Ndugu Mtanzania kuna usafiri mwingi kutoka bara hadi Dar - es - salaam ,utokapo Songea ni bora kutumia usafiri Rahisi ambao ni wa Super Fello , Nembo yao ni hiyo kulia kwako
MAKAA YA MAWE RWANDA MBINGA YA UNGUA KWA MOTO
Adam Nindi – Radio Free Afika – Moto Mbinga – 6/05/2006
Wananchi wanaoishi Kijiji cha Mdunduwalo Kata ta Rwanda Tarafa ya Naswea Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wapo hatarini kuteketea kwa Mto kama hatua za haraka hazitachukuliwa kuuzima Moto huo.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Mh. Gaudens Kayombo amedai kuwa mlipuko na Moto katika eneo la Mto NYAKAGUNDA umetokana na Makaa ya Mawe ambayo huenda Mlipuko huo umetokana na Gesi au wawindaji haramu ambao huchoma Moto ovyo kwa ajili ya kuwinda wanyama na Mto huo hatimaye Moto kudaka katika makaa ya mawe.
Mh. Gaudens Kayombo amedai kuwa eneo hilo liliwahi kuchimbwa Makaa ya Mawe na Wajerumani Mwaka 1945 na Uchimbaji huo ulikoma Mwaka 1953 Tabaka la Makaa ya Mawe yaliyopo katika eneo hilo, katika vijiji vya Mkapa, Ngaka, Liyombo, Mkulu na Mbuyula inakadiriwa kuwa ni Tani 99.25 Milioni. Tani zinazokisiwa kuungua mpaka sasa ni Tani Milioni 6. Moto huo umeanza kuwaka toka Mwaka 2003 Septemba.
Mh. Gaudens Kayombo amedai Moto huo usipozimwa mapema utaweza kuvuka wilaya jirani ya Makete Iringa na kuunguza Madini ya Mchuchuma ni Kilomita 32 kutoka Mto unapowaka. Pia Vijiji vilivyotajwa hapo juu vinaweza kuteketea. Radio Free Africa na Star Tv imeshuhida kuteketea kwa Makaa
UZIMWAJI WA MOTO ULO KUWA UKITEKETEZA MAKAA YA MAWE RWANDA MBINGA
Serekari ya Jamuhuri ya Mungano baada ya kusikia kilio cha wana mbinga hatari ya kuteketea kwa Moto ili tuma watalamu wake ili waweze kuuzibiti Moto huowatalamu baada ya kufanya utafiti ili baini kuwepo kwa madini ya makaa yamawe zaidi tani 400
Watalamu hao ambao waliongozwa na katibu mkuu wa widhara ya Madini kutoka Taifa alikuja na mwana Jiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma Geologia Dr Pascal Semkiwa kwa ajili aya kuangalia jinsi ya kuweza kuuzima moto huo
Watalamu walipanga mbinu ya kuchimba urefu wa mita 10 kwenda chini kuzunguka eneo lote linalo unguza madini ya makaa yam awe
Serekari ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania ilitumia kiasi cha shilingi milioni 59 kuuzima moto huo.
Nini faida ya kuuzima Moto huo jambo lakwanza wananchi wataweza kufaidi Madini yao kwa kufaidika katika nyanda zifuatazo, Elimu,Afya,Michezo, Pamoja na kupata mawazo tofauti na waliyo ya zoea kutoka kwa Wawekezaji wa kutoka nje.
Mwaka ulio fuata mbunge wa jimbo la mbinga mashariki Gaudensia Kayombo alitafuta wawekezaji ambao walitoka .
Mkurugenzi Campuni ya TANCOAL ENERGY Emmanuel Constantinides amesema uchunguzi uliofanywa mwaka 1952 ulibaini kuwepo kwa Madini ya Makaa ya Mawe Tani Milioni 79 Lakini utafiti uliofanywa Mwaka 2001 umebaini kuwepo kwa Madini ya Makaa ya Mawe Tani Milioni 200 – 4000
Campuni ya TANCOAL ENERGY kutoka Dar –es- salaam ikifadhiliwa na campuni ya Atomic Resources ya Asutaria imesema Inaanza malinganisho ya uchimbaji wa mkaa ya Mawe kazi itayo chukua mwaka mmoja
Nao Mtambo wa kufua Umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe ambao uta kuwa na uwezo wa kufua Megawat 400 uta kamilika baada ya miaka 3 kuanzia 2010 – 2013
Mtambo huo wa Umeme utaweza kutoa ajira kwa Watu 400, na uchimbaji wa Mgodi wenye urefu wa mita 300 kwenda chini wa makaa ya mawe utaweza kuajiri watu 400.
Naye mfadhili kutoka Kampuni ya Atomic Resources Limited iliyopo Australia, bwana Cilinton Cain amesema mradi mzima wa kujenga Mtambo wa Umeme wa Makaa ya Mawe utagharimu US Dolla za Kimarekani Bilioni 1.2
Mtaalam wa Geologia Dr Pascal Semkiwa amsema Tanzania itapata faida kubwa kwa kuweza kupata Salpha kwa ajili uengenezaji wa Simenti na Mbolea.Salpha itakayo patikana hapo itakuwa chini ya asilimia 1.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mashariki amesema juhudi zilizo fanywa na Serekari kuzima Moto uli kuwa ukiangamiza rasilimali za watanzania kwa kutumia shilingi milini 59 sasa uta kuwa ukombozi kwa taifa kuongeza kipato na uchumi wa Watanzania.
No comments:
Post a Comment