KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Tuesday, December 26, 2017

IBADA YA CHRISMAS MKOANI RUVUMA WAUMINI WAMETAKIWA KUZINGATIA MAADILI


Mhashamu ASkofu Mkuu wa kanisa la Redeemed Assemblies of God Tanzania amewataka waumini wa dini ya kikrsito kumkimbilia Mungu ili kuweza kukabiliana na mambo ya ufisadi na Dhuluma inayofanywa na watu wasio mwogopa Mungu.


Mhashamu Askofu Mkuu wa kanisa la Redeemed Asemblies of God  Simon Kisote Silumba ameyasema hayo katika ibada ya kusherekea sikukuu ya Crismas Mkoani RUVUMA, Amesema ili viongozi waweze kuwa waadilifu wanatakiwa kuachana  vitendo vya kudhulumu mali ya wanyonge



Naye Mhashamu Asikofu wa  KKT Dayosis ya Ruvuma Amon John Mwenda amewataka waumini katika kukabiliana na hali ya uchumi wajikite katika  kufanya kazi zilizo halali.

Mchungaji wa kanisa la Angilikani Erasto  Haule amewaomba  waumini kutokata tamaa katika maisha wategemee nguvu za Mungu Waepukane na viongozi wanao zingatia Rushwa.

Vijana waumini wa dini ya kikristo wameomba waumini wa dini ya kikristo kupingana na vitendo vya Rushwa.



Vijana wametakiwa kuwa mfano katika Jamii kwa kuzingatia Mila na Desturi za kitanzania kwa kusimamia usafi katika Maeneo yao na kuheshimu wakubwa wanaowazidi umri.

  Askari wa usalama barabarani wameomba madereva kuwa makini wakati huu wa sikukuu za kirismas na Mwaka mpya ili kuesha ajali zinazoepukika.

Katika kuendeleza Maadili mema kwa wanawake wametakiwa kujiandaa kuwa viongozi wa Familia siku za baadaye  huku wakimtanguliza Mungu
Mchungaji wa kanisa la REDEEMED Asemblies of God Hilda Silumba amewataka  vijana wava e mavazi yenye heshima.


Mkoa wa Ruvuma umesherehekea kwa usalama Sikukuu ya Krismas 2017 hasa kwa kuzingatia suala la Ulinzi wa Watoto kutowaacha peke yao, wazazi walio wengi wameonekana wakiambatana na watoto wao.