KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, September 14, 2012

KATIBU TAWALA MKOA WA RUVUMA AMTAKA KILA MMOJA KUWA MWALIMU KUHAKISHA MAAMBUKIZI YANA PUNGUA

Hivi ni kwanini kila Semina aende mtu mmoja hivi hakuna wengine wa kuwakilisha alihoji katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma .wewe ukiwa kiongozi uta kumbukwa kwa lipi Tuache kujilimbikizia safari

Magonjwa aliyo sahaulika hivi sasa magonjwa hayo yame chukua nafasi ya kujulikana Dr Idda Ngoi akiyataja Magonjwa hayo amesema ni Usubi,Ukurutu,Mabusha, sasa yana tibika.

Afisa Uchumi Jacline Tarimo kutoka kutoka sekeretarieti ya mkoa wa Ruvuma alihoji kuhusu wagonjwa wa Ukoma waliko Peramiho nini Msaada wao baada ya kubaini changamoto zinazo wakabili kwani hata Viato Hivi sasa Hawana


Mwanasheria kutoka Mkoani Ruvuma akiangalia jinsi ya kuweza kutatua Matatizo yanayowakabili sekita ya Afya kishelia

Mungu wangu Juhudi zina hitajika kunusuru maisha ya watu kutokana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na Kifua Kikuu

Ee kumbe kazi kubwa bado ipo ya kupambana na Maambukizi katika wilaya yetu ya Mbinga ni vizuri Vyombo vya Habari Visaidie kuhasisha watu ili Maambukizi ya Pungue, Afisa Afya Marimu Mkumba kutoka mbinga ambaye ameshiriki katika Tathmini kila wakati ana sikiliza kwa makini


Afisa wa TACAIDS Mkoa wa Ruvuma ameanisha ongezeko la watoto wanao ishi katika Mangira Hatarishi na kuomba wadau kushirikiana na serekari kuikabili hali shiyo

TB au Kifua kikuu ni Homa inayo Tibika jambo mhimu ni kila mwananchi kujua hali yake kiafya alishauri Dr Wilamu Mtumbuka

Tunapo ona hali ina kuwa mbaya kiafya ni juu yetu kutafakali jinsi ya kuepukana na Magonjwa ya kua,mbukizwa ,Tumeingia mkenge na Babu loliondo akiadai ana tibu Maambukizi ya UKIMWI lakini jawabu lake tume poteza watu wengi ambao walidai wamepona na kuacha kutumia dawa

Washiri wa semina ya Tasimini wakijadili kwa kina jinsi ya kunusuru roho za wana Ruvuma kiwango hata kama walio athirika ni kidogo nilazima tufute kabisa maambukizi,Hasa yanayo toka kwa mama kwenda kwa Mtoto

MKOA WA RUVUMA WENYE WATU 1,412.084 UNA MAAMBUKIZI YA UKIMWI ASILIMIA 5.8

Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma amewataka Viongozi wa hospitali kuweka kumbukumbu kwa mambo mema ikiwa na pamoja kupokezana semina ,swala la mtu mmoja kwenda semina mbalimbali kuna punguza ari kwa watumishi wengine,pia hata tarifa za mambo yanayo azimiwa mtu mmoja hawezi kuanisha yote mengine ata sahau

Dr Wiliamu Mtumbika amesema maambukizo ya kifua kikuu katika mkoa wa Ruvuma ni asilimia 29 ,kila mtu mmoja anaweza kuambukiza watu 15 - 20 kwa mwaka

Mwenyekiti wasemina ya Tathmini ya kuangalia huduma zinazo tolewa Mkoani Ruvuma zimefanikiwa kiasi gani na changamoto gani zina ukabili mkoa wa Ruvuma

Mjumbe wa Sekeretarieti ya mkoa wa Ruvuma Mama Nguruse akitafakari jinsi ya kuteremusha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ambapo ime bainika wilaya ya mbinga maambukizi ni 8.5 na wilaya ya songea nayo maambukizi ni 6.4 wakiti wilaya ya Tunduru maambukizi ni 2.0 sawa na Namtumbo kimkoa ni 5.6

