KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, May 31, 2016

WADAU MBALIMBALI KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOANI RUVUMA WAHAMASIKA KUUNGANA NA SHIRIKA LA PADI KATIKA KUWASAIDIA WAZEE.

 Shirika la PADI Tanzania limepanga kuwajengea Nyumba wazee wawili amb ao wanaishi katika mazingira hatarishi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo na wakuu wa Idara za halmashauri za Mkoa wa Ruvumas
 Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wameishukuru Serikali kwa kuwajali kwa kutenga madirisha ya wazee na kuwatambua wazee kupitia Wizara ya Afya wamesema wanachosubiri ni sera ya wazee kutungiwa sheria itakayowalinda na ukatili dhidi yao.
 Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini wameahidi kutenga Bajeti kiasi cha sh. milioni 50.5 kwa ajili ya kuwezesha mikopo kwa wazee kupitia vikundi.
 Wadau wa masuala ya wazee kutoka Halmashauri za wilaya ya Songea Vijijini, Songea Manispaa na Halmashauri ya Madaba wameamua kutosubiri Bajeti za serikali kuu katika kuwasaidia wazee bali wameanza kuwashughulikia kupitia vyanzo vya ndani na fedha zao za mifukoni kwa kuchangia mahitaji ya wazee wasiojiweza.
 Wazee wa barabaza Huru la Wazee wa Manispaa ya Songea wameomba Jamii kutambua umuhimu wa wazee katika jamii zao wamesema wapo watu ambao bado wanawabeza wazee na kuwasingizia kujihusisha na imani za kishirikina.
 Watumishi wa shirika la PADI wakifuatilia hoja za wakuu wa Idara katika kupanga maazimio ya namna watakavyoweza kuwasaidia wazee kwa kushirikiana na Shirika la PADI.
 Watumishi wa Manispaa ya Songea katika kuhudumia wazee wamewezesha wazee 600 kuwaunganisha na Hospitali za Misheni za Mtakatifu Benedict matogoro na ya Mtakatifu Camilius Manispaa ya Songea kwa kuwalipia gharama za matibabu ambapo kila Zahanati hupeleka milioni tatu tatu kwa mwaka kwa ajili ya matibabu ya wazee. Pia katika bajeti ya 2016/2017 wametenga sh. milioni 50 kwa ajili ya kuwahudumia wazee kiuchumi na matibabu.
 Afisa Biashara wa Manispaa ya Songea akielezea namna atakavyotumia mapato yatokanayo na Biashara katika kuhakikisha wananufaisha na wazee kupitia vikundi vya ujasiliamali.
 Wakuu wa idara wa Manispaa ya Songea wakipanga mikakati ya kuwaingiza wazee katika Bajeti kutokana na Bajeti wanayoipata kwa kila idara. Wakuu hao wamejadili hayo wakiwa katika viwanja vya shirika la PADI Unangwa Manispaa ya Songea.
 Wakuu wa Idara kutoka Halmashauri 3 za wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma walipokutana na wazee na Viongozi wa Shirika la Kuhudumia wazee la Padi na kuweka maazimio ya kuwasaidia wazee ikiwemo kutunga sheria ndogo ndogo katika kila Halmashauri za kuwalinda wazee.
Halmashauri ya Madaba imetenga Kiasi cha Shilingi Milioni 50,231,500 katika Bajeti ya 2016/2017 kwa ajili ya huduma za wazee  ikiwemo na kuwatengenezea vitambulisho vya matibabu.

Saturday, May 28, 2016

WAZEE MKOANI RUVUMA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA KISUKARI .KATIKA KUAZIMISHA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

 Wazee wapatao 3000 wamejitokkipima kujua Afya yakeeza kwa wingi Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kupima afya zao ikiwemo na ugonjwa wa kisukari mama kutoka peramiho akichekiwa na Wahudumu wa Zahanati ya St. Benedict Dr Hindu Mzambili na Bi Janet Mapunda
 Wazeeb wakiwa wame kaa kwenye fomu kungo zamu ya kumwona Dakitari kupima kisukari
 Hili ni bango la wafadhili walio fadhili upimwaji wa wazee kamaDA Kutoka kenye na Shirika la PADI Linalo shugulikia Wazee Nchini Tanzaniama linavyo someka ni Age Demands Action is a Help Age Global Network Campaign.
 Mkurugenzi wa PADI Issaca Msigwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu swala zima la siku ya kisukari duniani amesema magonjwa nyemelezi yanayo waathiri wazee ni pamoja na kisukari

