Dr Kayeke ameyasema hayo wakati akiongea na Vikundi vya wakulima wa Mashamba darasa yaliyopo Namtumbo yenye lengo la kuendeleza Kilimo cha Mahindi kwa kutoharibu aridhi kwa kutumia Mabingobingo(Napier grass) na meimea ya Desmodium ili kuongeza rutuba.
Shamba Darasa la Mkulima wakulima wa Namtumbo likionekana limestawi mimea ya mikunde ya Desmodiua kwa ajili ya kuzuia mbegu za viduha kuota na kufukuza wadudu waaharibifu wanaobungua mahindi shambani (Stock boores).
Wakulima wa Zao la Mahindi wakiwa katika shamba darasa ambalo limepandwa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo na Mtafiti wa Kilimo kutoka Mikocheni Dr Juma Kayeke chini ya usimamizi wa Mratibu wa mashamba Darasa wilaya ya Namtumbo Sammy Mwakyusa wameomba kuendelea kupewa Elimu ya Kitaalamu ili waachane na Kilimo cha Mazao na kulima Kilimo chenye tija.
Wakulima wa Namtumbo wakikagua Shamba Darasa lenye uoto wa mahindi, mabingo bingo pembeni na Desmodium katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mahindi.
Mimea ya Mabingo bingo ikiwa imezunguka shamba ili kuvuta wadudu wanaoharibu Mahindi kukimbilia kwenye mabingobingo badala ya kushambulia mahindi. Kwa mujibu wa Dr Kayeke mtafiti wa kilimo na Uendelezaji wa zao la Mahindi amesema mabingo bingo pia yakichanganywa na Desmodium ni chakula kizuri chenye vitamini kwa wanyama kama Ng`ombe na Mbuzi.
Dr Juma Kayeke na wakulima wa Shamba darasa la mahindi lililopo eneo la magereza Namtumbo wakielezea jinsi watakavyonufaika na kilimo hicho kwa kupunguza gharama za uendeshaji wa kilimo na kupata faida ya chakula cha mifugo kupitia mimea ya Desmodium na Mabingobingo.
Akiainisha faida za kutumia kilimo cha Sukuma Vuta, Dr Juma kayeke amesema lengo ni kudhibiti viduha lakini pia kupitia mimea ya Desmodium inasaidia kupambana na ukame kwa kuwa mimea hii inasaidia kuhifadhi unyevu.
Wakulima wa wilaya ya Namtumbo wameshukuru kuletewa Elimu hii wameomba iwe endelevu na isiishie kwenye zao la Mahindik pekee ili mkulima aweze kunufaika na Kilimo.
Dr. Kayeke akitoa ufafanuzi jinsi Mbegu za Desmodiuma zinavyofanya kazi zikiwa shambani .
Dr Kayeke amesema ataendelea kushirikiana na wakulima wa Namtumbo katika kushirikishana utaalamu wa Kilimo bora anachohitaji mafundisho wanayoyapata yasiishie kwenye mashamba darasa bali elimu waisambaze kwa wengine na kila mmoja aone manufaa kupitia shamba lake.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya namtumbo ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya hiyo katikati akiwa na watgaalamu wa Kilimo kushoto ni Sammy Mwakyusa mratibu wa Mashamba darasa na kulia ni Mtafiti wa Kilimo Dr Juma Kayeke katika Shamba Darasa Namtumbo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mtani Martin amesema Technolojia hii ni nzuri hasa kwa wafugaji kwa kuwa ikitumika vizuri hakuna cha kupoteza mkulima ataweza kuvuna kwa tija na upande wa pili atanufaika na chakula cha mifugo, Ameomba wakulima wawatumie wataalamu ipasavyo ili kunufaika na fursa zinazopatikana kupitia kilimo kwa ustawi wa jamii.
Kaimu Afisa Mifugo wilaya ya Namtumbo Said Lwanda amethibitisha umuhimu wa Mabingo bingo na Desmodium kwa mifugo na kwamba mimea hiyo haina madhara yoyote kwa mifugo.
Wataalamu wa Kilimo na Mifugo wa wilaya ya Namtumbo wakiongozwa na Mtafiti wa Kilimo kutoka Mikocheni wakizunguka mashamba darasa kujionea manufaa ya kilimo cha kutumia technolojia ya Sukuma Vuta.Shamba la Mahindi likiwa limezungukwa na Mimea ya Mabingobingo ili kuzuia viduha waharibifu wa mahindi.
Wakulima wa Mahindi wilaya ya Namtumbo wakipokea Elimu ya Kilimo bora cha kutumia technolojia ya sukuma vuta kupitia mimea ya Desmodium na Mabingo bingo.
Mratibu wa Vikundi vya Mashamba Darasa ya wakulima wila ya Namtumbo Sammy Mwakyusa amewaomba wakulima kuwashirikisha watoto elimu ya kilimo cha kitaalamu ili iwe na tija kwa familia nzima badala ya kushiriki wazazi peke yao kwa kuwa vijana ndio kizazi kinachopaswa kuendeleza kilimo chenye manufaa.
Shamba la Mahindi lililozingatiwa Elimu ya Sukuma vuta kwa kupanda Desmodiuma na Mabingobingo wilaya ya Namtumbo
Dr Juma Kayeke akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Namtumbo Mtani Martin alipotembelea moja ya mashamba darasa yanayosimamiwa na Dr Juma Kayeke katika kuendeleza zao la mahindi.
No comments:
Post a Comment