KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, January 13, 2017

WAZIRI WA KILIMO MIFUGO NA UVUVI DR CHARLES TIZEBA AMEWAAGIZA WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA KUACHANA NA SUALA LA KUPATIKANA KWA MAZAO YALIYO CHINI YA KIWANGO KATIKA VITENGO VYA WAKALA WA HIFADHI YA CHAKULA

Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi  Nchini Tanzania Dr Charles Tizeba amewataka Wakala wa  hifadhi ya chakula Nchini Tanzania (NFRA) kutafuta njia ya kisasa ya kukabiliana na unyaufu wa Mahindi kwa kutafuta mashine ambazo zitaweza kuondoa unyaufu katika Mahindi na kumpunguzia mkulima adha ya  kusubiri mahindi yakauke ikizingatiwa misimu ya mavuna inatofautiana kati ya kanda na kanda


Waziri wa Kilimo  Mifugo na Uvuvi Dr. Charles John Tizeba  ametoa agizo hilo baada ya kuangalia muda maalumu wa kununua Mahindi kwa wananchi na kugundua muda wa kuanza ununuzi unachelewa hadi mwezi wa nane kwa kusubiria Mahindi yakauke jambo linalopelekea wananchi kuamua kuuza mahindi kwa hasara kwa wafanyabiashara wadogo kwa shilingi 250 hadi 350  badala ya bei ya kitengo ya shilingi 600

Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi  Dr  Tizeba  amesema sasa hivi kila jambo linakwenda kwa teknologia  ya kisasa muda wa kutegemea jua kukausha mazao umepitwa na wakati. Jambo la muhimu ni kitengo cha kuhifadhi nafaka kuwa na mashine ya kuweza kukausha mahindi jambo  hilo litaweza  kumkomboa mwananchi kwa kuuza mazao yeke kwa muda Mwafaka.
Waziri wa Kilimo pia amekemea  suala  la mahindi kuwa na daraja la chini wakati kitengo kina maghala ambayo yana ubora  wa kisasa, akieleza hasara waliyoipata Serikari mwaka jauzi amesema zaidi ya tani 8000 zilikuwa na daraja la chini na mahindi hayo yalilazimika kuuzwa kwa shilingi 350 badala ya kuuza shilingi 600 kwa kilo .amesema jambo hilo hataki kusikia tena.


Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi  Nchini Tanzania Dr  Charles John Tizeba  katika ziara yake mkoani Ruvuma amewahimiza  wananchi kulima mahindi  kwa wing ili kukabiliana na hali ya hewa

Amesema  nyanda za juu kusini zitaendelea kuwa na mvua  nyingi, hivyo mahindi watakayozalisha mwaka huu yatakuwa na soko kwa kuwa soko la mahindi ni kubwa.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr. Charles John Tizeba amesema Mawakala waliokuwa wakisambaza Pembejeo  za Kilimo  Nchini Tanzania wamechelewa kulipwa  fedha zao kutokana na madai yao ya malipo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.1 kupishana na hali halisi ambayo ni shilingi milioni 238, Waziri amesema Serikali ingapata hasara kwa kuwalipa mawakala kiasi cha shilingi bilioni 4.1.


Waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi Dr Charles Tizeba amesema baada uhakiki na kubaini Malipo halali Serikali itanza kulipa Malipo halali yaliyobainika baada ya uchunguzi wa kina kwa kuhoji kila mtu aliyepata ruzuku ya pembejeo.


Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dr. Charles John Tizeba akizungumzia suala la ununuzi Mahindi kupitia Hifadhi ya Chakula amesema Serikali iliweza kuidhinisha ununuzi wa Mahindi Tani 22,000 lakini Tani zilizonunuliwa Hifadhi ya Kanda ya Songea ni Tani 10,000.

Waziri wa Kilimo Dr Charles Tizeba amesema sababu ya kupata Tani 10,000 imetokana na soko kukua, Hifadhi ya Chakula ilikuwa ikinunua kwa bei ya shilingi 580 kwa kilo vijijini na mjini kwa kilo shilingi 600 lakini hata hivyo wafanya biashara waliongeza na kununua kwa shilingi 680 kwa kilo jambo lililowapelekea wakulima kukimbilia kuuza mahindi yao kwa wafanya biashara. Jambo ambalo Serikali imefurahia kwa kuona Mkulima anafaidika na Kilimo na hiyo ndiyo shabaha ya Serikali kutaka kumuokoa mkulima.