Dr,Wilamu Mtumbuka amesema kila watu 100,000 kwa mwaka 2010 watu 145 walipatikana na TB kitaifa 2011 watu 61,648 walibainika na TB {Kifua kikuu} na Mwaka 2011 watu 140 walipatika na TB Kitaifa mwaka 2011 watu 63,453 walipatikana na TB {Kifua kikuu}

Dr Magaderena Zenda Mratibu wa UKIMWI Hospitari ya Mkoa wa Ruvuma akitafuta Takwimu sahihi za Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Katika kitendea kazi chake


Inasikitisha kuona Maambukizi ya Kifua kikuu TB na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Vikimshambulia mtu mmoja hapo waganga wana tafakari Tufanye nini ?

Mjumbe kutoka Mbinga upande wa Afya Mariamu Mkumba akisikitika baada ya kusikia maambukizi wilaya ya mbinga ni asilimia 8.6 alipo ulizwa na blog ya songea habari amesema juhudi zitafanywa ili maambukizi ya pungue kama Wilaya ya Namtumbo kuwa asilimia 2 tu.

wajumbe kutoka Tunduru wakisikiliza kwa makini juu ya ongezeko la watoto yatima mkoani Ruvuma

Wednesday, September 12, 2012

MATESO MAUMIVU NA MAJONZI KWA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI

Ndugu Mtazamaji Napenda kuomba Radhi kwa kuonyesha picha ambayo ni simanzi kwa waandishi wote Duniani Hayo ndiyo masalio ya Mwili wa Daudi Mwangosi baada ya kulipukiwa kikatili akiwa kazini Nyololo Mkoani Iringa kinacho julikana ni Jaketi alilo vaa .Mungu aiweke Mahali Pema Roho ya Marehemu Daudi Mwangosi


JEE NINI TUFANYE BAADA YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSO ?
Adamu Mzuza Nindi -Songea inayo songa mbele Ruvuma inayo Vuma



Waislamu wanasema sisi ni wmwenyezi Mungu na kwake tuta rejea ,(Ina lilahi waina Rajuni) Wakristo nao husema Bwana ametoa na bwana amechukua jina la bwana lihimidiwe.

Waandishi wa Habari Nchini kote Tanzania wanaendelea kulaani kifo cha Daudi Mwangosi kilicho tokea Mkoani Iringa Katika eneo la Nyororo wakati waharakati za Kampeni za CHADEMA za kufungua matawi pale wanapo fikia.



Waandishi wa Habari jambo ambalo nataka kuwaambia ni kuwa katika kifo kuna kitu kina itwa Kadiri na Kifo cha kawaida. Kadiri ni kifo ambacho Mungu hulazi mishwa kuchukua Roho yako baada ya Binadamu Mwenyewe kukiuka kanuni za Maisha

Kifo cha kawaida nikifo kile ambacho Mungu amepanga Taratibu za Maisha Ukiumwa uende Hosipitali na Madakitari na wauguzi wakishindwa kutoa matibabu basi Mungu hulazimika kurejesha Roho yake kwake.

Ninapo fikia tamko la Kadiri ni kifo ambacho kimelazimishwa ili Roho itoke kadiri ina tokana na kupuuza utashi ulio pewa na Mwenyezi Mungu ,Hakuna Mtu ambaye ahapewa kengere ya Hatari ukiipuuza Kengere hiyo ndipo kadiri inapo chukua nafasi yake.Na ninapo sema kifo cha kawaida ni kifo ambacho kina kuwa hakina masha uta sikia watu wakisema kazi ya Mungu haina Makosa.

Sasa tuangalie Mambo ya kufanya .Mwandishi ana Takuiwa kuwa kama Kunguru ,Kanuni ya Kunguru ni Kuhakikisha kila kilicho mbele yake ni Hatari na Niadui, Kwa mfano mwangalie Kunguru ukiwa mbele yake ukijikuna uka peleka Mkono Kichwani yeye anadai unamlenga muda huo huo huruka, hiyo nikanuni mzuri.

