Ndugu zangu popote pale mlipo Tanzania inaingia katika uchaguzi mkuu hapo tarehe 31/10/2010 nijambo la kujivunia kuona utawala bora una tekelezwa.
kwa mda wa miaka 49 toka tupate uhuru tume kuwa na amani na utulivu, hakuna anajua kabla la mwenzake au mtu kumtenga mtu kwa ajili ya dini huo ni ushi mkubwa kwa nchi yetu.
S.asa tunaingia katika kutayarisha maisha ya amani na utulivu jambo tunalo lifanya tarehe 31/10/2010 nijambo ambalo tuna weza kununua kifo au kuongeza amani. Ninge omba ndugu zangu kwa kuwa kuchagua mtu mwenye busara kuna tegemea akili zako ziko namuna gani ni mtu wa kufuata mkumbno au ni mtu ambaye una tegemea akili zako?
kama huna jibu ingia ndani ya chumba chako uombe Mungu ili akusaidie, kura yako ni risasi ya mwisho ya kulinda uhai wako kwa miaka mitano inayo kuja.
kura hihiyo ni sumu ya chokochoko ya kupoteza amani na utulivu tulio nao nimategemeo yangu kuwa kila mtu atazingati busara zake kutoa uamuzi Tumwombe Mungu atuongeze busara na utashi ili uchaguzi tutakao uamua uwe wa heri na amani.tuchague Diwani mwadilifu,Mbunge mwadilifu,na Rais mwadilifu vile vile
wenu Adamu Mzuza Nindi SongeaRuvuma Tanzania
No comments:
Post a Comment