Miche ya Miti 3,255,230 imepandwa katika Mashamba ya Miti ya Wino na Ifinga ikiwa na thamani ya shilingi Milioni 300. na Miche Milioni Moja bado ipo katika Vitalu vya Wino na Ifinga.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge akiwa katika eneo la Vitalu vya Miti lililopo Ifinga Halmashauri ya Madaba Songea Vijijini kujionea hali ya Mradi wa Uendelezaji wa Kilimo cha Miti kupitia Wakala wa Huduma za Misitu TFS
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na viongozi wa Halamashauri ya Madaba na wilaya ya Songea wakipokea maelekezo ya hali ya Mradi wa kuotesha Miche ya Miti wakati alipotembelea Vitalu vya Mkongotema Songea Vijijini.
Mkuu wa Mkoa akikagua Mradi wa Uoteshaji miti amesema kila mmoja ana wajibu wa kuhifadhi misitu kwa ajili ya kuepuka mabadiliko ya Hali ya Hewa yanayopelekea kuvuruga ratiba za mvua. Amesema mradi wa miti wa vijiji vya Mkongotema, Wino na Ifinga unasaidia kutoa fursa ya ajira kwa vijana lakini pia unahitaji wawekezaji kutokana na miti inayokuzwa katika hifadhi hizo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma mhandisi Binilith Mahenge katika Ziara yake ya kukagua uoteshaji wa Miti katika Mashamba ya TFS kwenye vitalu vya miti vya Ifinga aliona Miche 3,000,000 ikiwa imehudumiwa vizuri ameagiza wananchi na viongozi wa maeneo ya mradi kushirikiana na Wakala katika kusimamia kuhakikisha uchomaji wa moto unadhibitiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge amesema itakua ni aibu kuona jitihada zinazofanywa na wahifadhi wa mazingira zikififishwa na wananchi kwa kuchoma moto endapo itabainika uchomaji wa moto kiholela viongozi wa Serikali ya vijiji watawajibishwa.
Meneja wa Wakala wa Hifadhi ya misitu (TFS) anayehudumia Mashamba ya Miti ya Ifinga, Wino na Mkongotema Hamisi Ally Ghaji amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha inaimarisha mazingira mazuri ya vizazi vijavyo kwa kujenga uchumi kwa kupanda iti ambayo itakua Rasilimali ya Taifa Baadaye na kuongeza Mapato.
Afisa Maliasili Mkoa wa Ruvuma na Mshauri Mkuu wa Mali Hai akimwelekeza Mkuu wa Mkoa Mhandisi Dkt Binilith Satano Mahenge katika Chuo cha Mifugo Liti Madaba kuhusiana na Hifadhi ya Gesi Maso ambayo ina Rasilimali ikiwemo Mafuta, Gesi na Makaa Mawe. Amesema Hifadhi hiyo pia ina Bonde muhimu kwa Mazalia ya Samaki aina ya Mbelele, Ningi na Mbasa.
Baadhi ya Vibarua wa Upandaji miti ambao wananufaika na mradi huo kwa kujipatia ajira inayowawezesha kumudu kujenga nyumba na kuendesha maisha ya familia zao wakiendelea na kazi ya kuatika miche ya miti na kuhudumia katika vitalu vya Ifinga.
Afisa Maliasili Mkoa wa Ruvuma Africana Chares amesema katika kuendeleza Programu ya upandaji wa Miti ya Biashara Jumla ya Hekari 80,000 zimetengwa kwa ajili ya upandaji wa Miti.
Wakala wa Hifadhi ya Huduma za Misitu wanashirikiana na Halmashauri ya Madaba na Wananchi wa kawaida katika kuendeleza Mradi huo, changamoto kubwa ni miundombinu ya barabara hairidhishi kutoka Wino kwenda Ifinga katika eneo la vitalu jambo ambalo halmashauri ya Madaba pamoja na Meneja wa TFS wamekubaliana kushirikiana kuiboresha Barabara hiyo iweze kupitika wakati wote.
Pamoja na Jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali wa mazingira katika kuhifadhi Mazingira, Hifadhi ya Misitu ya Gesi Maso inakabiliwa na changamoto ya kuvamiwa na Jamii ya Wafugaji kuingiza Mifugo ambapo kuna Ng`ombe wapatao 18,403.
Changamoto nyingine katika Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira ni uchomaji wa Mkaa unaofanywa na baadhi ya wananchi katika kujitafutia ridhiki ambako kunasababisha ukataji miti ovyo na kusababisha jangwa.
Afisa Maliasili Mkoa wa Ruvuma Africa Chares akiwa na Afisa Wanyapori wa Ripalamba wilayani Mbinga akirekodi maagizo ya Mkuu wa mkoa katika kuboresha uhifadhi wa Mazingira.
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa nje ya Jengo la Ofisi za wakala wa Hifadhi ya huduma za Misitu walipotembelea katika Kijiji cha Mkongotema kuona kazi za uoteshaji miti zinavyoendelea.
Viongozi mbalimbali walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika kukagua shughuli za upandaji wa Miti zinazosimamiwa na Halmashauri ya Madaba. TFS na wananchi wanaozunguka eneo la Mradi.
Mwandishi wa habari wa ITV Joseph Mwambije akiendelea na Majukumu ya kuchukua picha katika eneo la Hifadhi ya Misitu Kijiji cha Mkongotema
Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Serikali katika Ukumbi wa TFS mara baada ya kuzungukia vitalu vya uoteshaji miche ya miti.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr Binilith Mahenge akisalimiana na Viongozi wa TFS na Wasimamizi wa Mradi wa kuotesha iche ya miti katika eneo la Kijiji cha Wino Songea Vijijini.