KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo
UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Friday, November 24, 2017
Wednesday, November 22, 2017
Sunday, November 19, 2017
Saturday, November 18, 2017
KAMBAS GROUP OF COMPANIES YACHANGIA MIFUKO 100 YA SIMENTI NA BATI 15O KWA AJILI YA UKARABATI WA MAJENGO YA SHULE YA MSINGI MIPETA KATA YA MUHUKULU SONGEA VIJIJIN MKOANI RUVUMA
Kampuni ya kambas Group
of Companies inayojihusisha na utafiti wa madini ya makaa ya mawe Kijiji cha
Maniamba Kata ya Muhukulu katika wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imetoa msaada huo wa bati 150 na simenti
mifuko 100 katika shule ya msingi mipeta
iliyoko Kata ya Muhukulu Songea vijijni vifaa vyote vikiwa na thamani ya
shilingi milioni 5.4
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Investment Yahaya Yusuph Kambaulaya amesema wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutatua changamoto mbali mbali za kijamii.Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Investment Yahaya Yusuph Kambaulaya amesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuripotiwa taarifa ya kuezuliwa kwa majengo ya shule ya Msingi Mipeta kulikotokana na upepo mkali ulioambatana na mvua na kusababisha uharibifu wa miundo mbinu ya majengo ya shule hiyo, hivyo wao kama wadau wa maendeleo waliona ni vizuri kuungana na Jamii ya wakazi wa Kata ya Muhukulu katika kusaidia ukarabati wa madarasa, Nyumba za Walimu na Ofisi za walimu.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Investment akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema katika kukabidhi vifaa hivyo amesema wao kama kampuni wamekuwa wakitoa misaada kwa jamii katika maeneo mbalimbali huku akiamini Serikali peke yake bila ushiriki wa Taasisi binafsi haitaweza kutatua changamoto zote.
Mifuko 100 ya Simenti na Bati 150 zikiwa ndani ya Gari katika Eneo la Shule ya Msingi Mipeta Kata ya Muhukulu muda mfupi baada ya kufikishwa kijijini hapo, Shule ya Msingi Mipeta ilipata maafa tar 09/11/2017 ambapo madarasa 4 yaliezuliwa, nyumba 2 za walimu na ofisi 2 za walimu
Mwenyekiti wa wa Kampuni ya Kambas Group Yahaya Yusufu Kambaulaya amesema kampuni yao ina guswa sana na matatizo ya kijamii . watoto wakikosa kusoma adhabu itakuja kwa wazazi na jamii inayowazunguka hivyo kampuni yake kutoa msaada huo ni sehemu ya wajibu wao kama wazazi ili watoto wasikose kupata Elimu.
Wananchi wa Kijiji cha Mipeta wakishusha Simenti katika Shule ya Msingi Mipeta iliyopo Kata ya Muhukulu wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Kamando Mgema amesema baada ya kufanya mawasiliano na Kampuni ya Kambas Investment Group imeweza kukubali kutoa msaada kwa shule ya msingi Mipeta shule yenye wanafunzi kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba ambao kwa sasa watoto wote husoma kwa zamu katika madarasa mawili ambayo hayakuathiriwa na upepo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akipokea Simenti toka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya kambas Investment Groups Bw. Yahaya Yusuph Kambaulaya.
Mkuu wa Wilaya ya Songea akimkabidhi Diwani wa Kata ya Muhukulu Simenti iliyotolewa na Kampuni ya Kambas Investment huku akisistiza kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mipeta akimshukuru mkuu wa Wilaya na Kampuni ya Kambas Investment kwa kuwapatia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa majengo yaliyokumbwa na maafa.
Mwonekano wa Baadhi ya Majengo yaliyoezuliwa na upepo katika Shule ya Msingi Mipeta
Majengo ya madarasa yaliyokumbwa na janga la kuezuliwa na upepo shule ya Msingi Mipeta Songea Vijijini.
Diwani wa kata ya mipeta Ameishukuru kaMpuni ya Kambas kwa msaada ulio tolewa na kusema umefika katika wakati mwafaka wakati mvua zina endelea kunyesha
Wananchi walioshiriki kupokea vifaa vya ujenzi wameishukuru Kampuni ya Kambas kwa kusaidia jamii katika kutatua changamoto mbalimbali wameomba wadau wengine wenye uwezo kuiga Mfano wa Kampuni hiyo kwa kuwa Mahitaji ya kukarabati majengo ya shule hiyo na Nyumba za walimu na ofisi ni zaidi ya bati 200 zinahitajika na simenti isiyopungua mifuko 300.
