KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Sunday, July 28, 2013

JEE UMEWAHI KUONA MWANA MKE MNNE ?

 

Mwanamke huyu ajulikanaye kwa jina la Mikell Rrufinel ana umri wa miaka 39 kiuno chake kina ukubwa wa
inchi40 upana wa makalio ni inchi 94 ameolewa na watoto wa nne mme wake anajulikana kwa jina la Ruggie Brooks naye ana umuri wa miaka 40 wote wawili wanaishi Los Angels

Wednesday, July 24, 2013

MAZISHI YA SHUJAA RODNEY NDUNGURU ALIYEFARIKI NCHINI SUDANI AKILINDA AMANI


Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majenshi Nchini Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameitaka Familia ya Marehehu Rodney Ndunguru na Watanzania wote kuwa na Moyo wa Subira kwa kifo cha Praiveti Rodney Ndunguru kilicho mpata huko Durfer Sudani  13/7/2013 baada ya kuvamiwa na waasi

Mheshimiwa Amiri Jeshi mkuu Jakayaya Mrisho Kikwete ameya sema hayo wakati akitoa salamu za Rambirambi kwa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru salalamu zilizo somwa na mwakilishi wa  Briged ya 401  Tembo  brged  kanaliGeorge Tomasi Msongole

 Jeneza la Rodney Ndunguru muda mfupi kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mjimwema Songea.
 Afisa Tawala Wilaya ya Songea Joseph John Kapinga katikati akiwa na Maafisa wa Jeshi katika Maombolezo ya Msiba wa Rodney Ndunguru Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma.
 Jeshila la Wananchi (JWTZ) lina taratibu zake katika kutoa heshima za mwisho kwa mwenzao anapofariki, hapo ni wanajeshi wakitimiza taratibu za heshima za mwisho katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema Songea ikiwa ni ishara ya kumuenzi Shujaa Rodney Ndunguru aliyefariki tar 13/07/2013 huko Darful Sudani akitekeleza Jukumu la Kimataifa la kulinda Amani.
 Jeneza lililohifadhi Mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likiwa limetolewa Bendera ya Taifa na Mavazi aliyokuwa akiyatumia tayari kwa kuingizwa kwenye Makao ya milele.
 Wanajeshi wakiwa katika viwanja vya Makaburi ya Mjimwema wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Rodney Ndunguru kadiri ya taratibu za ki Jeshi.
Katika mazishi hayo yaliyo fanyika katika makabuli ya Mjimwema manspaa ya Songea ya liweza kuhudhuliwa na viongozi wa serekari wa kiwakilishwa na katibu tawala Joseph John Kapinga ,jeshi la wananchi wa Tnzania ambapo heshima zote za kijeshi zilitolewa
 Wanajeshi walioshiriki msiba wa Mwenzao Rodney Ndunguru wakitafakari changamoto zinazowakabili katika kulinda amani.
 Mamia ya waombolezaji Wanajeshi wakiwa na huzuni katika kumsikitikia mwenzao aliyekufa kishujaa katika kutekeleza Majukumu ya Kitaifa wakiwa nyumbani kwa Marehemu Mjimwema Songea Mkoani Ruvuma kabla ya Mazishi.


Padre Noi Duwe akiendesha misa amesema swala la uvunjifu wa amani una tokana na kuto tii sheria zinazo tolewa serekari badala yake kuendeleza migomo na maandamano amewataka waumini waache kukashifu serekari

Msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amewaomba wa Tanzania kudumisha amani katika nchi yao bila ya amani ya kudumisha amani yata tupata yanayo tokea Sudani hivi sasa hatunge weza kumpoteza ndugu yetu Rodney Ndunguru lakini ni kutokana na kukosekana kwa Amani

Maafisa wa Jeshi wakitoa vifaa vya kazi (kofia, Sare, Mkanda na viatu) alivyokuwa akivitumia Marehemu Rodney Ndunguru wakati wa uhai wake tayari kwa Mazishi

 Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) wakitoa heshima zao za mwisho kwa Shujaa Rodney Ndunguru kwa kupiga Risasi  hewani mara baada ya mazishi yake katika Makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea

Captaini Patrick Kitosi kutoka kikosi cha 92 akisoma wasifu wa marehemu Rodney Ndunguru amesema Rodney Ndunguru alizaliwa 9/7/1985 Mjimwema mkoani Ruvuma alikuwa kijana shupavu, aliweza kufuzu mafunzo ya ukomandoo dalaja la pili na dalaja la tatu. Alisha wahi kwenda Dur fur mara mbili katika jitihada za kulinda amani Umoja wa Mataifa wa Nchi za Afirika alipata nishani akiwa Durfur Sudani


Mheshimiwa Rais  Jakaya Kikwete amesema Marehemu Rodney Ndunguru alipwatwa na mauti hayo wakati akitekeleza jukumu la umoja wa mataifa wa Africa la ulinziwa amanikatika eneowalilo shambuliwa ghafula ambapo yeye na wenzake 6 waliweza kupoteza maisha.

Kanali Goerge Thomas Msongole akisoma salamu hizo kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amesema msiba huu ni wa wa Tanzania wote na Taifa lote hivyo ni wajibu wetu watanzania wote kushiriki katika maombolezo na maombi ya kumwombea ndugu yetu Rodney Ndunguru

 Jeneza lililohifadhi mwili wa Marehemu Rodney Ndunguru likitolewa ndani nyumbani kwake Mjimwema Songea tayari kwa kuelekea Makaburini kwenye Makao ya Milele.

Wednesday, July 17, 2013

KUFUFUA ZAO LA KOROSHO NCHINI TANZANIA





Dr louis Kasuga Mtaalamu wa Utafiti wa Magonjwa ya korosho alisema baada ya juhudi za serikali kufanya utafiti na kubaini chanzo  cha matatizo na sababu zilizopelekeakuzotota kwa zao la Korosho iliweza kuongeza uzalishaji wake kutoka tani 16,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 158,000 kwa mwaka, kwa kutambua umuhimu wa zao hili la biashara ambalo ni la  pili Tanzania kwa kuingiza pesa za kigeni kutoka Nje.


Miongoni mwa kazi zinazofanywa na Kituo cha Utafiti wa Zao la Korosho Naliendele kilichopo Mkoani Mtwara ni kufundisha wakulima wa zao hilo mbinu bora za upandaji wa zao la korosho kwa njia ya ubebeshaji wa miche ya mikorosho. Picha unayoiona hapo juu ni Miche ya Mikorosho inaweza kupandwa kwa kubebeshwa kitaalamu

