KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, May 11, 2018

KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI WA MKOA WA RUVUMA KASSIAN NYANDINDI MWANACHAMA WA RUVUMA PRESS CLUB

 Safari ya mwisho ya mwandishi Kassian Nyandindi, waandishi wa habari wakiondoa mwili wa mpendwa wao tayari kwa safari ya kuelekea Mbinga kwa mazishi.
 Kassian nyandindi daima atakumbukwa kwa umahiri wake katika kazi kwa kusimamia haki na ukweli pasipo shaka.
 Makamu Mwenyekiti wa Ruvuma Press Club Marietha Msembele akitoa maelezo mafupi ya maandalizi ya Mazishi ya Kassian Nyandindi muda mfupi baada ya kuwasili na mwili nyumbani kwa marehemu wilayani Mbinga.
 Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika simanzi ya kuondokewa na mpiganaji mwanzao katika tasnia ya Habari ambapo walikusanyika kuungana na mamia ya wananchi wa wilaya ya Mbinga na maeneo mengine ya mkoa wa Ruvuma katika Mazishi ya Kassian Nyandindi.
 Waandishi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika maombolezo ya kifo cha Mwenzao Kassian  Nyandindi aliyefariki kwa ajali ya pikipiki wilayani Mbinga.
Waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali waliokuja kuungana na Waandishi wa Habari katika kumsindikiza Mwanahabari Kassian Nyandindi katika safari yake ya mwisho.
Kassian  Nyandindi mbali na Uandishi wake wa Habari pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mbinga.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma walioshiriki Mazishi ya Marehemu Kassian Nyandi wa Gazeti la Majira ambaye aliliandikia miaka kumi na tatu tangu 2005 mpaka mauti ilipomfika akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Mkuu wa wilaya ya mbinga Cosmas Ishenye amewaomba   waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma kuwa watulivu  na kumuenzi Kassian Nyandindi kwa kuendeleza jitihada  za Nyandindi za kupenda kuandika habari za kuelimisha jamii kwa kuwa saidia wananchi
ndugu wa marehemu Kassian nyandi wamesema wamempoteza kiungo muhimu katika Familia ameondoka wakati bado mchango wake unahitajika kwani Nyandindi alikuwa ni mtoto wa kwanza katika Familia na ameacha mjane na watoto 4 ambao bado wanahitaji msaada wa kuendelezwa
Kassian  Nyandindi alisoma shule ya Msingi Mateka  wilaya ya Mbinga mwaka 1987  -  1993, pia alihitimu kidato cha nne sekondari ya Mbinga day mwaka 1997, mwaka 2003 alijiunga na chuo cha Uandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya  institute of jonalism na kupata kazi katika kampuni ya bissnes  Times akiandikia gazeti la Majira tangu mwaka 20005
Waandishi wa Habari Mkoa  wa Ruvuma wamewahakikishia wananchi kuendeleza mapambano ya kufichua maovu ikiwemo ufisadi Rushwa na ubadhirifu  wa mali za umma, waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma wametoa Rambirambi ya shilingi 800,000 kwa mama Mzazi wa Marehemu na mke wa Marehemu

Polisi Mkoa wa Ruvuma imewahakikishia waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kuwa Mtuhumiwa aliyesababisha Kifo cha Mwandishi  KASSIAN  NYANDINDI anatiwa mbaroni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Gemin  Mushy amemtaka  aliyesababisha  ajali na kusababisha kifo cha Mwanahabari Kassian  Nyandindi  ajisalimishe kituo chochote cha Polisi
Hivyo ndivyo ilivyozima taa ya maisha ya Kassiani Nyandindi ambaye alikuwa na harakati nyingi za maendeleo katika dunia hii lakini mwisho wa yote ni kuingia ardhini, kifo cha Kassian Nyandindi ni fundisho kwa waandishi wa habari wengine tunapaswa kuishi tukifahamu kifo kipo wakati wowote na hakina umri wala mahali maalumu popote ulipo safari ya mwisho wa maisha inaweza kukukuta. Mungu aiweke Roho ya Kassian Mahali pema peponi.
Nyandindi pumzika kwa Amani Daima utakumbukwa kwa umahiri wako katika kazi na uthubutu wa kuliingia suala lolote.
                Mamia wakiendelea na maombolezo katika makaburi ya Misheni mjini mbinga,
Waimbaji wakiomboleza katika Mazishi ya Mwanahabari wa Blog ya GWIJI LA HABARI na Gazeti la Majira Kassian  Nyandindi
  Zoezi la uwekaji mashada ya maua likiendelea
  Ndugu wakionyesha upendo katika kaburi la Marehemu Kassian Nyandindi kwa kumuekea Mishumaa ikiwa ni ishara ya kumtakia nuru ya Milele.
                                      Mama Mzazi wa Nyandindi na Mke wa Marehemu
Familia ya Marehemu Kassian nyandindi ikiongozwa na mama yake mzazi na mke wa marehemu wamesema Nyandindi walikuwa wakimtegemea kwa mambo mengi lakini hawawezi kupingana na mwenyezi mungu kilichobaki ni kumuombea pumziko la milele.
Mama Mzazi wa Marehemu Kassiani Nyandindi amewashukuru waandishi wa habari wa Mkoa wa ruvuma kwa ushirikiano mkubwa waliounyesha toka alipopatwa na ajali mpaka katika msiba wake amewaomba kuendeleza ushirikiano huo na mungu atawalipa.
Nyandindi ni mwandishi ambaye alipinga sana unyanyasaji dhuluma na hakupenda kudharauliwa katika kazi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbinga Beda  Hyera amewataka waandishi wa Habari kumuenzi Kassian  Nyandindi kwa kuiga Mfano wake katika kuandika habari bila woga ili mradi ziwe za ukweli na zenye kusaidia jamii.
·        WANACHAMA WA RUVUMA PRESS CLUB: Wameondokewa na mwanachama mwenzao KASSIAN  NYANDINDI wa gazeti la majira aliyefariki kwa ajali ya kugongwa na gari akiwa kwenye pikipiki
 Waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa Songea nje ya chumba cha kuhifadhi Maiti ambako walikusanyika kufanya taratibu za kumuhifadhi Marehemu Kassian Nyandindi aliyefariki Alfajiri ya tarehe 10/05/2018 katika hospitali ya Mkoa
 Mwandishi wa Habari wa Magazeti ya Serikali Muhidin Amri amemuelezea marehemu namna walivyoshirikiana katika kazi masaa machache kabla ya kupatwa na ajali amesema Nyandindi ni mtu aliyependa kazi yake na kushirikiana na waandishi wenzake ambaye alikuwa na ndoto za kuendelea kutumikia Taifa kupitia kalamu yake atakumbukwa kwa kazi zake hasa kupitia blog yake ya GWIJI LA MATUKIO na gazeti la Majira.

wandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Katibu wa Ruvuma Press Club Andrew  Chatwanga wakiwa katika majonzi ya kuondokewa na mwenzao nje ya chumba cha kuhifadhi Maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambako mwili wa Marehemu ulihifadhiwa wakati maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Mbinga kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika jumamos tar 12/05/2018.
 Marehemu Kassian Nyandindi atakumbukwa daima kwa kazi zake na uthubutu wake katika kufuatilia jambo ambalo aliliona kuwa hili ni lazima alifikishe kwa umma alihakikisha analifuatilia mpaka likamilike.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ametoa Rambirambi na pole kwa familia ya Mwandishi wa Habari aliye fariki kwa ajali ya pikipiki akiwa kazini katika wilaya ya Mbinga

Mkuu wa wa Mkoa wa Ruvuma Chrisitine Mndeme  ametoa salamu za rambirambi akiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Songea amesema kifo cha Kassiani Nyandindi ni pengo kwa wananchi na Serikali kwa kuwa alikuwa kiunganishi kati ya Serikali na wananchi kupitia kazi zake kwa kuwapa habari wananchijuu ya maendeleo yanayo fanywa na Serikali
 Marehemu Kassian Nyandindi licha ya kazi yake ya uandishi wa Habari pia alipenda kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ili kusaidia jamii kama anavyoonekana piachani akitoa damu kwa ajili ya kuchangia Benki ya damu katika Hospitali.

Katibu wa chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Andrew Chatwanga ameushukuru uongozi wa Serikali ya mkoa wa Ruvuma kwa ushirikiano wa hali na mali walizo toa  ikiwemo sanduku na usafiri, pia jeshi la polisi mkoa wa ruvuma ambao wamekuwa bega kwa bega nao toka ajali mpaka maandalizi ya kifo bila kusahau uongozi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, Ofisi ya mkuu wa wilaya, PCB na wadau wengine ambao wameungana na waandishi wa habari katika msiba huu.

Mwandishi wa habari Kasiani Nyandindi alizaliwa 13/05/ 1979 katika Hospitali ya Lundo wilaya ya Nyasa amekuwa mwandishi wa Habari katika Kamapuni ya Majira na alikuwa na mtandao wa Blog iliyo julikana kwa jina la  Gwiji la Habari marehemu Nyandindi alipata ajali ya pikipiki kwa kugongwa na gari nyuma maeneo ya Sheli ya Hinju mjini mbinga siku ya tarehe 9/5/2018 majira ya saa kumi jioni jambo lililosababisha kifo chake. Tulimpenda sana lakini Mungu amempenda zaidi, Bwana alitoa naye ametwaa jina lake lihimidiwe