KILA WAKATI ANGALIA STAR TV NA KUSIKILIZA RADIO FREE AFRICA Matangazo

UKIWA NA TANGAZO TAFADHALI WA SILIANA NA SISI KWA NAMBA 0755731234 AU 0755061588
Tuna pokea Matangazo ya StarTV na Radio Free Africa. Wasiliana nasi kwa Email: adammzuza@yahoo.com au mzuzanindi@gmail.com | Simu: 0755 731 234 au 0655 731 234   kwa Mawasiliano zaidi unaweza kutumia NO 0755061588 Judith Lugoye ,shuguli zote za blog hii anaweza kukusaidia MATANGAZO , AU HABARI

Monday, October 31, 2011

MAENDELEO YA MJI WA LINDI

Mama mjasilia mali Hawa Selemani aishie katika manispaa ya Lindi akiwa katika jitihada za kugonga kokoto kwa ajili kuhudumia familia. Mama Hawa Selemani ana watoto 5 ambao wana tegemea shughuli hiyo ya ugongaji kokoto, amesema amefanya kila linalo wezekana kutaka kupata mkopo lakini shughuli yao mbele ya serekali haionekani kama kuna kitu.

Tukiwa tuna sherekea miaka 50 ya uhuru, wenzetu Tanzania bado wapo watu ambao wanatumia mtindo wa kizamani wa kusaga unga kwa kutumia mawe. Mama unae mwona hapo juu ni mama Lipu akisaga unga wa mtama kwa njia ya jadi kwa kutumia mawe mawili makubwa yakitumika kama mashine.

Tanzania inasherekea Miaka 50 ya uhuru lakini wananchi bado halizao ziko katika hali tete wana lala katika nyumba za tembe kama unavyo iona nyumba hiyo hapo juu hizo ndizo nyumba za watu wa lindi .Hiyo nyumba ipo katikati ya Manispaa ya Lindi eneo la Mtanda

Saturday, October 29, 2011

KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA AWATAKA WAANDISHI KUWA SAIDIA WATU WALIOKO PEMBEZONI

Mkurugenzi mkuu wa Bima ya Afya Tanzania akieleza mafanikio ya Bima ya Afya kwa miaka kumi iliyo pita tayari bima ya afya imepanga kuwa fikia wateja wapatao milioni 6 ifikapo mwaka 2012 hivi sasa Bima ya Afya ina wateja wapatao milioni 3.3

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na usitawi wa Jamii Blandina Nyoni amewataka waandishi wa habari kusaidia kuainisha matatizo yanayo wakabili watu walioko pembezoini na kusaidia kuhamasisha wananchi kujiunga na CHF ili iwakomboe pale wanapo patwa na maradhi

Mganga mkuu wa serekari Nchini Tanzania amesema waganga ambao hawata wajibika katika utendaji wa kazi ni juu ya waandishi wa habari kuwafichua kwa vitendo watakavyo fanya pia amewataka waandishi kupongeza vilevile kwa wafanyakazi wa widhara ya Afya pale watakapo fanya vizuri

Mkurugenzi wa TBC Daniel Mshana amepongeza kitendo cha Bima ya Afya kuwa shirikisha waandishi katika utafi wakujua mafanikio na changamoto zinazo wakabili wanachama wa NHIF na CHF

Thursday, October 27, 2011

MKUTANO MKUU 10 WA BIMA YA AFYA MOROGORO

Mafasa wandamizi wa Bima ya Afya mwanzoni ni Eugen MKONKOTI anaye fuata ni Rehani Athumani wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Joel Bendera wakati akifungua Mkutano mkuu wa Bima ya Afya Mkoani Morogoro

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua Mkutano mkuu wa Bima ya Afya unaofanyika Mkoani Morogoro, Mkuu wa mkoa amewaomba waandishi kushiriki katika kueleza maruzi yanayo fanywa na Mfuko wa bima ya Afya pamoja na kukosoa yale mabaya yanayo ikabili mfuko huu.

Mkuu wa Mkoa wa Mrorogoro Joel Bendera akipitia Kablasha la linalo onyesha utafiti uliofanywa na waandishi Tanzania Mzima

Waandishi wahabari na wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya wakiomboleza kuwakumbuka waliotangulia mbele za haki walioshiriki katika gurudumu la mfuko wa bima ya Afya katika kuleta mafanikio.