 Wazee wanaotakiwa ni wengi cha muhimu ni kupitisha elimu kwa wadau mbalimbali ili mzee ajue faida ya kupima Afya yake ingawa muda wa kufanya hivyo ni mdogo kutokana na mzigo anaotwishwa wa kulea wajukuu
 Hapo akina mama wakiwa wamejipanga foleni toka asubuhi na kusema hawaondoki mpaka wajue Afya zao
Unaweza kuona foleni ilivyokuwa kubwa huo ni mwitikio mzuri kwa wazee kujitokeza kujua Afya zao
Wahudumu wa Afya ya Msingi wakiwa katika juhudi za kuwa pima wazee pamoja na changamoto kubwa zinazo wakabili zakuelimisha wazee kuhusu lishe
Mama hapo baada ya kupima kisukari sasa ana pima BP Ili kujua map[igo ya Moyo
Mganga Mfawidhi Dr Exsavery Malekela wa Zahanati ya Misheni inayo milikiwa na Masisita wa ST Benedict iliyoko Matogoro Manispaa ya Songea akiendelea kupima wazee .
Kabla ya kuwa pima wagonjwa Mganga Mfawidhi Dr. Xsavery Malekela hutoa Nasaha ili kuwa weka sawa wagonjwa
Wahudumu wa Afya ya Msingi wamekuwa watu ambao wako mstari wa Mbele kuwahudumia Wagonjwa kama unavyo waona hapo
Moja ya Harakati ya Kumpima kila Mgonjwa aliye kuja kupima bila kubagua kutokana na hali zao
Mganga Mfawidhi Xsavery Malekela  wa Zahanati ya St Benedict ni kawaida yake kwanza kabla hajaingia kutoa Nasaha za kuwaweka sawa mgonjwa
Mhudumu wa Afya ya Msingi kwanza kabisa kabla ya kutoa huduma huchukua historia ya Maisha yake ili kujua ni kwa nini BP imepanda

Mzee kutoka Matogoro ambaye amekuwa na kawaida ya kujua Afya yake amesema kila baada ya Miezi mitatu huja kutaka kujua Afya yake                                                            UPIMAJI WA KISUKARI
                  Bango linalo onyesha Zahanati ya St Benedict ilipo ili wagonjwa wasipotee

Waganga walichukua siku mzima kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa kumi na mbili na nusu walipo maliza zoezi la upimaji wa kisukari ati ya wazee walio pimwa asilimia 20% walipatikana na kisukari
Ukiwa mwoga huwezi kupima kasinda kado lazima kakutoboe lakini hilo halikuwa kikwazo wengi waliendelea kupima
Mara baada ya kupimwa hutolewa darasa la kuwa fanya wale walio onekana hawana kisukali wafanyeje na walio patikana na kisukari nao wajilinde vipi
                            Wasee wakibadilishana mawazo baada ya kupimwa kisukari

                    Mwalimu kutoka Chuo cha walimu Matogoro akijisogeza kutaka kujua hali yake
Mhudumu wa Afya ya Msingi akimupima Mzee kisukari amesema Changamoto anazo kutana nazo anapo kwenda majumbani kutoa huduma hiyo ni kudhani wana beba chakula kwa ajili ya wazee, hiyo ni changamito kubwa unayo tokea mara kwa mara
Msimamizi mkuu wa Zahanati ya ST Benedict ,Zahanati hii ina vifaa mbambali vya mazoezi kwa wale wenye matatoizo ya Mgongo ,Kiuno kuuma,au Shingo una fanya mazoezi tu na ugonjwa una toka muda huo huo jaribu kutembelea Zahanati ya ST Benedict iliyo Matogoro Manspaa ya Songea

Friday, May 27, 2016

WAZEE WAWILI MKOANI RUVUMA WAISHI KWA KUBAHATISHA


Wazee hao kutoka vijiji vya Makemba na Luhimba Kata ya Mtyangimbole, Mzee Abdala Ally   na Bibi Paulina Nyoni  wameiomba Serikali iharakishe kutoa Pensheni kwa wazee wote ili kunusuru Maisha ya Wazee kwa kukosa mahitaji ya chakula na dawa.

