KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, June 28, 2015

SIKU YA MKULIMA AMANI LUDEWA YA PATA MAFANIKIO

Mradi wa Majaribio wa Kilimo Hifadhi wilayani Rudewa umetekelezwa kwa awamu ya kwanza katika Vijiji 10 vya wilaya Ludewa Mkoani Njombe katika kuhakikisha Kilimo kinamnufaisha Mkulima na kumletea tija. Shirika la ACTN kwa kushirikiana na mashirika ya Brigten, RUDI, AGRA na CRDB Banki wanaendesha  elimu elekezi ya kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa chenye tija. Pichani ni moja ya Mashamba darasa lililopo Kijiji cha Amani Wilayani Rudewa.
Mawakala wa mbegu wakitoa Elimu ya Matumizi sahihi ya upandaji wa mbegu bora katika sherehe za siku ya Mkulima zilizofanyika Kijiji cha Amani Kata ya Amani Wilayani Rudewa Mkoani Njombe.
Afisa Miradi wa Shirika la ACTN Tanzania Deogratias Ngotio katikati akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mr Naftali Mundo ambaye ni Afisa kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Ludewa (kulia)  na kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Kilimo Hifadhi kutoka Shirika la ACTN Abiud Gamba wakiwa katika sherehe za Siku ya mkulima zilizofanyika Kijiji cha Amani Wilayani Rudewa chini ya utekelezaji wa majaribia ya mashamba darasa kutoka katika Vijiji 10 vya wilaya ya Ludewa.
Mmiliki wa Shamba Darasa lililopo kijiji cha Amani Bw. Kastory Hotman Mlelwa akifurahia Mabadiliko ya uzalishaji wa zao la Mahindi baada ya Kupata Elimu ya Kilimo hifadhi toka kwa Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo Hifadhi yakiongozwa na Shirika la ACTN. Amasema Elimu ya Kilimo hifadhi ni nzuri kwa kuwa inapunguza gharama za vibarua kwa muda mfupi na upatikanaji wa mazao unakuwa wenye tija.
Bw. Emmanuel Christopher Mwakibala ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Dawa za kuua Magugu aina ya SYNGENTA , Primagram Gold akitoa Elimu ya matumizi sahihi ya dawa ya kuondoa magugu shambani kwa wakulima wa Wilaya ya Ludewa siku ya sherehe ya siku ya wakulima iliyofanyika Kijiji cha Amani na kujionea matokeo ya uzalishaji baada ya kupata elimu ya Kilimo Bora.
Wakulima wa Wilaya ya Ludewa wametoa ushuhuda wa faida wanayoipata baada ya kupata Elimu ya Kilimo hifadhi na Urutubishaji wa udongo wameongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutoka Majunia 5 hadi 7 waliyokuwa wakiyapata wakati wakilima kilimo cha mazoea na sasa ambapo wanapata gunia 15 hadi 25 kwa kufuata Elimu ya Kilimo Hifadhi.
Wakulima wa Ludewa wameyaomba Mashirika yanayoendesha Elimu ya kilimo Hifadhi na ya pembejeo za Kilimo kupanua wigo wa usambazaji wa elimu ya Kilimo Bora chenye tija ili iweze kuwafikia wakulima wengi kwa kuwa Kilimo ndiyo uti wa Mgongo wa Tanzania ambacho kinaajiri watu wengi hivyo elimu hii ikiwafikia wengi taifa litaepukana na umaskini.
.
Wakulima wa Vijiji vya Amani, Mkongobaki, Mavanga, Mundindi na vijiji vingine vya wilaya ya Ludewa wakiwa katika sherehe za siku ya Mkulima Kijiji cha Amani wameiomba serikali kusimamia suala la masoko ya mazao wanayozalisha ili wapate faida kupitia kilimo chao.
Wakulima wa Ludewa wameomba kutafutiwa masoko ya uhakika ili waongeze bidii wakiwa na imani ya uhakika wa kuuza mazao yao kulingana na kauli mbiu ya Kilimo kwanza, wamesema mwaka jana waliyumba katika masoko ambapo uzalishaji ulikuwa mkubwa lakini tatizo lilikuwa upande wa masoko.
Wakulima waliopata Elimu ya Kilimo Hifadhi kutoka wilaya ya Ludewa wamefurahishwa na elimu ya kilimo hifadhi wameomba kwa wale wanaohusika na usmbazaji wa pembejeo kuwafikishia pembejeo za kilimo kwa wakati ili kuendana na misimu ya Kilimo.
Shamba darasa la Kilimo hifadhi lililopo Kijiji cha Amani Wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe.
Wakulima kupitia Risala yao wameiomba Serikali kusimamia taasisi za Benki ili kukubali kupitisha fedha za rudhuku ya pembejeo za Kilimo kuzipitisha kwenye Benki zao ili wakulima wasihangaike.
Mawakala wa Pembejeo za Kilimo na mwakilishi wa Mviwata Mkoa wa njombe wakiwa katika ghafla ya siku ya wakulima kijiji cha Amani wilayani Ludewa.
Mgeni Rasmi katika sherehe za siku ya Mkulima Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wilaya ya Ludewa Mr Naftali Mundo akimpongeza Msoma Risala kwa niaba ya Wakulima wa Wilaya ya Ludewa. Kushoto ni Afisa Miradi kutoka Shirika la ACTN Tanzania Bw. Deogratias Ngotio.
Wawakilishi kutoka Mashirika yanayounda Mtandao wa Kilimo Hifadhi ya ACTN


