KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 30, 2017

BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYASA LIMEMFUKUZA KAZI AFISA UTUMISHI KUTOKANA NA MAKOSA YA KINIDHAMU KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Nyasa limemfukuza kazi Afisa Utumishi  wa wilaya ya Nyasa kwa tuhuma za kujipatia Mshahara hewa kwa njia ya Udanganyifu kiasi cha shilingi milioni 25

Katibu wa Baraza la Madiwani ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dkt  Oscer Mbyuzi amesema Baraza limeamua kumfukuza Afisa Utumishi  Maiko Alex Mbunda kwa kukiuka maadili ya Utumishi wa Umma.


Mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa amesema  Halmashauri ya wilaya ya Nyasa imeweka mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani wa Halmashauri hiyo ili  kuinua kiwango cha Elimu na  kurudisha hali ya zamani ya ufaulu ambapo huko nyuma  Halmashauri ya Nyasa iliweza kutoa wasomi wengi na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

 Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya kwanza katika mwaka 2017/2018 ulioanza july - october 2017 katika ukumbi wa Capten Komba Mbamba Bay wilayani Nyasa.
Wajumbe wa Baraza wakizungumza kuhusu kushuka kwa Elimu wamesema ili Elimu ipande kunahitajika ushirikiano baina ya wazazi, walimu wana siasa na jamii nzima kila mmoja akitimiza wajibu wake heshima ya halmashauri ya wilaya ya Nyasa kutoa wasomi wengi itarejea.
 Wajumbe wakiendelea kuchangia juu ya suala la Elimu wamesema inasikitisha kuona wazazi wamekuwa wakiwa wepesi kunyooshea vidole walimu pindi matokeo yanapokuwa hayaridhishi bila kujiuliza wao kama wazazi wanawajibika vipi kushirikiana na walimu katika kupandisha kiwango cha Elimu kwa watoto wilaya ya Nyasa.
Wilaya ya Nyasa katika Matokeo ya Mtihani wa darasa la saba 2017 imekuwa ya 171
mwaka jana ilikuwa nafasi ya 139kitaifa.
 Katika kikao hicho pia Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Nyasa limeweka mikakati ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kusogeza huduma kwa wananchi katika sekta ya Maji Kilimo na Uvuvi.
 Wajumbe wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Nyasa wakipitia Agenda za Kikao wakati mwenyekiti wa Halmashauri Alto Komba akiongoza Kikao.
Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Dkt Oscer Albano Mbyuzi amesema wilaya ya Nyasa ni wilaya yenye fursa nyingi za kiuchumi hivyo anaomba wadau mbalimbali kwenda kuwekeza viwanda vidogo vidogo katika Halmashauri hiyo.