Wakulima wa Zao la korosho kutoka mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma wamesema chanzo cha kuzorota kwa zaola korosho ni kuchelewa kwa pembejeo, bei ndogo ya kuuzia na ukosefu wa masoko
 Wahiriki 125 wa Mafunzo ya uendelezaji na ufufuaji wa Zao la Korosho yaliofanyika Manispaa ya Songea ukumbi wa Chuo Kikuu Huria yaliyojumuisha wakulima, Maafisa Ugani, Wapuliziaji na  Maafisa Ushirika wa vyama vya Msingi kutoka wilaya za Songea Vijijini,Namtumbo, Mbinga, Rudewa na Kyela.
 Washirikiwa Mafunzo ya ufufuaji na Uendelezaji wa zao la Korosho wakiwa ndani ya ukumbi wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika Mafunzo hayo yaliyoendesha na wawezeshaji kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Korosho Naliendele chini ya Dr. Louis Kasuga na kugharamiwa na CIDTF (Cashew Industry Development Trust Fund).
 Washiriki wa Semina juu ya ufufuajina uendelezaji wa zao la korosho wakifuatilia elimu Bora ya Kilimo cha zao la Korosho ili kuinua viwango vya ubora na uzalishaji bora wa zao hilo, namna ya kuanzisha zao la korosho, kulihudumia, kulifufua na kuboresha Shamba la zamani.
 Washiriki wa Mafunzo ya uendelezaji wa zao la Korosho kutoka wilaya za mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Njombe wakisikiliza mada kwa makini katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Huria Songea Manispaa.
 Wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa Zao la Korosho Naliendele wakiseti mitambo tayari kwa kuendesha mafunzo juu ya uanzishaji, ufufuaji na uendelezaji wa Kilimo cha zao la korosho.
 Wataalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa zao la Korosho cha Naliendele wakiwa Mkoani Ruvuma katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria kuwezesha mafunzo juu ya ufufuaji na uanzishaji wa zai la korosho. mwenye kofia kushoto ni Mtaalamu wa Magonjwa na wadudu wanaoshambulia zao la korosho Mr. Barnaba Maarufu kama BB, na wa pili mwenye laptop mbele ni Bw. Maiko Nkondora mwasibu wa Kituo cha Utafiti cha Naliendele.
Dr. Louis Kasuga aliyeshika Projekta kwenye meza akiendelea kuonyesha changamoto zinazozorotesha zao korosho kwa washiriki wa Mafunzo ya ufufuaji na ufuaji na uanzishaji wa zao la korosho yaliyofanyika manispaa ya songea na kujumuisha washiriki kutoka wilaya 5 za mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya. Mwenye Jaketi ya Bluu katikati ni Mwanahabari Mkongwe wa Kituo cha Utafiti wa zao la korosho Naliendele Bw. Fakii Mussa. na kulia kwake ni Mtaalamu wa uanzishaji wa shamba jipya na upandaji wa zao la korosho Bw. Swrtbert Magani.

Thursday, July 11, 2013

ORYX YA TINGA SONGEA


Habari njema kwa Wanasongea,

"Katika muendelezo wa kusogeza huduma na bidhaa za Oryx Gas kwa wateja
wetu, ORYX Gas imefungua rasmi duka na depot ndogo mtaa wa SIDO kituo cha
mafuta kwa Komba- Mjini Songea. Tunasema sasa adha ya kukatika kwa nishati
muhimu ya gesi katika mkoa wa Ruvuma sasa baaasi" alisema Bwana Mahfoudh
Maulid- Meneja Mauzo wa Oryx Gas.

Tunataraji duka letu litasaidia kuhakikisha upatikanaji wa gesi katika mkoa
wa Ruvuma kwa bei elekezi ili kumlinda mteja wa ORYX Gas. Tunawaarifu
wasambazaji wetu wa Oryx, kuchukua bidhaa za Oryx kutokea duka letu na
kukemea kupandisha bei kiholela. Oryx ilianzisha utaratibu wa bei moja nchi
nzima kuanzia Decemba mwaka jana na bei kwa mtumiaji wa mwisho imekuwa shs
22,000 shs 54,000 na shs 133,000 kwa mitungi ya kilo 6, kilo 15 na kilo 38.


Aidha, Bwana Mahfoudh alihimiza watumiaji kuhakiki mitungi ya gesi
wanayonunua ina vizibo maalum au "seal", na wadai kupimiwa katika mizani
wanunuapo gesi. Uzito wa mtungi pamoja na gesi iliyomo ndani ya mtungi
vimeandikwa juu ya mtungi.

Hali kadhalika, Mahfoudh alinadi utaratibu mpya wa "Piga Uletewe" kwa maana
ya kuwa huhitaji tena kuhadaika na mtungi wa gesi ila tu piga simu uletewe
gesi nyumbani, mgahawani na hotilini kwako. Namba ya simu ya mhudumu wa
duka la Oryx ni 0758 002 090.

Kwa msisitizo mkubwa, Mahfoudh amewaomba wananchi kuwa makini na kutokubali
kubadilishiwa mitungi isiyokuwa rangi nyekundu ya Oryx. Wateja wetu
wanadanganywa na kufanyiwa uhuni usiokubalika kwa mujibu wa Sheria za Gesi
ya LPG. Mteja atapopeleka mtungi wa Oryx kwa muuza duka, amtake kumpatia
mtungi wa Oryx wa rangi nyekundu na si vinginevyo. Usisite kutoa taarifa
kwa namba +255767062896 endapo utafanyiwa uhuni huu.  Hili ni kosa kisheria
na Oryx inao wajibu wa kuchukua hatua kali za sheria kwa watuhumiwa.