 Babu Pius Mayumba pichani ndiye anayemtunza Bibi Paulina Nyoni mwenye umri wa 78 ambaye pia ni mgonjwa wa kifua kwa muda mrefu hawawezi kumudu gharama za Matibabu na usafiri kutoka nyumbani hadi hospitali umbali wa km 64.
 Bibi Paulina Nyoni (78) Akiongea na Waandishi wa Habari walipomtembelea nyumbani kwake kutaka kujua changamoto anazokabiliana nazo na namna anavyoweza kumudu gharama za matibabu na hali anapoishi pamezungukwa na msitu yuko mbali na makazi ya watu wengine, amesema Analishukuru shirika la PADI kwa kumuibua na kuweza kuziainisha changamoto zinazomkabili zikiwemo na kushindwa kumudu gharama za matibabu na usafiri kwa kuwa kila anapokwenda Hospitali anatakiwa kulipa Sh. 5000 ili aweze kupata dawa. Pia mwendo wa kutoka nyumbani hadi Hospitali unamgharimu shilingi 2500 kwenda na kurudi ni sh. 2500.
 Bibi Paulina Nyoni amesema yeye mwenyewe hawezi kwa kuwa hana msaada wowote na ugonjwa anaoumwa unahitaji kupata dawa kila mwezi licha ya changamoto zingine za chakula, mavazi na mahali salama pakuishi. Anadai ili apate matibabu inamlazimu awe na sh 10,000 kila mwezi za kuweza kukidhi kupata dawa na usafiri. Ameiomba Serikali kuharakisha uwezeshwaji wa kutoa Pesheni kwa wazee wote pengine akipata pensheni itamsaidia kupata matibabu.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makemba Hassan Issa Kawenga alipoulizwa jitihada gani zinazofanywa na serikali yake katika kumuwezesha mahitaji Bibi Paulina Nyoni amesema Baada ya Shirika la PADI kukaa na Uongozi wa Serikali ya Mtaa na Wananchi kuhamasisha jinsi ya kuwasaidia wazee Mwaka huu wameazimia mara baada ya mavuno ya Msimu huu kila Mwananchi wa Mtaa wa Makemba kumchangia Bibi huyo kiasi cha kilo nne za mahindi ili ziwasaidie kwa ajili ya chakula.
 Hiyo ni choo ambayo huitumia Bibi Paulina Nyoni na Mume wake ambaye naye ni mzee unaweza kustaajabu bibi ambaye hana uwezo wa kutembea na ni mgonjwa yuko katika hali ya kutetemeka muda wote anawezaje kuifikia choo hiyo na imekaa umbali mrefu kutoka kwenye nyumba ambayo anaishi na yenyewe si salama.
 Bibi Paulina Nyoni akiwa anatoka ndani ya Nyumba anamoishi amesema kutokana na kukosa uwezo na msaada ameshindwa kutumia dawa kwa muda wa miezi minne sasa baada ya kukosa hela ya kuweza kumsaidia kupata Dawa na usafiri wa kufika Hospitali kwani hana uwezo wa kutembea umbali wowote zaidi ya kuingia ndani na kutoka nje.
 Hayo ni Malazi ya Bibi Paulina Nyoni ambaye hana wasaidizi wa kumsaidia zaidi Jamii ilimtenga lakini kupitia Shirika la PADI inaendelea kuhamasisha jamii ya eneo hilo ili imsadie huduma ndogo ndogo kwa sasa walau watu wanajitokeza kumchotea maji na shughuli zingine ndogo ndogo. Jitihada zingine zinazofanywa na shirika la Padi katika kuwasadia wazee hawa ni kuhamasisha wadau kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwajengea Nyumba ya kuishi ambayo itakuwa ni salama kwao.
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa ruvuma na Viongozi wa Serikali ya Mtaa wa Makemba Kata ya Mletele walipomtembelea Bibi huyo kujionea changamoto anazozipata na jitihada zinazofanywa na shirika la kuhudumia Wazee la PADI katika kuwasaidia wazee hao akiwemo Bibi Paulina Nyoni.
 Hilo Ndilo eneo ambalo anaishi Bibi Paulina Nyoni ambalo kwa mbali utaona limezungukwa na msitu hakuna Nyumba jirani. Swali la kujiuliza je endapo kunatokea shida za usiku na makazi ya ni ya aina hiyo wanawezaje kujinasua. Ni jukumu la Kila mdau kuguswa na Maisha ya Wazee hawa ambao wana mahitaji mengi Shirika la PADI peke yake halikidhi kuwafikia wazee wote wenye mahitaji ya aina hii. Pia  Jamii inapaswa kutambua thamani ya wazee.
 Shirika la PADI linalohudumia wazee Tanzania linafanya kazi kubwa ya kuwahudumia wazee na kuwaibua wenye mazingira hatarishi ili jamii iweze kuwasaidia na kuepukana na dhana mbaya kwa wazee kwa kukwepa Majukumu ya kuwahudumia. Piachani ni Afisa wa PADI Jackson akiingia ndani kumuona Mzee Abdalah Ally (77) ambaye anaishi kwenye nyumba hiyo na ni mgonjwa ambaye haamki kitandani kwa muda wa miaka 20 sasa katika Mtaa wa Luhimba Kata ya Mtwangimbole Madaba.

