Waumini wa Kiislamu
na Madhehebu mengine wametakiwa kuwa na huruma kwa kusaidia watu wenye shida
wakiwemo maskini, wafungwa na wagonjwa waliolazwa Hospitalini.
Katibu wa Msiki wa
Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mohamed Mfyule ameyasema hayo wakati akigawa
chakula kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
wapatao 1000.
Katibu wa Msiki wa
Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Mohamed Mfyule
amesema wakati wa Siku ya sikukuu mbambali ni wajibu wa Waumini wa Dini mbalimbali kufanya Hija katika
Hospitali kwa kuwaona Wagonjwa
waliolazwa na kuweza kuwafariji hiyo
nayo ni ibada
Wagonjwa akila chakula baada ya waislamu kuwa gawia katika kusherekea sikukuu ya idi
Akina mama waja wazito wakijipatia chakula katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma
P0amoja na sherehe ya sikukuu ya iddi waisilamu walijitolea kushinda hospitali
Wagonjwa wapatao 1000 mwakijipatia chakula na kuwaombea waisilamu waendelee na moyo huo huo
Ukiwa siyo mzazi huwezi kujua uchungu wa mimba pamoja na waislamu kujitolea kupeleka chakula lakini akina mama hawa wana sema chakula hakinogi wanaomba waislamu wawaqombee ili wajifungue kwa haraka
Waislamu wakiendelea kutoa chakula huku wakiwafariji waja wazito
muguzi mama mbawala akiwa wodini ,hapo ana washukuru waislamu kwa kutoa chakula na kuwaomba madhehebu mengine waige mfano huo
kweli moyo wawaumini upo kwenye matatizo ndivyo inavyo dhirisha katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma
Unapo sherekea sikukuu ni lazima ujue niviumbe vingapi vina kutegea hapo paka akiwa ameshiba baada ya kupewa chakula
Katibu wa Msikiti wa Hospitali akisimamia kwa makini mtu asikose chakula
Mambo hayo hapo ni kula tu waislamu wana fanya kazi
Waumini mbalimbali waliokuja kuwaona wagonjwa wao nao wameshukuru moyo ulio onyeshwa na Waislamu kwa kujitolea kutoa chakula kwa wagonjwa 1000
Wagonjwa mbalimbali waliolazwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wamewaomba wa watu mbalimbali kuja kutoa misaada
kwa wagonjwa kwani wako wagonjwa wengine ambao hawana ndugu. Nao wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma wamewashukuru waislamu kwa kuweza kutoa msaada wa chakula kwani chakula ni dawa ikiongozana na ufariji wao wagonjwa .