KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, August 29, 2011

MASISTA CHIPOLE SONGEA




Maporomoko ya mto chipole songea vijijini ambayo yanalipatia shirika la mtakatifu Aginesi umeme wa uhakika na umeme mwingine kukosa matumizi .wakati huo huo manspaa ya Songea ikiwa na Umeme wa mgao

MGENI KUTOKA ETHOPIA

katika ziara ya ndugu Douglas Huemmer, kutoka Ethiopia/USA akiwa katika ziara ya kusaidia watoto yatima na wenyeji wake aliye katikati ni Maula Chale na aliye kulia ni Adamu Nindi,

Sunday, August 28, 2011

MEYA WA LICHA NCHINI MSUMBIJI AKIWA SONGEA

katika kuboresha ujirani mwema kati ya Msumbiji na Tanzani Meya wa Jiji la Lichinga nchini Msumbiji Agugost Luis alitembelea Mkoa wa Ruvuma na kuingia mkataba wa Maendeo na Mkoa wa Ruvuma



Uti wa Mgongo wa uchumi katika Tanzania ni Kiliomo hapo ulionalo ni shamba la Chai liliopo katika eneo la Kibena Wilayani Njombe Mkoa wa Njombe,




Diwani wa kata ya Matogoro Chares Mhagama akiwa miongoni mwa madiwani wanao wania nafasi ya Umeya katika Manispaa ya Songea ,Akiongea na Glob ya Yaliyo jiri Mkoa wa Ruvuma amesma nia yake ni kuwaendeleza wana Ruvuma katika Kilimo na Elimu
NAMNA GANI YA KUINGIA KATIKA MCHAKATO WAKUPATA KATIBA MPYA YA JAMUHURI YA MUNGAONO YA TANZANIA
Na Adamu Nindi - Songea

Ndugu zangu wanahabari hivi sasa tumeingia katika kutafuta ukombozi kwa mwanadamu anaye ishi katika Nchi Teule ya Tanzania,Jambo la kwanza tunaingia katika mchakato wa katiba mpya jee katiba ya zamani ina mapungufu gani ,Jee ina ubora gani kwa Watanzania, nini kifanyike ili Tanzania ya Mwaka 1964 isiwe ya mwaka 2011,

Maswali hayo yote yana weza kujibiwa na wana habari .kwa mda mrefu tume kuwa tukipiga kelele jinsi ya kumfanya Mtanzania aishi kuendana na kauli ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano Tanzani Dr Jakaya Mrisho Kikwete ya kusema Maisha Bora kwa kila Mtanzania. Jee kauli hii ina managani kiundani ? kitu cha msingi ni kuona mtanzania ata ingiaje katika maisha hayo bora, Jee katiba iliyopo ita weza kumfanya awe na maisha bora, la msingi wana habari tuna kila zana ya kumfanya Mtanzania awe na maisha bora kwa kufuata Taratibu,Kanuni, na sheria za nchi,

Napenda kuwa julisha kuwa mimi kama mwana harakati kwa maswali niliyo yatoa hapo juu nita yavalia njuga ili kila mtanzani ajue jinsi ya kuingia kwenye mchakato wa katiba wale ambao wata taka twende sambamba na BLOG inayo julikana YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA . Ukitaka kuingia basi andika hivi http://www.songeahabari.blogspot.com/ ukimaliza hilo tupo pamoja naahidi sita waangusha wa Tanzania.

Mwisho nimalizie kwa kusema Tanzania ni nchi yenye Baraka zote za Mungu ni juu ya Watanzania kulinda baraka hizi kwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata katiba mpya

Wenu Adamu Mzuza Nindi - Songea

Saturday, August 27, 2011

ADAM NINDI – YALIYO JIRI SONGEA
Wanawake wametakiwa kuthubutu katika kutetea haki zao kwa kupambana na mfumo dume ambao unawa fanya wasiwe na sauti ya kudai haki zao.

Hakimu mkaazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Songea Janety Honoratus Mtega amesema hayo baada ya kufanya ziara katika gereza la Mahabusu la Songea na kubaini makosa mengi ya watu walio shitakiwa na kushitaki yamekuwa mengi zaidi kwa wanaume kuliko wanawake , sababu kubwa zaidi ni wanawake kukosa elimu ya kisheria pia umasikini ulio kisiri miongoni mwa wanawake

jambo hili huwa fanya wanawake wengi waridhike na lile wanalo fanyiwa na kuona kudai haki ni kupoteza wakati ,Pia vyombo nya kisheria vinavyo watetea watu wasio na uwezo havijitangazi ili mwanchi aliyoko pembezoni aweze kupata furusa hiyo.

, Hakimu mkaazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya songea Janety Honoratus Mtega Akitoa takimu ya mahabusu na wafungwa walioko gereza la songea amesema robotatu ya idadi ya wafungwa ni wanaume wanawake wapo kidogo sana,katika ziara aliyo ifanya tahehe 29/7/2011 alibaini kuwepo mwa mwanamke mmoja aliye shtakiwa kwa kosa la mauaji Aima Shabani, Mwanamke mwingine ni Sikujua Kaluwa anaye tuhumiwa kuvunja na kuharibu mali lakini yeye yuko nje kwa dhamana,

Habari ziliyo patikana inje ya mahakama zina sema Nyumba hiyo inayo gombaniwa ni mali ya Sikujua kaluwa .Nyumba hiyo inadaiwa imeuzwa kima kosa , Mpaka sasa nani iwe nyumba yake imebaki kuamuriwa na Mahakama nani ata shinda kati ya mdai na mdaiwa.

Hakimu mkaazi mfawidhi wa mahakama ya songea Janety Honoratus Mtega amesema kutoka na ziara yake gerezani amebaini kuwa watuhumiwa walio wengi hawana uwezo wakuweka mawakili ,Hakimu mkaazi mfawizi wa mahakama ya songea amewataka mawakili ambao hutetea watuhumiwa wakesi mbalimbali watembelee katika magereza ili wawasaidie wale ambao hawana uwezo wa kudai haki zao.

Akieleza kuhusu wanasheria amesema ni vizuri Jeshi la Police na wana sheria wakashirikiana kusukuma kesi zilizopo ili kuweza kupunguza mlundikano wakesi na kuweza kupunguza mahabusu gerezani
Umati wawaombelezaji katika msiba wa Ally Said Manya wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Songea Dr Emanuel John Nchimbi katika eneo la Nyumbani Kwake Lizaboni Manspaa ya Songea
Umati wawaombelezaji katika msiba wa manya wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Songea Dr Emanuel John Nchimbi
Wananchi wa Manspaa ya Songea walio hudhuria kumzika aliye kuwa Meya wa Manspaa ya Songea Hayati Ally Saidi Manya nyumbani kwake Lizaboni,
Mbunge wa Jimbo la Songea ambaye pia ni waziri wahabari utamaduni na michezo Dr Emanuel John Nchimbi akiongoza maombelezo ya aliye kuwa meya wa mnspaa ya Songea Ally Said Manya kabla ya kumpeleka katika safari ya mwisho.
Waziri Dr Emanuel John Nchimbi amesma fahari ya mtu anapo fariki dunia ni watu kushuhudia mema aliyo wa tendea watu, Alisisitiza Aly Manya alikuwa mtu wawatu alipenda maendeleo, kwa vigezo hivyo sasa tumpigie makofi

WATOTO WA SHULE ZA MSINGI WAKIWA WAMEBEBA KUNI KWA AJILI YA KUUZA KATIKA WILAYA YA NAMTUNBO


Wanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya mpya ya namtumbo wakiwa wame beba kuni kwa ajili ya kuuza
Jeshi la police Mkoani Ruvuma likiendesha msako kwa madereva wasio kuwa na leseni WP Veronica Futte akiwa barabani kuendesha zoezi hilo la ukaguzi wa leseni katika manspaa ya songea.

Friday, August 26, 2011

RAIS DR JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEMBELEA RUVUMA

Mjasilia mali ambaye ni Mfanya biashara Mashuhuri Mkoani Ruvuma Stanle Matembo yupo tayari kushirikiana na mfanya biashara yoyote Tanzania ,Ikiwa mazao,mbao,pamoja na bidhaa zipatikanazo mkoa wa Ruvuma kwa mawasiliano zaidi tumia mtandao huu



Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete alipo tembelea Mkoa wa Ruvuma hapo yupo uwanja wa ndege Luhuwiko Manspaa ya Songea akipokewa na Madiwani kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Cristine Ishengoma



Mlemavu Chares Mhagama ambaye alipata ulemavu jijini Dar -es -salaam mwaka 2006 mpaka leo haja pata matibabu ya kumwezesha kupata nafuu ana hitaji msaada kwa watu ambao wana weza kumsaidia yupo songea lakini hana mbele wala nyuma yoyote mwenye msaada atumie E-mail ifuatayo adam_nindi@yahoo.com




Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Cristina Ishengoma akiwa na mjukuu wa mkuu wa mkoa ambaye anaonyesha furaha akiwa ikilu ndogo mkoani Ruvuma




Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Crisitine Ishengoma Mkuu wa mkoa pekee ambaye historia yake haiwezi kuvunjwa kwa jinsi alivyo simamia maendeleo katika mkoa wa Ruvuma hasa katika kilimo amewezesha Mkoa wa Ruvuma kuweza kuzalisha Mahindi kwa wigi,zao la Tumbaku. pamoja na mazao mengine
BIASHARA HARAMU YA MIFUPA YA BINADAM YA INGIA TANZANIA
Adamu nindi –songea

Jeshi la Police mkoani Ruvuma limemtia mbaroni Said Kandamanje kwa tuhuhuma ya kumua Jafari Shabani Issa na kuchuna ngozi hatimaye kupangua mifupa yake,

Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda amelitaja tukio hilo kuwa lime tokea kata ya mhukuru kijiji cha nakawale Songea vijijini wakati Saidi Kandamanje alipo mrubuni Jafari Shabani Issa kuwa waende Mtoni kuoga ,

Said Kandamanje mara baada ya kufika katika mto Nakawale alimpiga na kitu kizito Jafari Shabani Issa ,hatimaye kumchuna ngozi na kumalizia kupangua mifupa, nyama na kichwa alivitia katika mfuko wa mbolea na kuviacha kando ya mto hadi ndugu walipo kuja kutambua mabaki ya mwili wa marehemu,

Jeshi la Police lilipo mhoji mtuhumiwa amesema Mifupa ya Binadamu na Ngozi ni bidhaa inayo uzwa katika nchi jirani,akithibitisha usemi wake amesema Makaburi mengi mpakani yana fukuliwa Watu walidhani ni Fisi kumbe ni kutokana na biashara hiyo haramu,

Thursday, August 25, 2011

KARANI WA WAANDISHI WA HABARI MKOANI RUVUMA

Karani wa chama cha waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma Judith Lugoye akiwa katika ofis za Star Tv Songea Mkoani Ruvuma

MEJA AHAMED ABASI JKT MLALE SONGEA

meja ahemed ahamed akiwa na kaimu mkurugenzi wa h/ya wilaya ya songea wakipokea kombe kutoka kwa vijana wa JKT Mlale Songea Vijijni.