Amesema huu ni uzembe wa wasismamizi katika vitengo vya Hifadhi amesema hataki kusikia suala la mazao kuwa chini ya kiwango (under grad) endapo suala hilo litatokea tena basi Mkuu wa Kitengo atakuwa amejifukuza kazi.



Waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi akifafanua kuhusu suala la vitengo kuchelewa kuanza msimu wa ununuzi wa mazao yakiwemo  mahindi hadi mwezi wa nane kwa madai ya kusubiri unyaufu , Waziri Tizeba amesema baada ya teknolojia za  kisasa kuongezeka hakula sababu ya kusubiri jua likaushe Mahindi, bali vitengo vya Wakala wa hifadhi ya chakula ya Taifa vitafute mashine ya kakaushia mahindi ili wananchi mara wanapovuna waweze kuvuna mara moja badala ya kukaa zaidi ya miezi mitatu wakisubiri kufunguliwa kwa magulio maagizo hayo yameenda sambamba na kuanza kwa gulio la Tumbaku.
Waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi Dr Charles Tizeba amesema kiongozi yeyote atakayesababisha kuteremka kwa daraja la Mazao yanayozalishwa na wananchi kuteremka baada ya kuingizwa ghalani basi kiongozi huyo atakuwa amejifukuza kazi


Waziri wa Kilimo akiongelea kuhusu suala la Ruzuku za Pembejeo za kilimo amesema mfumo wa ruzuku hauwezi kukwamua changamoto za kilimo amesema jambo la muhimu ni Serikali kushusha bei za Pembejeo kwa kuagiza kwa wazalishaji badala ya kununua kwa madalali, akitoa mfano amesema pembejeo imeteremka kwa asilimia 38% kwa sasa mfuko wa mbolea unauzwa kwa shilingi 48,000 Serikali inafanya jitihada pembejeo iweze kuteremka hadi iuzwe kama inavyouzwa sukari.


Dr. Tizeba akiwa Mkoani Ruvuma aliweza kutembelea Maghala ya watu binafsi na Maghala ya Serikali na kuona hali ya chakula na kuridhika kutokana na chakula kilivyo katika Maghala hayo.

Waziri amewaomba wanaouza chakula kwenda sambamba na kipato cha mtanzania bila kusababisha mfumuko wa bei ambao mtu wakawaida atashindwa kununua chakula hicho
Waziri wa Kilimo katika Ziara hiyo alitembelea soko la mazao la Manzese na kuongea na wananchi na wafanyabiasha ya mazao wa soko hilo lililopo Manispaa ya Songea
Waziri wa Kilimo Dr Tizeba akiongea na wafanyabiashara wa SODECO Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Waziri wa Kilimo aliwatembelea wafanya biashara hao kujua changamoto zinazowakabili katika zao la Mahindi.
Waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi  akiwa ziara katika manispaa ya Songea kusikiliza kero za wakulima katika msimu huu wa kilimo
Waziri akifafanua kwa wakaazi wa Manispaa ya Songea juu ya Malengo ya wizara ya kilimo katika kumsaidia mkulima aweze kulima kwa tija
Wafanyabiashara wa Soko la SODECO Manzese wakimsikiliza waziri wa Kilimo Mifugo na uvuvi alipowatembelea katika eneo lao
Waziri Mkuu aliweza kutembelea wafanya biashara ya Mahindi wenye maghala binafsi
Waziri na Wakulima Manzese Soko la SODECO Manispaa ya Songea
Wafanya Biashara ya mazao katika soko la SODECO Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
Waziri Tizeba akihoji juu ya Ununuzi wa Mahindi kwa wafanya biashara wadogo
Ghala la Mtu binafsi Mtakanini wilayani Namtumbo  ambalo alilitemb elea waziri wa Kilimo kuona namna waavyohifadhi mazao yao.
Waziri wa Kilimo akiongea na Mfanya Biashara ya mazao Mzee Alfani mwenye akiba ta Tani 80 za Mahindi ambaye ameagiza wataalamu kumsadia utaalamu wa jinsi ya kuhifadhi mahindi yasiharibike.
Waziri akishauri njia bora za kuhifadhi nafaka na kuzifanya zisiharibike amesema zisipohifadhiwa kitaalamu wafanyabiashara watapata hasara.
Waziri akiwa Nyumbani kwa Mzee Yasini mfanya Biashara wa Mahindi katika Kijiji cha Mtakanini wilayani Namtumbo Mkoa wa Ruvuma
Shehena ya Mahindi yakiwa katika Hifadhi ya Chakula ya Kanda ya Songea
Watumishi wa Wakala wa hifadhi ya Chakula Kitengo cha Kanda ya Songea wakipokea Maagizo toka kwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi