Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni (BRELA) wametoa elimu ya Biashara kwa njia ya mtandao kwa wananchi wapatao 700 wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma ili kuwafanya wakulima wanapofanya biashara za mazao yao waweze kuzirasimisha na kuuza katika mifumo yenye kuleta tija pasipo usumbufu wa kutafuta masoko.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Jenista Mhagama akiongea katika semina elekezi iliyotolewa na Brela amesema kila anapokaa amekua akifikiria jinsi ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili wapate maendeleo yenye tija pamoja na kuwaongezea nyenzo ambazo zitaweza kuwasaidi katika shughuli zao
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa BRELA Koyani Abubakari amesema ni wajibu wa BRELA kuwafundisha wananchi jinsi ya kusajili na kurasimisha biashara zao ili waweze kuendesha biashara zao kitaalamu kwa maendeleo yao.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria katika semina iliyoendeshwa na BRELA katika ukumbi wa NJUNDE peramiho Songea Vijijini
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Songea Simon Kapinga amesema elimu iliyotolewa kwa wananchi imesaidia kufahamu umuhimu wa kumiliki NEMBO katika biashara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Menas Komba amewataka wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Songea kuzingatia mafunzo wanayoyapata ili yawasaidie kubadilisha hali ya uchumi kwa familia na kuongeza pato la serikali.
Wananchi waliohudhuria Mafunzo ya BRELA wamesema wamefurahi kuona BRELA imetoa Elimu ya kuwawezesha kufanya usajili katika biashara zao pamoja na kuwafanya wapate leseni zitakazotumika katika biashara za Mazao ya kilimo pamoja na mambo mengine.
Semina iliyoendeshwa na
wakala wa Usajili BRELA katika eneo la Peramiho Songea Vijijini imweza
kuwanufaisha wananchi 700 kutoka kata zote za Halmashauri ya Songea Vijijini na
kusema kutokana na mwanga walioupata utaweza kuwasaidia kuinua biashara zao na
kuwa na kampuni zao.
No comments:
Post a Comment