Mwalimu mkuu wa Sekondari ya Matimila Songea vijijini Mkoani Ruvuma akiwa amejinyonga baada ya kutuhumiwa kubaka




Fundi seremala akiwa amejinyonga baada ya kumtuhumu mke wake kutembea nyinje ya ndoa


Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama akipokelewa na wanachama wa CCM katika kijiji cha igawisenga songea vijijini mara baada ya kuchaguliwa kuwa katibu wa wabunge wa chama cha mapinduzi


Mjasilia mali akipika Ugali kwa ajili ya kuuza katika wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma



wapimaji wa mipaka kutoka Msumbiji na Tanzania wakiwa katika kambi yao Lipalamba



Mwandishi wa Habari Adamu Nindi akitafuta habari kwa wananchi walioko pembezoni mwa mkoa wa Ruvuma


Wajumbe wa Tanzania na Wajumbe wa Msumbiji wakiwa katika kikao kujali jinsi ya kuitambua mipaka iliyo wekwa na serekari ya kijerumani .

MAADHALI YA MAZINGIRA YANAVYO ONEKANA KITONGA

Mto kitonga katika mkoa wa Ilinga angalia madhali yanavyo pendeza tunza mazingira ya kutunze


mwandishi wa habari Adamu Nindi akifurahia maadhali ya kijijini lipalamba



Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi Joisi Joliga akiwa Mpakani Msumbiji katika mto Nindi kata ya Lipalamba wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Katika kutafuta Habari za Pembezoni




kijiji cha Nindi kilichopo mpakani Msumbiji katika kata ya lipalamba wilayani mbinga mkoani Ruvuma

UWEKEZAJI NA JESHI LA POLISI RUVUMA

kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda akiwa shambani kwake akikagua shamba lake tayari kwa kilimo msimu wa mwaka 2011 -2012

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AKIWA KIUMA TUNDURU

Naibu Waziri wa Elimu Kasimu Majaliwa akiwa wilayani Tunduru akipokea CD ya Dini iliyo imbwa na wanafunzi wa cuo

MWANDISHI WA MKOA AKIWA MPAKANI MSUMBIJI

Mwandishi wa Habari wa mkoa wa Ruvuma Kasim Kashimba akiwa kilometa 100 kutoka Songea mijni katika kukagua mipaka kati ya Msumbiji na Tanzania

Wednesday, August 24, 2011

MKUU WA KITENGO CHA MIPANGO TGNP

Mjumbe wa Mtandao wa Jinsia Tanzani (TGNP ) Liliani Liundi akiandaa mada kwa ajili ya kuwawezesha wana Mtandao wa Ruvuma kuhusu haki za wanawake



Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania Liliani Liundi akiratibu maswala ya Jinsia kwa Mkoa wa Ruvuma




Kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda akitoa tarifa kwa Wandishi wa Habari kuhusu utumikishwaji wawatoto wakike katika nyumba za starehe Nchini Msumbiji kinyume cha sheria






Na Adam Nindi , Songea.

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma baada ya kutumia wataalamu wake wa Upelelezi wamebaini kuwa watoto walio chini ya Miaka 18 wapo Nchi jirani ya (Msumbiji) wakifanyishwa kazi zilizo kinyume na Sheria za Haki za Binadamu Duniani.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma Maiko Kamuhanda amesema kutokana na mkutano wa Ujirani Mwema uliofanywa kati ya Kamati ya Ulinzi ya Mikoa ya Mipakani Mkoa wa Nyasa Nchini Msumbiji na Mkoa wa Ruvuma Tanzania ulipeana mikakati ya kuzuia biashara haramu ya Madawa ya Kulevya pamoja na kusimamia haki za binadamu pamoja na kulinda haki ya watoto kutofanyishwa kazi katika machimbo na Kumbi za starehe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Maiko Kamhanda amesema kutokana na Mkataba ulio ainishwa kati ya msumbiji na Tanzania hakuna kizuizi kwa Askari wa Tanzania kufanya Uchunguzi wa kulinda na kutetea watoto walio chini ya miaka 18 .watoto kuingia Msumbiji na kufanyishwa kazinikosa

kamanda wa police mkoa wa ruvuma baada ya kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Nyasa imebainika kuwa katika mchimbo ya Turo msumbiji wapo watoto wasiopungua 50 ambao wanafanya kazi katika Majumba ya starehe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ameiomba Mitandao inayohusika na kusimamia haki za weanawake hasa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kusaidia Polisi kwa kutoa taarifa za vitendo vinavyo wazalilisha wanawake.

Mkoa wa Ruvuma wenye watu wapatao 1, 400,000 kutokana na kuwa na hali mbaya ya Kiuchumi kwa Ukosefu wa Viwanda, baadhi ya wazazi wanawatumia watoto wa kike kama Kitega Uchumi kwa kuwaoza wakiwa na umri mdogo au kuwaruhusu kufanya kazi katika Kumbi za starehe.
Mtandao wa Jinsia Wanawake kupitia TGNP umeanza Mchakato wa Kuzuia Hali hiyo.
MWISHO

MENEJA WA TANESCO MKOA WA RUVUMA MONICA BENJAMIN KIBARA

Meneja wa Tenesco Mkoa wa Ruvuma Kushoto Monica Benjamin Kibura akibadilisha mawazo na meneja wa benk NMB Tawi la Songea katika uwanja wa ndege wa Luwiko Manispaa ya Songea


ADAM MZUZA NINDI – UMEME – SONGEA

Bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni mbili zime haribika mkoani ruvuma baada ya ukosefu wa umeme wa mda mrefu.

Wafanyabiashara mkoani ruvuma wameileza radio free afrika kuwa kutokana na kukosa matangazo ya kukosekana kwa umeme wamekuwa wakiendelea kuagiza bidhaa kama samaki wabichi kutoka mtera,dar-es-salaam na mwanza,

Samaki hao wakiwa wabichi wameshindwa kusitahimili kutokana na majokofu kuto fanya kazi hadi wanaoza umeme huwashwa saa saba usiku na kuzimwa 11 alfajiri uta saidia nini walihoji

wamesema kwa kipindi cha wiki moja sasa wamesha tupa samaki waliooza wenye samani ya shilingi mioni 2,aidha lutengano lutengano amesema wamekuwa na kawaida ya kununua nyama zaidi ya kilo kumi ili watumie kwa mwezi kutokana na ukosfu wa umeme tayari kilo saba zime haribika.

Wakitoa masikitiko yao wamesema shirika la tenesco linapo dai bili za umeme hutangaza kuwa wasio lipa siku Fulani umeme una katwa jee hawawezi kutangaza hali ya kukosa umeme mji wa songea ili watu wasitegemee majokofu.

Nao madakitari ambao hawa kutaka majina yao ya tajwe wamesema kunaweza kuzuka ugonjwa wa njia za hewa kutokana na kuvuta hewa chafu ya cobondox ,au caboni ya mkaa kutokana na uwashaji genereta kiholela mji wa songea una jenereta zaidi ya 40 zinazo washwa wakati mmoja.

Alipo ulizwa meneja wa tenesco Monica Benjamin Kibara kuhusu hali ya kukosa umeme manispaa ya songea amesema haijulikani hadi yatakapo patikana mafuta. Aliye chukua tenda ya kuleta mafuta naye ameathirika na mgomo wa bei ya mafuta .

MAISHA YA ADAMU MZUZA NINDI
Ndugu zangu ni vizuri kwanza kujua nani una zungumza naye pili ana pendelea nini.
Kwa jina naitwa Adamu Mzuza Nindi, nilizaliwa 7/7/1954 katika kijiji cha Chiulu wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Elimu ya shule ya msingi nilianza nikiwa na miaka 7 katika shule ya msingi Gatoma nchini Zimbabwe ambako wazazi waliamu kwenda kufanya kazi katika machimbo ya Gatoma Mine Zimbabwe,

Nikiwa Zimbwabwe nilisoma hadi darasa la nne wazazi walipo amua kurudi Tanganyika ,baada ya kufika Tanganyika wakati huo mwaka 1960 nilirudia darasa la kwanza katika shule ya msingi chiulu liyoko Tarafa ya Mbambababay Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma nili rudia darasa ili nielewe lugha ya kiswahili, Nilianza maisha mapya katika kijiji cha Zoole kata ya Chiulu Tarafa mbambabay wilaya ya mbinga mkoa wa Ruvuma

jambo ambalo sita lisahau katika maisha yangu nipale tulipo tayarishiwa chaku wageni kuku alichinjwa na ugali ukawekwa mezani nili jaribu kukata ugali nilishindwa nikamuliza baba kwanini huku wana kula gundi ngumu baba alicheka akasema huu ni ugali wa mhogo ili chukua muda kuuzoea,

kitu kilicho nifurahisha baada ya kufika Tanganyika ili kuwa kupatikana kiurahisi kwa matunda aina ya ndizi tukiwa zimbabwe ndizi tuliziona tukilazwa hosipitali.

Nilisoma katika shule ya msingi chiulu baadaye nilihama kwenda kusoma shule ya msingi Nyoni Mbinga baada ya kufaulu darasa la nne na kuchukuliwa na dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo alikuwa mwalimu wa shule ya msingi nyoni kilometa 40 kutoka kijiji cha chiulu wilaya ya mbinga.

Nikiwa darasa la tano nilihama kwenda kusoma wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa na kujiunga na shule ya msingi Mdete nikiwa dada yangu Alice Nindi ambaye wakati huo aliolewa na na Oddo Matembo ambaye alikuwa ana fanyia idara ya kazi Wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa.

Nikiwa darsa la sita nilihama tena na kwenda kusoma shule ya msingi Wangingombe katika wilaya iringa nilisoma kwa mdu wa miezi sita hatimaye kurudi tena shule ya msingi mdete hadi nilipo maliza shule ya msingi mwaka 1967.

Wakati nikingoja majibu ya mtihani wamatokeo ya darasa la nane dada yangu Alice Nindi aliamua kunipeleka shule ya kulipia mkoani Dodoma ijulikanayo kwa jina la Y.P.Insitute Ovada ambayo ili kuwa iki milikiwa na Father super .

Nilijiunga na secondary ya ovada 1968 na kumaliza masomo yangu mwaka 1972 nilijihusisha na maswala ya biasha kwa kufanya biashara kati ya Tanzania ,Malawi.Zambia,Zimbabwe, Msumbiji, Mpaka Africa kusini. Katika biashara zangu kwa asilimia kubwa likuwa na Tembea kwa mguu pale ilipo bidi biashara za Mkononi hatimaye nafaka mbalimbali.

Mwaka 1974 ili jiunga kuandikia gazeti la Watu ambalo lilikuwa likichapishwa Dar –es –Salaam nilifanya kwa mwka mmoja na kujiunga na Gazeti la Sani nako sikudumu nikajiunga na Gazeti la Mwenge la dini linalo chapishwa Peramiho Songea kipindi chote hicho lilikuwa nikijiendeleza na masomo ya uandishi wa habari,

Mwaka 1980 nilichukua masomo ya dini ya kiislamu na kuweza kufaulu vizuri nilianza kufanya mahubiri katika nchi za Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na Zambia, na kuweza kufungua misikiti zaidi ya 5

Mwaka 1985 nililijiunga na Televisheni CNN ambayo makao yake yalikuwa Dar –es – Salaam nime fanyia Tv hiyo kwa muda wa miaka 4 na mwaka 1989 lianza kutuma habari Radio Free Africa na badaye kuanzishwa tv ambako niko mpaka sasa. napenda kuwa fahamisha elimu niliyo pitia na vyeti nilivyo pata na ambatisha hapa chini.

Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma wakijadili swala la elimu katika shule za msingi na shule za sekondary kuhusu utumiaji wa ligha ya kingereza, kutoka kushoto Juma Nyumayo na katikati ni Adamu Nindi kutoka kulia ni mdau wa Elimu dada Mbogoro

Katibu wa chama cha wandishi wa Habari Andrew Chatwanga na mjumbe wa NCCR Mageuzi ndugu Peter


ADAMU NINDI –ELIMU –SONGEA

Mkuu wa mkoa wa ruvuma Dr Cristina Ishengoma amesema ili kujenga uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne katika somo la kingereza wanafunzi wanatakiwa kusoma somo hilo toka shule ya awali.

Mkuu wa mkoa amesema hayo wakati akihojiana na star tv kwa nini watoto wa shele za sekondari wana shindwa kumudu somo la kingereza.

Wanafunzi wa shule ya secondary ya wavulana songea wamesema katika kuboresha lugha ya kingereza na somo la kingereza ina takiwa kuwa na walimu wenye wito.
,
Nao wanafunzi wa shule ya wasichana songea wamesema msingi wa somo la kingereza ujengwe toka shule za awali .

Inginia haruna makule ,afisa elimu secondary Justin mwingira mwalimu wa shule ya secondary beroya joseph matiko, meneja wa bima mkoa wa ruvuma moses senje wamesema walimu wanao ajiriwa wawe na ujuzizi wa somo la klingereza pia waajibike wajue wapo kazini kufundisha,

Mkuu wa mkoa cristina ishengoma amesema somo la kingereza lianzie shule ya awali na katika bunge lililo pita ili gusia kuhusu kupandisha kiwango cha elimu kwa somo la kingereza
Miongoni ya mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana miongoni mwake ni mkoa wa ruvuma, mkoa umejipanga kukabiliana na swala hilo.
Mwandishi wa habari wa Star Tv Adam Nindi akipeana mawazo na Mwaandishi wa ITV Mbeya Daniel Tweve katika ukumbi wa blue Pearl Hotel jijini Dar -es - salaam


ADAMU NINDI –ELIMU –SONGEA

Mkuu wa mkoa wa ruvuma Dr Cristina Ishengoma amesema ili kujenga uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne katika somo la kingereza wanafunzi wanatakiwa kusoma somo hilo toka shule ya awali.

Mkuu wa mkoa amesema hayo wakati akihojiana na star tv kwa nini watoto wa shele za sekondari wana shindwa kumudu somo la kingereza.

Wanafunzi wa shule ya secondary ya wavulana songea wamesema katika kuboresha lugha ya kingereza na somo la kingereza ina takiwa kuwa na walimu wenye wito.
,
Nao wanafunzi wa shule ya wasichana songea wamesema msingi wa somo la kingereza ujengwe toka shule za awali .

