KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Saturday, April 28, 2018

JEE UNAJUA VIVUTIO VYA ZIWA NYASA VILIVYOKO MKOA WA RUVUMA

  1. Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.
    Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.
    Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.[​IMG]
    Mwonekano wa Jiwe la kihistoria kwa ubavuni linalojulikana kwa jina Pomonda lililopo Ziwa Nyasa lililotumiwa kujificha na wananchi wakati wa Vita vya Dunia.

    [​IMG]
    Jiwe la POMONDA likionekana kwa nje katika Ziwa Nyasa eneo la Liuli.
    [​IMG]
    Kivutio kimoja wapo katika Mwambao wa Ziwa Nyasa katika eneo jirani na Jiwe la Pomonda ni Machweo ya Jua (SUNSITE)kama yanavyoonekana pichani kwa mbali
    [​IMG]
    Jiwe la POMONDA lililopo katika Ziwa Nyasa hapo ni nje ya Pango ambalo kwa ndani lina uwezo wa kuhifadhi watu 250 kwa wakati mmoja hapo ni namna maji kupwa yanavyoonekana pembeni mwa jiwe hilo.
    [​IMG]
    Ufukwe wa Ziwa Nyasa namna unavyoonekana pichani na kuvutia kwa Madhari ambapo shughuli za kiuchumi kwa Wananchi wa Ziwa Nyasa huzifanya eneo la Mwambao wa Ziwa Nyasa au kuvuka Nchi jirani ya Malawi ambayo imetenganishwa na Ziwa Nyasa.
    [​IMG]
    Washiriki wa Mdahalo wa Mabadiliko ya HAli ya Hewa uliofanyika Liuli Wilayani Nyasa kwa Ufadhili wa Foundation for Civil Society wakionyesha Jiwe la POMONDA linalovutia watalii mbalimbali wanaokuja kutembelea Ziwa Nyasa.
    [​IMG]
    Hapo ni Meli ya MV Songea ambayo hutumika kusafirisha Abiria na Bidhaa kutoka Tanzania kuelekea Malawi kupitia Ziwa Nyasa ikiwa imetia Nanga Liuli Ziwa Nyas

    [​IMG]

    Kutoka eneo la Ufukwe mpaka kulifikia Pango hili la Pomonda kuna umbali wa kilometa moja na robo. Pango hili la Pomonda limezungukwa na Miti ya Asili ambayo uneune wake hauzidi robo mita na umri wa miti hiyo yapata miaka 100,pango hili la Pomonda pia limezungukwa na Mawe yenye umbo la Mafiga Matatu kuzunguka eneo hilo mpaka kulimaliza unachukua muda wa saa . Hapo Mwandishi wa Habari Adam Nindi baada ya Kuzunguka katika kulifikia pango hilo inaonyesha jinsi gani alivyochoka akiwa amelala chini.
    [​IMG]
    Taarifa zilizotolewa na Wazee waishio katika eneo la Mwambao wa Ziwa nyasa wamesema kipimo cha ujazo wa Maji ya Ziwa Nyasa kujua yanapungua au yanaongezeka ni alama hizo zinazoonekana mistari mieupe na rangi nyeusi kuwa ziwa limepungua maji kwa kiasi kikubwa ambapo awali yalifikia katika mistari inayoonekana kwenye jiwe hilo ewa.

    Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.

    Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

    Eneo la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.

    Sababu ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani palikuwa na mpaka wa kimataifa kaskazini mwa ziwa. Baada ya 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyasaland). Kwa kusudi la kurahisisha utawala mambo yote yaliyohusu ziwa yaliwekwa chini ya serikali ya kikoloni ya Nyasaland.


    Baada ya uhuru Malawi ilijaribu kutumia uzoefu huo kama haki yake ya kitaifa. Polisi yake ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa baada ya uhuru. Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania halikusumbua tena wavuvu au feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.

    Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500). Aina chache tu zinavuliwa kama chakula lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki zenye rangi.



