KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Wednesday, August 24, 2011

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbinga Johhn Komba akipata wakafu wilayani mbinga wakufu alio pewa na Kadinali Pengo, kushoto kwake ni mhashamu askofu Norobet Mtega


ADAM MZUZA NINDI–SONGEA -
Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norbet Mtega amewataka wahitimu wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kutumia elimu waliyoipata kwa kuleta Maendeleo na sio elimu hiyo kutumia kwa kuwahujumu Wananchi.

Mhashamu Norbet Mtega ameyasema hayo wakati akitoa Hotuba kwa wahitimu 20 ambao 15 walitunukiwa Shahada na 5 Sitashahada katika Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Ruhuwiko Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma

Mhashamu Askofu wa Jimbo la Songea Norbet Mtega amesema nia ya Teknolojia ni kuleta Maendeleo, lakini Teknolojia hiyo hiyo inaweza kuwa sumu kwa watu wahitimu wanaweza kutumia elimu hiyo kwa kuangalia mitandao ya ngono na kusababisha ongezeko la ukimwi badala ya maendeleo tarajiwa..

Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norobet Mtega amewataka wa hitimu kuwa na moyo wa upendo kufanya kazi kwa bidii wakitumia elimu waliyo ipata kwa kuboresha maswala ya uchumi kuangalia soko la mazao mbali mbali kupitia mitandao

Wazazi walioshuhudia Wahitimu 20 wakitunukiwa Stashahada na Shahada wamesema ni vizuri Vijana wasomi wanaohitimu wakalenga kupeleka elimu waliyoipata Vijijini ambako Teknolojia hiyo inahitajika zaidi.

Mwenyekiti wa Chuo cha DMI Afrika kutoka India Jorog Arulraj amewataka wanachuo waliopata Shahada na Star Shahada kutumia vyeti hivyo kwa kutangaza maadili mazuri ya Chuo cha Mtakatifu Joseph kwa kufanya kazi ambazo zitatangaza sifa nzuri za Chuo kwa kufanya kazi zenye tija kwa Wananchi walioko pembezoni.

Mwenyekiti wa DMI Afrika Jorog Arulraj amesema Chuo cha Mtakatifu Joseph kitakuwa ukombozi kwa upande wa Kilimo, Chuo hicho kwa Mwaka 2013 – 2015 kinatarajia kuwa na Wanachuo 3000, pia DMI inatarajia kutumia Bilioni 1 kwa ajili ya kuendeleza Chuo cha Kilimo cha Mtakatifu Joseph kilichoko manspaa ya songea mkoani Ruvuma.

No comments:

Post a Comment