Mgeni Rasmi katika Sherehe ya
Siku ya Mkulima Edes Lukoe sherehe zilizofanyika katika Kijiji cha Nakahuga songea
vijijini .kijiji ambacho kimekuwa shamba la Majaribio kwa Mikoa ya Mtwara,
Iringa, Mbeya na Ruvuma amewataka wakulima kuzigatia
elimu wanayopewa na watalamu ili wapate mafanikio katika kilimo.
Wananchi walioshiriki Siku ya
Mkulima katika kijiji cha Nakahuga
wakiongozwa na Mary Ntani wameishukuru Serikali kwa kupewa elimu ambayo imewafanya kupata mavuno mara
mbili kuliko hapo awali
Mtaalamu wa Utafiti kutoka Uyole Deogratus Kisandu amesema Wananchi wa Kijiji
cha Nakahuga Songea Vijijini hivi sasa wamepata Mafanikio katika Kilimo cha
Mpunga kwa njia ya Umwagiliaji ambapo Hekta moja hutoa Tani 6.5 za Mpunga.
Mtaalamu wa Utafiti kutoka
Uyole Mbeya Deogratus Kisandu akiwa
katika siku ya mkulima nakahuga songea amesema katika Utafiti uliofanywa
umeweza kubaini Mbegu za Mpunga aina ya SARO 5 ina uwezo wa kutoa Tani 8 – 9
kwa Hekta ikipata Matunzo mazuri, hilo
limebainika katika Mashamba ya Nakahuga Songea Vijijini.
Mtalamu kutoka Uyole Deogratus Kisandu akitoa Maelezo jinsi mbegu ya SARO 5 ilivyo onsha mafanikio katika kilimo cha umwagiliaji kakika Bonde la Nakahuga Songea Vijijini
Kama unavyo mwona Mtoto Erasimo Ntani akicheza Ngoma ya Kitoto katioka siku ya Mkulima Songea Vijijini
Mradi wa umwagiliaji maji Kijiji cha Nakahuga Songea
Vijijini ambao umegharimu kiasi cha Sh. Milioni 295,504,200 umewawezesha
Wakulima wa Nakahuga kwa mwaka 2013 -2014 baada ya kulima hekari270 wana
tarajia kuvuna mpunga Tani 1755 kwa hekari 270
Wakulima wa Nakahuga Songea Vijijini wakiburudika kwa ngoma ya Kitoto siku ya mkilima iliyo fanyika kijijini Nakahuga
Mgeni Rasimi aliye mwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Songea Edes Lukoe akikagua shamba la mpunga katika shamba la mpunga nakahuga