  2. Nyati

    Nyati JF-Expert Member

    #2
    Nov 7, 2014
    Joined:Mar 6, 2009
    Messages:2,087
    Likes Received:417
    Trophy Points:180


    Thanks! Ni taarifa nzuri sana kwa kweli, lakini kama taarifa hii hujaitayarisha wewe ni vizuri ukamtaja mtayarishaji kama kutambua mchango wake katika kufanikisha kazi hii
  3. wiseboy.

    wiseboy. JF-Expert Member

    #3
    Nov 7, 2014
    Joined:Aug 11, 2014
    Messages:3,076
    Likes Received:2,420
    Trophy Points:280


    Malawi wanatutafuta nini? natamani sana tuwachape.
  4. p

    pembe JF-Expert Member

    #4
    Nov 7, 2014
    Joined:Nov 4, 2010
    Messages:2,058
    Likes Received:70
    Trophy Points:145


    Hongera sana kwa kutuelimisha vilivyo. Ila hujatutajia sifa za bandari ya Mbamba bay. Hilo pango waweke umeme wa solar watalii na wanafunzi waweze kuona muundo wake ulivyo. Kwetu walichimba mapango chini ya ardhi na vita vikija wanaingia humo na mifugo yao. Waliweka sehemu ya mifugo, kulala, tundu la kutokea mtoni kuchota maji, tundu la kutolea moshi n.k. Kwa kweli sayansi ya nyakati hizo ilkuwa kiboko.
  5. Mamndenyi

    Mamndenyi JF-Expert Member

    #5
    Jul 12, 2017
    Joined:Apr 11, 2011
    Messages:29,329
    Likes Received:7,283
    Trophy Points:280


    Haya mambo muhimu huwa hayana wasemaji;
  6. mrangi

    mrangi JF-Expert Member

    #6
    Jul 12, 2017
    Joined:Feb 19, 2014
    Messages:23,840
    Likes Received:10,430
    Trophy Points:280



    Ngj tumalize kamatakamata na kesikesi alafu tutakuja huko

    Ova
  7. MziziMkavu

    MziziMkavu JF-Expert Member

    #7
    Jul 12, 2017
    Joined:Feb 3, 2009
    Messages:39,728
    Likes Received:4,831
    Trophy Points:280

    Unaonaje na wewe ukaleta Historia yako na kumuweka aliye tunga hiyo Historia?
  8. Dragoon

    Dragoon JF-Expert Member

    #8
    Jul 13, 2017
    Joined:Nov 24, 2013
    Messages:6,775
    Likes Received:6,931
    Trophy Points:280

    asante na hongera sana mleta mada, ni elimu nzuri
  9. Che mittoga

    Che mittoga JF-Expert Member

    #9
    Jul 13, 2017
    Joined:Mar 28, 2017
    Messages:1,620
    Likes Received:1,574
    Trophy Points:280

    Asante sana Mzizimkavu kwa habari hii nzuri.
    Kweli Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii.
    Swali kwa wadau.
    Malawi wanasema ziwa Nyasa lote ni lao.
    Cha ajabu wanaidai Tanzania pekee lakini
    Msumbiji hawawadai wakati ziwa hilo linamilikiwa pia na Msumbiji.
    Ivi kwanini Malawi hawawasumbui Msumbiji katika kuwadai ziwa Nyasa na badala yake wanaisumbua Tanzania pekee ?
  10. Romaxtim

    Romaxtim Member

    #10
    Jul 14, 2017
    Joined:Jul 14, 2017
    Messages:8
    Likes Received:2
    Trophy Points:5


  11. Don san tan

    Don san tan JF-Expert Member

    #11
    Jul 23, 2017
    Joined:May 23, 2015
    Messages:398
    Likes Received:254
    Trophy Points:80

    KUMBE HAWA MALAWI WANATAKA KUPIGWAAA.. NAOMBA TUISHI VIZURI NA MAJIRANI ZETU HASA HAWA WADOGO WADOGO WAKINA MALAWI


  12. daaaah umeniludisha home kabisa kwetu lupingu nyasa ludewa ku



Friday, April 13, 2018

FURAHA YA KWANZA KATIKA DUNIA HII KWA MZAZI YEYOTE NI PALE ANAPOPATA MTOTO NA KUMUONA AKIWA NA USTAWI NZURI LAKINI JEE ULISHAWAHI KUJIULIZA CHANGAMOTO ZA MALEZI YA MTOTO HUYO AMA ULISHAFANYA MAANDALIZI KABLA YA KUPATIKANA KWA MTOTO

