
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh.Saidi Thabit Mwambungu akiwa amemwakia Meneja wa Tanroard Abrahamu Kisimbo baada ya kuona kampuni ya Progressive kutoka india ikiwa imebaki kwenye mipango yakinifu zaidi ya miezi 9. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mefikia hatua ya kuwasiliana na Waziri mwenye dhamana Mh.John Magufuri ili aweze kufahamu ni jinsi gani kampuni isiyo na uwezo kupewa kilimeta 187 ambazo zilitakiwa kupewa makampuni matatu .Tanroad imetoa notisi ya siku 28 kwa kampuni ya Progressive kwa kushindwa kwenda sawa na mkataba.

Meneja wa Tanroad Mkoa wa Ruvuma Abrahamu Kisimbo akiwa amebanwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu kuhusiana na kupewa kampuni ya Progressive utengezaji wa barabara kutoka Namtumbo hadi Tunduru huku kampuni hiyo ikiwa haina uwezo

Mipango Yakinifu inayo fanywa na Kampuni ya Progressive kutoka India ndiyo hiyo inayo onekana hapo juu
No comments:
Post a Comment