Au angalia Makarani wa Benki wamejiwekea kanununi wewe ukiwa mbele yao akili yao huwamtuma kuwa wewe ni Mwizi karani Huridhika baada ya wewe kuchukua fedha na kuondoka, Jambo Hilo huwa fanya wasiingie hasara pi hata kunguru huishi maisha marefu kuliko ndege yeyoyote yule.

Nivizuri kila Mwandishi akachukua Tahadhali za Kunguru, Mwandishi pia anapo Tembea anatakiwa awe na tahadhali kama Mahakama inavyo tumia mizani kutafuta haki ukiwa Mahakamani dalili ya kushindwa kesi ni mizani kukuelemea ukiona hivyo basi ujue wewe una chukua adhabu ya kifo ,kifungo au kupigwa faini.

Sasa ukiwa Mwandishi Nyosha mikono yako kuelekea Mashariki linako toka Jua ikiwa ni ishara ya kupata mwanga kwa jua linalo toka Mashariki, Mkono Mwingine elekeza Magharibi kunako zama jua ikiwa ni alama ya kuzama jua na kuingia kiza,

Baada ya hapo chukua Story yako weka juu ya mizani ukiona inaelea upande wa mashariki kwenye nuru unayo itegemea achana na Story hiyo ,ujue ni hasara kwako kwa Familia yako na Jamii kwa Ujumula, Ukiona Story yako ina uzito zaidi ya Roho yako basi hata mbio kimbia ili uonekana mjinga laki Familia ina kuwa imesalimika.

Sasa nisiwa choshe ndugu zangu Waandishi Michango ya Fedha Kulaani kitendo kilicho fanyika pamoja na Majuto havita weza kurudisha Upendo alio kuwa Daudi Mwangosi akiutoa kwa mke wake,watoto,Jamii kwa ujumula bali sisi sasa tujiepushe na Habari zinazo Hatarisha Maisha yetu, Waandishi tujue kuwa thamani yako iko mikononi mwa familiyako tu , Wewe kazi unayo ifanya ni kazi ya Mshumaa ukifa basi huo ndio mwisho wa Nuru ya Familia yako nani Kama Hayati Moringe ,au Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Rais Kened wa Marekani.


Tuesday, September 11, 2012

VETA NI MKOMBOZI WAWA NYONGE KWA KUONDOKANA NA UMASIKINI

Mkurugenzi wa VETA Nyanda za juu kusini Monica Mbele akiwa katika semina ya wakuu wa vyuo vya ufundi iliyo fanyika mkoani ruvuma na kuwakilishwa na wakuu 103

Joseph Joseph Mkirikiti Mkuu wa wilaya ya Songea akitoa msisitizo kuhusu viongozi wa vyuo vya ufundi sitadi kuwa na mazoea ya kuonana na uongozi wa wanafunzi ili kupunguza changamoto zinazo weza kutatuliwa baina ya uongozi na uongozi wawanafunzi

Wakuu wa vyuo mbalimbali vya nyanda za juu kusini wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyo fadhiliwa na VETA Nyanda za juu kusini

Washiriki kutoka vyuo mbalimbali vya nyanda za juu kusini wakiwa wamepiga picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh.Joseph Joseph Mkirikiti aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu

Mwandishi mwandamizi wa TBC 1 Cathelini Nyoni akichukua changamoto zinazo wakabili wakuu wa vyuo vya ufundi Stadi vya nyanda za juu kusini

Wakuu wa Nyanda za Juu kusini wakiwa katika semina ya siku 3 mkoani Ruvuma kuchambua changamoto pamoja na kutafuta jinsi ya kuongeza ufanisi kwa vyuo vya ufundi Stadinyanda za juu kusini

Washiriki walio hudhuria katika semina ya Wakuu wa Nyanda za Juu kusini wakiwa makini kuratibu mambo mbalimbali

Mzee Rutta Mwalishi na Mkongwe wa VETA akiwa mmoja wawashiriki kati ya wakuu 103 walio hudhulia semina hiyo

Masister kutoka Chipole wakiwa katika semina ya wakuu wa vyuo vya ufundi Stadi nyanda za juu kusini semina iliyo fanyika Mkoani Ruvuma

