KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, February 28, 2016

BRIGEDIA WA KANDA YA KUSINI KIKOSI CHA TEMBO 401 ASHIRIKI USAFI SONGEAMkuu wa Mkoa akiwa pongeza wana Ruvuma amesema dalili ya kuzingatia usafi ni pale unapo ona Kipindu pindu  hakija ingia mkoani mwako jambo mhimu ni kila mwananchi kuhakikisha taka anazo zizalisha zina wekwa mahali malumu tayari kwa kuzolewa.amesema katika maeneo yanayo zalisha taka kwa wingi ni katika Masoko jambo la muhimu ni kuhakikisha taka hizo zina zolewaMkuu wa wilaya ya songea  Besoni Mwampesia amewataka wafanya biashara kuzingatia usafi katika eneo lao nano wadau walio shiriki  usafi wamekiri kuwa usafi ni tabia aliyo zaliwa nayo mtu

Mkuu wa wilaya ya songea  Besoni Mwampesia amewataka wafanya biashara kuzingatia usafi katika eneo lao nano wadau walio shiriki  usafi wamekiri kuwa usafi ni tabia aliyo zaliwa nayo mtu


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka wanaruvuma kupingana na Maradhi mbalimbal kwa  kuweka usafi katika maeneo yao  ikiwemo  na kuchemmusha maji ya kunywa,kuepukan na kula vyakula vilivyo lala pamoja na kufuata kanuni zote za AfyaBregidia wa kanda ya kusini kikosi cha 401 cha Tembo Meja jenelali Goerge Msongole amesema usafi ni tabia ,wasio jua usafi wanatakiwa kujua maana ya amuri  Rais kaamuru kufanya usafi  kila mmoja ana takiwa kutii amuri hiyo kama Mkuu wa Mkoa ametii  amuri hiyo nani wa kuacha usafi,
Viongozi wa Serekari kutoka sekita mbalimbali wa kishirikiana na wananchi wengine wameshiriki kufanya usafi pamoja na kushiriki sherehe za kumbukizi vya vita vya majimaji ambavyo huadhimishwa kila mwaka mwezi wapili

Mkuu wa wilaya ya songea  Besoni Mwampesia amewataka wafanya biashara kuzingatia usafi katika eneo lao nano wadau walio shiriki  usafi wamekiri kuwa usafi ni tabia aliyo zaliwa nayo mtu

MKOA WA RUVUMA WA FANYA SHEREHE ZA KUMBUKIZI ZA MASHUJAA WALIO KUFA WAKATI WA VITA VYA MAJIOMAJI

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akiongoza kumbukizi ya sherehe za Mashujaa waliouwawa wakati wa Vita vya Majimaji
 Mnara wa Mashujaa walio kufa wakati wa vita vya Majimaji
 Jeshi la wananchi likitoa salamu za Maombelezo kwa Mashujaa waliokufa wakati Wa Vita vya Majimaji
             Maombelezo yakiendelea kwa kutoa heshima kwa Mashujaa wa Vita vya Majimaji
                                     Heshima ikitolea kwa Mashujaa wa Vita Vya Majimaji
 Makamanda wakionyesha Heshima na Utulivu kwa kuwakumbuka wenzao walio tangulia
 Shujaa chifu Songea alinyongwa katika maeneo haya na kichwa chake kukatwa na kupelekwa Ujerumani ikiwa ni kisasi baada ya kuwasumbua Wajerumani
Nihuzuni ya namuna yake kuwapoteza mashujaa lakini ni ushujaa ulio onyeshwa na wazee wetu wa zamani kupigania uhuru hadi kukubali kunyongwa na wajerumani

DAWATI LA POLICE WANAWAKE LA FANYA TATHMINI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma  Zuberi amewata askari police kushirikiana na Raia katika kuibua wahalifu n


Mwenyekiti wa uhamasishaji wa siku kumi na sita za ukatili wa kijinsia ndugu Mkude
Katibu akiwa anatoa darasa kwa kutoa tathmini ya mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia

Sunday, February 21, 2016

NAIBU WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO AFANYA ZIARA YA GHAFLA MKOANI RUVUMANaibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala amesema hata hospitali ya Mkoa wa Njombe am,bayo ilikuwa inakusanya shilingi  Milioni 3 kwa mwezi sasa inakusanya shilingi milioni 15 pamoja na mapungufu yaliyojionyesha ambayo kama hawatayarekebisha kwa  muda wa miezi mitatu Hospitali hiyo itaweza kufungiwa.Naibu Waziri wa Afya akiongeza kuhusu Madai ya Watumishi wa Sekta ya Afya, amesema Serikali inajipanga kulipa Madeni hayo imeanza Mwezi Januari Mwaka huu na itaendelea kuwalipa Watumishi wote wanaodai stahiki zao.Ziara ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dr. Kigwangala ni ya kushitukiza ameweza kutembelea wodi ya watoto, Maabara na sehemu ya Upasuaji na kukuta changamoto ya baadhi ya Mashine za maabara zikiwa mbovu na Sehemu ya Upasuaji Vitanda vikiwa vimepitwa na wakati. Akielezea kuhusu mafanikio ya kutumia mfumo wa Mashine za ELECTRONIC katika Hospitali ya Rufaa ya Mhimbili asema  mapato yame ongezeka mara mbili kuliko mwanzoPia amezipongeza Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma na Hospitali ya Mjimwema kwa  kuweza kuboresha Huduma za Mama na Mtoto.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya amesema Hospitali ya Mkoa hivi sasa baada ya kufunga Mashine za ukusanyaji mapato za ki electroniki imeweza kuongeza Makusanyo  kutoka shilingi milioni moja laki mbili hadi kufikia milioni 60 kwa mwezi   , Naye Mganga Mkuu wa hosptali ya Mkoa amesema Vifo vya Mama na Mtoto sasa vimepungua kila wanawake 100,000 vifo 95 tu vinavyotokea.

NAIBU WAZIRI WA AFYA JINSIA WAZEE NA WATOTO  DR. HAMISI  KIGWANGALA AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA NA KITUO CHA AFYA CHA MJIMWEMA NA KUKUTA CHANGAMOTO YA BAADHI YA MASHINE ZA MAABARA MBOVU NA BAADHI YA VITANDA VIBOVU KATK CHUMBA CHA UPASUAJI.

Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala ameyasema hayo katika ziara ya kusitukiza mkoani Ruvuma alipo tembelea Hospitali ya songea na Hospitali ya mji mwema Manspaa ya songea

Naibu Waziri wa Afya Jinsia Wazee na Watoto Dr Hamisi Kigwangala amesema ukusanyaji wa Mapato kwa kutumia Mfumo wa Electronic umeweza kuongeza Mapato katika Maeneo yote ya hospitali zinazotumia mfumo wa Mashine za ELECTRONIC
Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala amesema Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hapo awali ilikuwa inakusanya Mapato kwa kupata Bilioni 2 milini 700    kwa sasa inapata Bilioni 4 milini 400    kwa mwezi. Jambo ambalo linaweza kupunguza Changamoto zinazowakabili watumishi kwa kulipa Madeni ya Malimbikizi ya madeni wanayodai.


Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi  Kigwangala amesema hata hospitali ya Mkoa wa Njombe am,bayo ilikuwa inakusanya shilingi  Milioni 3 kwa mwezi sasa inakusanya shilingi milioni 15 pamoja na mapungufu yaliyojionyesha ambayo kama hawatayarekebisha kwa  muda wa miezi mitatu Hospitali hiyo itaweza kufungiwa.

Saturday, February 20, 2016

BENK YA POSTA NCHINI TANZANIA YA KARABATI VYOO VYA SHULE YA MSINGI MAKAMBI SONGEA


Shule ya Msingi ya Makambi Manispaa ya Songea yenye Wanafunzi 850 imepata ufadhili wa kukarabatiwa kwa vyoo vyenye Matundu 12 vikiwa na Thamani ya Shilingi Milioni 4.7
Afisa Mahusiano wa Benki ya Posta Noves Mosses amekabidhi vyoo hivyo  kwa Mwalimu Msaidizi  Kanisius Ngongi baada ya Uongozi huo kuomba ufadhili wa kukarabatiwa vyoo vitakavyo tumika  kwa Watoto  850 ambao walikuwa wakitumia vyoo hatarishi  

Afisa Uhusiano wa Benk ya Posta Noves Mosses ameitaka jamii kuwa na imani na Benki ya Posta kwa kutoa ushirikiano na Benki ya posta . pia amemeomba tasisi nyingine za kifedha kuji kita katika kuisaidia jamii kwa  kutatua changamoto zinazo wakabili kama  Elimu Afya na Shuguli zingine za kuleta maendeleo kwa jamii.

