NDUGU WA PENZI POPOTE PALE MLIPO,
KWA JINA NAITWA ADAM MZUZA NINDI NINA UMURI WA MIAKA 50 NAISHI WILAYA YA SONGEA INAYO SONGA MBELE AMBAYO IPO KATIKA MKOA WA RUVUMA ,RUVUMA INAYO VUMA
MKOA WA RUVUMA UPO KUSINI MWA TANZANIA , UNA PAKANA NA NCHI ZA MSUMBIJI NA MALAWI. KWA UJUMULA MKOA WA RUVUMA UNA WILAYA NNE,
SONGEA, MBINGA,NAMTUMBO,NA TUNDURU.
WILAYA YA SONGEA INA VIVUTIO VINGI KWANZA KABISA MLIMA MATOGORO NI MLIMA AMBAO VIONGOZI HUTUMIKA KWA KU SIMIKWA WANAPO CHAGULIWA KUWA MACHIFU.
WILAYA YA SONGEA PIA INA HISTORIA KUBWA ,KWA NZA KUHUSIANA NA VITA VYA MAJIMAJI . KATIKA VITA HIVYO WAZEE WALIO UWAWA KATIKA VITA HIVYO WALIZIKWA KATIKA KABURI MMOJA WAZEE WAPATAO 57, INGAWA WAZEE 7 HAWAJULIKANI WALIZIKWA WAPI.
PIA KUNA KABURI LA CHIFU SONGEA AMBAYE ALINYONGWA NA KUZIKWA KIWILIWILI TU NA KICHWA CHAKE KUPELEKWA UJERUMANI.
KATIKA MAMBO YA UTALII WILA YA SONGEA INA MBUGA YA SERUU AMBAYO IKO KILOMETA SABA KUTOKA SONGEA MJINI.
KATIKA MBUGA HIYO KUNA WANYAMA WA MAJINI KAMA VIBOKO MAMBA KATIKA MITO ,NA KATIKA MSITU MIKALI KUNA NYOKA WA AINA MBALIMBALI, SONGEA NI MAKAO MAKUU YA MKOA WA RUVUMA
UKIJA WILAYA YA MBINGA NAYO INA VIVUTIO VINGI ,IKIWEMO ZIWA NYASA AMBALO LINA KINA KIREFU IKIWA NA MAJI NYE RANGI YA SAMAWATI, KATIKA ZIWA HILO AMBALO LINA CHANGIWA NA NCHI MBILI MALAWI NA MSUMBIJI KUNA SAMAKI WA MAPAMBO WAAINA MBALIMBALI,
KANDO KANDO MWA ZIWA NYASA KUME ZUNGUKWA NA MILIMA YA LIVNGSTONE , UKIJA KILOMETA 40 KUTOKA ZIWA NYASA ANA KUTANA NA MLIMA WA MBUJI MLIMA HUU UNA SIFA YA PEKEE KWA WAKAAZI BONDE LA AGATA
MLIMA WA MBUJI UNA MAWE MAWILI AMBAYO YAMEPEWA MAJINA MAWILI, DUMENA JIKE MAWE HAYA YALIKUWA KIELELEZO CHA MAOMBI WAKATI MVUA INAPO KOSEKANA AU MARADHI YA MLIPUKO WAZEE MALUMU WALIKUWA WAKIOMBEA KWA DUA ZA KIMILA,
WAZEE WA JADI WALIKUWA WAKIOMBA KWA KUTUMIA KAFARA YA KONDOO MWEUPE AU MBUZI MWEUPE WA TUMIE TOGWA NI KINYWAJI BAIDI KINACHO TENGENEZWA KWA KUTUMIA ULEZI .
TUENDELEA NA WILAYA MBILI ZA NAMTUMBO NA TUNDURU KATIKA MAKALA YAJAYO.
No comments:
Post a Comment