Serikali Mkoani Ruvuma imetoa
tahadhari kwa wale wote waliojiandaa
kufanya vurugu wakati tukielekea katika uchaguzi kuvuruga Amani tuliyonayo, Serikali itachukua
hatua kali za kisheria za kupambana na
watu hao
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo katika futuru
ya Mwezi wa Ramadhani iliyoandaliwa Ikulu ndogo ya Songea na kujumuisha Waumini
wa Dini ya Kiislamu na Wakristu wakiwemo ma Askofu na Masheikh
Wanawake wakiwa katika futuru iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga wamewaomba wanawake wenzao kusimamia maadili ya vijana na watoto wao majumbani wanaokengeuka kwa kutamani kuchochea vurugu na kupoteza amani iliyopo. Wamesema wamama kama walezi wa familia wana wajibu wa kuelimisha watoto wao na kuzuia kujiunga na masuala yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria Futuru ya Mwezi wa Ramadhani iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Bakari Nalicho, Viongozi wa kisiasa na viongozi wa dini ya kikristo ngazi ya mapadre na Maaskofu
Waumini waliohudhuria katika Futari ya mwezi wa Ramadhani 2015 Ikulu ndogo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wameomba Viongozi wa Dini kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha Amani ya Tanzania inaendelea kudumishwa kwa kuhubiri amani upendo na Mshikamano katika Misikiti na Makanisa na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Oktoba 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said
Thabit Mwambungu amesema dalili ya mvua ni Mawingu lakini Serikali imejidhatiti
kukabiliana na Vurugu zozote zitakazojitokeza , Serikali haitamvumilia Kiongozi yoyote wa dini au wa
Kisiasa kufanya uchochezi kwa waumini
wake ili kuhatarisha amani serekari ita kuwa macho muda wote.
Sheikh wa Mkoa wa madhehebu la Suni Shaban Chitete aliweza kuiombea Nchi ya Tanzania
ili iendelee kuwa na Amani pamoja na kuwalinda viongozi waliopo .
No comments:
Post a Comment