Jambo pekee lililo changamsha ukumbi ni vile vigezo vinavyo wekwa na VETA kuwa washiriki wanao takiwa kujiunga na VETA niwale walio hitimu kidato cha nne huku watu wengine ambao hawaja soma hata darasa moja wakiweza kutengeneza Gari na wengine kuweza kutengeza mashine za kufua umeme, ufundi Stadi una takiwa kuwaenzi hao wote ili kuenzi ubunifu wao hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh. Joseph Joseph Mkirikiti

KATIBA NI KIINI CHA MAFANIKIO -JAJI JESEPH WARIOBA

Mh. Jaji Joseph Warioba akingia katika ukumbi wa Side Villa akiwa na Mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti

Mh.Jaji Joseph Warioba akiwa amepiga picha ya pamoja na waandishi wahabari Mkoa wa Ruvuma

Mh.Jaji Joseph Warioba akifafanua kuhusu utoaji wa Maoni kuhusu katiba,Pia alionya watu waache kupandikiza maneno ya kusema kuhusu katiba kwani katiba hiyo ni ya watanzania

Waandishi wa habari wakiwa na jopo la tume yamabadiliko ya katiba katika kupata habari za kina kuhusu utoaji wa maoni ya katiba ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba

CHUMVI NI MMOJA YA KUONGEZA MAGONJWA YA SHINDIKIZO LA MOYO (BP)

Dakitari Ansigall Stuffe OSB akiwa katika sherehe ya Jubeli ya miaka 25 toka huduma za Afya ya Msingi ilpo anza Katika Tarafa ya Ruvuma, Dr Ansigal Stuffe OSB amesema magonjwa yaliyo memengi kama Shindikizo la Moyo lina tokana na kutumia Chumvi kupita kiasi.

Mratibu wa Afya Tarafa ya Ruvuma akiwa na Dr, Ansigal Stuffe akimweleza mwendelezo wa miradi ya HAMU ambao una husu utokomezaji wa magonjwa mbalimbali katika Tarafa ya Ruvuma

Ukarimu wa Mngoni pale anapo pata kitu ambacho kina okoa maisha yake au kuleta kumbukumbu fulani kwa jamii basi jamii ya Wangoni hutoa Zawadi ya kinjenje kama anavyo pewa Dr Ansigal Stuffe kwa kazi kubwa aliyo ifanya ya kuokoa maisha ya watu katika Tarafa ya Ruvuma

Mratibu wa Afya katika Tarafa ya Ruvuma Abeli Mapunda akitoa tarifa ya maendeleo ya Afya kwa kipindi cha miaka 25 ya Jubelei ya DrAnsigal Stuffe amesema katika miaka 25 ya nyuma tarafa Ruvuma ilikuwa na changamoto ya magonjwa sugu kama Usubi, upere,kuhara,mafunza kwa watoto wa shule za msingi,ugonjwa wa maralia kwa asilimia kubwa magonjwa hayo yame tokomezwa kwa asilimia 75% na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa fedha za kitanzania

Wanafunzi wa shule ya msingi likuyu fusi waki toa pongezi kwa Dr Ansigal Stuffe OSB kwa kazi kubwa aliyo ifanya kuwakomboa kiafya tarafa ya Ruvuma

Moja ya mambo ambayo yata kumbukwa kwa Dr Ansigal Stuffe ni kuwa wezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapa miradi mbambalimbali hapo una ambiwa hiyo ni bras band inayo ongozwa na wanawake wenyewe

Unaweza kuona kupuliza Tarumbeta kama hili nikazi lakini mama huyo kwake ni sawa na mchezo wawatoto

WANDISHI WA HABARI WAMWOMBEA DAUDI MWANGOSI WAKIWA PERAMIHO MISHENI

Katika kumkumbuka Mwandishi wa Habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi wandishi mkoani Ruvuma walienda Peramiho Misheni kuomba mwenyezi Mungu amweke Mahali pema Marehemu Mwangosi

Kutoka kushoto ni Mwandishi wa Radio Jogoo anaye fuatia Mosses Konara wa Radio Maria na aliye fuatia ni Adamu Nindi wa RFA wa Mwisho ni Catherin Nyoni wa TBC 2,

Hapo kwa pamoja wote wakiendelea kuomba kwa bidii ili shari iliyo mkuta Mwandishi mwenzao Daudi Mwangosi iwe mwanzo na mwisho kwa kuweka pengo la kuhabarisha wananchi

Wednesday, September 5, 2012

HIVI MWANDISHI ANA THAMANI MBELE YA WANA SIASA AU NI KAMA SAWA NA MSHUMAA ULIVYO ?