Inginia haruna makule ,afisa elimu secondary Justin mwingira mwalimu wa shule ya secondary beroya joseph matiko, meneja wa bima mkoa wa ruvuma moses senje wamesema walimu wanao ajiriwa wawe na ujuzizi wa somo la klingereza pia waajibike wajue wapo kazini kufundisha,

Mkuu wa mkoa cristina ishengoma amesema somo la kingereza lianzie shule ya awali na katika bunge lililo pita ili gusia kuhusu kupandisha kiwango cha elimu kwa somo la kingereza
Miongoni ya mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana miongoni mwake ni mkoa wa ruvuma, mkoa umejipanga kukabiliana na swala hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Cristine Ishengoma akieleza maswala ya Elimu

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr Cristine Ishengoma akiwa ofisini kwake akieleza swala zima la uboreshaji wa Elimu Mkoani Ruvuma alipo kuwa akiongea na Mwandishi wa Star Tv Adamu Nindi

ADAMU NINDI –ELIMU –SONGEA

Mkuu wa mkoa wa ruvuma Dr Cristina Ishengoma amesema ili kujenga uwezo wa wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani ya kidato cha pili na cha nne katika somo la kingereza wanafunzi wanatakiwa kusoma somo hilo toka shule ya awali.

Mkuu wa mkoa amesema hayo wakati akihojiana na star tv kwa nini watoto wa shele za sekondari wana shindwa kumudu somo la kingereza.

Wanafunzi wa shule ya secondary ya wavulana songea wamesema katika kuboresha lugha ya kingereza na somo la kingereza ina takiwa kuwa na walimu wenye wito.
,
Nao wanafunzi wa shule ya wasichana songea wamesema msingi wa somo la kingereza ujengwe toka shule za awali .

Inginia haruna makule ,afisa elimu secondary Justin mwingira mwalimu wa shule ya secondary beroya joseph matiko, meneja wa bima mkoa wa ruvuma moses senje wamesema walimu wanao ajiriwa wawe na ujuzizi wa somo la klingereza pia waajibike wajue wapo kazini kufundisha,

Mkuu wa mkoa cristina ishengoma amesema somo la kingereza lianzie shule ya awali na katika bunge lililo pita ili gusia kuhusu kupandisha kiwango cha elimu kwa somo la kingereza
Miongoni ya mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana miongoni mwake ni mkoa wa ruvuma, mkoa umejipanga kukabiliana na swala hilo.

Walimu wa kufunzi wa chuo cha Walimu Matogoro manspaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiwa katika mgomo kuidai Serekari kiasi cha shilingi Miloni 56 ndipo warudi kazini


Adamu nindi –songea walimu

Walimu wakufunzi wa chuo cha walimu Matogoro katika Manspaa ya Songea mkoani Ruvuma wameazna mgomo wa wiki mbili kwa madai ya kuitaka serekakari ilipe madai ya shilingi milioni 56.3,47,000

Walimu hao wa chuo cha walimu wakiongozwa na Simoni Sainyeye na mwalimu Festo Siame wamesema hayo katika ukumbi wa chuo ccha walimu cha songea matogoro wakati wa kikao kati ya viozi wa chama cha walimu wilaya ya songea na walimu wa kufunzi wa chuo cha matogoro.

Walimu hao wakiwakilisha madai yao wame sema wana dai fedha za likizo, Makato ya nyumba za walimu ambazo wana katwa bila kuishi , pia kuto pandishwa vyeo kwa muda mrefu hivyo wamesema hawata ingia darasani kufundisha mpaka madai yao ya shilingi 56,347,000 zimelipwa.

Wanafunzi walimu wa Chuo cha Matogoro wamesema Serekari inatakiwa kutekeleza madai ya Walimu wakufunzi kwa kuwalipa madai ya fedha wanazo dai vinginevyo mgomo wao hauathiri Walimu wana funzi wa chuo Matogoro . Bali hali ya Elimu ita poromoka kwa kasi kubwa, hii ni sawa na Kulima Shamba bila kutia Mbolea vinginevyo huwezi kupata Mazao

.Mwenyekiti osimundi kapinga ameahidi kufuatilia madai ya walimu kwa muda usio pungua wiki mbili,mbali na hilo walimu wametoa angalizo endapo hawata lipwa malipo yayo basi watajitoa kwenye chama hicho kwa kuwa hakina maana kwao.

Mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya songea Osimundi Kapinga ambaye na uongozi wake wajumbe wapatao wanne hawata sahau kilicho wa kuta walipo fanya ziara katika chuo cha walimu. Wali kufungiwa katika ofisini za walimu kwa masaa 7 wakidaiwa wawasiliane na katibu mkuu wa Elimu taifa juu ya madai yao ndipo wata funguliwa baada ya kupata jibu sahihi

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbinga Johhn Komba akipata wakafu wilayani mbinga wakufu alio pewa na Kadinali Pengo, kushoto kwake ni mhashamu askofu Norobet Mtega


ADAM MZUZA NINDI–SONGEA -
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norbet Mtega amewataka wahitimu wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kutumia elimu waliyoipata kwa kuleta Maendeleo na sio elimu hiyo kutumia kwa kuwahujumu Wananchi.

Mhashamu Norbet Mtega ameyasema hayo wakati akitoa Hotuba kwa wahitimu 20 ambao 15 walitunukiwa Shahada na 5 Sitashahada katika Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma

Mhashamu Askofu wa Jimbo la Songea Norbet Mtega amesema nia ya Teknolojia ni kuleta Maendeleo, lakini Teknolojia hiyo hiyo inaweza kuwa sumu kwa watu wahitimu wanaweza kutumia elimu hiyo kwa kuangalia mitandao ya ngono na kusababisha ongezeko la ukimwi badala ya maendeleo tarajiwa..

