KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, December 12, 2015

SIKU KUMI NA SITA ZA UKATILI WA KIJINSIA MKOANI RUVUMA

 Siku kumi na sita za kupinga Ukatili wa Kijinsia mwaka 2015 Mkoa wa Ruvuma umeadhimisha kwa kutembelea makundi maalumu kama vituo vya kulelea watoto yatima, magereza na wazee wanaoishi katika mazingira hatarishi. Pichani ni Maandamano ya wadau siku ya kilele cha maadhimisho ya kupinga Ukatili wa Kijinsia Mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya Akimshaukuru Mwakilishi wa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Madini ya MANTRAS URENIUM katika kilele cha siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mkuu wa wilaya ya Songea katika Maadhimisho hayo amewaomba watu wa Migodi ya Madini kuzihudumia Jamii za Maeneo wanayofanya shughuli za uchimbaji wa Madini Mkoani Ruvuma.

 Maandamano yakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya sherehe za siku kumi na sita za kupinga ukatili wa Kijinsia Mkoani Ruvuma Bw. Renatus  Mkude akiwa na wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea viwanja vya Mashujaa wa Vita vya Majimaji Mahenge Manispaa ya Songea
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya amemuomba kurugenzi wa Kampuni ya MANTRAS  URAN inayochimba madini ya URENIUM wilayani Namtumba kuangalia uwezekano wa kuwapatia usafiri Dawati la jinsia la Polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma ili uweze kuwarahisishia katika kufuatilia masuala ya ukatili wa kijinsia.
 Kampuni ya URAN MANTRAS imehaidi kulichangia dawati la kijinsia Mkoa wa Ruvuma vifaa vya ofisi na vitendea kazivyenye thamani ya shil;ingi Milioni 12 .8 katika kuunga mkono mapambano dhidi ya ukatili wa Kijinsia. Pichani ni Mgeni Rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto Bi Khadija Pallangyo ambaye amemwakilisha Makamu wa Rais wa Kampuni ya MANTRA
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa Kijinsia Mkoani Ruvuma akipongezwa na Bibi Magret Ponela mmoja kati ya watu wanaoishi katika mazingira hatarishi ambao walitembelewa na wajumbe wa kamati ndani ya siku 16 nyumbani kwake Peramiho na kupewa zawadi za mahitaji ya chakula na mavazi vyenye thamani ya shilingi laki tatu. Pichani ni Bibi Magret akiwa amebeba zawadi ya Pamba kuikabidhi kamati ya sherehe shukrani kwa kumuona na kumsaidia mahitaji.

Mwenyekiti wa kamati ya sherehe za siku kumi na sita za kupinga ukatili wa jinsia na watoto mwaka 2015 Wakili wa Serikali Renatus Mkude ameweza kukusanya zaidi ya shilingi milioni 30 ikiwa nifedha taslimu na ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali katika kupambana na wimbi la ukatili dhidi ya mama na mtoto.
 Mgeni Rasmi Khadija Pallangyo akimkabidhi Bibi Magret kitoweo ili akapate supu.
 Mwenyekiti wa Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto ASP Ana Tembo amewataka wadau kushirikiana kwapamoja klatika kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia pindi vinapotokea katika jamii.
Kampuni ya MANTRAS imeomba kushirikishwa masuala ya maendeleo ya jamii ya mkoa wa Ruvuma watashirikiana. Mwakilishi wa Makamu wa Rais wa Kampuni ya MANTRAS  Khadija Pallangyo akisoma hotuba
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya akipokelewa na Wajumbewa kamati ya Maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijionsia katika viwanja vya Mashujaa Mahenge, kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya sherehe Renatus Mkude.

 Mgeni Rasmi Khadija Pallangyo akikagua kikundi cha ngoma ya lizombe wakati akiingia viwanja vya mashujaa Mahenge katika kilele cha Maadhimisho ya siku kuminasita za kupinga ukatili wa kijinsia.
 Mwakilishi wa Kampuni ya MANTRAS Tanzania amewataka wadau kuzingatia elimu kwa watoto na kuchana na vitendo vya kuwafanyia ukatili watoto kwani kufanya hivyo ni kuwajenga kisaikolojia katika ukatili na pindi wanapokuwa na wao wanarithi ukatili.
 Wajumbe wa Kamati ya Maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa jinsia.
 Katibu wa Kamati ya maadhimisho ya siku kuminasita za kupinga ukatili wa jinsia mkoani ruvuma kulia akitafakari kwa makini ujumbe wa wasanii wa ngoma ya lizombe juu ya vitendo vya ukatili wa jinsia.

 Kauli mbiu ya siku kumina sita za kupinga ukatili wa jinsia mwaka huu ni Funguka Mlinde Mtoto apate Elimu. Ni wajibu wa kila mmoja kuwa mlinzi wa vitendo vya ukatili wa jinsia na kuvikemea.

 Wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia mkoani ruvuma wamelaani vitendo vya wazazi wanapotofautiana kukimbilia kudhuru watoto kwa kuwaua na kujiua wenyewe ambavyo vimetokea hivi karibuni mkoani hapa mzazi kuwaua watoto na mke na baadae mwenyewe kujikata koromeo na kunusurika kufa kutokana na masuala ya wivu wa kimapenzi.
 Mwenyekiti wa Dawati la polisi wanawake Mkoa wa Ruvuma ASP Ana Tembo
Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya katika viwanja vya Mashujaa Mahenge

1 comment:

  1. Taarifa na picha nzuri. Huku ughaibuni niliko, nami ni mwenyeji wa Ruvuma (Litembo), zinanikumbusha nyumbani. Shukrani kwa kazi nzuri. Huyu dada mwenye miwani, shati jeupe na koti jeusi, anayetoa hotuba, namwona kama binti mojawapo wa mzee wetu Rashidi Kawawa, Simba wa Vita. Au macho yangu?

    ReplyDelete