UCHAGUZI NA WATANZANIA WA FANYIKA KWA AMANI.
Adamu Nindi -Songea- Ruvuma 8/11/2010
Watanzania mda mrefu walikuwa wakingoja kupiga kura ili wachague kiongozi wanaye mtaka na siku ya tarehe 31/10/2010 siku ambayo ili kuwa siku ya jumapili siku ambayo waumini wa dini ya kikristo hufanya ibada, ibada ya siku hiyo kwao ili kuwa kupiga kura,
watanzania walio jiandikisha kura nao hawakuwa nyuma katika kupiga kura.ieleweke kuwa watanzania walio wengi zaidi milioni 26 walijiandisha kupiga kura lakini walio piga kura walikuwa milioni 8
wengi wamejitokeza kusema watu walio wengi wali ogopa kujitokeza kwa sababu ya kuogopa fujo,wengine wakidai kuwa walio jiandikisha hawakuweza kuonekana majina yaokatika dafutari ya mpiga kura,
Jambo muhimu nikuwa watu walio chaguliwa na Mwenyezi Mungu ndio walio piga kura, wapo watu walio kufa kabla ya kupiga kura, pia wapo watu walio tiwa mbaroni kabla ya kupiga kura hao wote ni mapenzi ya mungu yalipita.
kila mtu huvuna alicho panda Rais mteule Mh Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake amesema katika mzunguko wa kuzunguka tanzania mzima ameweza kufanya mikutano 706 ikiwa na maana kila mkutano alio fanya aliweza kupata kura 7474.4
kwa maana hiyo ana takiwa kutathimini mikutano yoye aliyo fanya na kuangalia nini kero za watanzania walizo toa bila kujali ni wa chama gani kwani huduma atakayo tekeleza ita kuwa ni huduma ya watu wote.
watanzania hivi sasa wanatakiwa kuanisha kero zao na kuwapa Madiwani ,Wabunge,na Mawaziri watakao teuliwa na Rais ili upigaji wao kura uwe na tija, mambo ya malumbano hivi sasa yana takiwa yaachwe kwani hivi sasa kinacho takiwa ni kujenga nchi.
Napenda pia kumpongeza mwakilishi wa vyama vya upinzani nduguIbrahimu Lipumba kwa hotuba aliyo itoa wakati wa shukurani za kumshukuru Rais mteule ambaye hivi sasa ni Rais wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania Mh. jakaya Mrisho Kikwete na kuweza kumpa katiba ya chama cha CUF
Huo ni ukurasa mpya ambao kila cha cha upinzani ungeweza kutoa katiba yao ili Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania aweze kujua vyama vingine vilitaka kuwa hudumia vipi wa tanzania, yale mazuri Rais ange paswa kuya chukua,
jambo pekee lililo baki kila chama kiwe na dhana kuwa kime shinda uchaguzi kwani kila chama kime pata kura kutoka kwa wananchi chama cha mwisho kilipata kura 13,176 hao ni watanzania ,
Mgombea wa CHADEMA Wilibod silaha alipata kura 2,271,941 ni kura nyingi ambazo sera zake ziliungwa na watanzania hao, zaidi ya hayo sera ya chama cha mapinduzi kili pata kura 5,276,827 ambazo zilipatikana baada ya Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kufanya mikutano 706 ambapo sera zake zilikubalika na wana CCM na wale wasio kuwa na vyama.
Sija penda kuwa chosha ila ni kutaka kuweka mambo sawa ushindi ni wa watanzania wote hivyo tuungane kujenga nchi yetu, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wandishi wa habari kutibu majeraha yaliyo patikana wakati wa kampeni na siyo kuongeza majeraha ni jukumu la kila mmoja kutafuta njia ya kutibu majeraha.
Mtu yeyote atakaye onekana akiongeza majeraha ni juu ya watanzania kumsaidia ushauri nasaha asante wenu Adamu Mzuza Nindi kutoka mkoani Ruvuma Tnzania.
No comments:
Post a Comment