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norobet Mtega amewataka wa hitimu kuwa na moyo wa upendo kufanya kazi kwa bidii wakitumia elimu waliyo ipata kwa kuboresha maswala ya uchumi kuangalia soko la mazao mbali mbali kupitia mitandao

Wazazi walioshuhudia Wahitimu 20 wakitunukiwa Stashahada na Shahada wamesema ni vizuri Vijana wasomi wanaohitimu wakalenga kupeleka elimu waliyoipata Vijijini ambako Teknolojia hiyo inahitajika zaidi.

Mwenyekiti wa Chuo cha DMI Afrika kutoka India Jorog Arulraj amewataka wanachuo waliopata Shahada na Star Shahada kutumia vyeti hivyo kwa kutangaza maadili mazuri ya Chuo cha Mtakatifu Joseph kwa kufanya kazi ambazo zitatangaza sifa nzuri za Chuo kwa kufanya kazi zenye tija kwa Wananchi walioko pembezoni.

Mwenyekiti wa DMI Afrika Jorog Arulraj amesema Chuo cha Mtakatifu Joseph kitakuwa ukombozi kwa upande wa Kilimo, Chuo hicho kwa Mwaka 2013 – 2015 kinatarajia kuwa na Wanachuo 3000, pia DMI inatarajia kutumia Bilioni 1 kwa ajili ya kuendeleza Chuo cha Kilimo cha Mtakatifu Joseph kilichoko manspaa ya songea mkoani Ruvuma.

MKURUGENZI WA UPIMAJI WA ARIDHI TANZANIA

Mkurugenzi wa upimaji na Ramani nchini Tanzania wapili kutoka kushoto Dr Selassie Mayunga akiwa na Mkurugenzi wa Mipaka kutoka Msumbiji Josse Elias Mucumbo wakati walipo kuwa wakikagua mipaka katika kijiji cha Nindi kata ya Lipalamba wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma



Adamu Nindi – Mipaka –Msumbiji na Tanzania

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani nchini Tanzania Dr Selassie Mayunga na Mkurugenzi wa Mipaka ya Baharina Nchi kavu nchini Msumbiji Jose Elias Mucumbo wame wataka wananchi waMsumbiji na Tanzania kujenga mahusiano mazuri zaidi baada ya mipaka ya Tanzani na Msumbiji kukamilika.

Wakurugenzi hao wameyasema hayo wakati wakikagua kukamilika kwa mipaka iliyopo katika kijiji cha Nindi kata ya Liparamba wilayani Mbinga Mipaka yenye urefu wa Kilometa 51 ambayo ujenzi wake umegharimiwa na Serekari ya Ujerumani kwa kutoa uro 30,000.
Mkurugenzi wa mipaka ya nchikavu na Bahari Jose Eliasi Mucombo kutoka Msumbiji amesema mipaka isiwe chanzo cha kuwa tenganisha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Msumbiji bali iwe chanzo cha kuleta maendeleo

Mkurugenzi wa upimaji wa Ramani nchini Tanzania Dr Selassie Mayunga amesema wananchi walioko mpakani mwa Tanzania jukumu lao kubwa nikulinda Mawe yaliyo pandwa yasi ngolewe ,

Mkurugenzi wa upimaji wa Ramani nchini Tanzania Dr Selassie Mayunga amsema Serekari yaTanzani ita hakikisha zoezi la upimaji wa mipaka kwa nchi zinazo pakana na Tanzania hadi mwaka 2012 lina kamilika

Wananchi wa Tanzania wameshukuru Serekari yaTanzania na Msumbiji kwa kuweka mipaka ,Watanzania hao wamesema w Mkurugenzi wa mipaka ya nchikavu na Bahari Jose Eliasi Mucombo kutoka Msumbiji amesema mipaka isiwe chanzo cha kuwa tenganisha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Msumbiji bali iwe chanzo cha kuleta maendeleo

Kikao cha kwanza cha kupima mipaka kati ya nchi za Tanzania,Malawi na Msumbiji kilifanyika Belin Ujerumani na vikao kuendelea mwaka 1884,1923, 1925 kuweka mawe mpaka wa Msumbiji na Tanzania .Mwaka 1956 mpaka wa Tanzania na Malawi kuwa katikati ya ziwa Nyasa. Mwezi 8 /2011 kukamilisha kwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

MADIWANI WANA WAKE SONGEA WA DAI HAKI ZAO

Madiwani wa mkoa wa Ruvuma wakiwa katika mjadala wa kudai haki zao katika nyanja mbalimbali katika uongozi


ADAMU NINDI -Songea

Madiwani wa viti malumu wa mkoa wa ruvuma wameiomba serekari kurekebisha kanuni na miongozo ambayo ina wanyima haki madiwani wa viti malumu kugombea baadhi ya nyazifa katika halimashauri za wilaya na katika kata,

Madiwani Wanawake wa viti malumu wa Mkoa wa Ruvuma wamesema endapo hali ya kuwa tenga katika vikao vya bajeti au vikao vya kuibua miradi yenye kuleta maendeleo kwa wanchi katika kata .jambo watakalo fanya mara watakapo itwa ili kupitisha bajeti hiyo wata ikataa hadi watakapo shirikishwa.

Madiwani wakiendelea kuchangia hoja wakiongozwa na Prisca Haule wamesema kutengwa kwao kwa kunyimwa kugombea nyazifa mbalimbali katika wilaya zao wamesema ina tokana na miongozo na kanuni kuegemea upande mmoja.

