KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 31, 2016

MIZINGA UTUNDIKAJI STORY TWO

ZIARA YA KAMISHINA JENERALI WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI RUVUMAKamishina  Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Tanzania Thobias Andengenye amewataka amewataka Askari wa Zimamoto kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa uaminifu ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ameyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma, amesema Ziara yake inalenga kutaka kujionea changamoto zinazolikabili Jeshi la Zimamoto.Akizungumzia kuhusu Vifaa vya kuzimia moto na jinsi ya kutoa Elimu kwa wananchi ili wasiweze kupatwa na Majanga ya moto amesema, ni vizuri unapopata kiwanja kabla ya kujenga ukawasiliana na Viongozi wa Zimamoto na uokoaji ili wakupe elimu jinsi ya kuepukana na Majanga yanayotokana na Moto.

Askari wa Zimamoto Briged ya kusini 401 KV wakitoa heshima kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na ukoaji akiwa Ziarani Mkoani Ruvuma.


Kamishna Jenerali  wa Zimamoto Thobias Andengenye akielezea kuhusu Vifaa vya kuzimia moto katika maghari, ametoa ufafanuzi kuwa fedha zinazolipwa TRA ni kwa ajili ya ukaguzi na sio za kununulia mitungi ya gesi. Jambo linalowachanganya wengi.Kamishna  Jenerali wa Jeshi la Ziamamoto na Uokoaji amesema kwa hivi sasa changamoto inayolikabili Jeshi la Ziamamoto ni kukua kwa miji ambako ujenzi hauzingatii kujikinga na majanga.

Amesema kiutaratibu kinachotakiwa kila baada ya kilomita 15 kuwe na kikosi cha zimamoto.
Askari wa Jeshi la Ziamamoto na Ukoaji wa kikosi cha Briged ya kusini 401 KV wakiwa katika Ofisi za Kikosi hicho Manzese Manispaa ya Songea.
Vitendea kazi vya Jeshi la Zimamoto uokoaji vinavyotumika pindi majanga ya moto yanapotokea.
Magari ya Zimamoto yakiwa katika eneo la Kikosi cha Jeshi la Ziamamoto na uokoaji manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Askari wa Jeshi la Zimamoto wametakiwa kushirikiana na Vyombo vya habari katika kutoa Elimu ya kujikinga na Majanga ya moto badala ya kusubiri majanga yatokee kwa kuwa wao ndio wana wajibu wa kuzuia majanga kwa kuelimisha jamii kujikinga na majanga ya moto.

UTAFITI WA HALI YA MAAMBUKIZI YA VVU NA UKIMWI NCHINI TANZANIA KUFANYIKA KWA TEKNOLOJIA YA KISASA


Jumla ya watu 35,000 hufa Nchini Tanzania kutokana na Maambukizi ya VVU na UKIMWI na watoto 600,000 huachwa katika hali ya uyatima kila mwaka.


Akisoma Taarifa ya Takwimu za maambukizi ya UKIMWI  kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dr. Binilith Satano Mahenge  amesema Takwimu ni kubwa hivyo ili kuweza kupunguza ongezeko  hilo  inabidi kutumia njia shirikishi itakayo kuwa na idadi sahihi ya maambukizi 

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Mihayo Bupumba amesema njia ya kwanza ni kuhakikisha wale wote walioathirika wanajulikana kwa asilimia 90%, njia ya pili ni kutambua kama hao walioathirika wanapata dawa za ARV kwa asilimia 90%  njia nyingine ni kufahamu na kudhibiti maambukizi mapya kwa asilimia 90% kwa kufanya sense ya kitalamu bila kumlazimisha mtu

 Katika utafiti huo Mkoa wa Ruvuma utahusisha katika wilaya zote kinachotakiwa ni wale wanaotakiwa kuwakilisha kushiriki kikamilifu.
 Wadau wa Mapambano dhidi ya ukimwi kutoka halmashauri za Mkoa wa Ruvuma, Taasisi za Dini na Asasi zinazoshughulika na masuala ya UKIMWI wakiwa katika mkutano wa kupokea taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi unaotarajia Kufanyika Tanzania nzima kwa kaya wakilishi.
 Wadau wamesisitizwa kutoa ushirikiano katika zoezi hilo muhimu ili kufahamu Takwimu sahihi za hali ya maambukizi zitakazosaidia Serikali kujua namna ya kupanga Bajeti katika kuhudumia waathirika wa VVU
 Wataalamu wa Afya kutoka Kitengo cha Utafiti wa Viashiria vya VVU na UKIMWI
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akitoa taarifa ya namna walivyoandaa maeneo yatakayohusika na utafiti huo kwa kushirikiana na waratibu na watakwimu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Mihayo M. Bupamba akielezea teknolojia itakayotumika katika utafiti kwa kutumia electronic ambayo itatoa usahihi wa data.