KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, September 26, 2015

KUNING'INIZA MABANGO KWENYE NYAYA ZA UMEME NI HATARI KWA MAISHA SONGEA


Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Rafaeli Malini ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kwa sasa katika Manispaa ya Songea Vyama vya Kisiasa vimekuwa vikipachika Mabango kwenye Nyaya za Umeme, simu na Nyumba za watu ambapo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


Kampeni za Uchaguzi Mkoa wa Ruvuma zinaendelea kwa kishindo kila Chama kikiwa na uhakika wa kushinda Oktoba 25.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Rafaeli Malini amesema amejaribu kuwasiliana na Vyama vya Siasa kuwa aqmbia wanachama wao  kuacha kubandika Mabango bila idhini ya watu wanaomiliki katika maeneo hayo pia kuacha kuning’iniza mabango  katika nyaya za umeme

Mratibu wa CHADEMA Kanda ya Kusini Frank Mwaisumba amewaomba Viongozi wa Serikali za Mitaa mahali walipo kusimamia na kukemea kwa mtu yeyote atakayeonekana akibandika Mabango katika sehemu zisizohusika, Vijana wamewahimiza Vijana wenzao kuacha tabia ya kuhatarisha maisha yao kwa kuweka Mabango kwenye Nyaya za Umeme


Wananchi wa Manispaa ya Songea wametakiwa kuacha mambo ambayo yanaweza kuwafanya wapoteze maisha ikiwa ni pamoja na kupachika mabango kwenye nyaya za umeme.


Katibu wa Uwt Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja amesema kuning`iniza Mabango na kuchana Mabango ya Vyama vya siasa ni kinyume cha Sheria.


Kaimu Meneja wa TANESCO Haruna Mwachula akiongea kwa njia ya simu amesema kutundika Mabango kwenye Nyaya za Umeme ni kulihujumu Shirika la TANESCO na kulikosesha mapato. Pia ni kuhatarisha Maisha kwa wanao tundika na wapiti njia.

Friday, September 11, 2015

MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA CHADEMA MH. JOSEPH LUSIUS FUIME AMESMA SHABAHA YAKE KUBWA NI KUONDOA KERO ZA WANAWAKE NA WATOTO KATIKA HOSIPITALI YA MKOA RUVUMAMgombea Urais kupitia Ukawa  mh Edward Lowasa akiwa mkoani Ruvuma amesema endapo wana Ruvuma wata mpa ridhaa ya kuingoza nchi atahakisha madini yaliyoko nchini tanzani ya nawanufaisha wa tanzani kwa kupata ajira kutokana na rasilimali za madini

Mgombea Uraisi kupitia Ukawa  akiwa viwanja vya Matarawe Mkoani Ruvuma amesema wawekezaji watatakiwa kujipanga upya kwa kuwa sekita ya madini itapaswa iwe ndiyo mkombozi kwa vijana kwa kuwapa ajira,haita wezekana vijana wakose ajira wakati furusa zikiwa nyingi

Mheshimiwa Edward Lowasa akihutubia katika viwanja vya Matarawe Mkoani Ruvuma  amesema  Mikataba ya uchimbaji wa madini aina zote endapo  wananchi watamweka madarakani mikataba yote ita chunguzwa upya ili mikataba hiyo iwe na faida kwa wanchi na siyo vinginevo


Mgombea Ubunge kupitia cha cha chadema Joseph Fuime amesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge Jimbo la Songea ata hakikisha hospitai ya Mkoa ina jengwa upya ili iweze kukidhi changamoto zinazo wakumba wanawake waja wazito na WatotoThursday, September 10, 2015

VILOBA 17 VYA BANGI VYAKAMATWA NA JESHI LA POLICE SONGEA


Jeshi la Police Mkoani Ruvuma limefanikiwa kukamata Magunia 17 ya Bangi yakiwa na Uzito wa kilo 340. 

 Bangi iliyokamatwa ikiwa imepekiwa kwenye viloba kama inavyoonekana.

Kaimu Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma  Revocatus Malimi  amesema amesema Magunia hayo ya Bangi yamekamatwa katika Kata ya Subira yakiwa kwenye Gari lenye namba za usajili T588 BBJ ambapo Dereva wa Gari hilo na wenye mizigo walilitelekeza gari hilo.