Nembo ya Mfuko wa Bima ya Afya ambyo imekuwa kielelezo kizuri katika mkutano ,kuu wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoani Morogoro

MAENDELEO YA MJI WA SONGEA YANA TOKANA NANINI ?

kama nilivyo uliza maendeleo ya Songea yametokana na nini ,jibu niwanaruvuma wenyewe wamepitia kwenye michakato mbalimbali hebu angalia picha ya hapo juu huyo unaye mwona ni mtoto wa mzee Litunu ni mzee wa kwanza kuweza kununua basi sipidi ya basi lake ilikuwa haivuki 10,asiye taka aliambiwa teremuka.mtoto huyo hapo juu amefuata nyayo za baba yake lakini kinyume yeye ni Diwani wa Kata ya Majimaji Tunduru Mh Halifani Litunu

Bado nakuletea maendeleo ya manspaa ya Songea hivi sasa barabara nyingi zina lami ,hiyo nibarabara ya kati nyuma ya misheni yaRomani Cathoric wakati mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari C,Nyoni akifaidi maendeleo ya JK

Songea ya zamani siyo ya sasa hebu angalia Majengo yanavyo pendeza nini kinawafanya wanaruvuma kushindwa kuja kuwekeza nyumbani kwenu hiyo ni changa moto inayo tukabili sisi sote maeneo yapo ya kutosha mna ngoja wawekezaji wachukue maeneo ndipo tuanze kulalamika

Tuesday, October 25, 2011

BIMA ZILIZO IVA ZA LIPWA BILA MATATIZO MKOA WA RUVUMA

Mkoa wa Ruvuma katika kusherekea miaka 50 ya Uhuru imejidhatiti kuhakikisha ina ilipa Bima zote zilizo iva kwa wateja wake ikiwa na pamoja na kutoa elimu ya jinsi ya kupata huduma kamili kutoka kwa NATIONAL INSURANCE CORPORATION OF TANZANIA. Meneja wa Tawi la Songea Moses E.Senje ameya sema hayo alipo kuwa akionge na songeahabari.blogspot.com


Meneja wa Bima Tawi la Songea Moses E.Senje akiwa ofisini a kiendelea kuidhinisha cheki kwa Bima zilizo iva , karibu Robo tatu ya Mkoa wa Ruvuma amesha ifikia wale wote wenye Tatizo wana weza kumwona wakati wowote .

ANAYE TUHUMIWA KUUA LEVINA NDUNGURU GEST HOUSE

Kijana Tomas Jarara 22 anaye Tuhumiwa kumwua Levina Ndunguru aliyse kuwa mhudumu wa Mvula Mpenda ,Kijana Toma Jarara anaye tuhumiwa kumwua Levina Ndunguru katika Gest House ya Mikumi Mfaranyaki Songea pichani hapo juu,



kaburi la marehemu Levina Ndunguru aliye zikwa huko wilani mbinga ambako ndiko aloko zaliwa,


Jeneneza la marehemu Levina Ndunguru likisafirishwa kwenda Wilayani Mbinga

Monday, October 24, 2011

WANAHABARI WAPATWA NA MSIBA RUVUMA

MAREHEMU LEVINA NDUNGURU

Wanahabari wa Mkoa wa Ruvuma wamepatwa na msiba mkubwa kwa kufiwa na mhudumu aliye kuwa akifanya kazi katika ofisi ya Mpenda Mvula ambaye ni mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma,


Mhudumu aliye kufa au kuuwawa ni Levina Ndungu ambaye alikuwa na Umuri wa Miaka 26 .siku ya tukio marehemu akiwa ofisini alikuja kijana aliye julikana kwa jina la Tomas Jirara mwenyeji wa mwanza akidai ana taka kuchapiwa barua yake na kuweza kulipa shilingi mia tano.