Naye mwananchi Erasto Tegeta mkazi wa Kijiji cha Mipeta ameshukuru vyombo vya habari kwa kuonyesha matukio ya maafa yaliyowapata Kijijini hapo na kupelekea wadau kutoa miasaada hiyo.
Makabidhiano ya Bati na Simenti yamefanyika chini ya uongozi wa Kijiji cha Mipeta Diwani wa Kata ya Muhukulu na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mipeta.
Mwenyekiti wa kampuni ya kambas Yahaya Yusufu Kambaula amesema kampuni yake
baki ya kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa sasa mkoani shinyanga wana
jenga jingo kwaajili ya benk ya damu.
Thursday, November 16, 2017
Tuesday, November 7, 2017
NAPENDA KUWA PONGEZA WALE WOTE WALIO WEZA KUINGIA KATIKA BLOG YANGU YA SONGEA HABARI
Ndugu zangu mnao angalia Blog ya SONGEA HABARI napenda kuwa pongeza kwa kuweza kunipa moyo wa kuendelea kuwa pasha tarifa mbalimbali za Tanzania pamoja na tarifa za Nchi zinazo tuzunguka shukurani zangu ziweendee watu wanao ishi nchi zifuatazo .
WADAU WETU WANAO ANGALIA BLOG YETU KILA SIKU NI HAWA WAFUATAO U.S.A ,RUSSA.FRANCE,INDONOSIA.SPAIN,SWEDEN,CHINA,KENYA
NA TANZANIA. Naomba maoni yenu jinsi ya kuboresha BLOG HII YA SONGEA HABARI KWA
KUTOA MAONI HATA KUCHANGIA KIFEDHA KAMA WALIVYO FANYA WATU WA U.S.A Ni mimi Adam Nindi Mkurugenzi wa Blog ya
Sonjgea Habari ni Kishirikiana na Judith Lugoye
Sunday, November 5, 2017
rc dodoma na rc ruvuma star tv
BARAZA LA MAWAZIRI OKTOBA 2017
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora.
I. Waziri –
George Huruma Mkuchika
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI).
I. Waziri
- Selemani Said Jafo
II. Naibu
Waziri - Joseph Sinkamba Kandege
III. Naibu Wazri
- George Joseph Kakunda
Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
I. Waziri - January Yusuf Makamba
II. Naibu
Waziri - Kangi Alphaxard Lugola
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu.
I. Waziri -
Jenista Joackim Mhagama
II. Naibu Waziri
- Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana
na Ajira)
III. Naibu Waziri
- Stella Alex Ikupa (Walemavu)
Wizara ya Kilimo.
I. Waziri -
Dkt. Charles John Tizeba
II. Naibu
Waziri - Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
I. Waziri -
Luhaga Joelson Mpina
II. Naibu
Waziri - Abdallah Hamis Ulega
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
I. Waziri -
Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
II. Naibu
Waziri - Mhandisi Atashasta Justus
Nditiye
III. Naibu
Waziri - Elias John Kwandikwa
Wizara ya Fedha na Mipango.
I. Waziri
- Dkt. Philip Isdor Mpango
II. Naibu
Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji
Wizara ya Nishati.
I. Waziri -
Dkt. Medard Matogoro Kalemani
II. Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu
Wizara ya Madini.
I. Waziri -
Angellah Kairuki
II. Naibu
Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo
Wizara ya Katiba na Sheria.
I. Waziri
- Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko
Kabudi.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
I. Waziri - Dkt. Augustine Philip Mahiga
II. Naibu Waziri - Dkt. Susan Alphonce Kolimba
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
I. Waziri -
Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
I. Waziri
- Mwigulu Lameck Nchemba
II. Naibu Waziri
- Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
Wizara ya Maliasili na Utalii.
I. Waziri
- Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
II. Naibu
Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
I. Waziri
- William Vangimembe Lukuvi
II. Naibu
Waziri - Angelina Sylivester Mabula
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
I. Waziri
- Charles Paul Mwijage
II. Naibu
Waziri - Mhandisi Stella Martin
Manyanya
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
I. Waziri
- Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
II. Naibu
Waziri - William Tate Ole Nasha
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
I. Waziri
- Ummy Ally Mwalimu
II. Naibu
Waziri - Dkt. Faustine Engelbert
Ndugulile
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
I. Waziri - Dkt. Harrison George Mwakyembe
II. Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza
Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
I. Waziri
- Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
II. Naibu
Waziri - Jumaa Hamidu Aweso
Subscribe to:
Posts (Atom)