Kampuni ya kambas Group
of Companies inayojihusisha na utafiti wa madini ya makaa ya mawe Kijiji cha
Maniamba Kata ya Muhukulu katika wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imetoa msaada huo wa bati 150 na simenti
mifuko 100 katika shule ya msingi mipeta
iliyoko Kata ya Muhukulu Songea vijijni vifaa vyote vikiwa na thamani ya
shilingi milioni 5.4
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Investment Yahaya Yusuph Kambaulaya amesema wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutatua changamoto mbali mbali za kijamii.Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Investment Yahaya Yusuph Kambaulaya amesema wamechukua uamuzi huo baada ya kuripotiwa taarifa ya kuezuliwa kwa majengo ya shule ya Msingi Mipeta kulikotokana na upepo mkali ulioambatana na mvua na kusababisha uharibifu wa miundo mbinu ya majengo ya shule hiyo, hivyo wao kama wadau wa maendeleo waliona ni vizuri kuungana na Jamii ya wakazi wa Kata ya Muhukulu katika kusaidia ukarabati wa madarasa, Nyumba za Walimu na Ofisi za walimu.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Kambas Investment akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema katika kukabidhi vifaa hivyo amesema wao kama kampuni wamekuwa wakitoa misaada kwa jamii katika maeneo mbalimbali huku akiamini Serikali peke yake bila ushiriki wa Taasisi binafsi haitaweza kutatua changamoto zote.
Mifuko 100 ya Simenti na Bati 150 zikiwa ndani ya Gari katika Eneo la Shule ya Msingi Mipeta Kata ya Muhukulu muda mfupi baada ya kufikishwa kijijini hapo, Shule ya Msingi Mipeta ilipata maafa tar 09/11/2017 ambapo madarasa 4 yaliezuliwa, nyumba 2 za walimu na ofisi 2 za walimu
Mwenyekiti wa wa Kampuni ya Kambas Group Yahaya Yusufu Kambaulaya amesema kampuni yao ina guswa sana na matatizo ya kijamii . watoto wakikosa kusoma adhabu itakuja kwa wazazi na jamii inayowazunguka hivyo kampuni yake kutoa msaada huo ni sehemu ya wajibu wao kama wazazi ili watoto wasikose kupata Elimu.
Wananchi wa Kijiji cha Mipeta wakishusha Simenti katika Shule ya Msingi Mipeta iliyopo Kata ya Muhukulu wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti Kamando Mgema amesema baada ya kufanya mawasiliano na Kampuni ya Kambas Investment Group imeweza kukubali kutoa msaada kwa shule ya msingi Mipeta shule yenye wanafunzi kuanzia darasa la awali hadi darasa la saba ambao kwa sasa watoto wote husoma kwa zamu katika madarasa mawili ambayo hayakuathiriwa na upepo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akipokea Simenti toka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya kambas Investment Groups Bw. Yahaya Yusuph Kambaulaya.
Mkuu wa Wilaya ya Songea akimkabidhi Diwani wa Kata ya Muhukulu Simenti iliyotolewa na Kampuni ya Kambas Investment huku akisistiza kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mipeta akimshukuru mkuu wa Wilaya na Kampuni ya Kambas Investment kwa kuwapatia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati wa majengo yaliyokumbwa na maafa.
Mwonekano wa Baadhi ya Majengo yaliyoezuliwa na upepo katika Shule ya Msingi Mipeta
Majengo ya madarasa yaliyokumbwa na janga la kuezuliwa na upepo shule ya Msingi Mipeta Songea Vijijini.
Diwani wa kata ya mipeta Ameishukuru kaMpuni ya Kambas kwa msaada ulio tolewa na kusema umefika katika wakati mwafaka wakati mvua zina endelea kunyesha
Wananchi walioshiriki kupokea vifaa vya ujenzi wameishukuru Kampuni ya Kambas kwa kusaidia jamii katika kutatua changamoto mbalimbali wameomba wadau wengine wenye uwezo kuiga Mfano wa Kampuni hiyo kwa kuwa Mahitaji ya kukarabati majengo ya shule hiyo na Nyumba za walimu na ofisi ni zaidi ya bati 200 zinahitajika na simenti isiyopungua mifuko 300.
Naye mwananchi Erasto Tegeta mkazi wa Kijiji cha Mipeta ameshukuru vyombo vya habari kwa kuonyesha matukio ya maafa yaliyowapata Kijijini hapo na kupelekea wadau kutoa miasaada hiyo.
Makabidhiano ya Bati na Simenti yamefanyika chini ya uongozi wa Kijiji cha Mipeta Diwani wa Kata ya Muhukulu na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mipeta.
Mwenyekiti wa kampuni ya kambas Yahaya Yusufu Kambaula amesema kampuni yake
baki ya kutoa misaada mbalimbali ya kijamii kwa sasa mkoani shinyanga wana
jenga jingo kwaajili ya benk ya damu.
No comments:
Post a Comment