesha kufanya kampeni za Uzinduzi Rasmi wa kuanza kampeni
 Mgombea Udiwani kwa Tiketi ya chama cha Mapinduzi Kata ya Msamala Manispaa ya Songea akihutubia wananchi jinsi atakavyoendeleza Kata ya Msamala ikiwa ni pamoja na Kufungua Saccos, Vituo vya Mafuta na kuunda Vikundi mbalimbali.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Msamala Filipo Shemtembo akizindua Kampeni Kata ya Msamala.

Akina Mama wakisikiliza Sera mbalimbali kutoka kwa Wagombea wakati wa Ufunguzi wa Kampeni.

Madiwani watarajiwa wa Viti Maaluma Kata ya Msamala Asia Chakwela na Hapiness Haule wakiwa wamepiga magoti huku wakiomba wafanikiwe ushindi katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Akina Mama wakisikiliza Sera mbalimbali kutoka kwa Wagombea wakati wa Ufunguzi wa Kampeni.

USALAMA BARABARANI MKOANI RUVUMA

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akiwa na Kamati ya Usalama Barabarani wakitoa elimu ya usalama Barabarani kwa watumiaji wa Barabara. Amewataka Madereva wa Pikipiki kuzingatia usalama wao kwanza kwa kuzingatia sheria zilizowekwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Ruvuma Captn Mstaafu Filipo Shemtembo.
 Mtoa Elimu ya Usalama Barabarani Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Zuberi Muya akiwasisiza Madereva wa Pikipiki kujisajili katika vijiwe vyao na kutowakimbia askari wanapowasimamisha, kufanya hivyo kunawasaidia kujiepusha na ajali na matatizo yanayowakuta ikiwa ni pamoja na kunyang`anywa pikipiki na kuuwawa. Amewashauri kutoa taarifa kwa wenzao wanapokodiwa na watu wasiowafahamu hasa nyakati za usiku au katika maeneo hatarishi.aliye kulia ni Asikari wa Usalama Barabarani Joseph Lukasi Shimba
 Madereva wa Pikipiki maarufu kama yeboyebo wa Manispaa ya Songea wakisikiliza Elimu ya Usalama Barabarani iliyotolewa wiki ya usalama barabarani katika vijiwe vya waendesha pikipiki vya Mshangano Stend, Soko Kuu na Lizaboni stend wakati wa uzinduzi wa wiki ya Usalama Barabarani Mkoani Ruvuma.
 Kamada wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amewataka Madereva Mkoani Ruvuma kutoa taarifa za kuashiria kutendewa uhalifu pindi zinapotokea kwa kumpigia simu au kumbip au kutuma ujumbe wa tafadhali nipigie ili kupewa msaada na Jeshi la Polisi. Amesema simu ya Ofisi ipo kwa ajili ya kuhudumia wananchi pindi wanapotendewa uhalifu au kumtilia mashaka ya uhalifu mahali fulani.
Madereva wa Pikipiki na Magari waliokuwa wakipokea Elimu ya Usalama Barabarani wameliomba Jeshi la Polisi kutumia busara wanapowakamata madereva kwa makosa ya barabarani wasifanye kama wana uhasama na madereva wa Pikipiki hali hiyo inawafanya madereva wa Bodaboda kutojiamini pindi wanapokutana na Askari na kuwakimbia kwa kuona ni adui kwao.  Aidha wameomba Elimu ya Usalama Barabarani iwe inatolewa mara kwa mara ili kukumbushana isisubiriwe wiki ya usama barabarani pekee kwa kuwa watumiaji wa vyombo vya moto wanaongezeka siku hadi siku ambao wanahitaji Elimu.

Wednesday, August 19, 2015

WAJUE WA GOMBEA UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUVUMA HAWA HAPA

          Madiwani wa viti malumu wakiwa katika ofisi ya Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Songea
 Mgombea jimbo la Songea kupitia Chama cha Mapinduzi akisoma Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Songea
 Mgombea Ubunge Kutoka Tunduru kupitia Chama Cha Mapinduzi Injinia Ramo Makame jimbo la Tunduru kasikazini
                                                        Mgombea kutoka jimbo la Mbinga Mjini
                           Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho Mh, Jenista Mhagama
                                                 Mgombea Ubunge Jimbo la Madaba ndugu Ngonyani

Mgombea kupitia Jimbo la Songea Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM , Leonidas Gama amewaomba wagembea kupitia ccm kuacha kumzungumzia Mtu bali wajikite katika kutangaza Sera za Chama cha Mapinduzi.
Madiwani ka katibu wa CCM Songea Mjini wamesema wako viongozi walisukumwa kilometa mbili lakini hawajaiona ikulu hivyo nguvu ya CCM ina tegemea Mungu na wana CCM  walio Imara.

Mkurugenzi wa uchaguzi Jimbo la Songea Mjini Zacharia Nachoa amewataka wagombea Jimbo la Songea kuwa makini na kauli zao katika kufanya Kampeni.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Songea Mjini amesema, historia ya Jimbo la Songea limekuwa na Ustaarabu katika chaguzi zote, hivyo anategemea kuwa wagombea watatii  na kufuata taratibu na kanuni kwa  kujinadi kwa  ustarabu bila kuleta chuki .

Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Songea Mjini Zacharia Nachoa amesema , mpaka sasa vyama vilivyochukua fomu za Ubunge ni chama cha ACT Wazalendo na CCM, ambapo upande wa CCM ni Leonidas Gama na ACT  aliye chukua fom ni  Msabila Msabila.
 Wana CCM  Wakipeana mawazo kuhusu mfumuko wa wimbi wa kisiasa jinsi gani ya kukabiliana nayo
 Mariamu Simba akitabasamu baada ya kuona chama chake cha CCM kinavyo jiamini katika Uchaguzi Mkuu
                                 Wadau  wa CCM  Wakiwa na mawazo mengi kutathimini kuhusu uchaguzi
                                                Madawani wa Viti Malumu Kupitia CCM
Nimoja ya kufurahia uongozi , Uongozi ni Karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu cha Muhimu ni Hawa Viongozi kuwa waadilifu

Saturday, August 15, 2015

RUVUMA PRESS CLUB YAPATA VIONGOZI WAPYA JEE KUSONGA MBELE KUTA KUWA NA UWEZEKANO AU TUTEGEMEE NINI WOTE TUFUATILIE


Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Andrew Kuchonjoma amewataka waandishi wa Habari kuwa na umoja katika mambo mbalimbali, pia amewataka Waandishi kujiendeleza katika Elimu.


Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma (RPC) Andrew Chatwanga amewataka Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kuimarisha Vitega Uchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha Redio pamoja na kujenga Ofisi na Nyumba za kulala wageni. Mradi wa Redio mpaka kukamilika unahitaji shilingi Milioni 25.


Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma, Ngaiwona Nkondora ameombwa na wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kuwa mvumilivu na mtulivu katika kutekeleza masuala ya klabu ya waandishi wa habari wa Ruvuma Press Club (RPC)


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Marietha Msembele amewataka waandishi wa habari kushirikiana naye katika Uongozi, hakuna kitu ambacho kiongozi peke yake anajua.


Mweka hazina Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Alpius Mchucha ameomba kupewa ushirikiano na waandishi katika kutekeleza majukumu yake.


Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Ruvuma Press Club wametakiwa kuwasukuma Viongozi wa ngazi za juu ili walete Maendeleo ndani ya Chama cha Waandishi wa habari.