 Mzee Abadalah ally akiwa amelala kitandani kwenye kibanda ambacho hakina hata dirisha na mlango. Amesema katika maisha yake hakuwahi kupata mtoto wala kuoa lakini alianza kuugua kwa muda mrefu zaidi ya miaka 20 sasa.
 Mzee Abdala Ally anasema changamoto zinazomkabili ni kushindwa kutoka nje kwa kuwa hana uwezo wa kuamka haja zote anazipata akiwa kitandani ama kwa kuwekewa dishi na mtoto wa mdogo wake anayemtunza ambaye naye ana tatizo la Kifafa. Amesema endapo Serikali itatoa Penshen kwa wazee itamsaidia kukidhi baadhi ya changamoto.
 Mganga Mkuu wa Zahanati ya Luhimba George Palangyo amesema changamoto kubwa inayojitokeza katika kumuhudumia mzee Abdalah Ally kwa watoa huduma wa wagonjwa wa Majumbani, ni kukosa vifaa vya kuweza kumsaidia katika kumuhudumia vikiwemo vifaa vya haja kubwa na ndogo na will chair ambayo ingeweza kumsaidi kumtoa nje na kupata hewa ya nje na mazoezi ya viungo.
 Wazee wanahitaja msaada wa kila hali na mali toka kwa serikali, wadau na jamii kwa ujumla. hiyo ni hali ya choo ambacho kinatumika na mzee ambaye awali alikuwa na uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
 Pamoja na Changamoto zinazowakabili wazee wengi lakini wamesema wanaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuonyesha nia ya kuwajali wazee wanachokiomba ni serikali kutunga sheria ya wazee ili iweze kuwalinda na kuwa salama katika maisha yao ya uzeeni.
 Hiyo ni nyumba wanayoishi wategemezi wa Mzee Abdala Ally ambao na wao hawana uwezo na wana matatizo ya ugonjwa wa kifafa Unaweza kuona hii familia kwa ujumla ina hadha kwa kiasi gani. Shirika la PADI liliweza kumuibua Mzee huyu na kushirikisha HBC watoa huduma ya Afya Majumbani na kuanza kumtembelea kumfanyia usafi na kumnunulia Godoro la kulalia.
 Mzee Abdalah Ally akiwa amelala ndani alipotembelewa na waandishi wa Habari na Uongozi wa Shirika la kuhudumia Wazee la PADI nyumbani kwake Lihumbu Kata ya Mtyangimbole.
Baadhi ya watoa huduma ya Afya na Majirani wa Mzee Ally Abadala. Kwa yeyeote mwenye kuguswa na maisha hayo anaweza kutoa mchango wa aina yheyote wa wazee hao kwa kupitia Shirika la PADI chini ya Mkurugenzi wake Iskaka Msigwa. Shirika la Padi limeanza taratibu za kuzijengea Nyumba familia hizo mbili kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali.