ADAM NINDI – YALIYO JIRI SONGEA
Wanawake wametakiwa kuthubutu katika kutetea haki zao kwa kupambana na mfumo dume ambao unawa fanya wasiwe na sauti ya kudai haki zao.
Hakimu mkaazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Songea Janety Honoratus Mtega amesema hayo baada ya kufanya ziara katika gereza la Mahabusu la Songea na kubaini makosa mengi ya watu walio shitakiwa na kushitaki yamekuwa mengi zaidi kwa wanaume kuliko wanawake , sababu kubwa zaidi ni wanawake kukosa elimu ya kisheria pia umasikini ulio kisiri miongoni mwa wanawake
jambo hili huwa fanya wanawake wengi waridhike na lile wanalo fanyiwa na kuona kudai haki ni kupoteza wakati ,Pia vyombo nya kisheria vinavyo watetea watu wasio na uwezo havijitangazi ili mwanchi aliyoko pembezoni aweze kupata furusa hiyo.
, Hakimu mkaazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya songea Janety Honoratus Mtega Akitoa takimu ya mahabusu na wafungwa walioko gereza la songea amesema robotatu ya idadi ya wafungwa ni wanaume wanawake wapo kidogo sana,katika ziara aliyo ifanya tahehe 29/7/2011 alibaini kuwepo mwa mwanamke mmoja aliye shtakiwa kwa kosa la mauaji Aima Shabani, Mwanamke mwingine ni Sikujua Kaluwa anaye tuhumiwa kuvunja na kuharibu mali lakini yeye yuko nje kwa dhamana,
Habari ziliyo patikana inje ya mahakama zina sema Nyumba hiyo inayo gombaniwa ni mali ya Sikujua kaluwa .Nyumba hiyo inadaiwa imeuzwa kima kosa , Mpaka sasa nani iwe nyumba yake imebaki kuamuriwa na Mahakama nani ata shinda kati ya mdai na mdaiwa.
Hakimu mkaazi mfawidhi wa mahakama ya songea Janety Honoratus Mtega amesema kutoka na ziara yake gerezani amebaini kuwa watuhumiwa walio wengi hawana uwezo wakuweka mawakili ,Hakimu mkaazi mfawizi wa mahakama ya songea amewataka mawakili ambao hutetea watuhumiwa wakesi mbalimbali watembelee katika magereza ili wawasaidie wale ambao hawana uwezo wa kudai haki zao.
Akieleza kuhusu wanasheria amesema ni vizuri Jeshi la Police na wana sheria wakashirikiana kusukuma kesi zilizopo ili kuweza kupunguza mlundikano wakesi na kuweza kupunguza mahabusu gerezani
No comments:
Post a Comment