KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Thursday, April 28, 2016

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA SONGEA WATOA VITANDA 20 NA MAGODORO 20 KWENYE ZAHANATI YA MJIMWEMA SONGEA



Mpangala ameyasema hayo wakati akikabidhi Magodoro 20 na vitanda 20 vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 11,760,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabit Mwambungu.


 Regina Hyera na Mkuu wa Mkoa akipokea Msaada wa Magodoro na Vitanda kutoka Mfuko wa Taifa wa Taifa wa Bima ya Afya Songea

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu akipokea vitanda hivyo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya amesema kutokana na upungufu wa Magodoro 66 na Vitanda 77 sasa kutakuwa na upungufu wa Magodoro 46 na vitanda 57



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameomba Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya kuangalia uwezekano wa kuweza kukamilisha Magodoro na Vifaa vilivyobaki.

 Meya wa Manipa ya Songea  Shaweji Mohamed akiwaomba wafanyakazi wa Mjimwema kudumisha usafi kwa kusema mapato yanaongezeka ina m,aana magonjwa yame kuwa mengi

Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Ruvuma umetumia zaidi ya shilingi 239,373,881 kwa ajili ya kulipia wateja waliojiunga na Mfuko wa Bima ya Afya.
Kaimu meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Karistus Mpangala amesema wilaya ya inayoongoza kwa utoaji wa michango ya Mfuko wa Taifa wa bima ya afya ni Tunduru ambayo imeweza kupata shilingi 86,619,467.00


Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Jenifa amesema Manispaa ya Songea imepata Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kununulia Vifaa vya upasuaji katika Kituo cha Afya cha Mjimwema na wanatarajia kukopa Milioni 100 tena ili kumalizia chumba cha upasuaji cha mjimwema kianze kufanya kazi.

 Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katikati Mganga wa Zahanati ya Mjimwema Regina Hyera na kulia ni Carituus Mpangala


 Mkuu wa Mkoa akipokelewa na Mganga wa Manspaa ya Songea Chacha huku akiwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Beson Mpesya
 Jopo la uongozi wa Zahanati ya Mjimwema wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kukabidhiwa Magodoro na Vitanda
 Meya wa Manspaa ya Songea akijadiliana na Mkurugenzi wa manspaa jinsi ya kuweza kuhudumia wananchi wa Manspaa
 Mganga wa Zahana ya Mji mwema Regina Hyera akipokea Magodoro na Vitanda kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma baada ya kupokea magodoro hayo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Songea
 wauguzi wa manspaa ya Songea wame aswa kutumia vizuri vifaa vinavyo tolewa katika Zahanati zao pili wawe mbali na tamaa ya kudokoa vitu hivyo kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu
 Afisa Usitawi wa Jamii wa kwanza aliye vaa Tisheti ya Blue akisikiliza kwa makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa kuhusu wezi katika Hospitali
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Besoni Mpesya  Akiomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kutoa viwango ambavyo Mwananchi ana viweza hata kwa kutoa katika Mihula Mitatu

Monday, April 25, 2016

WAKULIMA HALMASHAURI YA MADABA WAMETAKIWA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA FURSA ZA MIKOPO YA PEMBEJEO NA KUWEZA KULIMA KILIMO CHENYE TIJA.


Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Madaba Prosper Luambano amewataka wakulima wa Halmashauri ya Madaba kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopa nyenzo za kulimia ikiwemo Matrekta.
Kaimu Mkurugenzi ameyasema hayo baada ya kupokea taarifa kwa NMB kuwa waliweza kukopeshwa shilingi Milioni 113 na kuweza kulima kitaalamu Hekari zisizopungua Hekari 522 za Mahindi.

wakulima wa Halimashauli ya Madaba wakisikiliza watalamu wa kilimo njia za kuweza kuendelea kwa kutegemea kilimo
 Akina mama Madaba wamekiri kuwa kilimo kinaweza kuwa komboa baada ya kuvuna gunia 30 kwa ekari moja
 Pamoja na hayo wananchi wa madaba wameomba elimu ya kilimo ianze kufundishwa toka shule za awali ili mtoto aondoe dhana ya kusema masikini ndio wanao sitahili kulima

Nao Wakulima wamesema wameshindwa kupuliza dawa ya magugu kutokana na upungufu wa Vitendea kazi kama Mabomba ya kupulizia dawa, Wakulima wa madaba wamesema ili kilimo kiwe na tija wange weza kukopeswa mikopo ya muda mrefu kutegemea na zao unalo lilima


WAKULIMA HALMASHAURI YA MADABA WAMETAKIWA KUJIUNGA KATIKA VIKUNDI ILI WAWEZE KUNUFAIKA NA  FURSA ZA MIKOPO YA PEMBEJEO NA KUWEZA KULIMA KILIMO CHENYE TIJA.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba Prosper Luambano amesema ikiwa wakulima wataanza kulima kwa kutumia Trekta hali ya uchumi itaongezeka, amewaomba wakulima wa Halmashauri ya Madaba kulima pia zao la Tangawizi ambalo kwa Ardhi ya Madaba inakubali. Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba amewaomba wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwenye Kilimo waweze Madaba.