Hayati Daudi Mwangosi alikuwa mwandishi hodari katika kuelimisha jamii mambo ya kisaikolojia na hata filosofi zaaina zote , katika ofisi yake kulikuwa na Vitabu mbalimba vya watu mashuhuri vilivyo onyesha namuna ya kutafuta haki, jee baada ya kifo chake watu wanalitambua hilo ?

Pamoja na Mapenzi mema ya Wanahabari kwenda kumuzika mwenzao lakini upepo wamajonzi ya Daudi Mwangosi uliwakumba wandishi na kutaka kupata Ajali


Mwandishi Fransi Godwini kulia akiwa amebeba jeneza la Daudi Mwangosi wakati wanaenda kuzika kushoto kwakwe Rais wa UPTC Cenes Simbaya


Picha hiyo hapo juu ina wachanganya Waandishi wa Habari na Jamii kuhusu kifo cha Daudi Mwangosi ,Jee wewe Raia baada ya kuona picha hii una wazo gani huoni wandishi ni sawa na mshumaa ,Tume kuwa tukipiga kelele kuhusu haki za wenzetu jee Raia mna tusaidia vipi Waandishi, Haya tujipe pole wote

Tuesday, September 4, 2012

WANA RUVUMA WA MKUMBUKA MWANDISHI SHUPAVU DAUDI MWANGOSI



Hayati Mwenyekiti wa Iringa Press Club akiwa na Jopo la Waandishi wa Habari Iringa watatu kutoka kushoto aliye vaa kisibau

Hayati Daudi Mwangosi alikuwa mtu mwenye kufikiri kila wakati huyo aliye inama ni Hayati Daudi Mwangosi akitafakari kuhusu Zoezi zima la Sensa na Makazi ya Watu akiwa iringa RUCO



ADAMU NINDI -SONGEA


Chama cha waandishi wahabari mkoani Ruvuma kimesitisha mahusiano ya kihabari na jeshi la Police mpaka uchunguzi utakapo fanyika kubaini chanzo cha mwandishi wa habari wa Daudi Mwangosio anaye tuhumiwa kuuwawa na jeshi la police Mkoani Iringa

Mwewnyekiti wa chama cha wandiahi wa Habari Mkoa wa Ruvuma Andrew Kuchonjoma amesma hayo katika kikao cha Dharura kilicho kite kutoa Tamko la Wandishi wa Habari wa mkoa wa Ruvuma kuhusu kujitoa katika shuguli yoyote inayo husu Jeshi la Police dhidi ya Kupinga mauaji yaliyo mpata Daudi Mwangosi akiwa kazini.

Mwenyekiti Andrew Kuchochonjoma amesema Jeshi la Police imekuwa mazoea kutumia silaha za moto kwa Raia badala ya kufuata kanuni ya kulinda Raia na mali zao. lakini silaha ina tumika kinyume na kanuni hizo .amesema hivyo nikiwa mwenyekitiRPC natangaza Rasimi kuvunja mahusiano na Jeshi la Police


Wandishi wa Habari kwa namnuna nyingine wameshangaa na nguvu za chama chasiasa kuweza kuwa na malumbano na dola kuna nini hadi kukiuka sheria zilizo wekwa na Dola tuta ilaumu serekari mpaka lini wakati usabaishaji upo bayana.

Wadau mbalimbali wa Habari Mkoani Ruvuma ambao hawakutaka majina yao yatajwe wamewaomba waandishi wa Habari kuthamini Roho zao kuliko kuhatarisha maisha yao .Wadau hao wamesema Vyama vya siasa kazi yake kubwa ni kuwaweka Raia na Waandishi wa Habari kuwa chambo ya kupandisha chaki ya vyama vyao huku raia na waandi wakiteketea