KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, May 14, 2012

SIKU YA MAMA DUNIANI NA SIKU YA FAMILIA NA SIKU YA WANAWAKE INA MAANA GANI KWA MTANZANIA ?

Nimeuliza swali kuwa mama na mwanamke ni nani jibu unaliona hapa watoto hao hapo juu ni watoto wakike lakini una weza kuona walivyo ng`aa hiyo ni kazi ya mama

Watoto hao hapo juu ni watoto wa vijijini lakini angalia walivyo pendeza hiyo ni kazi ya Mama ndiyo maana Tuna sema mama ana fanya kazi kubwa
Mwalimu mkuu wa Mtoto ni Mama hapo wapo katika Mkutano wa hadhara wakichukua elimu ili iende kwa mtoto nani kama mama
Pilipili mbuzi zikiwa kwenye mti jee unajua kwanini zina itwa Pilipili Mbuzi ni kwakuwa zina faa sana kwenye supu ya Nyama ya Mbuzi
Viumbe vingi hapa Duniani vina jali sana watoto hebu angalia vifaranga vinavyo mjali mama yao wakijua wazi kuwa ulinzi uko kwa mama yao
Vifaranga ulivyo viona hapo juu vimeingia kwenye mabawa ya mama yao baada ya mama yao kusikia sauti ya mwewe ili kuwalinda watoto wake unaweza kuona kazi ya mama
Mwanamke amepewa roho ya Huruma kwa Asilimia 100% pia amepewa ukatiri kwa asilima kubwa mwanamke akiwa na wazo la kuua mtoto wakati akizaa anaweza lakini wengi wamekuwa waungwana huyu hapo juu ni mwanamke yeye ameingia katika kazi ya kutibu watu kwa jina anaitwa Flora Ndembo.
Vijijini changamoto ni Maji lakini mtoto wakike yeye ndiye anaye kuwa tegemeo la kuchota maji kwa asilimia 100% kama unavyo ona hapo juu mtoto akivuta maji mita 20 kutoka chini Songea vijijini
Huyu ni Mtoto wakike lakini ukimwangalia utaona yuko makini kwa kujisomea hiyo ni karama waliyo pewa watoto wakike na Mwenyezi Mungu ili wawe walimu kwa familia yao hapo baadaye
Tunapo sema Mama kwanza nilazima ujue kuwa cheo cha kuitwa mama hakitolewi kiholela na mwenyezi mungu , Cheo hiki hupewa akina mama wenye moyo wa upendo na huruma hapo akina mama wakipata elimu ambayo kwa utashi walio pewa na Mungu huenda kuwa fundisha watoto wao nyumbani
Nini kazi ya Mama mama ana kazi kubwa sana ana takiwa awe na upendo huruma hapo mama akiwa hosipitali ya Peramiho Songea Vijijini akimuguza mumewe ambaye amepata upasuaji
Tunapo sema mwanamke ni umoja kwa wale walioko kazini wakiwa wameajiriwa na serikali au watoto wa kike walioko shuleni hii ina maana kwa ujumla, kuhusu mwanamke huyo hapo juu ni mmoja wa wanawake yeye ni afisa tawala wilaya ya Mbing.a

Thursday, May 10, 2012

MKUU WA MKOA WA RUVUMA MH.SAID THABIT MWAMBUNGU AMEWATAKA WAHISANI WANAO AHIDI KUCHANGIA MICHANGO WALIYO AHIDI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Thabit Mwambungu akitoa rai kwa kamati ya ujenzi wa jengo la Police wanawake kuwa makini katika kukusanya fedha zilizo ahidiwa na wadau shilingi milioni 32 zikusanywe kiuadilifu ili zimalize kazi iliyo baki

Ujumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la Police Wanawake ukiwa na wajumbe watano Ins Anna Tembo,A/Ins Fadhila Chacha, S/SG Mesia Mfupa, Mwenyekiti Mhamasishaji Adamu Nindi ,Mratibu Juma Nyumayo
Ujumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Jengo la Police Wanawake ukiwa na wajumbe watano Ins Anna Tembo,A/Ins Fadhila Chacha, S/SG Mesia Mfupa, Mwenyekiti Mhamasishaji Adamu Nindi ,Mratibu Juma Nyumayo
Mwenyekiti wa Mtandao wa Police Wanawake Ins Anna Tembo akipikea mchango wa shilingi 500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa jengo la police wanawake
Mdogo wa Nadia akisalimia wageni walio kuja kuwatembelea ofisini kwake
Nadia Mahamud akisalimiana na A/INS Fadhila Chacha alipo tembelewa nyumbani kwake
Mzee Marufu Mdau wa Police Wanawake Mzee Mahamud Dost akisalimiana na mtunza kumbukumbu A/INS Fadhili Chacha alipo tembelewa nyumbani kwake Msamala Manispaa ya Songea
Mwenyekiti wa Uhamasishaji Wa jengo la Police Wanawake Adamu Mzuza Nindi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa waruvuma
Mratibu wa Ujenzi wa Jengo la Police Wanawake Juma Nyumayo akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Said Thabiti Mwambungu
Mwenyekiti wa mtandao wa Police Wanawake Inspekita Anna Tembo akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu Ofisini kwake
Mtunza kumbukumbu wa ujenzi wa jengo la Police wanawake A/INS Fadhila Chacha alipo mtembelea mkuu wa mkoa ofisini kwake kutoa tarifa ya watu walio ahidi kuchangia jengo la Police Wanawake ambapo wadau mbalimbali waliahidi kuchangia shilingi milioni 32

Tuesday, May 8, 2012

MDAU WA POLICE WANAWAKE APATA NAFUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA ILIYO SABABISHA KWENDA KUTIBIWA NCHINI INDIA

kamati ya ujenzi wa jengo la Police wanawake walipo mtembelea mzee Mahamud Dost baada ya kupata ajali ambapo matibabu yake yalifanywa nchini India hivi sasa hali yake ina endelea vizuri
kikosi cha jeshi la wanachi wakiwa katika paredi kari ona ndugu yangu msamba kama wa Adamu Nindi unge weza kupasuka hilo siyo paredi bali ni balaa angalia mwenzangu
kamati ya ujenzi wa Jengo la Police wanawake wakiwa wame mtembelea Mahamud Dost kumfariji baada ya kupata ajal
kamati ya ujenzi wa Jengo la Police wanawake wakiwa wame mtembelea Mahamud Dost kumfariji baada ya kupata ajali
Hili ni Duka la Ndia Mahmud Dost ambalo liko katika maeneo ya kituo cha mafuta msamala kila kitu kina patika
Mwonekana wa Duka la Nadia Mahamud kwa ndani hivyo ni baadhi ya vipodozi

Ins Anna Tembo na S/SG Mesiah Mfupa katikati ni Nadia Mahamud akiwa nje ya Duka lake lijulikanalo kwa jina Zizzou Quick Shop dada huyu Nadia amekuwa mdau wa jengo la Police Wanawake Songea

Friday, May 4, 2012

UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI JENGO LA POLICE WANAWAKE SONGEA

Mwandishi wa habari wa Star tv Adamu Nindi akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu cha ufanyaji bora wa kazi kwa kuweza kuhamasisha na kuweza kufanikisha ujenzi wa jengo la police wanawake Songea ,
Mtoto ambaye aliokotwa na Police Wanawake baada ya kutelekezwa na Mama yake baada ya mama huyo kumtupa mtoto huyo katika shule ya msingi Mfaranyaki manspaa ya Songea
Police wanawake mkoa wa Ruvuma wakiwa katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la pilice wanawake ,jiwe la msingi lililo wekwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu
S/SG Measiah Mfupa akiwa katika sherehe za kuweka jiwela msingi wa Jengo la Police Wanawake
Mtoto aliye okotwa akiwa na kikosi cha Police wandamizi wa Police Wanawake mbele ya jengo lao baada ya kuwekwa jiwe la Msingi
Mtoto aliye tupwa na mama yake katika shule ya msingi mfaranyaki manspaa ya Songea
Police wakiwa na wandishi wahabariwalio simamia ujenzi wa jengo la police wanawake

kamanda wa police mkoa wa Ruvuma akipokea cheti cha utendaji bora wakazi hasa baada ya kusimamia jengo la polisi wanawake
juma Thomas Nyumayo akipokea cheti cha utendaji ulio tukuka baada ya kusimamia jengo la police
Asikari shupavu wa wa jeshi la Police Wanawake S/SG Mesiah Mfupa akipokea cheti cha usimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Pilice Wanawake
Insipekita Anna Tembo akipokea cheti kilicho tukuka cha usimamizi bora wa ujenzi wa jengo la police wanawake songea cheti kimetolewa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu
Diwani wa chama cha chadema Joseph Fyime akiwa changia ujenzi wa jengo la Police wanawake ambapo alitoa shilingi 50,000/=
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Thabiti Mwambungu akihamasisha harambee ya ujenzi wa jengo la Police Wanawake
Kamanda wa POLICE Michael Kamhanda akitoa tarifa ya ujenzi wa jengo la Police Wanawake mkoa wa Ruvuma
inspekita Anna Tembo akitoa Tarifa ya vitendo vya unyanyasaji katika mkoa wa Ruvuma
Mheshimiwa Jenista Mhagama Mbunge wa Jimbo la Peramiho akitoa hotuba kupongeza ujenzi wa jengo la police wanawake ameahidi kukarabati choo cha jengo hilo

MAPINDUZI YA KIJANI AFRICA ,KILIMO CHA KISASASA

WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARA WAKIJADILI KUHUSU KILIMO KATIKA KIJIJI CHA NAMANGULI WILAYANI NAMTUMBO
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbomkoani Ruvuma Exaveria Maketa akihimiza kilimo kupitia watalamu wa Uyole Mbeya
Kaimu Meneja Mradi Wiliamu Mmnali Akiratibu maswala ya Uboreshaji wa kilimokupitia Mapinduzi ya kijani ya Africa Chini ya uangalizi wa Kituo cha Uyole Mbeya
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Exaveria Maketa akipongeza Mradi wa Mapinduzi ya Kijani Africa jinsi walivyo bolesha kilimo kwa wilaya ya Namtumbo