MATUNDA UNAYO YAONA HAPO JUU YANA WEZA KUKUSAIDIA KURUDISHA UWEZO WA NGUVU ZAKO ZA KIUME KUFANYA KAZI VIZURI
Tatizo
la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa
na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4
kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo
hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu
za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa
mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume
na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi
umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja
kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi
wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu
nguvu ya kufanya tendo la ndoa.Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:-
1. PILIPILI [CHOBOLA]
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa
usambazaji damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya
mtu akawa na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale
wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si
kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
2. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya
tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa
watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi
na kwa upande wa wanawake husaidia kuongezamajimaji yenye utelezisehemu
za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.
3. NDIZI MBIVU
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza
juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na
yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu
unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa
hodari katika tendo la ndoa.
4. CHOKOLETI [KEKI ZENYE ASILI YA SUKARI ]
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha
mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake,
jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya
mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa
mawazo.
5. CHAZA NA PWEZA [SAMAKI WA BAHARINI ]
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na
chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha
msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
6. POMEGRANATE [MATUNDA DAMU ]
Ni aina fulani ya matundamekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa
kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili
na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa
kubwa.
7. MVINYO MWEKUNDU [NB;ZABIBU ]
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na
kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na
baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao
wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.
8. MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga
husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya
njema.
9. VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni
10. TIKITI MAJI
ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa
NINI SABABU YA KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME SOMA KWA MAKINI UELEWE
.Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye
kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke
akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa
amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea
nguvu za kiume taratibu.
Msaada unaohitajika kwa mwanamke
anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni
kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao
upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku
hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”
MWANAMKE KUGEUKA YEYE NDIYE MUME
Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo
la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na
watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea
kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo,
hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.
Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu
mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni
wa mchezo huo.
Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa
‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa
kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo
kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Inashauriwa
kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa
wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie
mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu
adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi
huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.
MWANMKE KUJIPENDA KIUSAFI NA KITABIA
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya
upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na
kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa
mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa.
Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.
MANENO YA KASHIFA
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za
kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala
miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha
ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza
kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi
unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume
zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao
hao.
MWANAMKE KUTOKA NJE YA NDOA YAKE
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo
kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana
moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi
ambayo humuondolea hamu ya tendo.
Mada hii imezungumzia zaidi
wanawake, lakini vipengele vilivyomo kwenye somo hili vinatumika pia kwa
upande wa wanaume kuwasababishia wanawake matatizo ya kupoteza msisimko
wakati wa tendo.
|
Nice blog
ReplyDelete