Mhudumu Levina Ndunguru bila kujua nia ya kijana Tomas Jirara alichapa barua hiyo na huku kijana huyo Tomas Jirara 22 akionyesha ukarimu wa hali ya juu kwa Levina Ndunguru hatimaye levina ndunguru kuanguka katika Mapenzi jambo ambalo kijana huyo Tomas Jirara 22 alikuwa amelipanga


Mara baada ya kumaliza kazi alimtoa out ingawa haijulikani ni wapi alimpeleka lakini kwa mujibu wa tarifa iliyo tolewa na kaimu kamanda waPolice mkoa wa Ruvuma .Zina sema Marehemu Devina Ndunguru akiwa na kijana Tomas Jirara walirudi saa 1.00 usiku walipewa chumba katika nyumba ya wa geni Mikumi Mfaranyaki , Tomas Jirara aliweza kumua Levina Ndunguru majira ya 8.00 usiku ,lakini alipohojiwa na POLICE ana sema aliweza kufanya kitendo cha kinyama kati ya saa 2.30 usiku au saa 2.45 akinukuriwa anasema mara baada ya kufanya mapenzi na Levina Ndunguru wakiwa kwenye mapenzi walikorofishana ndipo alipo mpiga ngumi moja nzito mwisho kumalizia kumvunja shingo alieleza mbele ya police bila hata kigumimizi.


Tomasi Jirara alipo fanikiwa kumua Levina Ndunguru alimpekua na kuchukua funguo za ofisi inayo milikiwa na Mpenda Mvula na kwenda kufungua na kuiba Comyuta moja ,Printer pamoja na Cheki yenye Thamani ya Shilingi 150,000

Baada ya kukamilisha wizi wake alianza safari kuelekea njia ya Lindi alipo kamatwa na Police, SASA HEBU ANGALIA PICHA YA MUUAJI NA BINTI ALIYE UWAWA HALAFU TOA MAJIBU, TUFANYE NINI NA MABINTI ZETU ?

Sunday, October 23, 2011

NIFURAHA IPI WEWE UME CHAGUA KATIKA MAISHA YAKO ?

Ndugu yangu katika Dunia hii kuna mambo ambayo mtu anatakiwa kuyajua ,Furaha zipo za aina nyingi lakini furaha ambazo hazikwepeki ni Mtu anapo zaliwa, Mtu anapo pata Ubatizo na pale Mtu anapo pata Kipaimara na mwisho anapo pata jiko au kuoa, uislamu ni kuzaliwa na kufunga ndoa, Jee katika mambo hayo wazee wana shiriki kutoa maadili ya mambo hayo yote ?kama hawa shiriki tufanye nini? Picha hapo juu Mwali anajianda kwenda kuolewa hebu saidia nini kifanyike ili ndoa yake iwe salama


Mpambaji wa Arusi manspaa ya Songea ajulikanaye kama mama ALUU Hapo tayari amempamba bi Harusi tayari kwa kwenda Ukumbini.

Saturday, October 22, 2011

MKUU WA MKOA AIWAKIA KAMPUNI YA PROGRESSIVE BAADA YA KUSHINDWA KUTIMIZA MKATABA WA KUJENGA BARABARA YA NAMTUMBO VS TUNDURU

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Saidi Thabit Mwambungu akiwa amemwakia Meneja wa Tanroard Abrahamu Kisimbo baada ya kuona kampuni ya Progressive kutoka india ikiwa imebaki kwenye mipango yakinifu zaidi ya miezi 9. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mefikia hatua ya kuwasiliana na Waziri mwenye dhamana Mh.John Magufuri ili aweze kufahamu ni jinsi gani kampuni isiyo na uwezo kupewa kilimeta 187 ambazo zilitakiwa kupewa makampuni matatu .Tanroad imetoa notisi ya siku 28 kwa kampuni ya Progressive kwa kushindwa kwenda sawa na mkataba.

Meneja wa Tanroad Mkoa wa Ruvuma Abrahamu Kisimbo akiwa amebanwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu kuhusiana na kupewa kampuni ya Progressive utengezaji wa barabara kutoka Namtumbo hadi Tunduru huku kampuni hiyo ikiwa haina uwezo

Mipango Yakinifu inayo fanywa na Kampuni ya Progressive kutoka India ndiyo hiyo inayo onekana hapo juu

Friday, October 21, 2011

BIMA YA AFYA NI MKOMBOZI WA WANYONGE

Wanufaika wa mfuko CHF Wanao tumia Bima ya Afya katika Hospitari ya Tunduru Mkoani Ruvuma
wafanya kazi wa wilaya ya Tunduru walio jiunga na Mfuko wa Bima ya Afya wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabith Mwambungu

Tuesday, October 18, 2011

MWANDISHI MWANDAMIZI ASHANGWA ZA NA VIVUTIO VYA RUVUMA

Bwana Beda Msimbe, Mwandishi wa Habari mwandamizi toka Dar akiwa tayari ameshiba maelezo ya kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Manispaa ya Songea mahala ambapo hakutarajia kuona matambiko yakiendelea katika kaburi la pamoja la watu 66 na lile la Nduna Songea Mbano Luwafu ambao walinyongwa na Wajerumani Tarehe 27/2/1906 na siku tatu baadaye Nduna Songea aliuawa na Kichwa chake kukatwa na kupelekwa Ujerumani. Mahali hapo alishuhudia pia pesa kibao za sadaka zilizowekwa na wafuasi wa mila za Kingoni. Hapa akitokea kwenye makaburi hayo na sasa anaelekea kwenye sanamu ya Askari wa JWTZ na zile 12 za Manduna wa Kingoni. [Picha na Juma Nyumayo]

Kaimu mkurugenzi wa H/wilaya ya Songea akiwa na wandishi wa Habari akitoa hali halisi ya Bima ya Afya katika H/ya Wilaya Songea

Makamu Mwenyekiti H/ya Wilaya ya Mbinga Prisca akieleza Bima ya Afya inavyo katisha tamaa wilaya ya mbinga. uhamasishaji umekuwa mdogo

Saturday, October 15, 2011

VIFAA VYA COMPYUTA VYA PATIKANA MBINGA


Mtaalamu wa Compyuta Matembo akijaribisha vifaa vilivyo letwa wilayani mbinga tayari kwa kuuza, ukitaka kifaa chochote cha Compyuta wasiliana naye kwa namba 0768302047 yupo mtaa NMB Bank

WADAU WA HABARI WAITAKA SEREKARI KUTOA RUDHUKU KWA WAANDISHI WA HABARI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Said Thabit Mwambungu akiwa na wadau wa Habari Mkoani Ruvuma wa kwanza Kulia ni Mstaiki Meya wa Manspaa ya Songea Chares Mhagama

Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wadau wa Habari katika kikao cha pamoja nawaandishi mkoani Ruvuma

Mwandishi wa Habari mtoji wa Changamoto Miongoni mwa Wanahabari Crensecia Kapinga aliye na mtandio akiwa kwenye kikao hapo anaonekana akiwa na washawasha kutaka kuchangia

wadau wa Habari kutoka vyama mbalimbali vya siasa na Madhehebu ya Dini wakiwa katika kikao cha kupata uelewa kuhusu Habari

Thursday, October 13, 2011

MADIWANI WALIO FUKUZWA NA CCM WILAYA WA SAMEHEWA NA CCM MKOA WA RUVUMA


Madiwani watano wa Chama cha Mapinduzi walio fukuzwa na kamati ya siasa ya wilaya ya Songea wamesamehewa na CCM Mkoa baada ya kikao kuwa hoji na kubaini makosa waliyo ya fanya ya kimaadili wakati wa uchaguzi wa Meya wa Manspaa ya kulikuwa siyo ya kusudia. Madiwani hao diwani Cristian Matembo,Victer Ngongi,Kula Besit diwani wa msamala,na Mhagama diwani wa mshangano. Katibu wa CCM Emanuel Mntyangingombe amesema kazi iliyoko ya CCM sasa ni kutoa Elimu kwa Madiwani wote wa CCM wote wa Mkoa wa Ruvuma

Wednesday, October 12, 2011

SAKATA LA UMEYA LAHITAJI BUSARA ZA MKUU WA MKOA WA RUVUMA

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imekuwa na Mafanikio baada ya kukagua ghala la hifadhi ya chakula mkoani hapa na kutembelea miradi mbalimbali na kujionea ufanisi uliopo ni jambo la kupongeza. La ajabu katika Ziara hiyo wakati wa hitimisho ilitokea suala ambalo linaashiria kuzorotesha Maendeleo ya Manispaa. Kwa nini CCM isichukue hatua ya kutatua mgogoro uliopo wa umeya, madiwani wa CCM wapo 21, Madiwani wa CHADEMA wako 7 wanapatata wapi nguvu ya kuitikisa Manispaa ya Songea? ni swali wanalojiuliza Wananchi wa Manispaa ya Songea hivi sasa wanangoja busara za Mkuu wa Mkoa mpya Mh. Said Thabit Mwambungu


Madiwani wa Manispaa ya Songea pamoja na Wafanya kazi wa Serikali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mh. Said Thabit Mwambungu alipofanya Ziara katika Manispaa ya Songea

KAZI YA MEYA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI NI KULETA MAENDELEO KATIKA MAENEO YAO

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea akiwa katika Ofisi yake akiongea na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma kuhusu kuendeleza ujenzi katika mpaka wa Msumbiji na Tanzania(Mkenda) ili kuwaletea uchumi endelevu kati ya Nchi hizo mbili

Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama akipongezwa na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahamadiyya Abid Bath baada ya kushinda katika kiti cha Umeya wa Manispaa ya Songea

JEE STENDI KUU YA MJINI SONGEA ITATENGAMAA LINI?

Manispaa ya Songea hivi sasa imeanza kutoa mtazamo mzuri wa Manispaa baada ya juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Songea kwa kuboresha barabara za lami eneo kubwa la mjini Songea. Hivi sasa jicho la Wananchi linaitazama Stendi kuu ya Mabasi yaendayo nje ya Mkoa, Swali ni kuwa usipoosha uso hata kama umeoga watu watasema huyu mtu ni mchafu hivyohivyo kukamilika kwa Stendi ni dalili ya Usafi wa Uso, juhudi gani zifanyike kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Songea Dr. Emmanuel John Nchimbi?

kipindi cha Masika kipo karibu stendi kuu ni kama inavyoonekana hapo juu juhudi zinahitajika za kuweka lami katika stendi kuu ya mabasi kazi hii itafanikiwa kwa ushirikiano kati ya wananchi, Madiwani na Mbunge wao

JEE WAKINA MAMA KWA HATUA HII WATAJIKWAMUA NA UMASKINI?

Wakina Mama wajasiliamali Mkoa wa Ruvuma wakihangaika kutafuta riziki katika barabara kuu iendayo Mbamba Bay, wakina Mama hao hulazimika kuuza Dagaa hawa Barabarani baada ya wateja kushindwa kwenda kununua bidhaa hiyo kwenye Soko Kuu

wanaoonekana katika ungo ni Dagaa wanaopatikana katika Ziwa Nyasa, akina mama hushindwa kuwasindika katika mifuko ili kuongeza ubora wa Dagaa hao kutokana na hali ngumu inayowakabili.

Tuesday, October 11, 2011

MKUU WA MKOA WA RUVUMA Mh.SAID THABIT MWAMBUNGU AWATAKA WAISLAAM KUDUMISHA AMANI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Saidi Thabit Mwambungu akisoma Gazeti la Mapenzi ya Mungu alilo pewa zawadi na Sheikh wa Ahamadiyya Mkoa wa Ruvuma Abid Bhatt


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Said Thabit Mwambungu amewataka Waislamu kuendeleza maombi ili Nchi yeyu iendelee kuwa Nchi ya Amani na Utulivu. Mkuu wa mkoa ameya sema hayo wakati akiongea na ujumbe wawatu watano kutoka Jumuiyya ya Waislaam waahamadiya walipo mtembelea Ofisini kwake



Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh.Said Thabit Mwambungu akipokea zawadi ya vitabu na Magazeti kutoka kwa Sheikh wa Ahamadiya Abid Bhatti alipo tembelewa ofisini kwake na wajumbe watano wa dhehebu la Ahamadiy

Monday, October 10, 2011

JEE WAJUA VIVUTIO VILIVYOKO KATIKA MKOA WA RUVUMA ?

Watanzania wamekuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa nchi za afrika Katika kupata uhuru picha ya hapo juu ni kiashirio cha Asikari Jeshi la wananchi Tanzania {JWTZ } wakati wa vita vya nduli vilivyo ongozwa na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kumtoa Nduli Idi Dada katika madaraka Nchini Uganda

Kaburi la shujaa wa kingoni Chifu Songea Mbano aliye nyongwa na Wajerumani na kichwa chake kupekwa ujerumani na kiwiliwili chake kuzikwa katika kaburi linalo onekana hapo juu.

kaburi la mashujaa 66 walio nyongwa na wajerumani 27/2/1906 na kuzikwa kaburi moja katika eneo la mashujaa Mahenge Manspaa ya Songea

Kaburi la mashujaa wa mkoa waruvuma walio pigana vita vya Majimaji wakiwa katika orodha kamili watu 66 walizikwa kaburi moja, kaburi hili lipo kata ya Mahenge Manspaa ya Songea


Nyumba hizi zilikuwa zikitumika na Machifu wa Mkoa wa Ruvuma kabla ya utawala wa wajerumani