Kaimu Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi  amesema baada ya kupata taarifa kwa Wasamaria wema walitoa tarifa ya kusafirisha bangi iliyo geuzwa kuwa ni Mahindi ,Mpunga  na Mkaa kumbe katikati ya Mpunga na Mahindi viliwekwa viroba 17 vya bangi kama anavyo eleza kaimu kamanda wa police Said Mohamed 
 Viloba vya Bangi ambavyo vilihifadhiwa katikati ya viloba vya Mahindi na Mpunga ili kuonyesha wenye mzigo walikuwa wakisafirisha mazao.
 Bangi ikiwa imefikishwa kituo kikuu cha Police Mkoa wa Ruvuma baada ya kukamatwa.
 Namba za Gari iliyokuwa ikisafirisha Mzigo huo wa Madawa ya kulevya aina ya Bangi,
 Bangi Iliyovunwa na kujazwa kwenye viloba ambayo ilihifadhiwa kwa ustadi mkubwa lakini Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limefanikiwa kuinasa Bangi hiyo.
        Viloba 17 vya Bangi iliyokamatwa kata ya Subira Manispaa ya Songea vikiwa vimepangwa pamoja.
 Pamoja na Serikali kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uzalishaji, wako watu wanalima kwa wingi na kugeuza kama zao la biashara kwao katika kujinasua na umaskini, shehena za viloba vinavyoonekana hapo juu ni mali ghafi ya madawa ya kulevya ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda kutafuta soko.

Kaimu Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi  amesema Jeshi la Police Mkoa wa Ruvuma wanamshikilia mwenye Gari  aina ya Fusso lenye namba za usajili T. 588 BBJ  Said Mohamed  kwa mahojiano . Bangi hiyo inasadikiwa  ili kuwa ikipelekwa mikoa jirani  . Kaimu Kamanda wa Police ameomba yeyote  mwenye taarifa za Uhalifu atoe taarifa Police.

 Police kwa kushirikiana na Wananchi wataweza kupunguza uhalifu wa watanzania, wanachoomba ni ushirikiano wa raia pindi viashiria vya uhalifu vinapotokea.
 Kaimu Kamanda wa police Mkoa wa Ruvuma Revocatus Malimi akitoa ufafanuzi wa jinsi walivyoikamata Bangi hiyo.
                                                                  Bangi.

Sunday, September 6, 2015

UMATI WA WATU UWANJA WA MAJIMAJI SONGEA NA STAR TV LIVE

Umati wawatu ulio kusanyika mkoani Ruvuma kumsikiliza mgombea urais John Pombe Joseph  Magufuli
Moja ya faida wanayo ipata wanchi kufurahia vyombo vya habari ni kupata matangazo mbalimbali yanayo husu Maendeleo. Hapo mtambo wa Star Tv ukitoa live kampeni ya kugombea Urais kupitia CCM
                 Fundi Mitambo Goerge kutoka Star Tv akiendelea kurekebisha Mitambo
            Wananchi Mkoani Ruvuma wakingojea mgombea urais kupitia CCM
                                                                                     Ruvuma na CCM
Msimamizi wa matangazo ya Star Tv Victer Chacha  aliye vaa miwani akirekebisha Mtambo wa kurushia Matangazowa Star Tv kuhakisha Matangazo yana enda Vizuri
Mtalamu ambaye ni fundi mitambo Goerge akifanya juhudi kuhakisha nmitambo ya kurushia TV Ina wafikia watazamaji
Maendeleo ni moja ya vitu vinavyo tegemewa kuonwa na wanchi  Gari hilo unalo liona ni Gali la kisasa lina mitambo ya kuweza kuonyesha picha  za video .pia ni jukwaa la kisasa
                                                                  Gari hilo ni mafanikio ya
                                                                                Mitambo ya Star Tv

BAJAJI MKOANI RUVUMA YA SABABISHA KUCHELEWESHA KWA MAZISHI BAADA YA KULIGONGA GARI LILILO BEBA JENEZA KWA AJILI YA MSIBA

 Pikipiki aina ya Bajaji ikiwa imepinduka baada ya kugongana na gari lililo beba geneza la msiba maeneo ya Shule ya Tanga Manspaa ya Songea.Cha ajabu ni kuwa Dereva anaomba wamalizane ingekuwa kosa ni la Dereva wa Gari ,Gari hilo linge chomwa moto.
 Wasamalia wema wakisaidi kuokota vitu  vilivyo vilivyo kuwa kwenye Bajaji ikiwemo kochi
 Jeneneza lililo kwenye gari lilisababisha msiba uchelewe kuzikwa baada ya kukutana na adha ya kugongwa
Katika wiki ya usalama barabarani Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela aliwataka madereva kuwa makini lakini kwa madereva wa Pikipiki imekuwa kinyume ,Madereva wa Pikipiki wamekuwa chanzo cha Ajali Nyingi Nchini Tanzania

WAZEE WANAWAKE WAOMBA MALIPO KWA AJILI YA UZAZI MKOANI RUVUMA

 Mwandishi wa Habari wa PST  Gidioni Mwakanosiya akiwakilisha katika kikao cha PAID
 Katibu wa Wawazee Joseph Mpangala akiwa katika kikao na Wandishi wa Habari kusisitiza pesheni kwa Wazee itolewe Haraka
 Mosses Konara akiwa katika kikao cha Wazee kinacho fadhiliwa na PAID Mkoani Ruvuma

Wanawake hao wazee wakiongea  katika Mkutano uliofanywa kati yao na waandishi wa Habari  na wazee wamesema, hakuna kazi kubwa hapa duniani kama kuzaa, kuzaa kunampa hali ya hatari Mwanamke  kupoteza Maisha. Asilimia 50% ya wanawake wanao poteza maisha hapa duniani  kutokana na uzazi.Aliye juu ni Mwenyekiti wa Mkutano huo Cresencia Kapinga

                                             Mwandishi wa Jogoo FM  Songea Adeni Mbele
                  Mwandishi wa TBC Raufu Mohamed akiwa PAID Unangwa Songea
                       Mzee ambaye anatetea haki za Wazee kuweza kupata Pesheni
 Mkiwa miliki wa Blog ya Songea Habari ,Ndigu Adamu Mzuza Nindi akiwa kwenye kikao cha wazee PAID  kusikiliza malalamiko ya wazee,
            Amoni Mtega wa Gazeti la Mtanzania akifikili jinsi ya kuwa saidia Wazee Mkoani Ruvuma

Wanawakew wazee wakiongea kwa uchungu wamesema vijana hivi sasa wanawaona wazee kama mzigo hawana njia nyingine ya kuwa toa duniani ni kuwasingizia kuwa ni Wachawi jambo liunalo pelekea waganga ambao wamesha waandaa kutoa dawa zinazo sadikiwa ni sumu  
Wanawake hao wazee wakiongea  katika Mkutano uliofanywa kati yao na waandishi wa Habari  na wazee wamesema, hakuna kazi kubwa hapa duniani kama kuzaa, kuzaa kunampa hali ya hatari Mwanamke  kupoteza Maisha. Asilimia 50% ya wanawake wanao poteza maisha hapa duniani  kutokana na uzazi.

Kuuwawa kwa wazee katika maeneo mbaimbali nchini  Tanzania kunatokana na vijana kuwa na hofu ya kutoweza kuwatunza  Wazee   na kusingizia kuwa ni Wachawi kwa kigezo cha kuwa na Macho mekundu.
Hayo yamebainika katika kikao kati ya wazee na wandishi wa habali wa Mkoa wa Ruvuma walipo kuwa wakijadili kuuwa kwa wazee kunako tokea katika kata Lilambo Mkoani Ruvuma  ambako wazee wamekuwa wakinyeshwa dawa inayo sadikiwa ina sumu na mara baada ya kunyweshwa hupoteza maisha.


Makamu Mwenyekiti wa Baraza Huru la Wazee manispaa ya Songea Sophia Hasara amesema Serikali baki ya kutoa Pensheni kwa Wazee wote, kwanza ingejumlisha kwa wanawake waliozaa kuwapa pensheni ya uzazi, pili kwa wazee wote wapate Pensheni.
    wanawake Wazee wa mkoa wa Ruvuma wamesema Serikali haitendi haki kwa kutolipa Pensheni kwa Wazee, wanawake ambao ndio nguvu kazi ya kuongeza watu katika Nchi.