Mwalimu wa  Shule ya msingi Makambi Jeni Lugongo akimwakilisha mwalimu mkuu  ameomba Wafadhili mbalimbali wakiwemo Benki ya posta kuwasaidia walimu  kukarabati  choo  cha walimu ili kiendane na hadhi zao kama walivyo fanya kwa wanafunzi
Afisa Uhusiano wa Benki ya Posta nchini Tanzania Noves Mosses   amesema nia ya  Benki  ya Posta kazi yake ni kuunga mkono juhudi za serekari katika  kutatua changamoto za  sekita ya elimu ,Afya na Ustawi wa Jamii  Benk ya Posta imekuwa ikisaidia jamii kwa kujenga Madarasa,Kutoa Madawati na sasa imeweza kukarabati vyoo vya Shule ya Msingi Makambi
Afisa uhusiano wa Benk ya Posta Noves Moses akibadilishana mawazo na walimu huku akiwa elezea faida ya kujiunga na Benk ya Posta .kwanza kuwa na uhakika wa kukopo na kufanya shuguli za kusaidia familia mojamoja pili kufungua Acount ya watoto kwa ajili ya Elimu hivyo ni juu ya kila mwalimu kuonyesha mfano wa kufungua Acount Benk ya Posta

Wanafunzi wa Shule ya msingi Makambi Manspaa ya Songea  wamesema wana ishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kukarabati vyoo kwani hapo awali Wanafunzi wote bila kujali jinsia walikuwa wakitumia choo kimoja  Jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa watoto wa kike kuweza kupata magonjwa ya kuambukiza. Wameomba  Tasisi za kifedha  zingine  kuiga mfano huo
 Wanafunzi wa shule ya msingi makambi manspaa ya songea wa kifurahia kupata vyoo vya kisasa

Benki ya Posta katika Mkoa wa Ruvuma imekuwa mstari wa mbele kuchangia upande wa elimu tayari ilishatoa Madawati 50 kwa  Shule ya Msingi Mbulani Kata ya Ruvuma na kutoa zawadi kwa Wanafunzi waliofaulu kwa kupata Division One katika shule  za mkoa wa Ruvuma.  

WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE KATIKA KAMPENI YA KUTOKOMEZA MAGONJWA HAYO ITAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said thabit mwambungu amesema watu waache ufahari wa kuona  busha  ni jambo la kujivunia swala mhimu ni kwenda kufanyi upasuaji na tiba yake ni bure


Mratibu wa Magonjwa yaliyosahaulika Tanzania Dr. Edward Kirundi  kulia amesema Magonjwa ya Matende, usubi, Kichocho, Trakoma na minyoo ni magonjwa yanayosababisha Umaskini katika jamii ya Watanzania  
 Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Magret Malenga akionekana kwa mbali meza ya kwanza akisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa kuhusu Magonjwa yaliyo sahaulika yanayo enezwa na mbu
 Zawa za kuzuia magonjwa yaliyo sahaulika ya Matende, Usubi, Kichocho, Trakoma na Minyoo


Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Songea amesema magonjwa hayo yote matano yapo la mhimu kwanza kuzingatia usafi na kumeza vidonge vitakavyo tolewa kuanzia wiki ijayo


 Mwenyekiti wa Halimashauri ya Nyasa akitoa hoja kuhusu kujua kama vidonge vitakavyo tolewa kama vina madhara yoyote kwa binadamu.Alijibiwa na Mratibu wa Mafunzo hayo kuwa vidonge hivyo havina Madhara ila wanafunzi wanapo kunywa vidonge vya Minyoo lazima wawe wame shiba kwanza
 Wakurugenzi wa Halimashauri za Mkoa wa Ruvuma wakisikiliza semina ya kampeni ya kumeza vidonge kwa magonjwa liyo sahaulika
 Viongozi mbalimbali walio hudhulia semina ya jinsi ya kutokomeza magonjwa ya Matende, Usubi, Kichocho, Trakoma na Minyoo
 Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Namtumbo akiwa karibu na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Tunduru
                                        Wadau kutoka maeneo mbambali ya Mkoa wa Ruvuma
Semina ya Uhamasishaji kuhusu Magonjwa yaliyosahaulika ilihusisha Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma pamoja na waganga, waratibu na Viongozi wa kisiasa ngazi ya Halmashauri.

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa  kumeza dawa zinazo  zuia kuenea kwa Magonjwa yaliyo sahaulika ya kiwemo Magonjwa ya  Matende, Usubi, Kichocho, Trakoma na Minyoo.
Mratibu wa Magonjwa Yaliyosahaulika Nchini Tanzania Dr. Edward Kirundi amesema Magonjwa hayo  yanatibika, Cha muhimu ni  kila mmoja kushiriki katika kampeni ya kya tokomeza Ma gonjwa hayo kwa kutoa elimu iliyo sahihi ili kuifanya jamii kuelewa tatizo lillo mbele yao