 Ni ukweli usiopingika kuwa furaha kubwa katika maisha ni kuwa na mtoto na kwa mzazi wa kike anaanza furaha ya mapenzi ya mtoto kbla ya kuzaliwa kwa mtoto lakini kwa baba furaha yake ya kwanza ni ile kuitwa baba hujikuta kuwa amepanda wadhifa fulani lakini baadhi ya wababa wanasahau kutimiza wajibu wao kwa watoto katika malezi jambo ambalo ni tofauti na mama.
 Hakuna Mzazi ajuaye Kesho yake, ni wajibu wa kila mzazi kutengeneza maisha ya baadaye ya mwanae mara tu wanapokuwa katika matarajio ya kuzaliwa kwa mtoto  kwani salio la maisha lipo mikononi mwa Mungu pekee. Pichani ni Bibie Sarah Gabriel akitabasamu kuashiria furaha ya kuingia katika malezi ya Mwanae kipenzi Hythamy ni wazi kuwa hata baba wa Mtoto ana furahi pia kumuona mtoto wake akiwa na bashasha Lakini Jee wanatambua wajibu wao kwa Mtoto katika kumtimizia mahitaji yake ya msingi na kutimiza ndoto zake?...!
Mtoto Hythamy akiwa na furaha haelewi lolote katika umri huu wa miezi mi nne akiwa ndo kwanza anayaanza maisha ya ulimwengu, jambo la muhimu kwa wazazi ni kufanya maandalizi mema ya kumtengenezea maisha mtoto wao katika malezi, elimu na msingi wa maadili mema. Siku hizi kumeibuka tabia ya wazazi kukwepa majukumu kwa watoto kwa kutotimiza wajibu wao na kupelekea wimbi la watoto wenye mmomonyoko wa maadili.

Turejee mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye ameanzisha kampeni ya kuwasaidia msaada wa kisheria wanawake waliotelekezewa watoto wao jambo ambalo halina hatia kwa watoto wetu, wazazi tunapaswa kujitathmini katika ili na kujiuliza sisi tumetoka wapi?

Aidha akina mama wanaotupa watoto wachanga ebu tumrudie Mungu jiulize mtoto kama huyo hapo juu ana kosa gani mpaka unamtupa kwa kisingizio cha ugumu wa maisha au kutoelewana baina yenu wazazi tambua watoto hawausiki hawapaswi kabisa kupewa adhabu ya makosa ambayo hawakuwahi kushiriki hata punje wala kushuhudia malumbano ya mahusiano yenu.

Thursday, April 12, 2018

WAKALA WA MAJENGO TBA IMEKABIDHI MABWENI MATATU NA MADARASA MAWILI YA WASIOONA SONGEA


WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wamekabidhi mabweni matatu na madarasa mawili ya shule ya msingi Luhira iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi huo na Manispaa ya Songea, Meneja wa TBA Mkoa wa Ruvuma Edwin Nunduma amesema mradi huo ulihusisha ujenzi wa mabweni matatu na ukarabati wa madarasa mawili kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 151
Kwa mujibu wa Meneja huyo wa TBA kila bweni Lina uwezo wa kulaza wanafunzi 12 hivyo mabweni matatu yatalaza wanafunzi wenye ulemavu 36.

Mkuu wa shule hiyo Joyce Konga ameishukuru serikali kwa kuwajengea mabweni ya kisasa na kukarabati madarasa mawili ambayo pia yana Mazingira rafiki kwa wenye ulemavu,  amesema shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 48 wenye ulemavu na kwamba baadhi ya wanafunzi wenye umri mdogo watalazimika kulala wawili wawili.

Shule ya msingi Luhira ndiyo Shule pekee yenye kitengo cha wasioona mkoani Ruvuma ambayo ilianzishwa mwaka 1929 na kitengo cha wasioona kilianzishwa mwaka 1982

Shule ya msingi Luhira ina jumla ya wanafunzi 1300 kati yao wenye ulemavu ni 48.Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alitembelea shule hiyo na kukabidhi magodoro 24 yenye thamani ya shilingi milioni 1.8 kwa ajili ya wanafunzi wasioona wanaosoma katika shule hiyo.