 Wakulima wa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wamefanikiwa kuzalisha Mazao ya Mahindi baada ya kupata Elimu ya Kilimo Hifadhi ambapo kwa Ekari hivi sasa hupata Magunia 25 na kuendelea.
           Wakulima hao wamesema baada ya kuachana na Kilimo cha Mazao ambapo walikuwa wakipata gunia 3 – 7 lakini hivi sasa wanaweza kuzalisha Mahindi kwa uwingi na kuweza kujikwamua kiuchumi na kuweza kujenga, kusomesha na kumudu gharama za matibabu kwa familia.



Mwaka 2014 -2015  Wakulima wa Wilaya ya Ludewa wameshindwa kufikia lengo la kulima  mazao ya chakula kwa wingi  kutokana na Mabenki kujitoa kutopokea Ruzuku ya kilimo kutoka Serikalini na kutegemea benki moja  ya Wananchi ya Njombe ambayo ilitoa kiasi cha shilingi milioni 50 tu kiasi ambacho hakikutosheleza.

Afisa Miradi kutoka shirika la ACTN Tanzani Deogratias Ngotio akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mr. Naftali Mundo wakati wa sherehe za siku ya mkulima Amani kukagua matokeo ya majaribi ya Mashamba Darasa kwa kutumia Elimu ya Kilimo hifadhi chini ya shirika la ACTN.
Bi. Mwantumu Omary  Kutoka shirika la utafiti ka Kilimo la IITA akitoa Elimu ya Matumizi Bora ya Ardhi katika Kilimo kwa wakulima wa Wilaya ya Ludewa.

 Kaimu Mkurugenzi wa Ludewa  Naftali Mundo  amewaomba wakulima kuunda ushirika ili waweze kuwafikiwa  na Wataalamu waweze  kutoa Elimu ya Kilimo Hifadhi kwa Wakulima wengi
Mwakilishi wa Kampuni ya SYNGENTA inayotoa dawa za kuuwa magugu  Prigram Gold Bw. Emmanuel Christopher Mwakibala amewataka wakulima kuzingati Elimu ya matumizi ya Pembejeo za Kilimo kwa kuzingatia wakati mwafaka na matumizi sahihi ili kuona tija.

Wednesday, June 17, 2015

ZIARA YA VIONGOZI WA UWT MKOA WA RUVUMA KUTEMBELEA MABARAZA YA WILAYA KUTOA HAMASA KWA WANAWAKE KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI

Wananchi wa Kijiji cha Majimaji Kata mpya ya Majimaji Wilayani Tunduru wakisikiliza kwa makini ujumbe walioletewa na viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma wakati wa Ziara ya kutembelea Mabaraza ya UWT kwenye wilaya za Mkoa wa Ruvuma iliyolenga kuwahamasisha akina mama kutoogopa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi.
Wananchi wa Kata ya Majimaji wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wakieleza kero zao kwa viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Mkoa wa Ruvuma  wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kusahauliwa katika fursa mbalimbali zinapotokea mkoani ikiwemo miradi ya TASAFU ya kaya Maskini.
Wananchi wa Kata ya Majimaji wakiwa katika Mkutano wa hadhara wakati wa Ziara ya Mwenyekiti na Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma.
Wazee wa Wilaya ya Tunduru wakiwa katika Mkutano wa Hadhara na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu muhagama katika viwanja vya Baraza la Idi mjini Tunduru.
Kijana Msanii mwenye kipaji cha uimbaji wa nyimbo za muziki wa HIP HAP Juma Selemani kutoka kijiji cha Mnenje Kata ya Majimaji  mwenye micro phone masikioni mara baada ya kutumbuiza.
Washereheshaji wa Mkutano wa hadhara wakitumbuiza katika mkutano wa hadha uliofanyika kijiji cha Majimaji Kata ya Majimaji Mkoani Ruvuma. Watoto wa kike wanaaswa kuzingatia masomo.
Wilaya za Tunduru na Namtumbo ndizo zinazoongoza kwa kushuka kiwango cha Elimu kutokana na Tatizo la Mimba za Utotoni zinazosababisha watoto wengi kukatiza masomo.
Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja akihutubia wananchi wa Wilaya ya Tunduru, amewaomba wana CCM kudumisha upendo kwa wapinzani ili waweze kuwashawishi kurudi CCM, amesema Mpinzani asigeuzwe adui awe rafiki wa karibu itasaidia kujua hali ikoje. Amesema pia wana CCM waache tabia ya kuwa ukimuona mwana CCM amesimama na mpinzani basi naye anatuhumiwa kuwa ni Mpinzani.

Wajumbe Ukumbini Baraza la UWT Tunduru.
Wajumbe wa Baraza la UWT wilaya ya Tunduru wakiwa ukumbini katika mkutano wa Baraza la UWT walipotembelewa na Viongozi wa Jumuiya hiyo kutoka Mkoani.
Mwaasisi wa UWT Wilaya ya Tunduru Bibi Husna Makanji amewaomba wakina mama wa UWT kuilea Jumuiya ya UWT na kuilinda kwa kudumisha umoja na mshikamano, waache malumbano yasiyo na faida  yataifanya kuiua Jumuia badala ya kuiendelea. Amesema katika Jumuiya za chama cha Mapinduzi jumuiaya ya akina mama ndiyo Msingi wa Chama ikiyumba jumuiya hiyo chama hakiwezi kwenda vizuri.
Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Tunduru wakiwa katika Ukumbi wa UWT wilaya ya Tunduru.
Mbunge wa Jimbo la Tunduru kaskazini Eng Ramo Makani amesema ni jukumu la wananchi kuwapima wagombea kwa yale waliyoyafanya na sera zao kuangalia ukweli uko wapi, wasichague kwa ushabiki.Amesema akina mama ndio Jeshi linalotegemewa katika kutengeneza Dola wanapaswa kuwa makini na wagombea wanaojitokeza.
Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Tunduru Mariam Msongela akiwa na Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamedi Masanja nje ya ofisi za UWT wilaya ya Tunduru wakati wa ziara ya kikazi ya viongozi wa Jumuiya ya UWT Mkoa kutembelea Mabaraza ya Wilaya.
Pamoja na yote pia wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura wakati ukifika wasiuze shahada watimize haki ya msingi ya kikatiba.
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Eng Ramo Makani akiwa Ofisini kwake Jimboni Tunduru.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu muhagama amewatahadharisha wanawake kuwa makini katika kuchagua viongozi waadilifu wakati ukifika wa uchaguzi wa Wabunge na Madiwani mwezi Oktoba.  Amesema ni vizuri kumchagua mtu atakayewasaidia wananchi, mwenye kushiriki katika kutatua matatizo ya waliomchagua.
Wanachama wa UWT Mkoa wa Ruvuma wakifurahia elimu ya Ujasiliamali katika Kikao cha Baraza la kawaida cha Viongozi wa UWT Wilaya ya Namtumbo na Uongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma. Kulia ni Diwani wa Viti Maalum Remina Nchimbi.
Mjumbe wa UWT Taifa na Mjumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma Doto Nyirenda akitoa Elimu ya Ujasiliamali kwa akina Mama wa UWT Wilaya ya Namtumbo. Amesema wakati umefika sasa ni lazima siasa zetu ziendane na uchumi kujikwamua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Chama cha Mapinduzi na katika Halmashauri zetu.
Amesema wakina mama wakifanya hivyo kwa kubuni miradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi itasaidia kuongeza wigo wa soko la ajira, ujasiliamali unapunguza tatizo la ajira.
Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wamehaidi kukipa ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi ujao.


Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Mohamed Masanja amesema utakuta Idadi ya wanawake katika Maeneo mbalimbali ni kubwa kuliko wanaume, lakini wanapogombea uongozi wanaume hutia fitina ambayo inawafanya wanawake wasimchague mwenzao tabia ambayo si njema iachwe  mara moja ili na wanawake wapate fursa ya kushika hatamu ya uongozi katika ngazi mbalimbali .

Katika  ziara hiyo ya viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma kikubwa wanawaasa wanawake kupendana na kuchaguana popote anaposimama mwanamke kugombea wengine wawe mstari wa mbele kumuunga mkono mwanamke mwenzao.
Nao Vijana wa UVCM kupitia vyuo vikuu wamewasisitiza wanawake kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kwa kuwasomesha watoto wao ili waje kuwa viongozi wa Ngazi za Juu, wamesema Mkoa wa Ruvuma ni Miongoni mwa mikoa yenye bahati ya kupata viongozi mahiri wanaosimamia ipasavyo Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha Maendeleo yanapatikana Mkoani Ruvuma.

Wanasema Ruvuma hivi sasa kuna Vyuo vikuu Vivyopungua vitatu lakini itashangaza kuona wengi wanaosoma katika vyuo hivyo ni waja ambao si wazaliwa wa Mkoa huo ni wajibu wa Jumuia ya UWT kwa kushirikiana na wadau wengine wa Elimu mkoani hapa kutoa msukumo wa vijana wao kupenda kujiendeleza kielimu. (Picha hiyo juu ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Ruhuwiko Songea)
Viongozi wa UWT wilaya ya Namtumbo, kulia mwenye kitenge ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Namtumbo Bi Maria Hamisi Kapinga.

Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Masanja amewataka wanaume kuwaunga mkono wanawake wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kuwachonganisha ili wasielewane na kushindwa kuwachagua wanawake wenzao katika Uongozi.



Katibu wa UWT Mkoa wa Ruvuma Chiku Masanja ameyasema hayo akiwa katika Baraza la UWT wilaya ya Songea Vijijini wakati wa Ziara ya kuzungukia Mabaraza ya Wanawake wa UWT katika wilaya zake tano.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Kuruthumu Muhagama amesisitiza Jamii kuacha tabia ya kuwaoza watoto katika umri mdogo kufanya hivyo ni kuwanyima haki ya kupata elimu.


Ziara ya Viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma imelenga kuwapa hamasa wanawake kugombea katika viti mbalimbali kuanzia mitaa hadi Taifa .Pamoja na kutoa elimu ya ujasilia mali  il wanawake waji kwamue katika umasikini  .

Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph Computer Enginiaring ambao pia ni wanachama wa UV CCM wakiwa katika kikao cha Baraza la UWT wilaya ya Songea Vijijini.
Katibu wa UWT Wilaya ya Songea Vijijini Selina Ngonyani akiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Mama Nguluse uliopo viwanja vya Nane nane Mjini Songea muda mfupi kabla ya kuanza Baraza la UWT wilaya ya Songea Vijijini
Wajumbe wa UWT wilaya ya Songea vijijini wakiwa katika Mkutano wa Baraza la UWT wilaya walipotembelewa na viongozi wa UWT Mkoa wa Ruvuma.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma, Kuruthumu Muhagama amewataka wanawake kushawishi jamii ili iweze kuwasomesha wanawake, mtoto wa kike akielimika anaweza kuwa mkombozi katika familia. Ameyasema hayo wakati akiwa ziarani wilayani Tunduru katika kutembelea mabaraza ya UWT wilaya za Mkoa wa Ruvuma.