Wataalamu wa Kilimo wamewataka Wakulima wanapolima waangalie mbegu za kupanda ili wanapovuna wapate kujiwekea chakula na kupata kipato baada ya kuuza mazao yao watalamu hao wamewaomba wakulima kutumia dawa ya kuua magugu kwa kuwa ina punguza garama ya palizi


Mkoa wa ruvuma kwa msimu wa Mwaka 2015  - 2016 wanatarajia kuvuka lengo la mwaka jana  la kuvuna Tani  million 1.8 na kuweza kufikia Tani Milioni 2 kutokana wakulima kuelimika baada ya kupata elimu kutoka kwa watalamu  wa Mashirika ya RUDI na ACTN kupitia Makampuni ya SEEDCO, SYNGENTA na YARA. Kwa mwavuli wa Green Luvolation

WATU 144 WAKOSA MAHALI PAKUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUANGUKA NA MVUA KUNYESHA MFULULIZO KWA SIKU TATU MKIOANI RUVUMA


Kaya 144 zimekosa mahali pakuishi katika Kijiji  cha Ngadinda Kata ya Gumbilo wilaya ya Songea vijijini baada ya nyumba 51 kubomoka na nyumba 91 kutetereka baada ya mvua kali kunyesha mfululizo  muda wa siku tatu mfululizo
Mkuu wa wilaya ya songea Bensoni Mpesya amesema licha ya nyumba kubomoka mvua pia imeathiri mashamba yapatayo  hekari 102 za nafaka mbalimbali zikiwemo mahindi mpunga na maharage
 Kufikia maeneo yenye maafa kunataka moyo hapo Gari la Mkuu wa wilaya ya Songea Bensoni Mpesya likiwa lime kwama na kusababisha mkuu huyo kutembea kwa mguu kukagua maeneneo yaliyo athirika katika kata ya Gumbiro

Mkuu wa wilaya ya Songea Bensoni Mpesya amesema maafa yaliyo tokea yametokea baada ya mto Hanga kufurika na kusababisha hasara kubwa lakini kamati ya maafa ya wilaya imejipanga kusaidia familia hizo katika ujenzi, chakula kipo cha kutosha
Mkuu wa wilaya ya songea Benson Mpesya amewaomba wananchi wa Songea ili kuepukana na majanga ya kubomokewa na nyumba wajaribu kufuata ushauri wa wahandisi wakati wa ujenzi, nyumba nyingi hubomoka kwa kukosa misingi imara

Friday, April 22, 2016

AMWOMBA RAIS WA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA DR JOHN POMBE MAGUFULI AMUSAIDIE KUPATA MIRATHI YA MUMEWE KATIKAQ MKOA WA RUVUMA


Mama Mjane aliyeachwa na mmewe miaka 10 iliyopita, sasa amuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr john Pombe Magufuli amsaidie kupata Mirathi ya Mumewe ili aweze kusomesha Watoto wake.

Mama Engetrauda  Alex Millinga mumewe alikuwa mfanya kazi katika hospitali ya mkoa Ruvuma kitengo cha meno na aliondoka kwa kibali cha Serikali lakini Serikali ya Mkoa wa Ruvuma imeshindwa kumsaidia hebu tumsikilize anasemaje kwenye Video hii,


Sunday, April 17, 2016

KITENGO CHA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA) SONGEA KIMELIINGIZIA TAIFA KIASI CHA TSH. 39,140,000,000 BAADA YA KUUZA MAHINDI TANI 103,000 KATIKA KIPINDI CHA 2015 2016.



Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea imefanikiwa kuuza Tani 103,000 za Mahindi katika Mikoa ya Tanzania iliyokuwa na Uhaba wa Chakula na kuweza kuliingizia Taifa kiasi cha Shilingi 39,100,000,000 kwa ajili ya uuzaji wa Mahindi. (Picha Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akiwa na Meneja wa kitengo cha hifadhi ya Chakula Songea Bw. Amos Mtafya.

Hayo yamebainika wakati Naibu Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akisomewa taarifa ya chakula kilichotolewa Mkoani Ruvuma kusaidia mikoa mingine yenye uhaba wa chakula Tanzania.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella  Manyanya alipokuwa katika hifadhi ya chakula Songea kununua Tani 5 za Mahindi kwa ajili ya wananchi wake waliopata Maafa ya Mafuriko katika Jimbo la Nyasa. 

