KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Friday, June 9, 2023

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MJINI CHARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI YA SEKTA YA ELIMU

 Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea Mjini kimeishukuru Serikali kwa kutoa kiasi cha Zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya sekta ya Elimu.


Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini James Mgego amesema Zaidi ya shilingi bilioni moja zimetolewa kutekeleza miradi ya miundombinu ya Elimu na vilevile katika Kata ya Mshangano zimetolewa Zaidi ya milioni 800 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya elimu jambo lililoungwa mkono na Diwani wa Kata ya Mshangano Samweli Mbano.

Chama cha Mapinduzi wilaya ya Songea Mjini kimeweka mikakati ya kutoa hamasa kwa wazazi kuchangia chakula cha watoto Mashuleni.


Wednesday, June 7, 2023

WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI BRELA WATUA RUVUMA

Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni (BRELA) wametoa elimu ya Biashara kwa njia ya mtandao kwa wananchi wapatao 700 wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma ili kuwafanya wakulima  wanapofanya biashara za mazao yao waweze kuzirasimisha na kuuza katika mifumo yenye kuleta tija pasipo usumbufu wa kutafuta masoko.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Jenista Mhagama akiongea katika semina elekezi iliyotolewa na Brela amesema kila anapokaa amekua akifikiria jinsi ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili wapate maendeleo yenye tija pamoja na kuwaongezea nyenzo ambazo zitaweza kuwasaidi katika shughuli zao 

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa BRELA Koyani Abubakari amesema ni wajibu wa BRELA kuwafundisha wananchi jinsi ya kusajili na kurasimisha biashara zao ili waweze kuendesha biashara zao kitaalamu kwa maendeleo yao.


Baadhi ya washiriki waliohudhuria katika semina iliyoendeshwa na BRELA katika ukumbi wa NJUNDE peramiho Songea Vijijini

Baadhi ya Mastafu wa BRELA walioendesha semina ya usajili wa biashara na Leseni
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Songea Simon Kapinga amesema elimu iliyotolewa kwa wananchi imesaidia kufahamu umuhimu wa kumiliki NEMBO katika biashara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Menas Komba amewataka wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Songea kuzingatia mafunzo wanayoyapata ili yawasaidie kubadilisha hali ya uchumi kwa familia na kuongeza pato la serikali.

Wananchi waliohudhuria Mafunzo ya BRELA wamesema wamefurahi kuona BRELA  imetoa Elimu ya kuwawezesha kufanya usajili katika biashara zao pamoja na kuwafanya wapate leseni zitakazotumika katika biashara za Mazao ya kilimo pamoja na mambo mengine.

Semina iliyoendeshwa na wakala wa Usajili BRELA katika eneo la Peramiho Songea Vijijini imweza kuwanufaisha wananchi 700 kutoka kata zote za Halmashauri ya Songea Vijijini na kusema kutokana na mwanga walioupata utaweza kuwasaidia kuinua biashara zao na kuwa na kampuni zao.


 

Friday, June 2, 2023

ELIMU YA MLIPAKODI KWA WAFANYABIASHARA MADABA

 https://www.youtube.com/live/aDXyrrpF3zo?feature=share

ELIMU YA MLIPA KODI MADABA - RUVUMA

02/06/2023

 

Wafanya biashara wa Mkoa wa Ruvuma wameipongeza Mamlaka ya Mapato TRA kwa kutoa Elimu ya Mlipakodi mlango hadi Mlango na kusogeza huduma karibu za kodi hususani katika Halmashauri za Madaba na Wilaya ya Nyasa.

 

Wafanya biashara hao wameyasema hayo wakati Timu ya Maofisa wa TRA ilipotembelea Halmashauri ya Madaba kutoa elimu ya mlipakodi.

 

Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Makao makuu ya Mamlaka ya Mapato TRA Lydia Shio amesema huduma ya mapato imesogezwa karibu na wafanya biashara ili kuwasaidia kupata huduma karibu na kupata uelewa jinsi ya kulipa kodi na jinsi wanavyokadiriwa mapato.

 

  Lydia Shio – Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi.

 

Wafanya biashara hao wa halmashauri ya Madaba Songea Vijijini wameipongeza Mamlaka ya TRA kwa kuwasogezea huduma za kikodi kwamba sasa watapata Maelekezo kamili ya jinsi ya kuweza kulipa kodi pamoja na jinsi ambavyo wao wataweza kujiendesha kibiashara.

 

                 1. Petro Ndiba – Mfanya Biashara Madaba

                 2. Salimu Seif – Mfanyabiashara wa halmashauri ya madaba

                 3. Ezekiel Mkombo – Mfanya Biashara

 

Mamlaka ya Mapato TRA imekua ikifanya juhudi za kuwasogeza wafanyabiashara ili waweze kupata manufaa kuhusiana na kodi wanazolipa na kuwaelimisha jinsi wanavyoweza kufanya biashara zao bila kuipunja Serikali wala kujipunja wao.