Wajumbe waliochaguliwa katika Kamati ya Utendaji ni, Kassian  Nyandindi, Mpenda Mvula,Geofrey Nilahi, Joseph Mwambije na
 Mpenda Mvula kiongozi wa Kamati ya Utendaji sijui ana fikilia kupiga Mzinga Gani bora afikili e Maendeleo

Picha hiyo ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Ruvuma Press Club wakiwa na Furaha baada ya kuwapata Viongozi

Picha hiyo ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Ushirika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

                   Mwandishi Andrew Mwaiki akiwa kwenye uchaguzi jengo la ushirika songea
Mwandishi Cerencesia Kapinga ambaye alikuwa katika kamati ya Utendaji kwa hivi sasa hakugombea kutokana na Jukumu la kugombea kata ya Ndirima Litembo hapo October 25 Mwaka huu

Wednesday, August 12, 2015

MWAMBAO WA ZIWA NYASA WA ENDELEZWA KWA KUJENGA NYUMBA ZA KISASAMkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema ili kuimarisha uchumi wa Mwambao  wa  Ziwa Nyasa Serikali imeamua kujenga karakana ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza Boti kubwa na ndogo

Wilaya y Nyasa ina Vitega Uchumi vingi ikiwemo Mali asili kama Milima ya Living Stone, Ufukwe wa Ziwa Nyasa, Samaki wa Mapambo, pamoja na visiwa ambavyo vinaweza kuwa vyanzo vya Utalii.

Mkuu wa wilaya ya Nyasa Neema Malenga akiwa na Mwandishi wa Habari Judith Lugoye wakiwa mwambao wa Ziwa nyasa


Njini ya ya Mitumbwi ni hizo kafia alizo chukua huyo kijana  ambapo kama huja shiba huwezi kuendesha mtumbwi
Vifaa duni vinavyo tumika katika kuvulia Samaki katika Ziwa nyasa hapo Vijana wanatoa mtumbwi tayari kwenda kuvua

Pamoja na utengenezaji wa Zana za kisasa Wananchi wa Kijiji cha Chiulu wameiomba Serikali kutazama upya samaki waliopo katika Ziwa Nyasa, wapo samaki ambao hawakui ambao ni pamoja na Vituhi, Unjukwa, ambao hata ukiwapasua utawakuta wakiwa na mayai, hali hiyo ni kuonyesha kuwa hawezi kukua tena, kukataza kuwavua ni kurudisha nyuma uchumi wa wananachi wanaoishi kando kando ya Ziwa Nyasa.

Hebu ona mtubwi ulivyo nesa kwa nyuma huku maji yakiingia hilo ni jambo la kawaida kwa wavuvi
Ndugu yangu usikie kitu kinacho itwa mutumbwi ukingia kama una BP basi ujue kila wakati roho ita kuwa juu hebu ona hawo vijana wakiwa katikati ya ziwa
Wavuvi wa Ziwa nysaa wakijiandaa kwenda kuvua samaki kilometa hamusini kutoka nchi kavu
                                                           Mwambao wa Ziwa Nyasa
                                    Moja ya samaki wanao patikana katika Ziwa Nyasa hao ni Mbufu na Kambare
Jambo mhimu ni wewe msomaji kuji sogeza Mwambao wa Ziwa Nyasa ili ukajionee jinsi samaki hawa unao waona walivyo watamu

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akiwa amekaa kando kando ya Ziwa Nyasa kutathmini Maendeleo ya Wilaya ya Nyasa yanavyosonga mbele.

Unavyo sikia swala la Utalili ni pamoja na viongozi kutembelea ufukwe wa ziwa nyasa na kuona uwekezaji uanao fanywa na watu mbambali hapo Mkuu waWilaya ya Nyasa akikagua Maeneo sehemu ya Bio Camp Lodge iliyoko Mbambabay

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa akiwa Bio Camp Lodge akipunga upepo kuonyesha mfano kwa watu wengine katika kudumisha utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vyetu.

Hii nimoja ya karakana ya kutengenezea Maboti ya kisasa ambayo ime gh'arimiwa na Serekari ya Tanzania kwa kutoa shilingi milioni
                                                             Bio Camp Lodge Mbambaba Nyasa
                                                                  Bio Camp Lodge Mbambaba Nyasa
                                                              Bio Camp  Lodge Mbambaba Nyasa
                                                                      Bio Camp Lodge

Pamoja na kuimarisha uchumi wa Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wanahitaji Vitega Uchumi, hapo ni uwekezaji mkubwa wa nyumba za kulala wageni zilizojengwa na Watawa wa kike Masista wa Shirika la Mtakatifu Vicent juu ya Mlima wa Mbamba Bay.


Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema pamoja na ujenzi huo Serikali inatayarisha majokofu ili wavuvi wawe na sehemu ya kuweka Samaki waliovuliwa lwakati wakisubiri bei nzuri kuliko kuwasukuma kwa bei ndogo.Wavvi katika Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema pamoja na kukosa Samaki lakini changamoto nyingine ni pamoja na kukabili kuchomewa Nyavu mara kwa mara.na  Afisa  Uvuvi wakidai kuwa ni nyavu ndogo jambo linalosababisha kuwaacha wavuvi katika hali ya umaskini.Wananchi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa wilayani Nyasa wameiomba Serikali kuwasaidia Zana Bora za Uvuvi ili kusaidia na kuepusha vifo vinavyotokea baada ya kukosa Zana Bora.
         Wananchi hao wameyasema hayo wakati walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari kuhusu kuporomoka kwa uvuvi katika Ziwa Nyasa kwa kupata Tani moja za Samaki wakati walikuwa na uwezo wa kupata Tani zaidi ya tatu.

Karakana ya Kutengeneza Boti za Kisasa imejianda kwa kuweza kununua Genereta za kuweza kusaidia endapo umeme uta katika
Hiyo ni garama ya Vitu utakavyo taka kuvitumia hapo Bio Camp kwa kweli pame pendeza  Bio Camp Lodge

Vitega Uchumi kwa ajili ya Watalii, Nyumba unazoziona hapo ni Nyumba za kulala wageni ambazo zinajulikana kwa jina la Bio Camp Lodge Mbamba Bay  yenye vyumba zaidi ya 40 na maeneo mengi ya kupumzika na kuburudika na michezo mbalimbali ikiwemo na ngoma za asili.
                                                                               Bio Camp Lodge
Umeme unao tumika hapa unategemea Kinyesi cha Wanyama hivyo umeme haukatiki muda wote njoo uone Bayo Gess inavvyo fanya kazi
Picha hizo zote ni kukufanya Msomaji uone hali halisi ya Bio Camo Mbambabay
Uezekaji wa Nyumba hizi ume tumika zaidi Nyasi hivyo pamoja Wilaya ya Nyasa kuna Joto lakini eneo hili ni Baridi kwenda Mbele kwa kweli Mbambabay Imependeza
Mwandishi wa Habari Judith Lugoye ambaye aliweza kubahatika kulala hapo amesema ukilala hapo ndoto unazo ota ni za kimaendeleo tu utajiri una kuwa mikononi mwako
Nyumba vilivyopo vina jitegemea kila nyumba ni chumba kimoja ,hiyo nihali halisi ya Bio Camp
Bio Camp ina jali afya za wateja wake chandarua unacho kiona mbuu akisogea mita moja tu kutoka kwenye chandarua basi ujue mauti yata mkuta hayo yote yanafanywa kulinda afya ya mteja
Mambo haya tulizoa kuya ona Ulaya lakini kitanda unacho kiona kipo Mbambabay kwenye Bio Camp ukifika huko utaona vitu tofauti na jinsi unavyo fikili maendeleo yaliyoko ni kama miujiza
Utalii unanda na Familia hapo Mkurugenzi wa Bio Camp akiwa na familia yake kuangalia Maadhari ya  Camp hiyo
Pamoja na Kuangalia Maendeleo ya wilaya ya Nyasa ni pamoja na kuhusisha wagombea wa kisiasa ona walio gombea majina yamepagwa kutokana na matokeo ya kura za maoni


Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema pamoja na ujenzi huo Serikali inatayarisha majokofu ili wavuvi wawe na sehemu ya kuweka Samaki waliovuliwa lwakati wakisubiri bei nzuri kuliko kuwasukuma kwa bei ndogo.