https://www.youtube.com/live/aDXyrrpF3zo?feature=share
ELIMU YA MLIPA KODI MADABA - RUVUMA
02/06/2023
Wafanya biashara wa Mkoa wa Ruvuma wameipongeza
Mamlaka ya Mapato TRA kwa kutoa Elimu ya Mlipakodi mlango hadi Mlango na
kusogeza huduma karibu za kodi hususani katika Halmashauri za Madaba na Wilaya
ya Nyasa.
Wafanya biashara hao wameyasema hayo wakati Timu ya
Maofisa wa TRA ilipotembelea Halmashauri ya Madaba kutoa elimu ya mlipakodi.
Afisa Msimamizi Mkuu wa
Kodi kutoka Makao makuu ya Mamlaka ya Mapato TRA Lydia Shio amesema huduma ya
mapato imesogezwa karibu na wafanya biashara ili kuwasaidia kupata huduma
karibu na kupata uelewa jinsi ya kulipa kodi na jinsi wanavyokadiriwa mapato.
Lydia Shio – Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi.
Wafanya biashara hao wa
halmashauri ya Madaba Songea Vijijini wameipongeza Mamlaka ya TRA kwa kuwasogezea
huduma za kikodi kwamba sasa watapata Maelekezo kamili ya jinsi ya kuweza
kulipa kodi pamoja na jinsi ambavyo wao wataweza kujiendesha kibiashara.
1. Petro Ndiba – Mfanya Biashara Madaba
2. Salimu Seif – Mfanyabiashara wa halmashauri ya madaba
3. Ezekiel Mkombo – Mfanya Biashara
Mamlaka ya Mapato TRA
imekua ikifanya juhudi za kuwasogeza wafanyabiashara ili waweze kupata manufaa
kuhusiana na kodi wanazolipa na kuwaelimisha jinsi wanavyoweza kufanya biashara
zao bila kuipunja Serikali wala kujipunja wao.