Kwa hali ya kipekee kabisa, nitoe tena shukrani za dhati kwa wateja wetu
wapendwa wa ORYX GAS, Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, wadau
mbalimbali ambao kwa pamoja tumekuwa tukishirikiana kunadi na kuelemishana
kutumia nishati mbadala kama ORYX GAS ili kutunza mazingira yetu.
Oryx Gas
ni nishati mbadala ambayo ni Safi, Salama, Garama nafuu, Chapchap na rafiki
wa afya na Mazingira.

Endelea kufurahia nishati yako ya Oryx Gas, na kwa wasambazaji wapya,
tafadhali tuma sms au piga simu namba kwa Sales Person wetu wa kanda
+255759588115 au moja kwa moja kwa Meneja Mauzo 0755 017 073.
Oryx Gas,
Mtindo wa Kisasa!

Wednesday, July 10, 2013

UNAPO INGIA KARINE YA 21 NILAZIMA UBADILI MAISHA KWA KUTUMIA TECONOLOGIA YA KISASA

 Kampuni ya ORYX GAS imewaletea huduma mhimu wakaazi wa Mkoa wa Ruvuma Ges yenye bei nafuu, unapo taka kuipata huna haja ya kusumbuka kutemea kufuatia kwenye maduka wewe kazi yako ni kupiga simu tu,Hebu angalia huyo mama anavyo faidi
Hiyo niges ikiwa katika viwango mbalimbali na una pata kwa bei nafuu ,Ges hiyo ina uzwa katika Sheli ya Komba iliyoko kati kati ya mji

Tuesday, July 9, 2013

USHIRIKINA UNAWEZA KUWA ADHABU KWA MABINTI PALE WANAPO TAKA KUPATA WATOTO

Mabinti hao wawili wakiwa kwa mganga wa jadi  Bint Ndembo wa Namtumbo Ruvuma kuomba wafunguliwe baada ya kumtuhumu bibi yao kuwa wame fungwa kizazi, Bibi yao alikiri kuwa kweli yeye ndiye aliye wafunga kibuyu alicho kamata binti wa kwanza kulia ndicho kilicho tumika kuwa funga hawo ma binti, Msomaji una maoni gani kuhusu hilo

Wednesday, July 3, 2013

MJUMBE WA UTPC ATEMBELEA RUVUMA PRESS CLUB -SONGEA

 Katibu wa Ruvuma Press Club Andrew Chatwanga akiwa na Mgeni kutoka UTPC  Mzee George Mkude akiwa katika ofisi za Asasi zisizo kuwa za kiserekari Mkoa wa Ruvuma ,RUNECISO [Ruvuma Network of civil society organization ] na aliye mshika bega katibu msaidizi Mosses Konara ni Makamu Mwenyekiti wa RUNECISO Adamu Mzuza Nindi
 Mgeni kutoka UTPC Mzee George Mkude akiwa na jopo la Viongozi wa andamizi kutoka kulia Juma Nyumayo Mratibu wa RUNECISO, Anaye fuatia kutoka kulia ni Moses Konara katibu msaidizi wa Ruvuma Press Club na anaye onyesha kibao ni Mzee George Mkude ,aliye kushotokwa mzee mkude ni katibu wa Ruvuma Press Club Andrew Chatwanga.
Mzee George Mkude kutoka UTPC amewataka waandishi wa habari kuwa chachu ya kuleta maendeleo hasa kuangalia watu wanaoishi pembezoni mwa mikoa ili waweze kujiondoa katika umasikini.pia amewataka waandishi wa habari habari zao ziwe kama dira ya kuwaongoza viongozi kujua changamoto zinazo wakabili watu wanaom ishi pembezoni