Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas
Group of Companies Yahaya Yusuph Kambaulaya amesema lengo la Kampuni yake
kuchimba Madini ya Makaa ya Mawe ni pamoja na kuongeza Ajira kwa Vijana na
kuleta Maendeleo kwenye kijiji cha Maniamba kwa kutoa ushuru unaopaswa kutolewa
kwa Halmashauri asilimia 0.03% na
Serikali kuu asilimia 4%
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Sera Bunge Ajira Vijana na watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama ameitaka Kampuni
ya Kambas LTD inayochimba Makaa ya Mawe kufuata Sheria zilizowekwa na Serikali
katika kuchimba Madini hasa Mrabaa unaotolewa baada ya kuchimba Madini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea Machimbo ya Makaa ya Mawe
yaliyopo Kijiji cha Maniamba Kata ya Muhukuru Songea Vijijini, Makaa
yanayotarajiwa kuchimbwa kwa miaka 40, Waziri amesistiza Mapato
yatakayopatikana kutokana na ushuru wa mgodi yafunguliwe Akaunt maalumu ili yawezeshe kufanya shughuli za Maendeleo ikiwemo ukarabati wa barabara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Kambas Group of Companies Bi Safina Nasoro amesema Kampuni
ya Kambas imeshapata Soko la kuuzia Makaa ya Mawe pamoja na bidhaa zingine
zitakazotokana na Makaa ya Mawe.
|
Mgodi wa Kambas una Eneo la
Hekarari 200 lakini ambazo zimeshapimwa na kubainika uwepo wa Makaa ya Mawe ni
Ekari 45. Mpaka sasa Sampuli ya Mkaa huo imepelekwa kwa wataalamu kuupima na
kubainika kuwa una ubora wa hali ya juu.