KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, May 26, 2017

WADAU WA SEKTA UTALII WILAYANI TUNDURU WABUNI MBINU YA KUTUMIA NDEGE KATIKA KUPAMBANA NA UJANGIRI WA WANYAMA PORI



Kaimu Mkurugenzi wa uzuiaji wa Ujangiri dhidi ya wanyama Pori Robert Mande  amewaasa wananchi kuachana na ujangiri kwa sababu sasa hivi biashara ya pembe za ndovu hazina soko kwa kuwa wafanya biashara wakubwa wa biashara hiyo wamesha kamatwa  kudhihirisha hilo hata mizoga ya tembo walio kuwa wana uwawa imepungua kutoka 184 hadi kufikia mizoga 84



Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Tunduru amewataka watu wanaomiliki Silaha za kijeshi kuzisalimisha kwenye Vituo vya Polisi



Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Tunduru ameyasema hayo baada ya Tembo wawili kuuwawa na mmoja kung`olewa meno yake katika Kijiji cha Wenje Tarafa ya Nalasi.



Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Tunduru Juma Homera amesema imebainika kuwa wananchi wanaoishi karibu na miapaka ya Nchi jirani wanapata silaha za kijeshi kwa kubadilishana silaha hizo na chakula amesema wale wote wenye silaha hizo wazisalimishe.



Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama Juma Homera amesema watuhumiwa waliokamatwa kuhusika na tukio hili la ujangiri wako 8 nane ambao walikutwa na silaha zilizotumika kuuwa wanyama na baadhi ya pembe za ndovu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wilaya ya Tunduru akiwataja watuhumiwa hao amesema wa kwanza ni Juma saidi Ally(36) , Mwinyi Omary (24), Salumu Charamanda Aski (46), Kalengo Mkenda( 45), Fadhili Mohamed( 43), Abduli Shaibu (37), Ahamad Yasini( 30), Rashid Hausi (46)
Naye Afisa Upelelezi kutoka Kitengo cha Ujangiri Makao Makuu Dar es Salaam amesema wahalifu wamekuwa wakifanya vitendo vya Ujangiri kwa kujidanganya watakuwa salama kwa kuwa wanatumia dawa za kienyeji zinazowaaminisha kutokamatwa pindi wanapofanya ujangiri huo.
Majangiri wamekuwa wakitumia silaha za risasi wakati wa kutekeleza dhima yao ya kuangamiza wanyama ambao ni rasilimali za Taifa jambo ambalo haliwezi kuungwa mkono na Serikali.


Kaimu Mkurugenzi wa Oparesheni za kuzuia Ujangiri Taifa amesema mpaka sasa kuna watu 320 ambao wamekamatwa kwa makosa ya Ujangiri na watuhumiwa 284 wamefikishwa mahakamani  pia kuna Taarifa ya watu 1006 kuwa  ni Majangiri amewataka watu wanaojihusisha na Ujangiri wajisalimishe.

Kaimu Mkurugenzi wa Kikosi cha Kupambana na Ujangiri Taifa akitoa Elimu kwa wananchi wa wilaya ya Tunduru juu ya Madhara ya kuangamiza waanyama pori na kutumia kitoeo pasipo kuzingatia taratibu za kiafya.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru amesema wananchi waliohusika na tukio la ujangiri na kukimbia watasakwa popote walipo ili kuhakikisha wanachukuliwa hatua stahiki na vyombo vya dola.
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika Tarafa ya Nalasi eneo la Tukio ambako Tembo wawili waliuwawa na wananchi.
Afisa Upelelezi akionyesha dawa ambazo zimekuwa zikitumiwa na wanaojihusisha na Ujangiri na kuamini wakifunga dawa hiyo serikali haiwezi kuwakamata inawalinda.


Mratibu Maximillan Janes wa Shirika la  PAMS Foundation linalojishughulisha na Mapambano dhidi ya Ujangiri  amesema shirika lime toa ndege mbili ambazo zita husika na kulinda wanya wasiingie katika makazi ya watu pia kufuatilia mienendo ya watu wanao jihusisha na ujangili



Aidha Mratibu amesema wananchi wakiona wanyama wameingia katika makazi watoe taarifa ofisi ya mtendaji ili kuweza kusaidia  mara moja kuwafukuza wanyama hao, pia katika kuepukana na uvamizi wa tembo wananchi katika mashamba yao wajaribu kupanda pilipili kwa kuwa adui mkubwa wa Tembo ni pilipili



Shirika la kimataifa la PAMS Fondation lina fadhili njia mbalimbali za kupambana na ujangiri na kulinda usalama wa wanyama na mali za raia katika maeneo jirani na hifadhi kwa kuhakikisha wanyama wana kuwa salama muda wote, Wananchi kuanzia watambue kuwa  Wanyama walioko katika mbuga zao ni mali yao kwani fedha za utalii zinazo patikana zinasaidia Nyanja mbalimbali katika jamii ikiwemo Elimu,Afya,na mindombinu mbalimbali.

Nao wananchi wa wilaya ya Tunduru wameomba Serikali kuwadhibiti wanyama waharibifu kabla ya kuleta madhara kwa binadamu kwa kuharibu mashamba ama kuvamia makazi ili kuepukana na migongano inayojitokeza kati ya Wananchi na Viongozi wa Serikali.
Wananchi hao wakiwa katika Mkutano wa pamoja na viongozi wanaohusika na kupaambana na Ujangiri wamesema wao wapo tayari kufuata taratibu kwa kulinda wanyama wa asili lakini wanaomba Maafisa wanyamapori wanapotembele doria katika Hifadhi kutumia busara badala ya kutoa vitisho kwa wananchi.