Meneja wa Kitengo cha hifadhi ya Chakula (NFRA) Songea Amos Mtafya akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Elimu amesema katika kipindi cha 2015 – 2016 Hifadhi ya Chakula Songea imeweza kusafirisha Tani 88,000 kwa mikoa ya Tanzania bara yenye Upungufu wa chakula na Tani 10,000 kwa Shirika la  chakula Duniani (Word Food  Program– WFP) na Tani 8,000 kuhamishiwa katika Hifadhi ya Dodoma na Tani 5 kununuliwa kwa ajili ya watu waliopatwa na maafa jimbo la Nyasa na kitengo kimebakiwa na tani 11,000

Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amesema miundombinu ya barabara na usafiri wa majini Serikali imeweza kusaini Mkataba wa kutengeneza Barabara ya Kitahi  -  Lituhi na Mbinga hadi Mbamba bay kwa kiwango cha lami.(Picha Gari ya Naibu Waziri ikiwa imenasa katika Tope akiwa ziarani Jimbo la Nyasa)

Nao wananchi wanaoishi vijijini wametakiwa kufuatilia kwa ukaribu Miradi inayofadhiliwa na Serikali, Miradi inayofanyika vijijini inatakiwa kuwa imara kusiwe na visingizio vya kujenga miradi chini ya kiwango kwa kudai ni miradi ya vijijini.


Mhandisi Stella Manyanya ameyasema hayo baada ya kuona Mradi wa ukarabati wa Kituo cha Afya cha kata ya Linga Wilayani Nyasa uliogharimu shilingi Milioni 27 simenti ya sakafu ikionyesha imepasuka kabla ya kumaliza mwaka mmoja.

Mhandisi Stella Manyanya amesema hakuna kisingizio cha kukarabati ovyoovyo miradi ya Vijijini na kusingizia miradi ya vijijini inatakiwa kulipua Wananchi wawe macho katika kusimamia miradi hiyo.(Pichani Mhandisi Stella Manyanya akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya Litumba Kuhamba Kata ya Linga.)

Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya amesema katika Jimbo la Nyasa kutakuwa na mashindano ya ufaulu kubaini shule gani imefaulisha vizuri, mwalimu atakayeshindwa kufaulisha vizuri wanafunzi itambidi apishe nafasi hiyo ichukuliwe na wenzake watakaoweza kufundisha vizuri.Mh mhandisi Stela Manyanya ametoa agizo kiloa shule iwe na shamba darasa kwa ajili ya somo la kilimo

Naibu Waziri wa Elimu Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kuhusu Sekta ya Elimu amesema katika Tanzania kuna vyuo vikuu zaidi ya 50 na chuo kingine cha Madaktari bingwa wa Moyo na Mishipa ya Damu kinajengwa Mlogazila Dar Es Salaam ambacho kitachukua wanafunzi 15,000 wa fani ya Udaktar

Mhandisi Stella Manyanya amesema Serikali katika kuinua uchumi wa Watu wanaoishi Mwambao wa Ziwa Nyasa tayari mkataba wa kutengeneza Barabara ya Mbinga MbaMba Bay umeshatiwa sahihi kwa ujenzi wa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Elimu amewahimiza Wazazi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuboresha Elimu katika mambo yanayowahusu wazazi , kama kutoa chakula kwa watoto, Madawati pamoja na kuboresha eneo la kusomea.

Wananchi wa Maeneo yaliyopatwa na Maafa ya Mafuriko wamemshukuru Mweshimiwa Mbunge kwa kuweza kukimbia Jimboni na kutoa pole kutokana na Maafa yaliyowapata.

Akiongea na Wananchi wa Jimbo la Nyasa Mh. Naibu Waziri wa Elimu amesema ili uweze kuingia katika Vyuo hivyo unahitajika kufaulu vizuri kwa kupata Daraja la kwanza (Division One).

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu amesema pamoja na kurahisisha mawasiliano ya usafiri katika Ziwa Nyasa, pia ujenzi wa Bandari ya Ndumbi unaendelea,  na meli tatu zinaundwa, mbili zikiwa za mizigo na moja ya Abiria ambazo zitasaidia kusafirisha mizigo na Abiria kutoka Mbeya hadi Mbamba Bay.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Manyanya amesema wako watu wachache ambao wanawakatisha tamaa wenzao kuhusu Elimu, lakini watu hao ni wa kuwapuuza jambo muhimu kwa wazazi ni kutoa ushirikiano kwa Walimu kwa kuboresha Mazingira kwa kujenga Nyumba nzuri za walimu. 
Mheshimiwa Stella Manyanya alikuwa katika Ziara ya siku mbili katika Jimbo la Nyasa kwa ajili ya kutoa pole kwa wananchi waliopatwa na Maafa ya kukumbwa na Mafuriko.