Nao Madiwani kutoka wilaya ya tunduru Tunduru wamesema mara zote wanapochangia michango yao katika vikao vya baraza la madiwani hudharauliwa na kusema wao ni madiwani wa viti malumu .

Katika kukabiliana na ubaguzi wakuwatenga wanawake wa viti malumu mjumbe kutoka songea winfrida komba amesema dawa pekee wanawake ni kujizatiti katika chaguzi mbalimbali ,wanawake waungane ili kuhakisha watakao gombea kuanzi ngazi ya kata hadi jimbo wana shinda

Wawezeshaji kutoka mtandao wa jinsia TGNP kutoka makao makuu jijini Dae –es – salaam Badi Darusi ambaye ni Mchambuzi wa Bajeti, na Nema Duma mjumbe wa Bodi ya TGNP . wamesema msingi mzuri kwa madiwani wote ni kuhakikisha fedha zinazo tolewa na serekari katika kuleta maendeleo kwa wanachi zina fanya kazi iliyo pangiwa .

MWISHO

MEYA WA MANSPAA YA SONGEA AFARIKI



Jeneza la aliye kuwa meya wa songea Hayati Ally Said Manya akipelekwa kuzikwa makaburi ya Lizaboni Songea




ADAMU NINDI –SONGEA –KIFO MEYA
Mmanspaa ya songea na vitongoji vyake iko katika majonzi baada ya kumpoteza aliye kuwa Meya wa Manspaa ya Songea Ally Said Manya ambaye amefariki tarehe 30/7/2011 katika hospitali ya peramiho songea vijijini.

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi James Makene Diwani wa Matarawe Manspaa ya Songea amesema mazishi yaliye kuwa Meya wa Manspaa ya Songea yata fanyika siku ya Jumaa Tatu majira ya saa saba mchana.

Mwenyekiti wa mazishi James Makene amesema kamati ya mazishi imeanza mandalizi ya mazishi .kamati ina watu watano wakiwemo viongozi wa serekari na vyama vya siasa.watu ambao wamesha fika katika eneo la msiba ni pamoja na viongozi wa chana serekari.

Mkuu wa mkoa wa ruvuma Dr Cristina Ishengoma ametoa salamu za Rambi Rambi kwa wafiwa , Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Cristina Ishengoma pia ametoa salamu za Rambirambi katika ofisi ya waziri Mkuu [ TAMISEMI] na wa Bunge wote wa Mkoa wa Ruvuma.
Walio toa tarifa za kushiriki mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Habari na Utamaduni Dr Emanuel John Nchimbi ambaye ni mbunge wa jimbo la songea.Marehemu Ally Saidi Manya alikuwa akisumbuliwa na Kisukari amefariki akiwa hospitali ya Peramiho Songea vijijini, ina lilahi waina rajuni,[sisi ni wamwenyezi mungu na kwake tuta rejea] Rohoho ya marehemu Ally Said Manya Mwenyezi Mungu aiweke mahari pema peponi

ADAM MZUZA –SONGEA -24/08/2011
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norbet Mtega amewataka wahitimu wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kutumia elimu waliyoipata kwa kuleta Maendeleo na sio elimu hiyo kutumia kwa kuwahujumu Wananchi.

Mhashamu Norbet Mtega ameyasema hayo wakati akitoa Hotuba kwa wahitimu 20 ambao 15 walitunukiwa Shahada na 5 Sitashahada katika Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma

Mhashamu Askofu wa Jimbo la Songea Norbet Mtega amesema nia ya Teknolojia ni kuleta Maendeleo, lakini Teknolojia hiyo hiyo inaweza kuwa sumu kwa watu wahitimu wanaweza kutumia elimu hiyo kwa kuangalia mitandao ya ngono na kusababisha ongezeko la ukimwi badala ya maendeleo tarajiwa..

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norobet Mtega amewataka wa hitimu kuwa na moyo wa upendo kufanya kazi kwa bidii wakitumia elimu waliyo ipata kwa kuboresha maswala ya uchumi kuangalia soko la mazao mbali mbali kupitia mitandao


Wazazi walioshuhudia Wahitimu 20 wakitunukiwa Stashahada na Shahada wamesema ni vizuri Vijana wasomi wanaohitimu wakalenga kupeleka elimu waliyoipata Vijijini ambako Teknolojia hiyo inahitajika zaidi.

Mwenyekiti wa Chuo cha DMI Afrika kutoka India Jorog Arulraj amewataka wanachuo waliopata Shahada na Star Shahada kutumia vyeti hivyo kwa kutangaza maadili mazuri ya Chuo cha Mtakatifu Joseph kwa kufanya kazi ambazo zitatangaza sifa nzuri za Chuo kwa kufanya kazi zenye tija kwa Wananchi walioko pembezoni.

Mwenyekiti wa DMI Afrika Jorog Arulraj amesema Chuo cha Mtakatifu Joseph kitakuwa ukombozi kwa upande wa Kilimo, Chuo hicho kwa Mwaka 2013 – 2015 kinatarajia kuwa na Wanachuo 3000, pia DMI inatarajia kutumia Bilioni 1 kwa ajili ya kuendeleza Chuo cha Kilimo cha Mtakatifu Joseph kilichoko manspaa ya songea mkoani Ruvuma.